Obama anazidi kutesa, ameshinda kitongoji kingine kinachoitwa Hart.
Ushindi wake wote si wa mchezo maana anashinda kwa zaidi ya asilimia 80%. Historia inadhihirisha kwamba wagombea 19 kati ya 28 walioshinda majimbo mawili ya mwanzo yaani Iowa na New Hampshire, waliweza kunyakua nafasi ya ugombea (nominee) wa chama.

Mhabarishaji maalum wa uchaguzi Marekani,
Mdau Jacob.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 18 mpaka sasa

  1. Duh!! afadhali...angalau na sisi afrika mashariki tutoe raisi wa marekani!!

    ReplyDelete
  2. wewe jacob wewe, kwanini unakomalia uchaguzi wa nchi ya watu, yanakuhusu nini wewe? why dont you go and find the second job, ili angalau usaidie ndugu zako bongo? kila siku jacob, jacob, mpaka umejipatia cheo eti mhabarishaji maalumu wa uchaguzi toka Marekani. Leave the TV alone and go find a job. sisi tumekuja huku kutafuta, sasa kama wewe una muda wa kushinda saa zote kwenye TV kufuatilia mambo yasiyo kuhusu, ni aibu sana kwako.

    ReplyDelete
  3. Wacha uxushi kwenye kitongoji cha kwanz aalishinda kwa kupata kura 7 kati ya kura 16 ikiwa sawa na asilimia 43.Wacha kuongeza chumvi.Obama akishinda februari kwenye primaries kubwa ndio atakuwa na chance.Sio hizo primaries ambazo hata Bill Clintoa alishindwa na akaja kushinda baadaye ndio maana akaitwa the come back kid.Mambo bado sana kuanza kukata mbeleko.

    ReplyDelete
  4. Rais wa marekani awe mweupe awe mweusi hakusaidii chochote. Wee panga mikakati yako na fuatilia kampeni zako kwa gharama zako na za jamaa zako. Ushabiki wa siasa ni sawa na mpira. Kuwepo Tanzania hakukufanyi lazima uwe mshabiki wa Taifa Stars. Unweza kushabikia timu ya Brazil au kweye baketball unaweza kushabikia Celtics au San Antonio Spurs. Hivyohivyo kwenye siasa unaweza ukawa mshabiki wa siasa za ulaya au marekani au Japan. Sio lazima kushaikia siasa za nyumbani hayo ni mapenzi ya mtu. Kama unaburudika kushabikia mchezo wa siasa za kina Obama na Clinton endelea. Kama unaburudika na siasa za kina Kikwete na kina Lipumba endelea. Kikulacho ki nguoni mwako. Mtaka cha uvunguni sharti ainame. Asiyesikia la mkuu huvunjika guu.

    ReplyDelete
  5. Du!!!!
    Yaani huyo mshikaji naoana anajitahidi kutoa habari kwa moyo kweli.
    Utasema ni Mmarekani bwana.
    hahahahaaaaaaaaaaa
    Kwanza utambue tu kuwa watu wote wanaoweza kuaccess hii blog ina maana wa internet connection na wanaweza kutafuta habari zozote watakazo popote pale wakakapo.
    Sasa wewe unatoa hivyo vihabari vya ajabu, na isitoshe vimejaa uongo kweli.
    Unafikiri nani hajui bwana weweeeeeee

    ReplyDelete
  6. Mdau Jacob leo Boksi halibebeki? Acha uzushi with all respect to Barak Obama and as mush as most of us want him to win, kushinda kwa 80% kama unavyoota sio realistic

    ReplyDelete
  7. "mhabarishaji maalumu toka marekani", vipi mbona hujibu mashambulizi? au saa za kubeba mabox zimefika nini? au ukweli unauma. mimi kama mdau kop hapo juu alivyosema, nakushauri utafute kazi ya pili, kama kubeba mabox ni ngumu basi tafuta angalau ya kuosha kinyesi kama baadhi ya wenzio mlio marekani wanayofanya (sio wote). angalau usomeshe ndugu zako.

    ReplyDelete
  8. JACOB ENDELEZA LIBENEKE, HAO WANAOKUAMBIA UKATAFUTE KAZI YA PILI WAO WANAPATA WAPI MUDA WA KUSOMA TAARIFA ZAKO MUDA WOTE NA KURESPOND?

    ReplyDelete
  9. Wabongo bwana kwa kukatishana tamaa bwana, mtabaki kuwa masikini wa akili, kiroho na kipesa kutokana na tabia zenu za kijinga jinga. Unajuaje kama anafanya kazi na pia ana uwezo wa kuangalia tv huku akifanya kazi.

    Tupunguze kuwa na negative minds ktk jamii zetu na tutakuja kuendelea, mawazo yenu kama haya ipi siku yatakuja kuwafikisha pabaya. Hii ni aibu.

    Mbadilike na Mbarikiwe.

    ReplyDelete
  10. jacob eeh achana na hawa watu wenye majungu inaonekana walikosa visa za kwenda marekani ndio maana maneno mengi utafikiri wao tu ndio peke yao wanataka habari alaa..wewe bwana endelea kutupa habari kama michuzi alikuwa anahitaji wahariri basi angewaajili wao..waambie huna muda wa kujibu wenye majungu we endelea kutuhabarisha...

    ReplyDelete
  11. Obama akishinda kwenye primaries 5 Februari ndio atakuwa kwenye nafasi nzuri ya kuwa mwakilishi wa Democrats kwa sababu mbili kubwa.Kwanza majimbo hayo ni makubwa na yana wapiga kura wengi na pili wanachama pekee kutoka kwenye chama chake ndio wataopiga kura tofauti na sasa kwani sasa indepedents wengi wamepiga kura na wengi ndio wamemchagua Obama.Mtihani wake mkubwa ni kuona kama atakubalika na wanachama wa Democrats kwenye majimbo makubwa yenye wanachama wengi.

    ReplyDelete
  12. Ee bana michu eeh!
    Samahani kwa ukimya nilikuwa nimeenda kumtumikia mzungu kidogo, ndo nimerejea.
    Wacha waosha vinywa waendelee kubwabwaja, lakini dogo anaendelea kuwachanganya watu vichwa huko New Hampshire.
    Bill Clinton ameshaanza malalamiko kumtetea mkewe na kujifitinisha na vyombo vya habari, ni hatari!!!
    Mimi ntazidi kuumwaga hadharani mpunga wa bw' mdogo obama bila kujali wazushi. Udumu mtandao wetu!!!!
    Mhabarishaji wa uchaguzi Marekani, Jacob.

    ReplyDelete
  13. Naona kuna jamaa wengi wanawashambulia watoaji maoni ndani ya blog yako.Lakini naomba kuwaelimisha kwamba kila mtu ana uhuru wa kusema analolitaka ili mradi hamtukani mtu au kukashifu kundi lolote au mtu yoyote.Wengi nadhani hawafahamu katika ya Debate na Maoni.Kwenye debate unaweza kupinga hoja yoyote lakini mtu akitoa dukuduku lake hivyo ndio yeye anavyofikiri na sio kumpingana nae.Toa maoni yako then ondoka na sio kukashifu maoni ya mtu, haipendezi na unakatisha tamaa watu wengine kutoa maoni yao.kumbukeni ni maoni ya watu ndio yakikusanywa watu wanaweza kufanyia utafiti na kuja na msuluhisho kamili, wacha maoni yaflow ndipo utakapoweza kujua mawazo tofauti ya watu wote.Ni kwa ajili ya maoni watu wengi wanaweza kujifunza mambo mbalimbali.kumbukeni pia kila mtu anakitu anachokipenda na uwezi kumlazimisha mtu apende kuangalia kitu ambacho hakipendi.watu wengine wapo interested kusikiliza uchaguzi wa US wengine wanapenda nani hii..............nk

    ReplyDelete
  14. Michuzi naona kabla ya post uzushi wa watu kama jacob nakuomba hata wewe uwa unasoma kwenye mtandao kwani kama ni jimbo la NH Obama kashindwa na hilary clinton aibuka kidedea kwa hiyo huyu jacob aache uzushi kabisa kwani hata sisi tuna mitandao na tuko maraekani

    ReplyDelete
  15. wewe mdau unayejiita jacob niliposema sehemu ina watu wasiozidi 20 nilikuwa najua ninachoongea na matokea ndiyo hayo Hilary kashinda NH na hivo breaking news zenu za Obama kushinda ziko wapi?
    Hapa siyo swala tu la kushabikia rangi hapa ni mahali pa kuleta habari zilizo sahihi ili tupashane na tuelemishana siyo kushabikia tu after all bongo tuna matatizo yetu.
    Najua utatamani kubadili kauli yako. Tunamuombea Obama ashinde lakini si kutuletea habari ambazo si sahihi na za kishabiki

    ReplyDelete
  16. Mbona hutupi matokeo ya New Hampshire??Au bado hayajatoka???Tunasubiri Breaking News!!!!!!!

    ReplyDelete
  17. New hamshire yameshatoka Baraka Obama kapigwa chini na mama Hilary,mimi nimeishi marakani muda kibao kabla ya kurudi maulaya,napenda kuwafahamisha hii kwa sasa,,,kwamba piga ua marekani bado kuwa na rais mweusi....kumbukeni hii,kwa nyinyi mnaona tu marekani kwenye tv hamnyuhi unyama unaofanyika katika ubaguzi ndani ya nchi.

    ReplyDelete
  18. Wewe unayesema aache mambo hayamhusu wewe ndio hayakuhusu kwa hiyo tuachie wenyewe... Wezako tushahamia na kura tunapiga kwa hiyo haya yanatuhusu sana tu....home sweet home lakini maisha yanaendelea kwa bush ...sasa kama uchaguzi haukuhusu wengine tuko macho sana...

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...