wadau wakikatiza posta mpya dar, upande wa maboksi. je kifanyike nini ili tuondokane na njia hii ya kizamani ya kutuma na kupokea barua kwa njia ya p.o.box?

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. mpange miji ili kuwe anwani kwenye kila nyumba. wakati mwingine michuzi huwa unaweka vitu ambavyo mtu mwenye akili timamu asingeuliza. Wewe unadhani manzese watapataje barua zao? Kigilagila je?

    ReplyDelete
  2. Michu

    Bado "snail mail" yaani post office boxes zina mchango na umuhimu wake ndani ya uwanja wote wa mawasiliano. Yap!! email imeshika hatamu na hakika hakuna atakayepinga kwamba ndiyo njia rahisi na ya haraka ya kuwasiliana. Lakini bado haya masanduku ya barua na kuwailiana kupitia huko bado kuna nafasi kubwa tuu.. ni kama wewe hapa ukiangalia kati ya blogi na gazeti!!! (dRU)

    ReplyDelete
  3. Michuzi hii itakuwa sekand hendi in couple of years ahead maana siku hizi application ya kazi mtu unatuma kwenye email sidhani kama hivi visanduku vinamatumizi sana, mie nashauri vivunjwe kijengwe kitu cha maana hapo.

    ReplyDelete
  4. MJI WA DAR NI MJI AMBAO SEHEMU KUBWA HAZIKO KIMPANGILIO NA MAANA HAKUNA MITAA YAANI NI MJI OVYO KULIKO YOTE KATIKA BARA LETU,SIJUI HIZO WIZARA ZINAZO HUSIKA ZINAFANYA NINI?HUKU NILIPO NALETEWA BARUA MLANGONI WALA SIJUI POSTA INA FANANA VIPI SABABU KUNA MITAA,HUKO MANZESE BARUA ZITAFIKA VIPI?

    ReplyDelete
  5. Ni Suala la maendeleo. Kama hapa kwetu kuna watu, taasisi, ofisi nk ambao hawatumii sana P.O.Box, kwa sababu wanatumia mtandao, ems, DHL nk. Lakini kupata nyaraka 'Original' ni lazima kutumia Box. Hii hata Ulaya ipo, labda tofauti ni kwamba mabox yapo katika nyumba zao au ofisi zao, jambo ambalo linahitaji mipango miji na miundombinu yakueleweka.

    ReplyDelete
  6. Kaka Michuzi,hayo hayatawezekana kabisa,jiji nchi yenyewe majumba sasa hivi hayana hata mpangilio,serikali inagawa viwanja ovyo ovyo,zamani mikoa yote kulikua na mitaa na namba za nyumba,sasahihivi ni aibu,nyumba nzuri lakini hazipo mtaani,post man atasambazaje barua ktk majumba ambayo hata namba hayana?

    ReplyDelete
  7. Dawa ni moja tu, mpe kila mtu computer na simu, utaona kama kuna mtu anaenda hapo, labda tukipata vifurushi toka kwa wabeba mabox wakati wa x-mas na new yr!!!

    ReplyDelete
  8. Njia ya mabox haiweziisha.
    Mfano; Tekinolojia ya kusafirisha Imbute (Muhongo Mvundifu)katika kipeto toka Kigera Etuma au kumuvuzisha kafurushi ka Senene toka soko la Katerero hadi mwisho wa Lami Dar ELEKTILONIKALI haijavumbuliwa hata kwa Mzee Pori.

    Kitu ambacho ungesema ni kuboresha huduma ya hayo mabox yaweze kuwa karibu au majumbani na maofisini mwa watu.

    Hilo litawezekana endapo tu mazingira yafuatayo yatakuwepo.

    1. Nyumba ziwe zimekaa kimpangilio ziweze kuwa na anuani zinayojulikana yaani mtaa na namba ya nyumba.

    2. Hizo Nyumba / Ofisi ziweze kufikiwa kwa urahisi. Hapa tunaongelea uhimarishaji wa miundo mbinu yetu.

    3. Watumishi wa posta,wakala wao na hata watumshi wa muda (vibarua) wake wawe waaminifu vya kutosha si tu kufikisha hizo Senene bali kwa idadi kamilifu na katika hali yake. Yaani mpokeaji wa imbute aipate bila mmegeko fulani ndani ya wakati muafaka. Maana vinginevyo sasa itakuwa inabidi kukodi majeshi ya KUSAFISHA NA KUSOGEZA (CLEARING & FORWARDING) ili mlaji akabidhiwe kipeto chake cha Imbute kabla haijabadilika kuwa Udaga.

    TANBIHI:
    SUALA LA UAMINIFU NI CHANGAMOTO KUBWA KWETU SOTE WATUMISHI WA UMMA NA WANGINE WOTE SI TU KWA WATUMISHI WA POSTA.

    ReplyDelete
  9. Tanzania tunachekesha hasa ukiwa msafiri wa mataifa mbalimbali.

    Kuna sehemu kwenye zile kadi za immigration unapoenda nchi nyingine mpakani unatakiwa ujaze kitu kinaitwa YOUR ADDRESS sasa watanzania wengi pale hupenda kujaza P.O BOX NUMBER.Nilishawahi kutukanwa nchi moja wakasema hivi watanzania kwa nini Sehemu ya Address mnajaza P.O BOX ina maana watanzania wanaishi na kuamka kwenye POSTAL OFFICE BOX?

    Lakini ni kwa sababu nyumba za nyingi Tanzania hazina NUMBER, STREET NAME na NUMBERS ndiyo maana wengi huandika P.O BOX Wakiulizwa kuhusu Address zao.

    Anyway wacha posta waendelee hivyo hivyo hadi mitaa itakapopangwa vizuri kwa mpangilio,na nyumba zipewe namba na makazi yakae vizuri,miundo mbinu itengenezwe vizuri mijini na vijijini ndipo jamaa hawa waweza fanya vizuri zaidi kazi zao na ufanisi zaidi.

    Ufanisi wa Postal services hutegemea zaidi mipango mizuri ya miji na vijiji.

    koloboi@yahoo.com

    ReplyDelete
  10. Michuzi naomba uiweke hii.
    Acheni kujidanganya hii staili bado ipo sehemu nyingi tu duniani.Sema tofauti ni kuwa nchi nyingine kama Marekeni,UK,France,nk wana Street address #'s na P.o.box #'s.Na uzuri wa hizi P.o.box numbers ni cheap kuzi-operate kwa nchi maskini kama yetu.Ingawaje street address #'s zina-create ajira kwa wananchi ni expansive kuzi-run kwa nchi majalala kama yetu.
    Kinyume na kwetu ambapo hii system ni cheap ambapo Mtu mwenye hitaji la kuwa na P.o.box anagharamia mwenyewe Mara moja tu,kwa nchi kama Marekani,customer anagharamia mara mbili,nikimaanisha anakuwa analipia street address #'s(home or apartment) na P.o.box #'s.Kumbuka kwa nchi zilizoendelea(eg:-US) P.o.box numbers ni chaguo la Mteja anafungua sanduku la barua kama vile wateja wanavyofanya Tz.kwa hiyo huku majuu P.o.box ni expansive kuliko huko Tz.
    NB:Na kutokuwa na mitaa inayopitika kwa nchi yetu si kosa la Sirikali ni kosa la sisi sote tunaojenga kiholela bila mpangilio.Watu tunakatiana viwanja kijinga jinga,mtu akipata sehemu ya kuweka vyumba vitatu anajenga bila kujali kama gari linaweza kufika mlangoni kwake ama la.Kuna sehemu nyingi ambapo wananchi walisha-shauriwa na Sirikali wasijenge bila kupimwa lakini wakawa vichwa ngumu.Hivi sasa mmefika majuu mnataka kuleta kujuwa,nyooooo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...