Bwana Issa Michuzi,
nashukuru kwa kuweka waraka/malalamiko yangu kwenye blog yako. Nasikitika net inanisumbua naweza kusoma comments lakini nashindwa kutoa comment/kujibu bloguni hivyo nikaona sio busara kukaa kimya na kupotezea watu muda kwa kushauri na wasipate majibu, naomba uweke majibu yangu bloguni kama itawezekana.
Kwanza nachukua nafasi hii kuwashukuru wadau wote kwa michango yao, nashukuru sana sana. Pili nakataa huyo anayedai ndiye Mume wangu, sijui nilizaa mtoto mmoja yeye akiwa masomoni, sio kweli kabisa, hakuna kitu kama hicho, sielewi kwa nini baadhi yetu tunaamua tu kuwa na dhihaka katika kila japo.
Any way, kautumia uhuru wake pia, ama nayeye ana skendo kama yangu, sijui. Haikuchukuliwa kirahisi kama nilivyofikiria nyumbani kwangu, japo nashukuru finally nimeutua MZIGO!, thanks God!
Sikuwa na niya ya kumdhalilisha mume wangu kama alivyoichukulia kwani hata sikuweka jina lake, na hata la huyo mke wake sikuliweka, nashangaa imegeuka kwamba namdhalilisha na kuwatangaza Dunia nzima! Ni kwamba kaondoka nyumbani kwangu na mke wake kwenda wanakojua wao, na kwamba KANIACHIA ZAWADI YA WATOTO.
Not big deal kwani pamoja na kuwepo kwake bado hakuwa na msaada wowote. Ninamshangaa kama alikuwa na pa kwenda kwa nini basi hakuondoka siku zote hizo kuepuka kutangazwa hadharani/Duniani.
Nawashukuru sana Wadau wote kwa michango yenu, najua hamkuwa na niya ya kuvunja ndoa yangu kwani tayari ilishavunjika ndani kwa ndani. Nasema tena samahani kuwapotezea muda wenu kwa namna moja ama nyingine kuja kuanika matatizo yangu hadharani.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 39 mpaka sasa

  1. Nimefurahishwa na pose na language ya huyu dada.
    Kwangu mimi that says everything.
    Mungu atakusaidia dada no doubt about it.
    Kuvunjika kwa ndo we si wa kwanza wala hutokuwa wa mwisho (hata Mama Winnie Mandela aliachika )Na wala si mwisho wa dunia
    Kazana lea watoto na fungua ukurasa mpya wa maisha
    Good luck (You may need it )
    Mr Dar

    ReplyDelete
  2. Umefanya kosa kubwa sana kumdhalilisha mmeo au mzazi mwenzio. Hata wanao wakia watakusuta! Hivi nikuulize; ukimpata mme mwingine mwenye vituko zaidi ya huyo utamweka tena kwenye hii blog tumjadili?!

    It was a grave mistake you will live to regret!

    ReplyDelete
  3. Nashukuru sana dada yetu kama umeshachukua hatua nakupa pongezi sana. Nakukumbusha pia uchukue hatua za kiusalama pia, habari hizi julisha vyombo vya usalama ili wamfuatilie huyo mtu asije akakufuata na kimada wake kwa nia ya kukudhuru kwa sababu ya wivu wake wa kijinga. Ataendelea kuwa na wivu, si wa kimapenzi, bali wa kuona wewe una maisha mazuri wakati ya kwake kayakoroga mwenyewe. Pole sana, hongera kwa hatua uliyochukua, na ninakuombea uzidi kuwa na nguvu.

    ReplyDelete
  4. Mungu akubariki kwa uvumilivu.

    ReplyDelete
  5. kwa kweli ni ajabu,unataka kuniambia kuwa huwezi kutoa maamuzi yako mwenyewe mpaka kadamnasini?
    unajua kuna wanawake wanainjoi abuse,haki ya nani nilisoma mahali!they do exist!
    try to be a master of your life,huku globuni naamini kuna wanawake wana story kama yako lakini naamini most of them walifanya uamuzi kabla ya marefu uliyopitia!

    gal, mwisho wa siku utaingia mwenyewe six feet under, why let someone tena uliekutana nae ukubwani akakuamulia maisha kwa mtindo huo?

    he!haki ya nani dunia ina wanawake wa ajabu!huchelewi na kujitoa gazetini kudai mgawo!kha!jitegemee dada kimawazo pia!
    hayanikuti hayo mie, kisa?

    ReplyDelete
  6. Hongera dada kwa kujikwamua, wakati mwingine si lazima kutumia mabavu kutatua matatizo yetu hata nguvu ya kalamu tu inatosha. Imeonyesha ni jinsi gani kalamu ilivyoweza kutatua matatizo yako.

    Dada kuna fundi seramala hapo karibu? NAKUSHAURI BADILISHA KITASA CHA MLANGO KWA USALAMA WAKO NA WATOTO WAKO.

    Nadhani utakuwa umenielewa namaanisha nini.

    Nakutakia kila la heri kwa kuondokana na abusive people!

    ReplyDelete
  7. dada pole sana na hongera kwa kutua hilo zigo, na m'mungu akuepushie hilo na jingine. maoni yangu hayatolewi hii najaribu tu. KWA WALE WOTE WANAOKUKANDIA KWA UAMUZI WA KUJITOA KWENYE BLOG HII, ACHANA NAO, WAPUMBAVU, NA PENGINE NDIO WOTE HAO WENYE TABIA ZA KISHENZI KAMA ZA HUYO JAMAA. ENDELEA NA MAISHA YAKO, HAO MALAIKA WA MUNGU WALEE KWA MOYO WAKO WOTE, KWANI HAWANA MAKOSA. USIKATISHWE TAMAA NA WAPUMBAVU. MUNGU ATAKUSAIDIA.

    ReplyDelete
  8. DADA WAZUNGU WANASEMA PROBLEM SHARED PROBLEM HALVED!!! NA MIMI NASEMA PROBLEM SHARE PROBLEM SOLVED SOMETIMES!!

    ACHANA NA HAO WATU KAMA ANON WA PILI HAPO JUU ETI "THAT WAS A GRAVE MISTAKE"" HOW??? MIMI SIONI KAMA NI MISTAKE. SAA INGINE KWENYE HAYA MAISHA UNAJIKUTA UPO KISIWANI NO ONE TO TURN TO!!

    YEYE KAANDIKA SHIDA YAKE, NA THE REST REMAINED ANONYMOUS!! SASA SHIDA WAPI, NA KAMDHALILISHA NANI. UNLESS KAMA WEWE UNAMJUA WHICH STILL IS NOT A BIG DEAL.

    DADA HONGERA ENDELEA NA MAISHA, KAMA ALIVYOSHAURI KITHUKU USALAMA WAKO NI MUHIMU HIVYO WAONE WAHUSIKA. BADILISHA VITASA AND TRUST NOBODY FROM NOW!!! KWANI HUYO JAMAA ATARUDI TUU TENA KWA MAPENZI MAKALI NA MACHOZI YA MAMBA.

    ALL THE BEST OF LUCK KWENYE MAISHA!

    GIRLS POWER!!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  9. Mungu akikupitisha kwenye njia yenye miba na matope, lazima atakupa gumboots za kuhimili kuchomwa na miba na kukanyaga matope, naye atakupa nguvu, usiangalie nyuma, yaliyopita si ndwele, ganga yajayo, najua itakuwa ngumu lakini for the sake of ur kids. huyo mfa maji achana naye atapetape. kila unapokwenda kulala piga goti umshukuru Mungu kwa yote.
    nana

    ReplyDelete
  10. dada kama ni kweli wameondoka nakupongeza!!!usivunjike moyo saidia hao watoto kuna siku watakukumbuka..ingawaje sio rahisi watoto wa kambo kumdhamini mama wa kambo..lakini wewe fanya kama umefunga macho...na muombe mungu sanaaa...bwana yesu akutangulie dada

    ReplyDelete
  11. We dada uko na issue your self.
    Haujafundwa kwenu we? Haujapata muda wa kutosha shule we? Huu mbona ni upuuzi na uswahili wa vibarazani ambao umepitwa na wakati. Yako ni yako woman.
    Tafuta psycologist dada au upungwe.

    ReplyDelete
  12. Umefanikiwa katika hilo, lakini kwa umri wako utaweza kuishi kama "mtawa" ( bila mwanaume ) na ni kijana gani siku hizi atakayekubali kuoa mwanamke mwenye watoto watatu? Kama tamaa za mwili wako zimekwisha, then utamudu maisha lakini kama bado utaangukia kwa mwanaume wa wenzako kama huyo mama alivyoangukia kwa mume wako. Kila la Kheri.

    ReplyDelete
  13. Shoga jana nilikupa pole leo nakupa hongera,the decision they took is an advantage to you and your kids.It wont be easy,you obviously love your husband.Funga roho angalia mbele sasa,ndoa inaleta heshima kwa mwanamke lakini alicho fanya mumeo nikukudhalilisha,only you know how you feel about your hubby,na sisi wanawake roho zetu tunazijua wenyewe utasema simtaki mbele za watu ukiwa peke yako unabembeleza arudi,mtu mzinifu hana dawa fikiria wanao endapo huyo baba atakuletea AIDS,ni watoto watao suffer.Kwahiyo shosti chukua hatua yao ya kuondoka kama blessing,try to move forward na wanao,and be kind to your step kids,you also need to take time to heal your wounds before you move to another man dont rush wanao kwambia mie hayanikuti hayo it's because they've never been there once they're there they'll be singing a different tune.Ulikua kwenye matatizo na ulitaka solution kichwa kimoja si sawa na vichwa zaidi ya 70,watu wamejitokeza kutoa maoni kwa sababu story yako ilikua disturbing leo watapata faraja kama ulivyo pata faraja but you have to hold on to that and dont let go of it,sema na moyo wako.Kama nilivyo kwambia jana if it gets too much join an evening class or gym it really does help usiwasikilize wanao ku put down.

    ReplyDelete
  14. Pole sana dada,
    Leo ndiyo nimesoma haya. Wala usiwe na shaka kuweka mambo yako wazi hiyo moja ya ukombozi. Mambo ya kuficha ndiyo unajikuta unauliwa ndani ya nyumba.Waache hao wanaoweka mambo ndani huku hata raha hawana. Na hao watu wanaokusema vibaya ujue ni wanaume wenye tabia kama ya ex mume wako. Kama kweli ulimpenda huyo kaka na kwa moyo wote na ulijitahidi kadri ya uwezo wako kuokoa ndoa yako na imeshindika basi Mungu atakulipa na utashangaa. Muombe mungu najua ni ngumu ukiwaza watoto lakini kama mtu ni shetani muache na ushetani wake na aende zake. Unaona umejitahidi sana. Usijali maneno yawatu ambayo yako negative hao ni wanaume wenye tabia hizo or kama ni wanawake bado hayajawakuta. Michuzi usijali, umuoni Oprah kawa tajiri kwa kurusha vipindi kama hivi. Hasa hivi ni vipindi vya kuwekwa kwenye sehemu kama hii nakupata ushauri maana ni vitu ambayo viko kwenye maisha ya binadamu kila siku na ni wanawake wengi wako kwenye giza na wanapata shida kwa kutoweza kupata ushauri au kuogopa mpaka wanakufa kwa maradhi bila sababu na watoto wanaharibika bila sababu. Eti vitu vya ndani viwekwe ndani huyo mwanaume kwenda huko kuzaa nje kama bata alishatoa mwenyewe siri za ndani na kuweka nje. Maana mume mmoja na mke mmoja, Nakwenda huko nje tayari umeshaexpose vitu nje kunasiri tena??????Waache watu wajue . Wanawake juu huna kosa ulilokosa hii ni kujikomboa. Inakupa more confidence. Way to go Girl. U ROCK!!!!1

    ReplyDelete
  15. Ila kwa kweli wewe dada ume-expose vitu vingi sana tulikuwa hatujui! Kumbe kuna wanawake wengi sana wamechanganyikiwa na ndoa! My DOG! Kama huyu annon 29: 10;04 hapo juu nadhani yeye ndo ana hali mbaya sana!

    Poleni sana wanawake, lakini mengi ya matatizo kwenye ndoa huwa mnajitakia wenyewe. Siye si sana. We mwanaume unaoa mwanamke mrembo na mvuto kama Viola hapo chini, baada ya mwaka anakuwa kama mke wa rais wa bongo aliyepita! Unadhani nikiona vitoto vya mvuto huko barabarani nitashindwa kubip!


    Shauri yenu! Mtalialia sanaaaaaaaaaaaaa! Na hatuachi ng'o! That is the only World Order accepted everywhere!

    ReplyDelete
  16. Mimi naona hao watoto wa Kimada wapeleke ustawi wa Jamii, maana wanaweza kutumika kukudhuru wewe au watoto wako, though tunasema watoto ni malaika.
    lakini hatujui ni ya hao wawili walio ondoka, then nenda mahakamani upate order wasikaribie au kuonekana karibu ya nyumba yako au mahali ulipo.
    ukiwapeleka ustawi huyo mwizi wako atasikia uchungu atawafuata.

    ReplyDelete
  17. Nlikuwa nasubiri uje umalizie usanii wako!Roho yako nyeupe unajiona mjanja kwa shuhulisha watu kujibu stori yako ya uongo! Unaona watu wablog hii wote hawako makini eeh. Hao 54 uliowapata ndo hao hao, blg hii inatembelewa na wastani wa watu 70 elfu kwa siku, sasa katika 70 elfu umewafanya wajinga 54 tu, au pengine si ujinga bali na wao waliamuwa kukufanya mjinga. Asie weza kung'amuwa kwamba ile ilikuwa stori ya kutunga basi, na upeo wake wakuchanganuwa mambo ni mdogo, hawezi hata kutumia simple "logic" na ndo umenisaidia kuamini kwamba "commonsense is not common to all" Hongera hadithi yako tamu, ilofanya wengine waamini kuwa ni ukweli, nakumbuka hata nyakati zile za kuingia hizi cinema tulikuwa tunaamini kwamba ni kweli!!Na hadi leo baadhi ya vijiji wanaamini kwamba nikweli kila kinachooneshwa, na ndicho ulichofanikiwa wewe hapa. Jitahidi nategemea kusoma vitabu vyako vya Riwaya zenye msisimko zaidi hapo baadae.
    Tack

    ReplyDelete
  18. Una bahati umempata mme mwenye subira na busara. Ingekuwa mimi ningekukamua mpaka nyongo kwa kunidhalilidha hivi! Ningeng'oa na kizazi kabisa. Wewe! Umeniudhi sana kwa kutusema wanaume bila sababu ya msingi.

    ReplyDelete
  19. Pole hongera na Mungu yupo tu.....

    Hao wanaokukandia achana nao...wewe umeombaushauri na umeupta na maneno yamewachoma na wameondoka but watch your back.....

    Na huyo anayesema siju unawatoto watatu kupata mume sio rahisi...he doesn't know what he is talking about....wanaolewa watu wanawatoto sita sembuese wewe una kazi yako na ya maana.........

    ReplyDelete
  20. Dada nimekupenda sana kuweka vitu kama hivi wazi as longer uliweka siri ya majina. Unajua ni wanawake wangapi hapo tu Tanzania wanateseka namna hiyo na umewasaidia wanawake wangapi ambao wamesoma hii habari kwenye maisha ya utumwa na kupewa magonjwa yasiyo yao. Nimependa sana. Mr. Michuzi weka vitu kama hivi hii inasaidia sana kwenye jamii kama zetu za kiafrika ambazo zimejaa na wingi wa giza na kuona wanawake ni kama pipa la taka na kutothamini maana ya mwanamke hapa duniani. Mr. Michuzi kupitia hii blog yako itasaidia sana jamii hasa wanawake wanaoishi kwenye abuse. Endelea na hii. Kwanza ulitakiwa hata umuweke huyo Mzee wako jina lake. Maana katoa sababu ya kijinga sijawahi kuona, badala ya kujenga anazidi kubomoa huyo si mwanamme kama adhabu angekupa pale pale iwapo kama ni kweli ulicheze rafu huyo ndiye manamme lingali, kama aliendelea kuishi na wewe akawa weak basi si mwanamme thabiti ana matatizo yake.

    ReplyDelete
  21. Anon wa 08:00 pm.
    Kama wewe ni mwannamke lijaha basi wewe ndio ukatafute huo msaada sio mwenzio. Na kama ni mwanamke ambaye unampenzi au umeolewa subiri kufa na pressure.

    ReplyDelete
  22. pole mwaya w wanauem wengine, wana balaa wanakuachia kitoto kidogo, unakua huna cha kufanya, utaona haat visichana vidogo vingi, vilivyozaa umri mdogo, waume zaow anaviachaia vitoto, ndio maana wanakua hawana mbele wala nyuma na vitoto vyao, maisha yankua kama yamewaelemea maana raha anataka lakini kuna kitoto ndani, basi wanavyofanya ni wapo wapo tu, maana kimwanaume kikikuachia kitoto, kinaenda kutembea na wengine, kisichana kinabaki hakina cha kusema,w asichana muwe makini sio kuzaa zaa ovyo, vingine, vinakua na mimba halafu vinafunga ndoa, mwe makin, kabla kuvikubali vianaume vyenu.

    ReplyDelete
  23. MARA NYINGI TUNAJISIFU ETI WAAFRIKA TUNAONGOZA KUTUNZA NDOA ZETU KULIKO WATU WA MABARA MENGINE;

    UCHAMBUZI YAKINIFU SASA UNAONYESHA KUWA SISI TUNAONGOZA KUTUNZA UNYUMBA(KUISHI CHINI YA PAA MOJA LA NYUMBA) NA SIO NDOA AU PIA UNAWEZASEMA TUNAONGOZA KUENDELEA KUTUNZA CHINI YA PAA MOJA NDOA ZILIZOVUNJIKA SIKU NYINGI.

    MAMA ASANTE KWA KUCHOKOZA HII MADA.

    SIOMBEI NA SIDHANI ITATOKEA, LAKINI IKITOKEA NIKAFANYIWA HIVYO (ULIVYOFANYIWA)NA MKE WANGU BASI TUTAFUTANE KAMA UTAKUWA BADO HUJAWA FULI BUKUDI ILI TUTAFAKARI NDOA ZETU MBILI ZILIZOVUNJIKA KISHA TUSIMAMISHE NDOA MOJA ILIYOPITISHWA KWENYE TANURU CHINI YA PAA MOJA!

    ReplyDelete
  24. HAINGII AKILINI HATA CHEMBE, SI STORY YA KWELI, NA KAMA NI KWELI BASI WEWE NI MPUMBAVU.

    ReplyDelete
  25. ASANTE nimekusoma,being a master of my own destiny hayo hayanikuti kamwe!na please elewa kuwa wanaotoa mawazo na mawaidha some of them have passed thru that road, so hakuna kuimba different tune wala melody!
    hakuna kitu kinaua kama kukosa konfidense,huyo alikuwa hana na hata huyo mumewe hakuwa na hofu ya mkewe kwa sababu naamini alijivua utu wake na kuwa tegemezi kwa huyo mume!mume analeta hawara na watoto ndani???lazima mwenzetu si kwema!na unataka kuniambia haya aliyoyaandika humu ndio yamefanya bwana akimbie?wapi jamani mbona mnatufanya watoto wenzenu?

    ReplyDelete
  26. Sister walka usikonde. wamekusaidia snaa kurahisisha mambo kwani kuondoka kwao ni tijara kubwa kwako. La msingi sasa ni kujifunga kibwebwe kuhakikisha kwamba watoto wanakua na wanasoma. Usiseme hoo baba yenu mhuni kaondoka la hasha uhuni wa baba ni wake na ni tatizo la wewe na yeye watoto wasipewe majukumu ya kuchanganya.I Wish you best of luck na sasa pursue divorce yako kihalali asije baadaye akaleta gozigozi si unajua tena!!!!

    ReplyDelete
  27. wanaume punguzeni tamaa za ovyo ovyo, mridhike na mlichonacho, pia visichana vinavyopenda kuzaa umri mdogo,w ala haviko tayari na maisha, muwe makini kwani maisha baadae yatawashinda.

    ReplyDelete
  28. Kama Michuzi pamoja na Wanakijiji wa Blog hii.
    Hadithi ya huyu aunt, si yeye peke yake, mimi nina mdogo wangu ambaye alikuwa na matatizo hayo hayo utafikiri ni yeye aliyeandika. Yanafanana sana, sisi tulikaa na shemeji yetu miaka 24 alikaa kwenye nyumba yetu, kwa sababu wazazi walifariki. Muda wote huo hakuwa na kazi, mdogo wetu alimlisha, na watoto walikulia ujombani. Mungu aliwajalia mdogo wangu alipata kazi nzuri, akajenga nyumba. Wakahamia. Shemeji nae alipata kazi baada ya hapo alileta mwanamke na vitoto viwili. siwezi kuendelea kwani yote ni kama nilivyoeleza hapo juu. Mdogo wangu alifukuzwa kwenye nyumba ile, akarudi nyumbani tena.!

    Sisi tulichofanya ni kwenda kwa wakwe kwani wao na sisi tulikuwa kundi moja. Shemeji mdogo, alichofanya ni kumpiga kaka yake pamoja na yule bi mdogo, shemeji alivunjwa taya, na walitolewa kama mbwa kwenye ile nyumba.
    Sasa hivi mdogo wangu amerudi kwenye nyumba yake, shemeji na mke wake wameenda kupanga chumba kimoja huko mtaani.

    Sasa hivi mdogo wanngu anaendelea vizuri na maisha yake mapya. Maisha ndivyo yalivyo, ukishangaa yako kumbe kuna wengine wana matatizo kama hayo.

    ReplyDelete
  29. Dada kwanza nakupa hongera nyingi kwa kutua mzigo uliokuwa umekulemea. Kama weye ni muamini Mungu aliyehai, usiache kumshukuru kwa hili. Pili ni kama walivyokwisha changia hapo juu ni kuwa toa taarifa kituo cha polisi kupotelewa na hao watu upate RB, huwezi jua wanapanga nini cha kukuhujumu. Taarifa yako Polisi ndiyo itakuwa mkombozi wako. Tatu ni juu ya hao watoto ulioachiwa, si vyema ukaendelea kukaa nao (it sounds too rude, but that's reality) wanaweza tumiwa na mmeo na mke wake kukuhujumu or huwezi jua likawapata lolote kwa mapenzi ya Mungu ukaishia kulaumiwa. Hujui walipokimbilia wazazi wao, ama wapeleke ustawi wa jamii or kwa wazazi wa mmeo. Hawa wanaokuandama umemdhalilisha mmeo hawakutendei haki kabisa na ni wanyanyasaji wa wanaweke, achana nao na usiyaweke akilini yote waliyosema. Wanataka ufanye wema gani zaidi ya huo uliofanya, ambao ni ngumu kupata wa aina yako, badala yake wakaishia kukudharau na kukutukana!
    Wanadamu sijui kwa nini huwa hatupendi wenzetu wawe na amani

    ReplyDelete
  30. I am happy to hear that your husby ameamua kuondoka mwenyewe na Kimada wake one thing i dont understand him ni kwa nini hakuondoka mapema mpaka asubiri kutolewa kwenye blog ndio aondoke shame on him!!!

    dont listen watu wanaosema au vile your husby says kwamba umemdhalilisha kumtoa kwenye blog actually yeye ndiye aliyekuzalilisha kwa kukuletea kimada ndani ya nyumba yani he made you look cheap!! cz i know men generally cheat but wengi wao wanafanya sana siri wake zao wasijue. iam no longer suprised kuona wanawake walioolewa siku hizi wanacheat waume zao sababu cz wanachoshwa na upuuzi kama hizi dizaini no one wants stress now adays.

    all that i can advise you ni kwamba hao watoto wa nje tafadhali sana naomba uwapeleke kwa wazazi wao maana huyo mama hakuwa kind enough to respect you and by the way if she is still alive kwanini asilee mzigo wake anakuachia wewe? hebu wapeleke kwao.

    last advise sasa hivi ndio muda wako wa kushine mama maana umeondokana na mizigo sasa inabidi ujipendezeshe na pia ubuni miradi ili uwe bize unatakiwa usahau hao wapuuzi yani kwa ufupi inabidi umkomeshee huyo ex husby wako umwonyeshe kwamba hie was a clog to your development. yani hakikisha unafanikiwa in life i think umenipatapata i dont need to elaborate more.

    watoto wako make them feel there is no gap la baba yao (i know its not right bwana wee sometimes inabidi tu sasa utafanyaje)ensure wanapata basic needs na extras!!

    All the best mama

    ReplyDelete
  31. Wanawake kweli mama yenu ni mmoja, tofauti ni baba tu! Ebu angalia mawazo ya huyu annon Jna 30 12:41 hapo juu! Yaani ni kichaa tupu. I cant imagine yukoje huyu mama!! Duh!

    ReplyDelete
  32. Sasa huyo alikuja kulea watoto wake nyumbani kwako iweje leo amewaacha tena !!!

    ReplyDelete
  33. anon.jan 30,2:17 samahani kidogo mimi sie unaempa huo ujumbe ref. hapo juu mi ni mwengine ila kuna neno umelitumia kwenye sentensi yako mwanamke lijaha ni typing error au unamaana gani? naogopa kughilibika hapo, mimi nimezowea kuskia neno rijali,shababi,shupavu
    jabal kwa mwanamme na kwa mwanamke nimezoea bibie, alanisa, habibt. sasa hilo geni kidogo nataka kuongeza kamusi yangu ya kiswahili tafadhali.

    ReplyDelete
  34. Michuzi mimi ni yule niliyesema mume wake huyo mama, kumbe siye. Maelezo yake yalifanana kabisa na malalamiko ya mke wangu baada ya kumtambulisha kwa mama wa watoto wangu wa nje ya ndoa. Lakini kwa jinsi nilivyosoma maoni ya watu, ninataka nitafute nafasi mimi mke wangu na huyu mama wa watoto wangu tuzungumze tuyamalize. Sioni tena sababu ya kuumiza roho ya mke wangu ambaye nilimuoa kanisani. Tatizo la huyo mama wa kwenye blogu limenipa simanzi kubwa sana. Nitamwomba mke wangu msamaha naamini atanisikia. Nimejifunza!

    M.K.

    ReplyDelete
  35. Watu wanaosema vibaya kuwa huyu mwanamke kwanini kaweka. Nyie ni wale wanaume mno tesa wanawake. Kuna dada mmoja alisema lazima wanaume wote waende wakufundwe namna ya kuishia na mwanamke nimeamini. Wanawakwe wengi wako kwenye giza na hawana support, itasaidia jamii nyingi sana kwenye haya mambo kuweka juu. Wewe kaka ambaye umekuwa unaongea negative Aaacha tabia hizo za kunyanyasa wanawake. Tatizo la waafrika tunakimbia ukweli tunapenda kuka kwenye uongo na unafiki ndiyo maana ni masikini wa roho na wa mali. Thumbs up girl. Naamini hata kama watu hawajajibu wamepata somo kubwa sasa kutokanna na hii. Wewe kaka uliyesema eti mbona hamna mtu anajibu ni wengi wanapitia hii blog. Sasa kwa taarifa yako they are good listener and always a good listener wins!aaahaahhahh hawawezi kuandika upuuzi kama wewe uliyeandika hapo juu. Sisi ni wanawake tunaogombea ukombozi wa waanawake wenzetu waliokaa kwenye giza na kujiona hawana thamani ya kuishi wakati duniani tunaishi mara moja tu. U have to enjoy every single moment u have.

    ReplyDelete
  36. Nimeamini, wanawake wana matatizo. Nilidharau usanii wa hadithi hii mwanzoni, lakini nimegundua kuwa ndoa zina problems, kama huzijulii!

    Hata hivyo, wengi wa wanawake ni waosha vinywa tu hapa. Sana sana ni zle loose au wale ambao hawajui kukaa na familia. Ukisoma comment kwa makini inakupatia picha hiyo. Kwa kusoma hizi comments, Wanawake wote walioa maoni hapa au kwenye ile message ya mwanzi hawajatulia na ndiyo wana problems kwenye familia zao. KIla kitu kinajieleza.

    Kwa mfano, kuna mwingine anafika kusema ni bora kutoka nje kufanya mapenzi! Sasa uko nje unafanya mapenzi na nani, mbwa au mwanamme kama yule uliyemwacha home? Pia ukisoma comments zaidi utakuwa kuwa hawawezi kwenda mbele bila mwanamme.

    Kwahiyo nawashauri wanawake, kabla ya kuvunja ndoa, na kudai uhuru wa kujtanua, angalia tatizo ni nini? Vumilia sana na anagalia tatizo hasa kiini chake. Tatizo linaweza kuwa wewe mwenyewe! Na ndiyo ilivyo mara nyingi sana.

    Bye

    ReplyDelete
  37. Michuzi asante sana...

    Nimesoma yote na nimeona jinsi maoni ya watu yalivyogawanyika kwenye hii isuue.
    Ukweli ni kuwa Bongo bado tuko kwenye giza...yaani GIZANI sannnnnaaa tu....kwa haya mambo


    Kuomba ushauri ni jambo la kawaida na kama hamna msahuri wa maana sio vibaya hata kuweka na jina hapa....Nini cha ajabu....mtu akiomba ushauri wengine eti wanasema ameanika mambo yake nje....Eti mbya...anajifanya....Na wanawake wengine wanampatia mamneno mazito tu


    lakini ukweli ni kuwa wengi waliomjibu kwa bugudha huyu mama mwenye kuomba ushauri
    a) ndio wanzinzi wenyewe na wanaishi maisha hayo wanaona aibu haya mambo yakisemwa hadharani.

    b)ni wanaume wanaoogoba mabadiliko ya kijamiii wanawake kuwa open minded ni kama bomu limepasuka kwenye vichwa vyao

    c) ni wanawake wanaoishi kwa wanume wa watu wanaona aibu mambo yao yamesema hadharani

    d) yao wanayakalia kwenye mkaa wa moto na kujifanya sio shida hii eti hii ni culture yetu .....na ukimwi ni culture yetu?????

    Itabidi tuamke saaana...kuwa single sio kitu cha ajabu siku hizi....Na ni bora uwe single uone watoto wako wakikua kuliko kufa na UKIMWI jamani.....

    It is about time kwa watu wenye kufikiri kuwa wao ndio wanaconquer the world alone.

    Kama unaoa mke wa pili kwa vile dini yako inakuruhusu iwe hivyo lakini mambo ya vimada ...Mimi naona sheria iwe kali kwa hili.....

    Na kama hao watoto wake mpelekee au mwambie aje awachukue awatunze mwenyewe. Fadhila mabazo utalipwa mateke wala usiziendekeze


    Michuzi usiitume kapuni comment yangu ....

    ReplyDelete
  38. kaka michuzi nakuheshimu sana!
    Pia naiheshimu sana blog yako kwani iko juu mno!
    Hivi kaka unasababu gani ya kuweka comments zinazotutukana tuliotoa maoni yetu?
    Na nyie watoa maani wenzangu, acheni mijumuisho;kama ummshindwa mkeo,usiseme wanawake wote ovyo na kinyume chake pia.
    Inyala vazant alieandika ACTS OF FAITH anasema "man is a mind thing,whatever is in your mind u will find it in a man"

    ReplyDelete
  39. hi Dada,
    Hujafanya kosa kuanika mambo yako hapa,i always pity womens cuz u sometimes hurt and no body comes between ur problems,big girls dont cry,naomba nikupe pole na nakuomba ukishasoma hii,tafadhali nenda mtafute consellor yeyote bila woga,trust him,and trust me,mwamie kila kitu,atakushauri,then post matokeo kwenye hii blog unambie!,u will be 100%free from stress!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...