Siku ya Jumamosi waandishi wa habari wa Gazeti la Mwanahalisi Bw. Saed Kubenea (pichani) na Ndimara Tegambwage walishambuliwa na watu wasiojulikana ambao waliwasababishia madhara mwilini. Watu hao walivamia mida ya karibu saa tatu za usiku kwenye ofisi za Magazeti hayo huko Kinondoni huku wakiwa na mapanga na visu!
Bw. Kubenea ambaye ni Mkurugenzi wa magazeti ya Mwanahalisi na Mseto alipata majeraha makubwa zaidi hasa baada ya kumwagiwa tindikali (acid) machoni ambayo imempotezea uwezo wake wa kuona ingawa kiasi cha madhara hayo bado hakijajulikana chote.

Bw. Tegambwage yeye naye alijeruhiwa mwilini na kulazimika kushonwa nyuzi karibu 15 kuganga majeraha hayo. Hadi hivi sasa Bw. Kubenea yuko Hospitali ya Taifa Muhimbili huku Bw. Ndimara akiuguzia maumivu yake nyumbani

Je mashambulizi haya yana maana gani kwa waandishi? Je ni nani inawezekena akawa anahusika na serikali inaweza kufanyanini kuhakikisha usalama wa waandishi wetu? Hayo ni baadhi ya maswali ambayo ninajaribu kujibu katika matangazo yangu ya leo kwenye
http://www.klhnews.com

Tafadhali karibu kwenye tovuti yetu mpya ambapo tunaanza pole pole kuwaletea habari moja kwa moja toka nyumbani. Tayari Forum yetu imeshaanza kazi kama nilivyoaahidi na wote mnakaribishwa na hoja na mijadala yenu. Kuna mambo mengi ambayo ni kutembelea na kujaribu ndio utaweza kuona utajiri mkubwa ambao tumeanza kuwakea
Title: KLH News Episode: Kushambuliwa kwa waandishi alama mbaya kwa Tanzania
http://mwanakijiji.podOmatic.com/entry/eg/2008-01-06T22_22_34-08_00
Enjoy!
NB: Tafadhali hakikisha unajiandikisha kwenye tovuti ya KLH News ili niweze kuhakikisha nina email yako kwani baada ya muda tovuti hii ya huku tutaifunga na sina jinsi ya kuhamisha email zote hapa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. jamani mi ni kilaza tu sio mwandishi wala mwanasiasa,ila huyu bwana namjua alishawahi kufika kibaruani kwangu kuomba msaada kwa vile anabaniwa kila kona kuchapisha magazeti yake, mara ya mwisho mpaka wiki mbili mbele gazeti lilikuwa halijatoka, maana mpaka makaratasi walimnyima sijui kina nani!
    sitaki kusema naukubali ufisadi,ila kwa mtu mmoja kama huyu kushindana na ufisadi anaotaka kuutokomeza sio rahisi, mambo anayotaka kuyaanika sio rahisi aachwe hai, anyway, nasikitika kwa yaliyompata,lakini making a difference inataka sacrifice kubwa mno.

    sasa michu unibanie na koment yangu maana ndio visa vyako!

    ReplyDelete
  2. Nimesikitika sana kuona mzee Tegambwage anashambuliwa hivyo.namemfahamu miaka mingi tangu nikisoma na mwanafamilia wake.michu please mpe pole ukimuona na ufanye msaada uniombee mawasiliano na Amani Tegambwage.jkigwambaye@yahoo.com.very sorry kwa kwenda nje na topic

    ReplyDelete
  3. Japo in a true sense huwezi kumwita Kubenea kuwa ni mwandishi wa habari, inasikitisha sana KUSOMA YALE YALIYOMPATA. WALAANIWE SANA WATU HAO, NA WATAFUTWE WAPELEKWE MBELE YA SHERIA.

    Wanaosomaga gazeti la Mwana Halisi watakubaliana nami kwamba gazeti hilo linaandika umbea na habari zake sio za kuamininika. Sio gazeti naamini hivyo.

    Pamoja na hayo, Kubenea ana HAKI YA KUISHI NA HAPASWI KUVAMIWA na yeyote. Wasioridhika na anayoyafanya wafuate sheria zinazohusika.

    ReplyDelete
  4. Lakini waandishi mapaparazi wanakera sana mpaka mtu kafany hivyo ujue kuna kitu mimi binafsi sioni huruma mpaka nipale ukweli wa jambo hawa watu wanabomoa sio kujenga kila siku fikiria kama mtu anakutangazia wewe una ukimwi wakati sio kweli halafu mtu uwezi kuprove wrong tena utafanya nini naunamjua aliyekuharibia unafanya kweli tu

    ReplyDelete
  5. Hii kichwa cha habari kibadilishe.Kwani kinaonyesha dhihaka na dharau.Ingekuwa ni mdogo wako ndio kamwagiwa tindikali usingefanya dhihaka.Tuwe serious kwenye mambo yanyohitaji kuwa serious.Hata usipotoa comments zangu lakini ujumbe umefika.

    ReplyDelete
  6. Tunawapa pole wandishi wetu kwa yaliyowakuta. jamani Tanzania lini tutakuwa na Demokrasia ya kweli na ulinzi wa kweli?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...