kila kona porojo za leo ni kuhusu sakata la benki kuu. hapa ni kijiwe cha empress kwa fundi mussa

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. kaka michuzi huuu wanaofanya hapa unaitwa upashkuna, upuchupuchu na ushang'winda kichaka.Midume mibishi!!!cheki yule mmbea mmoja hata mguu kaweka juu ili aongeze hasali.

    ReplyDelete
  2. hapo waswahili hawakawii kukuambia hii news nilipata last week kutoka jamaa wa usalama wa taifa ila akanionya nisiseme

    ReplyDelete
  3. Kazi wanafanya saa ngapi hao? Maana naona wako kijiweni muda huu badala ya uwa kazini!

    ReplyDelete
  4. Kwa wale ambao umri mdogo na wasio ijua DSM. Empress ilianza kabla ya salamanda. Muulizeni Papa Msove. Mambo ya mishen Tauni miaka ya 70 na 80 yaliaanzia hapo. Wadau "Chenji Mani" mnaikumbuka. We Ano unauliza kazi wanafanya saa ngapi? Inaelekea mambo ya TAuni mgeni au uko ughaibuni.Huku huwahatuulizani.Ni sawa na kumuuliza mama mkwe anaondoka lini, wakati ndio kwanza kafika.Njoo Bongo upate somo.

    ReplyDelete
  5. Bongo nchi ya wasiokuwa na haraka,watu wako kijiweni wamerelax kweli kweli,hamna haraka kabisa.Hii hulka ya damu ya kibongo ya kuwa slow na kurelax kwa sana inachangia nchi kuwa nyuma kimaendeleo.Wabongo wengi mabingwa wa longo longo na porojoporojo.

    ReplyDelete
  6. HAPO JAMANI NI MCHANA, KIJIWE CHA MTU MMOJA AMBAE HAPO NI KAZINI KWAKE, KUNA WENGINE NANE SIJUI WANAPIGA STORY MWENZAO ''ANATENGENEZA'' PESA, KIMSINGI JAMAA MTENGENEZA PSA NAE NI KIASI KIDOGO SANA, SIJUI HII MAMBO ITAKUWAJE, BORA HAO WANGEUNDA SACCOS YAO WAKAENDA KUCHUKUA MABILIONI YA JK!!

    ReplyDelete
  7. Mission town bwana, mijitu mikubwa inatoka asubuhi, inaaga wake na watoto nakwenda kazini, wengi matapeli hapo, wala hakuna wa maana hata mmoja. Wangekuwa na point wangepitishia kwenye blog kama hii wengi wakaisoma sio, kupangusa viatu na ujinga

    ReplyDelete
  8. Msilete upumbavu wenu hapa wa kujifanya hamuijui hali halisi ya huku nyumbani. Hao watu hawana kazi na hili ni tatizo kubwa sana la kijamii. Kubeba kwenu maboksi msitake kujifanya eti nyinyi ndo wachapa kazi sana, hata huku kwetu kungekuwa na maboksi mengi ya kubeba baadhi ya hawa wananchi wasingetaka kukaa hapa na kupiga porojo.

    ReplyDelete
  9. We anon 2008 7:00:00 PM EAT, inaonekana na wewe ni misheni tauni, mbona mkali hivyo. Yaani hakuna kazi au watu hawataki kufanya kazi! Basi kalia hivyo hivyo "KAZI HAKUNA" utakufa siku si zako, una mind mabox shauri yako!

    ReplyDelete
  10. Ni kweli kazi nyumbani hakuna na ukweli mtupu

    ReplyDelete
  11. Hiyo ndiyo hali halisi hapo ndipo mjini mibaba mizima imekalia porojo anasubiri mtu apite ambomu pesa ya kula. Hapo hujafika nje ya mji maeneo kama Temeke, Tandika, Manzese, vijiwe kibao watu wamekaa eti kazi hakuna. Bora hata wanaouza mitumba Karume na walio sokoni Kariakoo wanafanya kazi.

    Halafu kutwa kulalamika umasikini, umasikini. Wakati watu wanasubiri Mana zishuke kutoka mbinguni. Kwa mtindo huu wa vijiwe nchi hii haitakaaa iendelee kamwe. Na itendelea tu iwapo watu watakubali kufanya kazi. Na asiniambie mtu kuwa kazi hakuna, kwani kazi si lazima ya kuajiriwa. walio nje ya nchi wanafanya kazi yoyote bila kuchagua tena kwa bidii kwa sababu hakuna mjomba huko wa kumuomba ugali au kubom sigara!

    SIE HUKU HOME UVIVU UMETUJAA MPAKA UNATIRIRIKA MASIKIONI.

    ReplyDelete
  12. hao wapiga soga bure. kuna wapiga soga profeshino hao hawakutani empress kwa fundi musa wao wanakutana dodoma. wanalipiwa usafiri, chakula na malazi kupiga soga na kunyatiana usiku.

    ReplyDelete
  13. Msiseme sana hivi vijue ..siku moja utamuona baba yako, mtoto wako, mjomba wako au hata binamu yako kakaa humu kwenye kijue...Msisahau mlikotoka ...mliacha familia jamani...wengine mnajisahau sana utazania ukoo wenu wote ushavuka bahari...mfwaaaau .....

    Nilonge nisilonge ni wangapi mmeacha watoto bongo????? Sasa hivi hata hamuwasaidii kabisa...na wengine tunawaona mmeshaona huku... halafu mnasema vijue hivi. Kesho watakaa kwenye vijiwe hivi hihi wanao halafu ndio utasema sana kwa vile hata sura huifahamu.........

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...