shule ya msingi bunge. kwa mbali shoto ni maegesho ya magari ya benki kuu ambapo mduara ni jengo la ukumbi wa mikutano wa twin tawa

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 31 mpaka sasa

  1. kaka michuzi asante sana kwa kuweka hii shule nimesoma hapo msingi and had wonderfuly memory of my childhood tulipewa elimu na msingi mzuri sana ambao umeniletea mafanikio mengi nimemalizahapo 89 tafathali wadau wote waliosoma hapo tuanzishe umoja wakuwasiliana nilikuwa 7bla mwalimu kisebengo sijue bado yupo na mama masasi kinachonifurahisha katika shule hiyo tulisoma na watoto wa rais, gavana na jaji mkuu na watoto wengi wa mawaziri na ilikuwa ni shule ya bure kitu ambacho watoto wetu hawatapata kama huna pesa ya internation za siku hizi ambazo ni nyingi na biashara asante kaka michuzi umenipeleka mbali leo baada ya kubeba wazee one love

    ReplyDelete
  2. Eeh bwana shule yangu hii. Naona imechoka sana. Jamani Bunge Alumni popote mlipo tuipige tafu hii shule yetu pendwa.

    ReplyDelete
  3. Asante kaka michuzi. Bunge Primary imenikumbusha mbali. MM-Htown

    ReplyDelete
  4. Ilikuwa shule ya watoto wa vigogo.Kupata nafasi hapo ilikuwa taabu kweli kwa mlalahoi.

    Sasa hivi iko hoi baada ya shule za English Medium za binafsi kuanzishwa. Watoto wa vigogo hawasomi hapo tena wamewaachia watoto wa madereva wao,mamesenja wao na watoto wa walalahoi wafaidi hilo kombo la shule inayofundisha kiswahili masomo yote.

    ReplyDelete
  5. Mi Michuzi unaniuaga hapo tu,

    Jana umetuonyesha IFM Canteen, ukaweka na BALALI TOWERS,

    Leo unatuonyesha BUNGE PRIMARY pia unatuonyesha na hizo BALALI TOWERS,

    Inaelekea hizo Towers zimekukuna sana,
    Sie zinatukumbishia machungu mtu wangu, next time jaribu kuchukua photo bila kuzihusisha, Zinaturudishia hasira zetu za Mabilion yaliyopotea.

    Halaf sorry, kwan jamaa anarudi lini??
    Maana viza yake si imeisha??

    ReplyDelete
  6. aaaaaah kaka Michuzi asante saaaaaana yaani umenikumbusha mbali.............
    Jamani wana bunge wenzangu (ambao tumepoteana) hasa wewe anony wa juu hapo wa 7B mwaka 89 (ni nani ), tuwasiliane ??
    Mama Masasi, our wonderful Mwalim Kisebengo (na zile talk zake za darasani....!! she shaped my life) Mama Sabuni,Mama Sebastian, Mwalim Talib.........i can go on and on....
    Mama Chigana...(hehe) kaka Mwamedi maembe, Issa, Mako (ice cream...), indeeed it was fun.........I had a great time.Bunge guys if, you are out there email yangu ni .(mmungula@hotmail.com)please give me a shout !

    Kaka Michuzi Mungu akujaalie sina cha kusema zaidi kwa kazi unayofanya zaidi ya shukrani za dhati. p.s Naomba niwe mdau wa millioni moja (ha ha ha !)

    ReplyDelete
  7. Du, kaka michuzi umenikumbusha mbali sana, mimi nilimaliza mwaka 1989 jamani mwal mkuu alikuwa Masasi, mwalimu wa hesabu kisebengo, kiswahili seba, du, kipindi hicho shule ilikuwa bab kubwa.

    Du, nawapa hi wana bunge wote popote pale mlipo!!! kama alivyosema blogger mmoja itakuwa vizuri tukianzisha umoja wa wana bunge.

    Umenikuna sana michuzi leo.

    ReplyDelete
  8. michuzi hii imetulia mungu awe nawe daima, salimia wadau wote wa bunge, popote pale walipo, pia kwa wale waliomaliza 7c mwaka 1995.

    ReplyDelete
  9. kweli wanafunzi wote wa bunge, tuanzishe umoja na tufanye reunion kwa kweli, michuzi na wewe lazima uwepo.

    ReplyDelete
  10. anonymous hapo juu anayesema hii ilikuwa shule ya viogog tu, sikubaliani na wewe. Mie nimesoma hapo nimemaliza 1991 ni mtoto wa mkulima. Nilipata nafasi ya kusoma hapo. Ndio kulikuwa na watoto wa Vigogo, kuanzia Raisi, makamu wa Raisi, Waziri Mkuu, Jaji Mkuu na mawaziri wengi. Ila kitu kimoja kikubwa ni tulikuwa WOTE SAWA. Yaani hakuna ubaguzi huyu mtoto wa Raisi wala nini..ukichelewa geti linafungwa unakumbana na Kisebengo au Seba unakula fimbo zako kabla hujaingia class. Shule hii imenijengea msingi imara wa mafanikio. Jamani wana Bunge tukumbuke hii shule angalau tukarabati angalia hapo juu kule 7B and 7A na staff ya walimu inavyooneka kuchoka. Bati kutu tupo. Nilipokuwa hapo kulikuwa na bango kubwa linasema SHULE YA MSINGI BUNGE naona silioni hapo kwenye picha labda ukata shule haiwezi kugharamia. Alumni wote jitokezeni tusaidie hii shule yetu tukufu

    ReplyDelete
  11. asante sana michuzi yyote mwenye wazo la reunion ni sawa tu, fanyeni mambo tuwe na reunion party.

    ReplyDelete
  12. michuzi wewe kiboko aisee, sasa itabidi ujitahidi kuandaa reunion ya wanafunzi wote waliosoma bunge.

    ReplyDelete
  13. Big up Michuzi,umenikumbusha mbali sana na mimi pia nimesoma hapo Bunge nimemaliza 1989, nilikuwa 7b. Nawakumbuka sana hao walimu wote waliotajwa na wadau wote. Salamu kwa Bunge alumni wote duniani.Lets do this Bunge re union kama wenzetu wa mlimani primary!

    ReplyDelete
  14. fanyeni sasa mpango nyie wote wenye maini yamekaa sawa kabisa, sasa mtu ajitolee na kuandaa alumni association ambazo tutakutana mara kwa mara, na kujadili mambo mbalimabli, michuzi unaonaje hii, tangazia wana bunge wote tafadhali.

    ReplyDelete
  15. sasa mimi naomba kuuliza hiyo reunion tunaifanyaje ?, maana kila mtu anony, anony, kasoro huyo jamaa na mam (ambao usikute si majina yao) alietoa email yake, kwani si kila mtu ajitaje tuu jina hata moja na weka na at least email yako tuwasiliane,it doesnt matter........Jamani kama kuna mtu anukumbuka maneno ya ule wimbo wa mstarini mchana na zilengoma pleeeeeeeease anikumbushe......"mwameeeeeedi maembe yamedoooda...." Man ! Bunge was one of the Best Primary Schools ,if not the Best of them all, tulijengewa msingi wa maisha mwema sana.Wewe niambie shule gani ya primary ilikuwa na party za darasa kila mwisho wa mwaka ??it was fun .... Walimu wa Bunge popote mlipo duniani, natoa heshima zangu,Mama Kisebengo.......you were simply something else......asante sana mama. Jamani na mie ni Anony wa 7B, 1989.

    ReplyDelete
  16. asante sana kaka michuzi, unatukumbusha enzi hizo, kweli peperusha salamu zangu kwa wadau niliosoma nao 7c, mwaka 95 kina peter nkinda, rehema malinda, neema nawita, ceci, brenda, jamila, bhimji, gloria, paskalina, andrew, edith, martha,daniel mkokota, naomi, na wengineo pia, wa madarasa mengine, michuzi asante sana.

    ReplyDelete
  17. michuzi aisee unatukumbusha mbali sana, hii shule ilikuwa bomba sana sana, we acha tu mstarini asubuhi, breki, halafu mambo ya tuition, yaani michuzi umekuna wadau wa bunge kinoma, asante sana salamu kwako kaka. Mguu pande, mguu sawa, na mengineyo jamani wadau wa bunge, popote pale mlipo, dumisheni upendo na amani daima, lazima tuwe na bonge la reunion.

    ReplyDelete
  18. Bunge alumni lets do this reunion party for really.My suggestion is we need to have web sight that we can all chip in ideas on how we can organize this event. Amani kwa 1989 7c,babu Deus,Paul, Ruta, Eric mpoo?Step up jamani!

    ReplyDelete
  19. Bunge alumni I have an idea why don't we do re union party memorial day in Columbus Ohio. Michuzi lazima uje .Any ideas??

    ReplyDelete
  20. Jamani wana Bunge wote pakuanzia ni hapa BUNGE
    Hiyo Re-union itakuwa vizuri sana. kama zile party zetu za kufunga muhula.

    ReplyDelete
  21. Yaani wewe annon Jan 19:9;38 umesoma shule nzuri ya Bunge lakini umeishia kubeba mabox huko Columbus Ohio, Marekani?!! Hii nini tena!?! Hii ni fadhaa tupu kwa kweli!

    ReplyDelete
  22. wadau wote wenye maoni hapo juu mimi, mmoja wa bunge primary school, nakubaliana na nyinyi nyote pamoja na michuzi pia, sasa hayo maoni ya mwisho nyinyi ndo muanzishe website kwa kweli, na muitangaze sehemu zote za media, na hapa kwa blog ya michuzi, hapo ndio sasa tuanze events, na mambo mengine mengi sana sana, ushauri mzuri sana, columbus ohio wengine wako sehemu mbalimbali, sasa fanyeni hivi, iwe reunion kubwa sana bongo, labda summer mwaka huu, au anzeni na maideas na mmpeperushie michuzi wadau mnaonaje, hii imekaa poa sana, basi anzeni na hiyo website haraka muitangaze hapa, halafu ije mambo ya metings tuzidi kutangaziana humu kwa kaka michuzi.

    ReplyDelete
  23. wewe wa columbus sasa wewe ndio uwe, mtarayarishaji na kuandaa wasiliana na michuzi mutangaze humu, na kuwataarifu wanafunzi wote wa miaka yoyote ile, tujadili mambo mbalimbali. asante sana kaka michuzi.

    ReplyDelete
  24. wee unaetoa suggestion ya party columbus Ohio lazima uwe mtu kama Chacha vile?hahaha hujaacha tuu..! Kwanza nielewavyo memorial day si siku ya huzuni sasa wewe unapendekeza reunion party pamoja na memorial day inakuwaje ? Anyway kama kuna Ma-Web designer wowote kati yetu please mjitokeze kuunda hiyo website/blog easier. tukiita "Bungeprimaryalumni.blogspot.com" sio mbaya ama mnaonaje hii ?.Itakuwa rahisi kuwasiliana na humo hatutaki U-Anonymous, Halafu ikiwa tayari mtujulishe wengine kupitia kwa kaka Michuzi ili tuweze kuwasiliana.

    ReplyDelete
  25. Reunion party maana yake ni kufanyikia ile sehemu yenye hizo kumbukumbu sasa wewe hii Reunion unayopendekeza ya Columbus mzima kweli wewe? nae ni nani wewe ? Jamani tuna uwanja mkubwa sana wa michezo kule nyuma ya madarasa(kama sio zilipo hizo parking za BOT nizionazo kwenye picha, mana bongo noma!!) Anyway yanapigwa maturubai yale meupe na kiwanja kinafanyiwa marembo venue ndio hiyo tuu, the fact is it has to be inside the school na hii ni kwa sababu kama kuna fundraising yeyote itakuwa rahisi watu kuona hiyo pesa itaifanyia nini shule ama mnasemaje ?? tengenezeni hiyo website tuwasiliane zaidi mana suggestion ni nyingi na kaka Michuzi hawezi kuweka hii picha milele hapa na akiitoa tuu watu mtaingia tena mitini...... SO I DARE SOMEONE TO CREATE A WEBSITE or bungeprimaryblog within one week!!! go on guys mimi ningevolunteer bila shaka but I am crap at computers!.......by the way kaka Michuzi mimi naona ndio mdau wa Milioni tatu ama??

    ReplyDelete
  26. Mimi pia nilimaliza bunge 7c na ni mwaka 1995. Kuna anony wa Saturday, January 19, 2008 6:38:00 hapo juu kaandika majina ya waliomaliza embu nitumie email nikusalima maana ingawa mimi hujanitaja nilikuwa darasa moja na wewe na ho nilimaliza nao. Email R32wow@hotmail.com Ni vyema kutuwekea picha nzuri kama hii.

    ReplyDelete
  27. imekaa poa na mwenye kujua mambo ya computer amwambie kaka michuzi haraka, na wengine tutajoin tu asante sana michuzi.

    ReplyDelete
  28. we wa hapo juu majina ni mengi ongeza tu la kwako na wengine wowote unaowajua, hizi ideas zote mtu aziweke, hii imetulia wadau, michuzi amenena sana hapa.

    ReplyDelete
  29. Huyo blogger wa jumamosi Jan 19 2008, 3:36:00 alitaka kujua tulikuwa tunaimba vipi mstarini, tulikuwa tunaimba Mwamedi maembe yamedoda, mwamedi maembe yamedoda, huyo Mwamedi alikuwa anauza maembe na pia alikuwa anafanya usafi chooni. Mnakumbuka enzi ya maembe ng'ong'o na pia wakati wa kugombe chipsi?

    Jamani kwa yeyote aliyemaliza Bunge mwaka 1989 darasa la mwalimi seba naomba tuwasiliane naitwa Immaculata Kadyanji my e-mail is: imma752000@yahoo.com Umoja wa wana bunge ni muhimu sana tuharakishe jamani.

    ReplyDelete
  30. yaani michuzi katutoa mbali sana sana, wakati wa break ilikua chips na mishikaki.

    ReplyDelete
  31. michuzi wewe ni kiboko sana, unatukumbusha mbali sana, asante kaka.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...