ukiangalia kwa makini utakuta hapa zenji watu wengi hasa watoto hawapendi kuvaa viatu. hii imekaaje wadau...

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 18 mpaka sasa

  1. RAHA YA MCHANGA WA PWANI UUKANYAGE PEKUPEKU.

    ReplyDelete
  2. Michuzi Ulikua na jibu.Na swali lilikua Kwanini watoto hawana viatu? jibu umasikini sio swala la kutopenda

    ReplyDelete
  3. mi nafikiri ni mazingira ya pwani na hali ya hewa unakuta watu automaticaly tu hasa watoto wanakua naturally atrtracted peku peku inakua more comfortable,lakini kwa sababu nchi yetu maskini swala zima miongoni mwa watanzania ni umaskini yawezekana sikani,ila huku uluya wakati wa summer wazungu wanabeba viatu mkononi na wapekua kama kawa katika mitaa ya kati ya jiji ambao inakua inasafishwa kwa hali na mali,zenji mchanga wa kumwaga mazingira yanaruhu.

    ReplyDelete
  4. Big up anon,jan 16,9:53
    we michuzi unataka kunambia ulipokua unaenda kwa bibi yako umatumbini ulikua unatetha thana sijui zilikua ndala zile au matairi yale, tena tumbo wazi, na ukiamka asubuhi unaonyeshwa muembe wako ule nenda kapate breakfast, lunch unaambiwa utapata hukohuko porini ukienda kwenye kuni so dinner ndio unaipatia home sima na mlenda.Leo umekua unazunguka dunia unaanza kashfa ee, tutakuwekea wanted kama masanja usiingie huko kwenda kunutha marashi ya karafuu. Hiyo inaitwa alokupa we kiti baba ndo alompa kumbi mwengine. abaa weye kunkwenda huko na kufukunyua khabari za wenetu, haya changisha harambe kwa kunadi ile t-shirt yako kauka nkuvae tupate funds za kuwanunulia hao watoto raba za shule walau alooo weye weye.

    IMEKAAJE? jibu analo John walker IMEKAA VIBAYA TENA HAIJATULIA.

    ReplyDelete
  5. michuzi unataka kuleta issue wewe hapa naona,lakini jibu najua hao watoto wengi wao hawana viatu na hakuna hali ya hewa wala nini ni njaa tuu

    ReplyDelete
  6. Si watoto wa Zenj tu watoto wote hawapendi kuvaa viatu. Ni si kama hao watoto hawana viatu la hasha, maana skuli lazima waende na viatu ila tabia za watoto, viatu mpaka umshikie fimbo na tena wewe mzazi umuone pale anapotoka. Nenda wanakocheza mpira watoto utakuta raba zimewekwa kando ya goli wanacheza peku peku. Hasa watoto wa kiume, ila ni nadra sana kukuta watoto wa kike wanatembea peku peku na ukimkuta mtoto wa kike anatembea peku peku basi ujue hali ya nyumbani kwao ni ngumu kweli kweli.

    Michuzi hukuwatendea haki hao watoto ungewauliza kwa nini hawakuvaa viatu wangekupa jibu maridhawa.

    Mie wakati mwingine nikirudi kutoka kazini nawakuta watoto wangu wanacheza bila viatu, pamoja na kusema kote sijui kuna minyoo na kuwatisha wapi. Wakikuona yuule unakuja ndio watakimbia mbio kwenda kuvaa viatu na ukikagua miguu unakuta michafu vumbi tele lakini iko ndani ya viatu basi mara moja najua hapa mpira ulikuwa unachezwa peku peku, wamevaa viatu baada ya kuniona.

    Kweli wakati mwingine yawezekena ni suala la umaskini lakini asilimia kubwa ni utashi tu wa watoto kucheza bila viatu na wala msilaumu wazazi maana hao wanavyoponyoka hata huwezi kujua ametokea mlango gani. Na kwa umri huo saa ya kuoga nayo ni vita nyingine huwa hawapendi kabisa kuoga!! Sijui kwa nini lakini!!!

    Mzazi!

    ReplyDelete
  7. Wazungu huwa wanapekua kwa upendo ukizingatia kwamba wana uwezo wa kununua viatu na pekua yao siyo through out the year, year after year ni wakati wa summer tu na isitoshe siyo kwamba watapekua summer nzima.

    Hao watoto ni sababu ya umasikini. Ukizingatia jua la kwentu, majira ya saa nane tisa jua uwa kali kiasi kwamba linaunguza miguu na ningedhani kwamba kila mtu agependa atumie hata kandambili.

    Hivyo viatu ni vya muhimu kwa kila binadamu kwa protection hasa kwa magonjwa. Ndiyo maana unakuta majority ya waafrika wana miguu mikubwa na ina magamba, sababu ni kwamba tangu wamezaliwa ni pekua na kama wana viatu watavivaa wakati wanakwenda kanisani, hospitali au kwanye tafrija maalumu.

    Huyo anayesema kuwa ni sababu ya hali ya hewa hawezi kunihakikishia kwamba ukiwanunulia viatu hao watoto juu watavikataa. Kama ni tatizo la joto, at list wangevaa sandals.

    ReplyDelete
  8. lakini karibu wataingia katika utu uzima watavya malapa, (open shoes) kama ilivyo jadi.

    ReplyDelete
  9. Peku peku ndio yanoga babu,kwani hujui...?lol

    ReplyDelete
  10. Mzazi umeongea vema yote uliyoongea sawa, hata wa kwangu ni hivyo. ila kwanini hujui wako hivyo naomba nikutoe wasiwasi. swali lako nimeliweka katika mafungu matatu
    1.maumbile. mtoto anakua anavijitabia ambavyo kuvibadili inahitajika juhudi ya ziada mf. uvivu, uchafu, ujeuri na ubishi n.k

    2.uelewa mtoto akili yake inakua bado haijapambanua mambo mengi mf. umaridadi, ushindani au umuhimu, hivyo anaona sawa tu labda kidogo siku za sikukuu waima hiyo kila mtoto hahimizwi kuoga wala kuvaa viatu ili akatambie tu huo umaridadi wake kwa wenzake. kadri anavyokua kidogodogo anaanza kuelewa ala! kumbe kuna ushindani wa kupendeza hapa? kumbe kuna ushindani wa darasani hapaee kunaushindani wa kufanya wema nk.baadae anaelewa kumbe ni muhimu nifanye hivi ili niwe hivi hapa!

    3.mazingira yanayomzunguka kama ni ya hali ya juu au ya duni yanachangia kumuweka mtoto katika hali yoyote .mwisho kumbuka wewe ulipokua mtoto likua vipi ulifanya mavituko yepi

    ReplyDelete
  11. Mie siwaelewi!

    Kuna wa2 sijui ndio frustration za maisha ya huku ughaibuni(frustration hailetwi na hali duni tu ya maisha) au ni ulimbukeni wa kufika huku ughaibuni au ndo wanataka watu wajuwe kwamba wapo ulaya au amerika basi hata sijui ni nini? Unakuta mtu yaani anajifanya kuidharau nchi yake na kuponda maisha ya nyumbani utafikiri yeye alizaliwa huku ughaibuni, au labda amehamisha familia yake yote iko huku na harudi tena!! Mtu hawezi ku comment mpaka aanze kutuambia."...huku ulaya..." au ebo acha upuuzi usitake kutulinganishia maisha ya ulaya na kwetu..wao wanamaisha yao na sisi yetu si kila afanyacho yeye na sisi tufanye au tukubali kwamba vyakwao vizuri. Usiwafanye kuwa ndio refence ya ustarabu na style ya maisha kwetu.Kutokuvaa ndara au viatu inategemea na tabia au hali ya kipato cha mzazi kwa hapa kwetu, kuna ambao wanauwezo viatu wanavyo na bado watoto hawataki kuvaa viatu seuse kuoga, na kuna ambao hawana viatu sababu ya uwezo lakini hata vingekuwepo pia wasingevaa vile vile kuna ambao wanatamani wangekuwa navyo viatu wavae lakini hawana uwezo (hawa utawakuta wengi wao ni kule vijijini). Hii picha inaonesha imepigwa sehemu ya mjini zanzibar, picha yenyewe na hali ya watoto wenyewe inakwambia kwamba watoto hawa hawataki kuvaa viatu lakini kwao viko.Logic;ukiangalia flana na suruali walizovaa, niza bei si mnaona?au unaweza kumnumnulia mwanao flana ya 7000halafu usimnunulie ndara ya 500?! Angalia na mtaa wanaoishi ni nyumba za tofali, si aghalabu mzazi mwenye mjengo kama huo akashindwa kumnunulia mwanawe ndara ya 500!Mambo ya nyumba za kupanga zanzibar ni chache tena majumba ya serkali michezani na kikwajuni (Hizo sio zakupanga).

    Hivyo ombi langu mdau silazima kila post u comment hata kama jambo hulijui,utatuzidisha hasira wakati tumekuja kwenye blog kupunguza stress, pili hatuna haja yakujuwa unaishi wapi au uanfanya kazi gani tunachohitaji ni upeo wako wakile kinachozungumzwa ili tupate nasie faida (elimu), mwisho kabisa lakini muhimu zaidi USIACHE M'BACHAO KWA MSALA UPITAO naRejea shairi la diwani ya mloka"USIONE UKADHANI" anasema usione jogoo kuwika ukadhani anaimba wala usione ndege kuruka ukadhani anaringa..." Bablii

    ReplyDelete
  12. VIATU WANAVYO, LAKINI WAZAZI WAMEVIFUNGIA KWA AJILI YA SIKU KUU...

    ReplyDelete
  13. joto kali zenj ndio maana yake wanaogopa watoto kufanya fangasi za miguu au miguu kutoa harufu mbaya na ikiwa wao wenyewe ndio kwanzaa wachanga..... wanajikinga na fangasi hao

    ReplyDelete
  14. Swala la umaskini mimi nalipinga kabisa. Hapa kijijini kwetu ni sharti kila mtoto avae viatu akienda shule na wote wanavyo. Lakini wakifika shule huvivua (hasa watoto wa kiume). Ukienda kanisani jumapili watoto wote wamevaa viatu lakini wakitoka kanisani kuelekea makwao wanavua na kuanza kucheza peku. Mimi nafikiri kuna raha sana kuipa miguu fresh air! Sisi wakubwa pia tunatamani hilo hila tunaona aibu tu. Wenzetu wazungu (nilipokuwa huko) mpaka supermarkets wanaingia pekua wakati wa summer. Mbona na sisi wakubwa tukitoka kazini jambo la kwanza ni kuvua viatu? Vinakera! Hata maofisini ukipata nafasi unavivua na kuacha miguu yako huru. Kweli hao watoto wana enjoy!

    ReplyDelete
  15. hali hii sio watoto wa zenji peke yake bali ni tanzania nzima huwa hawavaagi viatu na hii inasaidia kupata vitamin c

    ReplyDelete
  16. wewe kaka michuzi vipi? utaulizaje watoto hawana viatu.wewe si unao uwezo uwanunulie, sio unakashfu watoto wa kizanzibar,kwani tanzania nzima umasikini umejaa,ukienda hapo dar ndio mji mkuu utawaona watoto kibao hawana viatu,acha hiyo tabia ya kuuliza ujinga kama huu ,mimi sikupenda wewe msomi mzima uulize swala kama hili.kwani wewe ulitokea wapi?si ulitokea huko huko,hakuna mkamilifu ila mungu,hawakupenda kuvaa viatu ,au wamependa hilo sio swala la kuuliza hao ni watoto hawana kosa wewe vipi kaka na umewatoa watoto wa znz tu nenda dar kawatoe acha zarau wewe umeumbwa tu na aliekuumba ndie aliekupa na hashindwi kukiondoa,acha zarau kusema znz wewe tanzania nzima masikini tu na hawa watanganyika ndio wanaowasababishia waznz kuwa masikin .kila kitu wanajichukulia kwao tu znz hamna maendeleo kila kitu tz acheni vicheko tanzania sote masikini.acha kuulizia watoto kama watoto si uwachukue wako kwanza na uwaoneshe humu halafu uulize,acha hiyo haifai vitu kama hivi wewe umeumbwa bwana iko siku utakwenda tu. na nione usitowe coment yangu.

    ReplyDelete
  17. Ahsante anon wa jan 17, 2:16
    umeongea point ya maaana,hao watoto sio kama hawana viatu hiyo ni kawaida ya watoto wengi waki afrika kutembea peku peku sio ajabu tu kwa watoto wa kiznz, waznz ni watu waliostaarabika kwa miaka na hilo linajulikana kwahiyo wambili ni wambili tu na wa mbili havai moja.

    ReplyDelete
  18. sera za nyerere na ccm yake hiyo. wacha watoto, watu wazima siku hizi wanavaa mitumba mpaka chupi !!!, miaka ya sitini watu walikuwa na uwezo wa kuwanunulia watoto nguo mpya na viatu, mnakumbuka enzi za viatu vya "prefect" vya bata vilikuwa raisi kila mtoto wa shule alikuwa navyo, viatu vya kilipa ilikuwa kawaida, mtakatifu wetu akaanzisha viatu vya bora, basi wacha wamatumbi waanze kuiba, doddoma walichoma ghala ya bora mtaa wa mwangaza, kila mtu anajua pesa zimeibiwa sasa watasingizia moto.kinjikitile ngwale alianza vita vya maji-maji dhidi ya wakoloni kwa sababu ya kunyanyaswa, kupuuzwa,umaskini n.k. sijui bongo tutaanza ngarambe lini ? tumeleweshwa na huyu rais mastaili (jk) mikogo na pose hizo utafikiri anataka awe movie star.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...