Home
Unlabelled
shimo la mungu
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
MichuziBlogV2Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
sababu ni rahisi sana. ni kwamba ukiingia humo kwenye hilo shimo utakutana na Mungu. Kama unabisha jaribu :))
ReplyDeleteMjomba, habari za hii sehemu zinatisha kweli. Lakini nasikia pia wabunge wengi tu wanakwenda huku kupata thawabu na kujichukulia kura za wananchi kisha wanasahau kule walikotoka.
ReplyDeleteAcheni uongo, hamna chochote cha ajabu ndani ya shimo hilo mi nishaingia mpaka chini kabisa na kutoka na mzigo wa kuni, enzi za Oljoro JKT, ni hadithi tu hamna maajabu yoyote!!!!
ReplyDeleteEmbu acheni uongo nyie hapo juu,
ReplyDeleteMara mnasema panatisha, mara anakaa mungu, ina maana mungu anakaaga mahali panapotisha??
Na hao wanaoenda kuchukua thawabu, hawaogopi mahali panapotisha??
Kama wanazichukua kwa mungu then wanasahau walipotoka, mungu si angewaadhibu??
Kwa taarifa yenu hapo panaitwa hivyo kwa vile ni eneo zuri tu lenye majani na bstani nzuri tu kama peponi,
Aisee michuzi hapo mahali asikuambie mtu, panavutia kishenzi
"Acheni uongo, hamna chochote cha ajabu ndani ya shimo hilo mi nishaingia mpaka chini kabisa na kutoka na mzigo wa kuni, enzi za Oljoro JKT, ni hadithi tu hamna maajabu yoyote!!!!"........
ReplyDeleteNilipitia Oljoro JKT operation Nidhamu ni kweli hilo shimo lipo na ni sehemu iliyokuwa ya ajabu, nyasi zake zinafikia urefu wa mtu na kwa jinsi nilivyopaona hakuna kiumbe anayeishi mle. Vijana wa JKT tulikuwa tukienda kuchukua kuni kwa matumizi ya kikosini. Naamini walipaita vile kwa kuwa utokeaji wake unaonekana kama wa crater, sehemu ambayo ina very steep slopes all around going down to approximately about 200metres deep!
Nakubaliana nawe Major,huwa hakuna chochote ila ni hekima za mababu zetu wa zamani walizitumia katika kutunza mazingira yao kwa ajili ya kuweka rasilimali hizo zisipotee kwa kuharibiwa, Nakumbuka nilikua jku Zenjy, kambi ya KAMA kipindi hicho ukifika tuu unaanza kupewa ilani na wanawake wenzio kua kuna sehemu bondeni chini haturuhusiwi kwenda kuna chemchem ya bi fatuma hataki wanawake wanaokua kwenye MP.Ikatokea siku nikafikia hicho kipindi na kulikua hakuna mtu wa kunisaidia maji kuruta wote wako paredi hivyo nililazimika kwenda mwenyewe kwa vile nilikua naumwa sana nikasema huyu bi fatuma ni mwamnamke mwenzangu nategemea hii hali anaitambua kwanini nishindwe kutumia maji yake eti hataki uchafu, kwa hasira na kujitoa mhanga nilioga na kufua nguo yangu hukohuko ila nilikaa mbali na ile chemchem sikuiacha uchafu ukaribie chemchem hiyo kisha kwa haraka nikatoka nikarudi nikiwa na hofu ya kupata adhabu za bi fatma ila sikupata lolote na sikumshirikisha mtu ila palikua safi kila mtu anakua makini hata hao wanaume hawaogi karibu ya chemchem wanapaogopa pia. Hapo nilijifunza kua ni vitisho tu, pia nikapata wazo pia ni sehemu waliitenga waitumie sana wanaume , kwani walihofu kule kuchanganyika inakua sio vizuri, Na misitu mingi ni hivyo waliitunza kwa ajili ya dawa zao za asili na siri zao walizokua wanazijua wao, ndoi mapokeo yakaendelea. Ila ni hekima nzuri ingawa ni ya vitisho kidogo.
ReplyDeleteMi naona Wadau wote mmtoka nje ya point!! Oljoro na Nyumba ya Mungu wapi na wapi?? Hivi hamjaona hapo juu mtumaji kasema Newala, yani Mtwara. Sasa nyie mnakurupuka tu hebu fanyeti utafiti kabla hamja kurupuka. Eh bwana Allen ahasante sana kwa kunikumbusha home. Yani hapo ukirudi nyuma kidogo ndio kwa Father, Mother na mashangazi. Hapo karibu na uwanja wa ndege. Dah! Long Time haki ya mungu mi ntalia!!!
ReplyDeleteNyie kweli hamnazo...mnapiga kelele za paka bila sababu mwenzetu brother Michuzi anawacheka tu. Mie nilishakutana naye Michu pale wakati naenda kutafuta vitu fulani. Siku siitaji ila Michu nadhani anajua hiki kitu. Michu wapashe vijana wako hawa juu ya hili shimo!
ReplyDelete