THE WHITE HOUSEOffice of the Press Secretary
January 25, 2008
STATEMENT BY THE PRESS SECRETARY
President and Mrs. Bush will travel to Africa from February 15-21, 2008. They will visit Benin, Tanzania, Rwanda, Ghana, and Liberia.
This trip will be an opportunity for the President to review firsthand the significant progress since his last visit in 2003 in efforts to increase economic development and fight HIV/AIDS, malaria, and other treatable diseases, as a result of the United States robust programs in these areas.T
he President will meet with President Yayi, President Kikwete, President Kagame, President Kufuor, and President Johnson-Sirleaf to discuss how the United States can continue to partner with African countries to support continued democratic reform, respect for human rights, free trade, open investment regimes, and economic opportunity across the continent.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. Kuna mtu mmoja alifariki dunia na akaenda kwa Mungu,alipofika akakuta saa za ukutani nyingi sana zimetundikwa. Akauliza "Hivi hizi saa ni za nini huku?" Akajibiwa na Askofu mkuu aliyemkuta huko, "Kila saa ina dhambi za kila Binadamu,ikizunguka mara moja ina maana ametenda dhambi mara moja". Yule jamaa akauliza "mbona hizi hapa zimesimamani mbovu? Akaambiwa hiyo ni ya Ayub,Eliah na Ibrahim na inamaanisha kuwa hawakutenda dhambi kabisa ndio maana imesimama,Jamaa ikabidi aulize tena, hivi saa ya George Bush iko wapi kati ya hizi? akajibiwa ya Bush iko ofisini kwa Bwana Yesu mwenyewe maana anaitumia kama feni kwa jinsi inavyozunguka mara nyingi na kwa kasi.

    ReplyDelete
  2. Rias wa several trillion dollars economy kwa siku 7 anatembelea nchi 5.... carl peters inabidi ajifunze katika hili

    ReplyDelete
  3. Zawadi kubwa wadanganyika tunayokuomba utuletee anko Kichaka siku utakayokuja ni kajamaa kamoja kanaitwa Ballali, tafadhali njoo nako kama kweli unapenda haki itendeke.

    ReplyDelete
  4. Kweli waTanzania tunamtaka huyo bwana atutembelee hapo nyumbani,jamani hadhi na heshima yetu iko wapi???I can't believe the cheek this man has, deciding to use us as a publicity stunt for his agenda as Africa's wellwisher. He supports the illegal occupation in Israel, he bombs middle-eastern countries for their oil, he refuses to help stop global warming...why exactly should we welcome him? I, for one am saying'usije bwana', so maybe he'll get the messaage they we're not as gullible as the few people back home who voted him in.

    ReplyDelete
  5. Hana lolote huyo anatafuta mafuta ya bei nafuu na yasiyo na purukushani ya kuchimba akishastaafu (manaake atakuwa hana majeshi tena ya kupora mafuta) na keshasikia huku kwetu yapo.

    ReplyDelete
  6. Michuzi na wadau wengine
    Naunga mkono mawazo ya anon wa 7.45

    Naomba wanaomfahamu Mheshimiwa Bernad Membe waziri aliyetetea na kuendelea kutetea safari za JK wampatie ujumbe na asome ili aelewe maana ya ziara. Maana JK hizo anazofanya si ziara bali anakwenda kuishi, ndio maana tunahoji.

    Tujifunze jinsi ya kubana matumizi na umasikini wetu

    nawakilisha

    ReplyDelete
  7. Haki ya Mungu, huyu mwizi anakuja kutapeli nini yarabi toba? Mafuta siyo mmmh sawa

    Akikoswakoswa na maandamano ya wanaharakati wanaopinga sera zake, atakuwa ameokoka.Nakumbuka ya mabosi sugu wa world bank

    Sasa vile ameamua kuja, aje naomba atulelee mwizi wetu Balali, na ahakikishe walioficha fweza kwake tukiwabaini (hata kama ni watuhumiwa tu)anatukabidhi kama alivyong'ng'ania akabidhiwe mtuhumiwa wa ugaidi

    ReplyDelete
  8. Ni wakati sasa Watanzania tujiunge kwenye kampeni ya 'Anti-Bush Africa Tour', kwa maana huyu dubwana ni a very good hypocrite. Machoni anajifanya kuwa rafiki wa Waafrika, moyoni mwake amejawa na chuki dhidi ya binadamu wenzake wasio waMarekani na waIngereza.

    Mheshimiwa Membe, najua huna ubavu wa kuzuia safari ya dubwana huyu, lakini mfikishie salamu kuwa ANANUKA. MIKONO YAKE IMEJAA DAMU YA WANYONGE. Hatutakwenda kumpokea. Atapokewa na kulakiwa na WANAFIKI wenzake wale wanaojikomba kwake.

    Ciao!!

    ReplyDelete
  9. Bwana muacheni raisi wa watu. Wengine wote hapo kutoelewa habari kukandia tu hata hamlijui jambo.Kila siku mnaomba visa kukimbilia nchini mwake. Komeni kumsema baba wa watu. Kwani kuna rais perfect humu ulimwenguni?

    Kwanza hata mshukuru Raisi wa taifa hili kubwa ameitambua TZ na kutaka kuitembelea. Ni maraisi wa ngapi wa USA wameshawahi kutembelea nchini mwetu?

    Chill out guys...


    Toeni boriti kwanza kwenye jicho lenu wafisadi wakubwa

    ReplyDelete
  10. Liacheni hilo jitu lije Afrika,mwonyesheni mbuga za hifadhi za Ngorongoro,Serengeti halafu mchukeni Kilimanjaro na Unguja na baadae afunge virago na lirudi popote pale lililotokea!!!
    Lakini kabla ya haya yote msisahau kuchukua cheki nono kwa jina la zakaa msaada na sharti iwe kuwa hilo cheki nono liwe direct transfer kutoka american treasury to akaunti yetu huko uswisi na tuhakikishe kwamba hata nusu senti watanzania walalahoi hawataliona au hawataligusa!!!

    ReplyDelete
  11. Basi hapo "Vasko Dagama" si bichwa hilo!
    Karibu lipasuke! Amefanikiwa kuwaleteeni 'Rais wa Ulimwengu'
    Bado sasa Papa Benedikto.
    Si amewaahidi kuwaleteeni pia?

    ReplyDelete
  12. Kelele za mlango hizo hazimzuii mwenye nyumba kulala! Nani hapa katika dunia hii ana ubavu wa kumzuia huyo Joji asiende kwenye nchi yake zaidi ya Iran? Ni hiyo nchi peke yake ndio hana control nayo nyingine zoote he just has to use his remote control anytime, anywhere he is and he will click and change the screen as he wish!

    Hakuna ubavu bwana wala msijifanye hamjui siasa na uchumi wa dunia hii unavyoenda. Huyo bwana mkubwa atakuja na hakutakuwa na ubavu wa mtu kufungua mdomo wake. Eeh sijui mwaka huu watapiga deki barabara zipi maana enzi ya Mume wa Hilary bwana eeh sie tuliokuwa Arusha tulijionea mambo, barabara zilipigwa deki na baada ya hapo zikafungwa zisipate mavumbi mpaka alivyopita ndio na sie makapuku tukaruhusiwa kupita!

    ReplyDelete
  13. Mzee wa kichaka akiona kichaka tu anataka kujisaidia huyo.
    sijui anakuja na yule mnyama(dog) wake wanaefanana sura

    ReplyDelete
  14. Hiyo BORITI itoe wewe,ok?Watu si wajinga kama kina fulani wanavyofikiri!Ni heri tutembelewe na wacheza sinema kama George Cloney wenye kujali binadamu,hasa maskini.
    Wale waliotokewa na maafa kule New Orleans wamesaidiwa zaidi na wacheza sinema sio Bush,eti leo aijali Afrika,Tanzania???!Hebu msinichekeshe..

    ReplyDelete
  15. Mzee Michuzi nami nina yangu machache kuhusu ujio wa Bush. Hata sielewi nianzie wapi lakini kwa ujumla yanayotokea kuhusu huu ujio yananmishangaza na kuniaminisha kuwa watanzania baadhi TUMEOINDA. Nimepata taarifa kuwa Bush alivyoingia Dar mawasiliano yamekatwa hadi atoke, barabara zote anakopita zimefungwa. Sisi ni Masikini bado unafunga barabara ina maana tunaongeza umasikini maana uzalishaji unapungua kwa kiasi fulani. Ukichambua kwa kina utakuta hoja hii ni ya kweli. Sasa nimesikia hapa nilipo Arusha Bush anakuja na hivyo bara bara ambayo inahusika in main road na ikifungwa hata barabara zingine haziwezi kufanya kazi. Hii ni barabara ya Arusha Moshi hadi Kona ya Nairobi na huelekea Arusha airport.....kutoka Kilimanjaro International Airport. Sasa hebu jaribu kutafakari hii bara bara wanasema itafungwa kuanzia saa mbili asubuhi hadi saa tisa jioni. Hii ina maana gani kwa uchumi wa tanzania??? ina maana hata ikatokea kuna mgojwa basi asipelekwe hospitali maana BUSH yupo. Mimi nimefadhaika na hili. Hivi Bush ni nani??? Na swali la msingi zanid ni Hili: Raisi wa Tanzania anavyokwenda Marekani huwa inakuwa hivyo?? au ndo tunamuabudi wakati tunabaki kuendelea na hali ile ile ya uchumi??? Bush anaweza kutuletea utajiri tukaondokana na umasikini??? Huu ni muujiza ambao watanzania tuusahau maana hautatokea. Hatutakiwi kumwabudu kiongozi yeyote kama serikali inavyofanya sasa. Haya Naombeni ndugu zangu mniambie kama Alipokwenda marekani hapa majuzi alipokelewa kwa namna hii. Basi kama hakupokelewa kwa namna hii sisi ni hatuna akili au kuna kitu gani???



    Zaidi ya yote tujiulize, Bush amekutja Tanzania kwa ajili gani?? siku nne zote Tanzania??? anafanya nini??? Tufuatilie kwa makini>



    Naomba tujadili na tupembue kwa makini na mchanga utakaobaki kwenye sufuria tuuchambue pia.



    Natumai tutachangia sote tujue kilichokweli.



    Asanteni watoa maoni wenzangu/.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...