mwenyekiti wa yanga enzi hizo mangara tabu mangara akipokea kombe la ubingwa wa soka kwa nchi za ist afrika mashariki na kati toka kwa kocha tambwe leya huku nahodha gibson sembuli akiangalia. hakujapata kutokea kiongozi kama mangara, kocha kama tambwe leya na mshambuliaji kama sembuli hadi sasa. nyuma ya mangara jamaa kavaa kanga iliyoandikwa 'pele na santos wageni wa yanga' yaani almanusra mzee huyu amlete pele na santos bongo kwa jinsi soka lilivyokuwa tambarare miaka ya 70 na 80. lakini lunyasi wakapiga zengwe ngoma ikatemwa

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. wW Misupu,kabla hujakimbilia kumsifia mzee Tabu Mangara hebu jiulize maswali yafuatayo:
    1.Kwa nini mwenyekiti wa yanga mzee Kondo Kipwata alijiuzulu hadi akapelekewa 'bao' kisha ndio akarudi kwenye uongozi(wakati huo Mangara(RIP) akiwa makamu wake)?
    2.Kwa nini timu ya Yanga ilifanya vibaya east and central january 1976?
    3.kwa nini ulitokea ugumu mwaka 1975 wa kuwapandisha first division kina Rishard Adolf,Mapango Godian,Pondamali,Mkweche na wenzao?nani alizuia ili kina Sunday,Sembuli,Elias Michael,Kitwana, Chitete,Kapera etc waendelee kutanua hata kama ni wazee?
    4.Ni nani alisababisha kocha wa Yanga Tambwe na wa Simba Nabi Camara wapigwe PI?
    5. Pamoja na milioni 2.7 alizotoa Mzee Karume kujenga uwanja wa Yanga,siku anafukuzwa Mzee Mangara kwenye kasha la fedha Yanga zilikutwa sh ngapi?hadi leo hii uwanja wa Kaunda una jukwaa?
    ndugu yangu Issa,we kama mwanahabari you know better than me and you should learm to praise where it is due lakini chumvi acha.
    Wartanzania lazima tukubali kwamba matatizo ya mpira tanzania yameletwa na kina Mangara baada ya kuanza kuwakumbatia kina .....(jamaa zetu wenye asili ya .....)

    ReplyDelete
  2. Michuzi wacha unazi.Leo ndio umedhihirisha wewe Yanga ingawa unajidai kushabikia Pan.Lunyasi wangetia zengwe vipi??Hebu fafanua.Ilikuwa usanii tu wa kuuza kanga hamna cha Pele wala Santos.Sema ukweli hata kama unauuma.

    ReplyDelete
  3. Ahsante sana mchangiaji wa 7.54 EAT. Ukweli ni kwamba Mangara alichangia sana kuvunjika kwa Yanga na kuzaliwa 'kandambili' na 'raizoni'. Aliitumia Yanga kujitajirisha yeye na familia yake. Hakujatokea mshambuliaji kama Gibson Sembuli na kocha kama Tanbwe Leya!? Oh! Please! you can tell the lie to those who were in recently years. We know better than that. Hivi ni kwanini watu hutaka kupindisha ukweli bila hata aibu!?

    ReplyDelete
  4. Haya longolongo za picha ya black and white zimerudi tena!

    Basi tucheze na facts sasa. Hio combination ya Tambwe Leya, Mangara na Sembuli ilishinda makombe mangapi klabu bingwa ya CECAFA? Je yanga walifika wapi makombe ya CAF. Zikiwekwa data hizo basi tutaanza kumwaga sifa zinazostahili.

    ReplyDelete
  5. huyu mzee alikuwa kibaka wa nyerere,alisababisha kugawanyika yanga. tatizo ilikuwa wanakula pesa,ukaja uhasibu wa david kanyanka, halafu kocha Tambwe leya akasema wachezaji walipwe mishahara, basi hapo nyerere kupitia vibaka wake akasema bongo ni nchi ya kijamaa hatulipi wanamichezo, next thing Tambwe na Camara wa simba wakafukuzwa kazi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...