Mr.Michuzi,

We join all peace loving people of the World especially Tanzanians living home and abroad to celebrate New Year 2008!.Picha hizo mbili,moja ni mimi na Mai Waifu wangu(kama unavyosema wewe!) na ya pili ni mimi na mai dota wangu Beverly Mtui.

Greetings to my sisters Grace and Hellen Mtui,my brothers Conrad,Francis,Deo and Edward Mtui in Dar.My sister Mariam Abu in New York,Sister Sharon Dotto Abu in Washington,Pauline Maokola,Omary&Hashim Abu and Thomas Maokola.Dada Hanifa na Malilo.Sister Angela na shemeji Walter in Singapore.Shemeji zangu Twisa,Habib,Jameson,Della,Claudia.God Bless you all.

Peter Tuheri Mtui

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 38 mpaka sasa

  1. Wow......you have a very very beautiful daughter...GOD BLESS HER!!

    Sheky

    ReplyDelete
  2. jamani mimi mwenzenu mshamba sana hivi wakizungu na wakibongobongo kwa majonjo ni tambarare tu au nani zaidi. msaada kwenye tuta.

    ReplyDelete
  3. Karumekenge cha muhimu ni hisia gani unazipata kutokana na mapenzi unayotoa,or unajisikiaje wewe mwenyewe endapo
    ukiwa na wa kibongo au wakidhungu, pia ni manjnjo ganiunayoyapendelea wewe binafsi kama ustaarabu wa kudhungu au wa bibongo namini unanielewa nakusudia nini. wazungu wana mihashuo yao ambayo sisi wabongo inakua fedheha kwa wewe na watazamaji wa kibongo ila wadhungu is okay inategemea ladha gani unapata kutokana na upendo unaompenda yule unaekua nae pale ukiwa katika kipindi cha kawaida au cha sita kwa sita,sasa unapomuona mwenzio yuko tambarare na ntasha au na mbongo ukadhani utapata ladha anayoipata mwenzio wengine hupenda hivi wengine vile pia kumbuka utamu wa peremende mate yako mwenyewea hapo hakuna nani zaidi majibu yatakuja meeengi And remember love always to give then u take.

    ReplyDelete
  4. sio kwamba najisifia lakini nishajaribu aina zote za wanawake mpaka wafilipini akina Katrina, morgana na Kina lorrea.

    Asikuambie mtu wabongo safi sana yani katika hali ya kawaida,

    Wazungu ni wazuri ukiwakuta wale wanaofanya biashara lakin maana nilipelekwa mpaka nikazimia

    ReplyDelete
  5. Kaka Peter heri ya mwaka mpya na familia yako pia, you all looking gud!

    Samahani hii Mtui's family, mliwahi kuishi Dodoma miaka ya nyuma? nawajua watu wanaitwa Grace and Deo, Mtui as their sir name, sasa sina uhakika kama ndio nyie, if so just say hello to them,

    Be Blessed.

    ReplyDelete
  6. Wow, kakangu mzuri jamani hadi katuzalia a very beautiful daughter, look at those dimples! kafanana na babake hadi dimples. Your wife is also beautiful.
    Msaada kwenye tuta, kaka mtui umewanyima wadada wa kichaga bahati ya kuolewa ukaikimbizia Austria. embu ona sasa data za madunga embe zinaongezeka Marangu maana wee umeingia mtini. Ila wachaga na wamarangu kwa ujumla wanapendaga wazungu. kila anaeenda kusoma lazima arudi na mtasha. wachaga wanaita wanaosha jina/nyota. hahah, mchuzi usiibanie hii.

    ReplyDelete
  7. Ndio hao hao Mtui wa Dodoma, wakamia Dar miaka ya 80, walikua majirani zetu Oysterbay , ila na shangaa huyu ni Mtui yupi manaa sijaona Mtui nao wajua mimi ana jina linaanzia na P..lol .. maana wale ni wako A.B.C.D.E.F.G.H.

    ReplyDelete
  8. Anonymous hapo juu kweli unawajua maana hata mimi najua wanaanziwa na A,B,C,D,E,F,G,and H huyo pia simjui but you never know if he knows them then ni ndugu zake.Stayed blessed P.Mtui and your family

    ReplyDelete
  9. Mimi ninacho wapendea wanawake wa kithungu ni kutokuwa ving'ang'anizi kama walivyo dada zetu wa kibongo.Ukimwambia Iam not feel any more, I don't get exicited when I see you. Anakuuliza kama you need a break, na anakupa break mpaka utakapo kuwa tayali au ndiyo imetoka.Lakini dada zetu wewe! ugomvi hataki kuachwa, Mimi sijisikii tena bwana,sitaki basi ina tosha,yeye hataki. Ooooo umenitumia, umepata ulicho kuwa unatafuta..ooooo sikubali,ugomvi ugomvi ugomvi Khaaa!

    ReplyDelete
  10. OMBI KWA WATANZANIA WOTE WALIO ZAA NA WATASHA NI KWAMBA WATOTO WETU WOTE LAZIMA WAENDA BONGO HAKUNA DAMU KUTOPEA.DAMU YA MBONGO NI NZITO SANA NA TUSIKUBALI KUPOTEZA WATOTO WETU HATA KIDOGO! KWA HESABU ZANGU ZA HARAKA HARAKA KUNA TAKLIBAN WATOTA 50,000 WAMEZALIWA NJE YA BONGO AU NA WAZAZI WABONGO AU NA MATAIFA MENGINE.
    OMBI

    ReplyDelete
  11. Napenda kuwashukuru Anonym wote kwa comment zenu na kwamba hamkuvunja heshima ya Familia yangu.Kwa Anonym wa 4:47,ni kweli hao ndio ndugu zangu,sisi tunachangia baba ambae sasa ni marehemu(R.I.P).Kwa Anonym wa 5:40,asante sana wewe umenichekesha sana..lakini ni kweli dota wangu tumefanana sana hasa kwa zile dimple!, na yeye alicheka sana aliposoma. Kwa Anonym wa kwanza kabisa Sheky,umemfurahisha sana Dota wangu kwa comment yako but I'm a very protective father !!!
    God Bless you all- Peter Tuheri Mtui

    ReplyDelete
  12. Aah Mzee Mtui wa kichaga shimbonyi mbee!Familia yako nimeizimia.

    Aise ni lugha gani unapandisha na mwanao? maana katika mazingira ya huko ambapo hata kingereza hakiongewi watu wengi hujikuta wakisalimu amri na kuongea kijerumani na familia nzima.

    ReplyDelete
  13. yaani wewe kamongo ulivyo niudhi,hujui tu,vipi unatu kandia dada zako namna hiyo,umesahau kama na wazungu wakikataliwa wanatoa roho yako na za kwao pia.usiwape ujiko bure,pamoja ukweli watoto wa mixed race wanatoka so sweet,kama binti mtui anavyoonekana,lakini muulize kaka peter jinsi anavyofikiria siku atakayo kosea step nini atafanywa na wifi.

    peace

    ReplyDelete
  14. Wanawake wa kizungu bwana hawana adabu kabisa, yaani wakikasirika hata mbele ya mama yako hawaoni aibu wanakutolea uvivu tu.

    ReplyDelete
  15. BROTHER MTU MAMBO VIPI AISEE? MAISHA YANASEMAJE VIENNA? WAKATI ULE HUKURUHUSU MAONI WAKATI WA JUBILEE YA MIAKA 2 YA BLOG.SASA NAONA UMEAMUA KUWASIKILIZA WAOSHA VINYWA. AISEE BEVERLEY ANAPENDEZA SANA NA ANAFANANA NA WEWE.MAY THE ALMIGHTY BLESS&PROTECT HER
    BROTHER EE KUNA SCHOLARSHIP ZA MASTERS HAPO AUSTRIA LAKINI HATA SIJUI NAMNA YA KUZIPATA KAKA.MIMI NIPO ISTANBUL SASA NAMALIZIA DEGREE YANGU ILA NATAKA ENDELEA.NAOMBA MAIL YAKO BROTHER
    TUWASILIANE.STAY BLESSED BROTHER

    ReplyDelete
  16. BROTHER MTU MAMBO VIPI AISEE? MAISHA YANASEMAJE VIENNA? WAKATI ULE HUKURUHUSU MAONI WAKATI WA JUBILEE YA MIAKA 2 YA BLOG.SASA NAONA UMEAMUA KUWASIKILIZA WAOSHA VINYWA. AISEE BEVERLEY ANAPENDEZA SANA NA ANAFANANA NA WEWE.MAY THE ALMIGHTY BLESS&PROTECT HER
    BROTHER EE KUNA SCHOLARSHIP ZA MASTERS HAPO AUSTRIA LAKINI HATA SIJUI NAMNA YA KUZIPATA KAKA.MIMI NIPO ISTANBUL SASA NAMALIZIA DEGREE YANGU ILA NATAKA ENDELEA.NAOMBA MAIL YAKO BROTHER
    TUWASILIANE.STAY BLESSED BROTHER

    ReplyDelete
  17. Kamongo acha kusaga wewe hiyo habari ya likizo kwanza umeitoa.... huko ulipo sio. Nai heshimu hii familia lakini ningekupa zako. Wee tatizo lako hujatulia tulia ukibanwa makelele acha hiyo wanatujua sana dada zetu..

    ReplyDelete
  18. Dada zetu ni wagomvi hawapendi kuachwa.hilo ndiyo tatizo lao.Ooo umenitumia,ooo umepata ulichokuwa unataka.Sasa kosa liko wapi? kwani lazima kuendelea iwapo umepata ulichokuwa unataka?Ugomvi ugomvi ugomvi,Khaaa!

    ReplyDelete
  19. Bro naona uko connected na familia ya mzee Abu Ally, umewataja wote Ndema hukumgusa.. mimi ni rafiki yake hivi yuko wapi na anafanya nini? wadada wazuri sana wamelelewa kwenye maadili.

    ReplyDelete
  20. Kwa Anonym wa sunday 11:51.Asante kwa kunieleza,nilijua lazima nitamsahau mtu kwani ndugu zangu ni wengi sana kwani Mungu amenijalia kuwa na ndugu hao wote.
    Ndema is my lovely sister,yeye alikuwa Norway kwa PHD yake,juzi juzi alikuwa London baaada ya Boston kwa semina,sasa yuko tena Dar.Ndema anasafiri sana kikazi but we manage to speak everytime.Mariam,Ndema,Sharon(Doto) na Omary tunachangia Mama.Its very special and I'm proud have all my brothers and sisters!

    ReplyDelete
  21. mie nimemtamani huyo mtoto jamaniiii! cheki tabasamu lake...full of life??! mweeeeeeeee!nimekupenda njoo tucheze wote mwaya...
    Ney.

    ReplyDelete
  22. Ello bro..naomba kuuliza kwani francis bado yuko hai?? nadhani niliwahi kusikia kama kulikuwa na msiba kwenye familia yenu?? anyway maybe nimejichanganya

    U HAVE A LOVELY FAMILY..

    ReplyDelete
  23. Mr mtui hongera kwa binti mzuri kama wewe na mamake mleeni vema bint huyo ili aje kua faraja au mkombozi wa ndugu zake wengi huku bongo, nakubaliana na wazo la jan 5: 1:28 lakamongo msisahau kumweleza asili yake mtoto huyo pia katika hadithi nyingi za kina princess arora(slepping beauty) beauty and the beast na cinderellear usisahau kumpa kisa cha kontakinte aliyetetea asili yake na kupandikiza ile roho(spirit) ya utashi wa kurudi kwao mpaka kwa wajukuu walijua historia ya babu yao na walikotoka, ingawa yeye hakujaliwa tena kurudi maskini ila mjukuu akafanikiwa kuwakuta kina kunta orignal wamejaa kibaoooo, nawasifu sana wachaga wanautaratibu nzuri ya kuhiji home kila mwaka ni vizuru sana, kwani watoto hujifunza vitu vingi sana wanapokwenda kwa bibi na babu mimi nilikua naenjoy sana nilipokua mtoto tunapelekwa kwamkole korogwe nilijabia kila nilichoona nilijifunza kuishi maisha mengi duni ambayo yameniwezesha kuishi vema na wagine ninapokua ninashida najua kujiweka katika hali yoyote ile,na pia nafahamu asili yangu kwa kiasi flani .kuna neno linasema mlee mtoto katika njia bora hataisahau.

    ReplyDelete
  24. Anonym wa Jan 7,10:35. Nakushukuru sana kwa wazo hilo.Mimi nina vitabu vya hadithi vya kiswahili ambavyo nilinunua nilipokuwa Bongo.Huyu mtoto wangu kwanza kabisa ni Mtanzania,halafu ni mchanganyiko wa Kichaga na Kinyamwezi kama mie baba yake.Mama yangu mie ni Mnyamwezi wa Tabora.Ni kweli kabisa jukumu langu ni kumlea vizuri na kumfundisha desturi za nyumbani ili ajue anakotoka.
    Kwa Anonym wa 2:35 my beloved brother Francis is very well na anadunda kawaida.Thank God.

    ReplyDelete
  25. Kweli kaka Mtui hongera familia imetulia, unanyuso za furaha, amani na upendo. Mungu wabariki sana. Ombi langu la kwanza binti kesha kuwa jamani mpeni mdogo wake basi, msiogope maisha kila kitu kinampango wa Mungu kaka yangu. Ongea na wifi muongeze baby.
    Ombi la pili nataka kuja kwenye siku ya vijana duniani inayoandaliwa na Kanisa katoliki itakayofanyika July-AUgust 2008 huko huko Australia. Sasa nahitaji contact za makanisa niweze kupata mwaliko kwenye parokia yangu unatanisaidiaje?

    ReplyDelete
  26. Duu, dunia ndogo, Ndema was my classmate UDSM akiwa anachukua Msc statistics. She is intelligent and cool, ana maadili kweli mdada wa watu. I hope her husband Habib is taking good care of her. Akimnyanyasa kaka Mtui umtokee huyo Abib Engineer akueleze inakuwaje. Godbless you and your family.
    mdau wa Marangu Mamba kwa lekule.

    ReplyDelete
  27. Umesema kweli hata hapo namuona Beverly ameshikilia zawadi zake mwenyewe, kama sikosei ni vitabu.nimekusisitizia hilo kwani hata mimi historia ya wazazi wa babangu walitoka comoro wakasegea tumbatu wakaingia zanzibar kisha wakaweka maskani Tanga, mamayangu alitokea malawi wakakutana na babangu Zanzibar nikazaliwa huko, nilipokua mkubwa nilisafiri pekeyangu hadi Malawi Karonga hadi Namwera mpakani na msumbiji ilikua safari ndefu sana na nilikua na watoto wangu wawili mizigo tabu hadi niliibiwa njiani ila nilifika alikotoka mamangu ilikua vilio vya furaha wengine. pia ninamtoto anarangi kama huyo wako ila yeye babayake ni mpemba asili yake oman, sasa nikitafakari ni mwanangu atakua amechanganyika makabila mengi na wote ni ndugu zake, kaaazi kwelikweli

    anon 7 jan, 10:35

    ReplyDelete
  28. Hee Mr Anonym Jan 7,4:35...kweli umesoma na Dada yangu Ndema hapo UDSM!!!Greetings to you from my Family.Ni kweli Ndema is cool and intelligent.Sasa Dada yangu na Habib(shemeji yangu) wamekutana,yaani they are both very deep people.Yaani Habib hata mimi nina mu"admire".He takes care of his family so commitedly.
    Anonym wa code name"jan7 10:35 historia yako lazima uiandike katika kitabu ,its very interesting.Love to you all.

    ReplyDelete
  29. Mh! mimi ninaye demu wa kizungu naishi naye miaka tatu sasa. Lakini naogopa kuzaa naye kwa sababu moja tuu, ambayo ni uzungu wake.

    ReplyDelete
  30. kwanini uogope kuzaa nae? what is uzungu? i dont think ni uzungu, bali ni tabia zenu zinapishana. Kuna wazungu wana behave vizuri tu kama umemtoa mndenyi, wana adabu haswa kasoro tu hawajui kupiga goti la kinyakyusa saa akikupa maji ya kunywa. ivo basi kama hamwezani ni kuwa hamwezani tu, and that has nothing to do with her race/uzungu, whatever u call it. Ukiwa una date na mkashindwana, chukulia yaliyokushinda kwa binti/mkaka ni personal/individual behavior, wangapi mna date watu mmekua pamoja tangu mkicheza mdako utotoni na mnashindwana kwenye relationship! usi judge mtu kwa utaifa wake utapotea kakangu. haya, kama uzungu wake umekushinda, inabidi umrudie yule ex girl friend wako uliemtosa upige magoti na kumwomba radhi, labda hukupangiwa kuoa mzungu, umepangiwa mnyalukolo wako! so listen to ur heart, kama hujisikii mkimbie tu, huezi jua labda Mungu anakuepusha kitu kwa mzungu wako, au huyo Mzungu nae Mungu wake anamwepusha kitu kuwa na wewe, hehehehe, marry krismas to u all.

    ReplyDelete
  31. duh! anony hapo juu umeniweka sawa! ingawa sikubaliani na wewe. Tatizo ni kwamba hapa ninapoishi mimi wanawake wa kiafrika wapo wachache sana na wengi wao ni "ndaza" washaolewa huko walikotoka na washazaa watoto. Huyu demu wangu wa kizungu ana tabia nzuri sana. Tatizo ni kwamba najishtukia na kujiona kama nawasaliti dada zetu, na pia najisaliti mimi mwenyewe kujikabidhi kwa mzungu jumlajumla. I might be wrong but your advice will be appreciated.

    ReplyDelete
  32. hey kaka Peter,

    mi ni anon wa 4:47 frid 4, leo nimepita globuni kusoma soma habari nikakuta pic yenu ina comments 31, nikajisemea ngoja nione watu wanalonga nini,

    You know what, ur so luck, comments zote ni positive, sijaona comment mbaya hata moja, there must be something about u i dont know or even other people they dont know, kwa sababu siamini eti 31 comment hakuna mtu ameandika vibaya, basi inabidi niwasifu wana blog, na hii inaonyesha watu wamekuwa wastaarabu,

    nasema hivi kwa sababu huwa sielewi watu wanachangia nini, wakati mwingine wamejaa chuki na maneno mabaya kwa wenzao, unakuta mtu innocently kapost pic yake au hata habari, wana i manipulate na kuandika mambo mabaya hata huelewi wamaanzia wapi na wanafikiria nini, ila watanzania kwa kulonga mhh, na wengine hawajiheshimu kabisa, sababu humu globuni watu huwa wanashambuliwa sana bila sababu,

    hii inapendeza jamani na imekaa vizuri, sio kutoleana maneno mabaya wakati mwingine bila hata sababu za msingi, mara oo hajapendeza mara ohh sijui nini, hivi tutakuwa kweli, manake watu wengine hawakui eti badala ya kwenda mbele wanaudi nyuma,

    michuzi hii haijakushangaza kweli,
    penye kukosoa tokosoane penye ukweli na ukweli uwepo kwenye uongo na uongo uonyeshwe sio kuandika tu mradi kuandika,

    good day, salam wadau wote, mungu tubariki na ibariki nchi 'inji' yetu.

    ReplyDelete
  33. Anon wa jan8.7:18 hata mimi nimependa sana yaani hivi ndivyo inavyotakiwa kutokana na ustaarabu wetu wabongo, kihistoria tuko waungwana sana, hizi lugha mbofumbofu ay kubongabonga ovyo hazifurahishi kwa msikilizaji maskio huwa yanawasha, huu ndio ukomavu unaopendeza. kwani kuna maneno yanasema limjazalo mtu ndilo limtokalo, na huwezi kumjua mtu tabia zake ila pale anapofungua mdomo wake kuongea anatoa yale yaliyoujaza moyo wake unaweza kumtambua huyu ni wa jamii ipi.Endapo mtu ameleta mada au wazo lake, au ombi la msaada ajibiwe kwa upendo na lugha laini nyepesi na murua sio jeuri au chuki au kejeli kwani utapungukiwa nini endapo utasema pole kwenye kukosea, hongera kwenye ushindi au jipe moyo kwenye kukata tamaa? basi tungekua tunafundishwa namna hiyo na waalimu wetu madarasani tungekua na jamii gani jamani? vichekesho vizuri vinapendeza havina shida hata kama utachekesha kwa kumchokoza mtu ila tusipitilize mpaka. hongereni wadau wote kwa ukomavu

    ReplyDelete
  34. ni mimi tena, kwako unaeogopa kuoa mzungu wako, kwa kuogopa uzungu wake, kwa kuogopa kuwasaliti dada zako tz, siamini kama kweli uko serious na unataka kuoa. How could you feel sorry for our sisters? Do you think kwa kukataa kwako kuoa mzungu utatatua tatizo la madunga embe nyumbani? sana sana utaoa apo mmoja ambae wala sio chaguo lako maana umemchagua kwa kumwonea huruma. Unachotakiwa kujali ni wewe unataka nini katika maisha yako! usioe kwa kuhurumia mtu au kwa kuangalia jamii itakuonaje? Wee sikiliza moyo wako and make decision itakayokufurahisha wewe, at the end of the day uwe happy. You cant please kila mtu kwenye jamii, ata ukioa next door neighbor remember, criticisms za hapa na pale hazitakosekana. Kumridhisha kila binadamu huwezi, listen to ur heart and please mpeleke huyo wifi kanisani au msikitini au kwa mwanasheria mkafunge hizo pingu muda ukifika. Hizi za race, kuoa home, doesnt make sense to me, as long as you are happy, wee chukua tu! ila kaushauri kadogo, chagua apo mzuri angalao usimkimbie saa ya kupiga picha. duu! iga mfano wa kaka Mtui! si umeona yeye na kaportable kake walivopendezeana! usichague ambae ukimweka kwenye blog tutaanza kujiuliza huyu ndo mkewe au mama mkwe! hehehe, just kidding.

    ReplyDelete
  35. nyie maanony wawili hapo juu msiwe mafala. Comments za kibwegebwege na chukichuki zimetumwa lakini michuzi amekataa kuzitundika.

    ReplyDelete
  36. Poa dada wa wa january 9th, 4:51:00 hapo juu (nimekwita dada kwa sababu umetumia neno wifi, nimechukulia kuwa wewe ni mwanadada, sorry kama nimekosea)

    Nitautafakari ushauri wako, na wifi yako anataka kuolewa haraka sana, ingawa haitokuwa kanisani wala msikitini. Kama ndoa itafungwa, basi itafungwa kwa baraka za Kolelo, Mungu wa kweli wa wazaramo na walugulu.

    Miungu wa kigeni nilishaachana nao kipindi sasa, karibu miaka nane imepita.
    Asante.

    ReplyDelete
  37. Kuna mtu kagusia kuwa mtui aongeze mtoto mwingine. Mnasahau watoto huletwa na Mungu! Swali la utaongeza lini mtoto ni personal jamani! mi siulizagitena, maana kwa kufanya hivo tunaweza kuwa tunawaumiza wahusika! impliedly, huenda amesaka sana mtoto mwingine kwa miaka hakubahatika! secondly, may be wanahitaji mmoja wataeweza kumlea kumpa elimu nzuri na kumfurahia, kuliko umati wa watoto hata majina unaweza wasahau! so swala la mtoto mmoja au wawili ni personal choice, na pia health ya wazazi ikiruhusu unaweza ongeza, vikigoma unamshukuru Mungu kimya kimya! Wabongo tuache kusakama watu na swali la "mtoto lini" ukipata mmoja, hata hujasahau labor pain wanakuanza tena " wa pili lini" ukieka wa tatu, wa nne lini! so mnachoshaaaaaaaaaaaaaaaa!

    ReplyDelete
  38. we mwenye domo kaya, ni weye pekeyo ndo ulobaniwa ile comment yako ya matusi mbele ya mtoto na familia ya muungwana hapo juu,kwani huoni soni mpaka kutamka street language hapo, peleka mitabia yako ya ajabuajabu huko mtaani sio humu mwaka huu 2008 wa mabadiliko hatutaki wivu wa rejareja hapa. angekua anabania hata hii angeibania ingezidi kupendeza na wewe ukazidi bata ushungu walai

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...