
Afrika tuna sifa ya kuongozwa na marais wazee sana. Na idadi ya viongozi wale waliokaa madarakani kwa zaidi ya miaka 10 ni kubwa kidogo. Kama nchi nyingi zilivyoanza kuwa na term limits, kuna haja ya kuweka age limit pia kwa viongozi. Kwa kweli Mzee wa Miaka zaidi ya 75 anahitaji kuwa mshauri tu kwa vile katika umri huo hawezi kupambana na purukushani ziendazo na majukumu yake ipasavyo. Huishia kuwa wanatuma wasaidizi wawafanyie mambo na hivyo kuruhusu makosa mengi ya kiutendaji.
Angalia jedwali lifuatalo lililoandaliwa linaloonyesha jina la kiongozi, umri wake, nchi anayoongoza na muda wake madarakani:
Kundi A: Wenye umri wa zaidi ya miaka 70
1.Robert Mugabe - 83 - Zimbabwe (1980-Todate = 27 years)
2.Abdoulaye Wade - 81 -Senegal (2000-Todate = 8 years)
3.Hosni Mubarak - 79 - Egypt (1981 - Todate = 26 years)
4.Anerood Jugnauth - 77 - Mauritius (2003 - Todate =4 years)
5.Mwai Kibaki - 76 - Kenya (2002-Todate = 5 years)
6.Paul Biya - 74 - Cameroon (1982-Todate = 25 years)
7.Bingu wa Mutharika - 73 - Malawi (2004- Todate = 3 years)
8.Lansana Conté - 73 Guinea (1984-Todate = 23 years)
9.Abdullahi Yusuf Ahmed - 73 - Somali (2004 - Todate = 3 years)
10.Hifikepunye Pohamba - 72 - Namibia (2005- Todate = 2 years)
11.Omar Bongo - 72 - Gabon (1967 - Todate = 40 years)
12.Zine El Abidine Ben Ali - 71 Tunisia ( 1987-Todate = 20 years)
13.Abdelaziz Bouteflika - 70 -Algeria (1999- Todate = 9 years) .
Kundi B: Zaidi ya miaka 60
1.John Kufuor - 69 - Ghana (2001-Todate =7 years)
2.Ellen Johnson-Sirleaf - 69 Liberia (2006-Todate = 2 years)
3.Sidi Ould Cheikh Abdallahi - 69 -Mauritania (2007 - Todate = 1 year)
4.Tandja Mamadou - 69 - Niger (1999-Todate = 7 years)
5.João Bernardo Vieira - 68 -Guinea-Bissau (2005 -Todate = 2 Years)
6.José Eduardo dos Santos- 66 - Angola (1979-Todate =28 years)
7.Thabo Mbeki - 65 -South Africa (1999-Todate =8 years)
8.Teodoro Obiang Nguema Mbasogo - 65 -Equatorial Guinea (1979 - Todate = 29 Years) 9.Muammar al-Gaddafi - 65 - Libya (1969 - Todate = 39 years)
10Armando Guebuza - 64 -Mozambique (2005-Todate = 2 years)
11.Denis Sassou Nguesso - 64 - Congo Brazaville (1997-Todate =10 years)
12.Festus Mogae - 68 - Botswana (1998- Todate = 9 years)
13.Yoweri Museveni - 63 -Uganda (1986 - Todate =21 years)
14.Omar al-Bashir - 63 - Sudan (1989- Todate = 19 Years)
15.Laurent Gbagbo - 62 -Ivory Coast ( 2000 - Todate = 7 Years)
16.François Bozizé - 61 - Central African Republic (2003 - Todate = 4 years)
Kundi C: Zaidi ya miaka 50
1.Amadou Toumani Touré - 59 - Mali (2002-Todate = 5 Years)
2.Levy Mwanawasa - 59 - Zambia (2002 - Todate = 5 years)
3.Jakaya Kikwete - 57 - Tanzania (2005 - Todate = 2 years)
4.Blaise Compaoré - 56 - Burkina Faso (1987- Todate =20 years)
5.Idriss Déby - 55 - Chad (1990- Todate =17 years)
6.Boni Yayi - 55 - Benin (2006 - Todate = 1 year)
7.Ernest Bai Koroma - 54 - Sierra Leone (2007 - Todate = less than 1 year)
8.Meles Zenawi - 52 - Ethiopia (1995 - Todate = 12 years)
9.Marc Ravalomanana - 58 - Madagascar (2002 - Todate = 5 years)
10.Paul Kagame - 50 - Rwanda (2000- Todate = 8 years)
11.Umaru Yar'Adua - 51 - Nigeria (2007 - Todate = less than 1 year)
Kundi D: Chini ya miaka 50
1.Pierre Nkurunziza - 44 -Burundi (2005 - Todate = 2 years)
2.King Mohammed VI - 44 - Morocco (1999- Todate =8 years)
3.King Letsie III - 44 - Lesotho (1990 - Todate = 17 Years)
4.Yahya Jammeh - 42 - Gambia (1994 - Todate = 13 years)
5.Faure Gnassingbé - 41 - Togo (2005 - Todate = 2 years)
Kundi la wenye chini ya Miaka 40
1. King Mswati III- 39 - Swaziland (1986 - Todate =21 years)
2. Joseph Kabila - 36 - Congo (2001 - Todate = 6 Years)
Mdau
Tatazo tukiwachagua vijana watakua kama RAIS wetu JK , kila kukicha safari za matanuzi leo UK kesho USA office zao uziona kama MOTONI
ReplyDeleteJamani huyo alievaa suti nyeupe ni Arap Moi wa Kenya au macho yangu.Sioni kifimbo lakini je,ndiye?
ReplyDeletemi naona bora wawe wazee to beacuse they it is known that wisdom comes with age..hata hivyo mayanki especially from Africa hawajatulia kabisa (hata msinune na kuguna ni kweli..matapeli kabisa!)..mara utasikia president yuko na model huyu, mara yuko na miss..so ni bora kama wakiwa watu wazima, wameshasoma, wameoa na wametulia..they become good role models in society
ReplyDeleteWe namna gani...yaani huoni kuwa huyo ni MOI? Yaani umeshikilia mkia wa mbwa, halafu unauliza ananyea wapi?
ReplyDeleteHapa mimi nakubaliana na ule usemi wa wengi wape. Hao vijana pia tunaweza kuangalia mfano wa hao rais vijana. Mfalme Mswati ana wake kumi kidogo, nakumbuka kuna wakati aliamua kuwanunulia kila mmoja gari mpya aina ya BMW, jambo ambalo lilileta utata kuhusu matumizi yake ya fedha za wananchi.
ReplyDeleteSio marais tu waafrika wazee, hata Papa Benedict XVI wa catholic church aliyechukua nafasi baada ya Papa John Paul nae aliteuliwa akiwa zaidi ya miaka ya sabini.
Sasa hapa inabidi tuwe makini hasa kwa kuangalia mifano ya viongozi vingwangwa na hao vijana yupi aongoze yupi awe msaidizi
Marubani wa ndege, majemadari wa vita, majaji wakuu, maprofesa wa fani zote za elimu hata madaktari na viongozi wa dini huwa ni wazee!!!
ReplyDeleteWengi wanaopata Nobel Peace Prize huwa ni wazee!!!!!!
Ma-CEO na Presidents wa makampuni ya biashara huwa nao ni wazee!!!
Kwa nini viongozi wa siasa wa Afrika kukaa madarakani kwa muda mrefu hakuambatani na kuona/kujifunza mengi --- kusiwasaidie kuongeza ujuzi wa uongozi?
Marais vijana wa Africa nao wame-"prove" kuwa "mere let down": Blaise Compaoré kamwua mwenzake Thomas Sankara; ya Samuel Doe yaliishia wapi? Na huyo Yahya Jammeh wa the Gambia kazi kujigamba kuwa kagundua dawa ya ukimwi!
Je vijeba vya USA Rais Mstaafu Marehemu Ronald Reagan, mgombea wa McCain wa Republican caucus 2008, Fidel Castro, Waziri Mkuu msatafu wa India Moraj Desai, Waziri Mkuu Marehemu Golda Meyer au aliyekuwa waziri mkuu Italy Aldo Moro wote umri wao ulikuwa zaidi ya 70. Ni mifano michache ya mingi nje ya Afrika.
ReplyDeleteWaafrika tuangalie na kujivunia utendaji wa viongozi wetu, na siyo sura zao au umri wao. Na kiafrika 'uzee ni dawa' hivyo tusiwabeze viongozi wanaoweza kuboresha maisha ya wananchi wao na uchumi wa nchi zao hata kama ni vijeba kama Nelson Mandela.
Mdau
Amanzimtoti
Kwa-Zulu Natal
Republic Of South Africa.
anon. jan 8, 7:08 taratibu jamani mbona umetumia mithali kali sana kiasi siku nyengine atakua na hofu kutafuta msaada kwako hapo ungetumia lugha tauria (lugha murua) hapo ungemwambia mwenye macho haambiwi tazama ingetosha au ungemwambia unauliza jibu? au ungem-bainishia tu kua ndiye yeye mzee moi wa kenya,huwezi kujua labda anatatizo la kuona vema au kupambanua au hamjui vizuri mzee Moi utakua hujamtendea haki kwa kutompasha habari sahihi ili kuondoa wasiwasi wake.
ReplyDeleteMimi kwa mtazamo wangu uongozi siangalii ni mzee au kijana cha muhimu ni hekima zake tuu ziwe nzuri. kuna vijana wazuri na wanahekima kubwa mfano wa king solomon, ila kwa vile walokula chumvi, na wameona mengi. wengi huwa kidogo wamekinai hiyo huwa na utulivu kuliko vijana, ndipo watu wengi huamini kua wazee ni bora kua maraisi au viongozi wa juu.
I don't care what people say we are blessed with nice people in Tanzania despite corruptions we never had to cry out loud.We have few problems with corruption being the first one but I can't think of any president we hate in Tanzania so we are still in good shape.I WILL ALWAYS LOVE MY MOTHER LAND.Look on that picture our president shine like a simbol of peace.Hureeee!!!!!
ReplyDeleteAnon wa 9.01am asante kwa ukarimu wako,watu wengine wanaamka vibaya in the case ya huyu anon wa 7.08pm inaonyesha kashinda vibaya na vile comment yake ni time ya usiku namsamehe.
ReplyDeleteSababu ya kuuliza nimeishi Kenya for few years but it's about 17 years ago when I left that country and have been abroad ever since,I have not seen the poor man,not even on telly,I know of Kibaki taking over from him.So would you blame me for not being sure if that was Moi or not.The time I lived in Kenya he always had this stick like a horses' tail where is it now?was it his sign of power now that the power has gone the stick is gone with it?
Moi anacho kirungu mkononi zoom this picha utaona...Anacho kinang'aa sana
ReplyDeletemimi napendelea middle age presidents...ambao wameshaenjoy life lakini hado wanaubongo wao kufanya critical thninks and decisions ...too young ...NOOOOOO...kikwete anatushinda kwa matanuzi tooo old nadhani nao watakua wanarun nchi chini ya watu wengine... wao wapo tu pale kwa jina...
So btn 65 to 77 it is my kind of presidents..
Karibu tena anon jan 9, 10:37, nimefurahi vile umemsamehe anon wa 7:08, ila mi sidhani kama kaamka vibaya, nahisi ni mtundu sana pia alitaka ku execise mithali yake hiyo ila alikua ya juu sana kwa hapo alipoitumia hakutakiwa, hiyo angeitumia mahali penye ugomvi ndiyo ingekua safi maana adui hapo ingembidi ajipange upya ila hapo hapakua na vita yoyote ni kupashana habari tu, Ila alipotusikizisha nahisi kuna wengi nikiwa mmoja wao macho na masikio yaliwasha sana.
ReplyDelete