Hi Bro Michuzi!

U mzima?

inakusalimu sana sana, pamoja na wapenzi wote wa blog hii popote pale mlipo. Tuzidi kuendeleza libeneke katika maendeleo ya kulijenga Taifa letu la Tanzania, hata kama upo nje ya inchi usisahau nyumbani.


kila lakheri! Salamu sana kutoka hapa Cesena-Italy.


BARAKA FRANCO CHIBILITI.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 23 mpaka sasa

  1. Dahh... Ndugu Yangu nakusikitikia sana.. inaelekea hapo ulipo ni choka mbaya sana.. hata samani za maana umeshindwa kununua.. Jamani Sio lazima tuwaone.. kama mko katika hali kama hizi basi mnawavunja moyo hata wale waliopo Bongo wanataka kuja Huku ulaya..manaake wakiona picha kama hizi zisizotofautisha kati ya ulaya na keko kwenye samani za kuchongwa na wamakonde basi wanaona mmh.. Bora wakae wale ugali maharage.. Salam zikurudie tena na wewe.
    mmh ama kweli MAISHA!!!!! NACHOKA KABISA.

    ReplyDelete
  2. uko wapi hapo mjomba,mbona fenicha za enzi za babu Adam???

    ReplyDelete
  3. kaka habari ya huko?
    emwanaee unaonaje ukabadilisha angalau hako ka desk top kako manake siku hizi kuna flatscreen,sas ukiuzia sura hilo bichwa harafu uko abroad ndio mambo gani?

    ReplyDelete
  4. Hivi wewe baraka kweli ni 'mbichi chana' chababu tulikwambia rudi nyumbani wewe huchikii kabicha, sasa unapata upweke peke yako.

    ReplyDelete
  5. Hiyo Picha imepigwa Italy kweli au ??????

    ReplyDelete
  6. Duhhhh! hoyo Computer baraka ulitoka nayo bongo au? kweli imechoka au picha ulipigia bongo kabla ya kuchomoka kwenye kiwanja. Bro Michu najua hutoweka hii post yangu kwa mantiki kwama ina hate..basi mtumie mshkaji kiana asije kwa jamaa zake

    ReplyDelete
  7. mmamaaaaaaa mbavu zangu,

    yani kweli wadau hapo juu mmenivunja mbavu zangu, yani nimecheka hadi machozi hasa wewe anon wa 3:13:00, mhh halafu nikikumbuka na maoni ya nyuma ya pic ya huyo kaka kuwa yuko mpweke basi mhh, yani unaona misoup, nimeanza siku kwa kucheka,thats why we always pray 4 u,

    well.. ila wadau acheni kabisaa, bora huyo kaka anahizo fenicha unanunua na kuweka hakuna biashara nyingine, yani hapa mie fenicha zangu nyingi ni za Argos, basi wee mpaka hiyo fenicha ije isimame kamasi zitakutoka, manake unaunga kitu kimoja hadi kingine mpaka kama ni meza, kiti, kabati au chochote hadi kimalizike, hakuna cha jirani atasaidia, kaka dada au hata mjomba, kivyako vyako tu, kuna meza ya tv hata niliunga kwa wiki nzima, sasa hizo antigue ni bora sana, hahaaaaaaaaaaaaa, haya Baraka salam kwako pia

    ReplyDelete
  8. Chibiliti bin computer jaribu kubadili desktop yako kipato kikiruhusu. Prof Dr Ing

    ReplyDelete
  9. Jameni, DESK TOP manayake nini? Mnaongelea CPU au Monitor (screen)? Acheni kusagia watu. Nimeshafika viwanja tofauti nikaona ya ajabu: Hapo labda jamaa kakodi nyumba na fenicha zake na PC ndani. Labda ana LAPTOP yake iko mvunguni. Au yuko ugeni kapigwa picha. Mie nina Samsung 21" yangu ya 3 years niitupe ati kuwa vijana wanajua flat screen? Mbali ya kufuata wakati pia tuangalie nguvu ya mfuko, umuhimu na utumiaji wa vitu (na sio show off)nk. Iwapo PC ni kwa ajili ya messenger, skype na kuangalia blogs za bongo hiyo screen nafikiri inatosha. Wewe mbeba boksi lanini truck lenye 5.7Lit na 400hp wakati kwenye campus hata parking huwezi kulipia? Nunua japanese vehicle.....
    Blackmpingo

    ReplyDelete
  10. kaka chibili nchumari, kwa mtaji huo lazima uwe mpweke. hakuna REA huko ukamate tu samani.Ila all the best kaka mchumia juani.....,mvumilivu...... wa mbili,,,,, mwisho hakuna marefu yasiyo na ncha.
    Dunia itafunguka tu

    ReplyDelete
  11. naomba tukumbuke kuwa Ulaya si mahali ambapo pana kuwa na mabadiriko ya ghafula, ni mahali panapotunzwa sana historia. Huwezi kuamini utakapofika Roma na kuona nyumba zilizo chakaa kupita hata kwetu Tanzania.

    ReplyDelete
  12. Unajua kuna tofauti ya mbeba box na mwanafunzi. Kama mshikaji anakula kitabu siyo rahisi kununua hizo samani mnazoziongelea jamani. Kumbuka wengine ni watoto wa wakulima wanajibana kuitafuta hiyo elimu! baba zao sio akina Balali! Harafu watu mipango ni tofauti, inawezekana mshakji anapiga buku akimaliza arudi zake home, sasa ya nini kununua samani agahli?

    Jamani kabla hatuja criticize mtu, ni vyema kuwa waangalifu. we are so materialistic! Hapana, si fresh.

    Mkuu wewe piga mipango yako...achana na hao wanaotaka uwe na flat screen! At the end of the day, utanunua tuu, tena zinazidi kutengenezwa nzuri zaidi! wewe tafuta elimu.

    ReplyDelete
  13. duh hiyo kama sikosei ni windows '98 ama less.
    Halafu sisi wabongo kwa kukandia tumezidi.

    ReplyDelete
  14. Kwi Kwi kwi! Duh! Kaka Chibiliti, hio PC yako nadhani ni moja ya zile Pentium 1 za miaka ilee, kabla ya Windows 95! Naamini XP ama Vista haitakubali humo! Kwa Tanzania ya sasa nadhani ni ngumu sana kupata Pc za namna hiyo, kwani mpya ni bei rahisi sana. Rudi nyumbani ununue moja!
    Ni hilo tu

    ReplyDelete
  15. Vya kisasa, vya kisasa, vya kisasa, vya kisasa, vya kisasa, vya kisasa, vya kisasa, vya kisasa, vya kisasa, vya kisasa, vya kisasa, vya kisasa, vya kisasa, vya kisasa, vya kisasa, vya kisasa, vya kisasa, vya kisasa, vya kisasa, vya kisasa, vya kisasa, vya kisasa, vya kisasa, vya kisasa, vya kisasa, vya kisasa, vya kisasa, vya kisasa, vya kisasa, vya kisasa, vya kisasa, vya kisasa, vya kisasa, vya kisasa, vya kisasa, vya kisasa, vya kisasa, vya kisasa, vya kisasa, vya kisasa, vya kisasa, vya kisasa, vya kisasa, vya kisasa, vya kisasa, vya kisasa, vya kisasa, vya kisasa, vya kisasa, na kama ikiwezekana, vilivyotoka leo!!!

    Ndio sababu kuna rushwa na ufisadi BOt, Ikulu, Wizarani, NGos, na kwenye vya ubinafsi = KUKOGANA!

    Na kama sifanikiwi, nitapora, iweje, isiweje!

    Watanzania, tungekuwa tunavitengeneza, lingekuwa jambo murua!

    ReplyDelete
  16. Hao wpte wanaozungumzia maisha ya bwana Kibiriti hasa kuhusu fenicha sidhani kama hata wamejiuliza huyu Kibiriti huko Cessena anafanya nini? Kama walivyosema wengine pengine ni mwanafunzi sasa hayo mafenicha ya Argos na Ikea na wapi sijui ya nini wakati akimaliza shule anatimkia zake Bongo kama ni kweli!

    Mimi ni mwanafunzi chumba changu zaidi ya kitanda, shelf ya vitabu, meza ya kusomea (umeundiwa hapo hapo haisogezeki)kiti cha kukalia cha plastic kama cha baa, printer na laptop yangu nimemaliza. Sina cha TV wala huo muda wa kuangalia TV. Napiga zangu shule bwana ya mwaka narudi zangu Bongo huko ndio ntajua mambo ya fanicha sijui TV sijui nini. Ndio maana namuelewa bwana Kibiriti.

    Kwanza kwetu nimezoea mikeka na majamvi nayamiss kweli kweli!!

    Mswahili

    ReplyDelete
  17. Kweli watu hawana adabu,wanaojifunzia kuchonga ni humuhumu,wenye furstration zao wanatupia humuhumu,ili mradi kuchonga tu.Any wa Am confused.Jamani kinachohitajika ni nini,ni uzuri wa kompyuta ama ni matumizi yake,ndio maana in our country some of guys have got expensive phone with diversity of feutures which are not applicable. Mtu ana simu ya bei mbaya lakini anitumia 0.4445% ha ha ha haaaa!!! si ungenunua mshindi tu,sasa fashion manake nini,ni kuwa nayo tu bila kuitumia ama ni kuwa nayo na kujifunza matumizi ya hizo features. When, I was in Germany at a particular juncture, I was very suprising to meet a CEO who drives Mercedes Benz, but in some occasion meet him riding a bicycle, because of the attitudes towards ethical behaving and environmental under social responsibility. I couldn’t imagine at that time, and there is a time when the Minister responsible for finance rode a bicycle whilst carrying the Budget Portfolio, and they branded that budget as Environment Budget.

    Sasa mnavyomzogoa mshikaji ni kwa nini,jeje kama yeye ndiyo kipenda roho chake hicho,muache uzoba,si kila mtu anapenda mwingine apendacho,ndiyo maana unaweza kuta kuna magari ya zamani yanauzika bei mbaya,ni kwa sababu what matters sometimes is someone’s taste and not fashion.Ingawaje ukichacha kuuza ni matatizo ha ha ha ha ah!!!Labda upeleke museum ma umrudishie Bill gate.Another confusion!!

    Guys,mimi nyumbani Dar ninayo Dudu Proof Radio maalum,I like it so much,nashangaa wanagu mara ,Ipod,mara game, I buy for them.


    Tuache kulazimisha watu waishi unavyoshauri wewe,kama wewe umeamua kusihi hivyo basi ni wewe na siyo mwenzako.


    Bwana mimi nakupa hi,wewe usisikilize ya hao washamba hao. But remember don’t be rigid sometimes flexibility sounds nice.


    Dr.Confusion

    ReplyDelete
  18. Hivi wapi huyu kijana wa watu kasema mpweke,mie naona picha ya shosti pembeni kwenye kikabati karibu na suitcase,hana upweke wowote,ila yuko kwenye hali yakubana maisha.cherryade_19@yahoo.co.uk

    ReplyDelete
  19. jamani huyu kaka ndio kaingia tu huko siku si nyingi. Nahisi hiyo pc ni yakuanzia maisha. Nyie wabongo maneno mengi sana. Kama uko bongo unayo flat screen good for you, lakini hela uliyonunulia ni ya dhambi tupu. Rushwa na hata ulivyoiingiza nchini si ajabu ulikwepa ushuru shame on you.

    Na kama mko nje ya nchi mnamshangaa nini? Ni wangapi mlikuja na vitu vyenu toka bongo? Si mlianzia huko huko? Tusidanganyane hapa. Wanaoanzia juu kwa juu huku ni wale watoto wa baba zao wanaoiba hela TZ kila siku kwenye uchumi wetu. Na mwisho au matokeo ya hao watoto tunawajua kila siku. Uizi umewajaa sana, hawana bank atm card kwa vile bank zimeshawashtukia michezo yao ya uizi uizi na wengine wanaishia jela au wanarudi bongo kwa vile life ya huku ya kula kwa jasho lako hawaiwezi. Wamezoea fast life na uizi kama baba zao.

    Kwa hiyo nampa hongera sana huyu kaka. kajitahidi sana kwa miezi michache aliyo nayo.

    kwanza mnaokosoa hivyo vifaa vyake s ajabu unatumia the same monitor mpaka sasa. Wekeni picha zenu tuzione. Much know wakubwa ndio maana rushwa na uizi havituishi nchini. Catch up na vitu vizuri wakati hela ya kuvilipia hamna... Hiyo ni yake na uwezo wake umefika hapo.

    ReplyDelete
  20. Nyinyi msifikiri huyo bwana Baraka ni mpumbavu yeye mambo yake yote kaelekeza bongo si nyinyi malimbuke mnaishi ulaya kama mpo kwenu mnasahau hata mlipo toka sasa kwa taarifa yenu siku mkishuka bongo baraka naye atawacheka. kwani vitu ambavyo mnajivunia huko ulaya yeye kavieneza Bongo.

    ReplyDelete
  21. ila hapana mazee tuacheni utani hata kama kuna wengine mko serious ila jamaa ni kweli yupo Italy? manake hivyo vifaa ni noma, alafu watu kama hao ukiwa unaongea utasikia wanajivunia ah mimi ninaishi ulaya napiga buku! ahahaha kama buku lenyewe kama ndio hivyo hata huko ulaya siendi kusoma!! alafu kakunja nne! alivyokaa anaonyesha yupo so uncomfortable manake hilo sio sofa kwa hiyo hapo anavumilia tu! kochi gani ukikaa unazisikia chaga! mimi ningependa jamaa atuonyeshe anapolala! michuzi pleaze muombe jamaa pic! ahaha alafu mwambia nimeipenda batiki! kwa mbali unaweza sema kamwagikiwa na mrenda ama sufuria la kisamvu!

    ReplyDelete
  22. MH! PROF, DR, ING? I VE NO IDEA WUTS GOIN ON HERE? TWO TITLES ONE PERSON? JUST LIKE BABA, MTOTO DING?

    ReplyDelete
  23. yani mnenichekesha sana....

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...