Hi Bro Michuzi!

Mimi napenda kutoa maoni yangu kwa wale wote watoa maoni. Wakati nikituma au tukituma picha, salamu na habari mbalimbali, hasa lile nililo nalo moyoni, nilituma salamu zangu na picha, wengi wameniponda sana, lakini mimi binafsi ninafurahi sana maana ni kawaida sana ya sisi binadamu kupondana.


Picha hiyo nimeituma hapa majuzi tu, wengi wamenisaga sana kuhusu meza, computer n.k,kuwa ni feki na vya zamani. kuwa hata Tz hamna vitu kama hivi, utafikiri sipo majuu, sawa nakubali.


Ila ninachotaka kusema, hivi nyinyi mnafikiri kuishi lazima uwe na vitu vya kifahari? Halafu hivi vitu kwa hapa vinathamani nyinyi hamjui, vitu vya zamani kwa hapa vina bei sana, hasa fenicha, ulizeni walio ishi huku Italy watawaambia. Pia mimi hii nyumba si yangu kwanini nihangaike na fenicha? Kuhusu computer nyinyi mnataka nini, si ilimladi inafanya kazi? Tena inakula mzigo si mchezo! Nyinyi mnatakaga vitu nje ya uwezo wenu sasa nini hii?


Nyinyi mnafikiri Ulaya hela za kuokota tu, ukifika unazipata za kumwaga, huku watu wanapiga kazi sana pamoja na uwezo walio nao lakini kazi ni mbele, tuacheni hizo tujitume kwa bidii ili tujikomboe na haya maisha tuliyo nayo magumu, sio kuchekana tu na vitu tulivyo navyo, tuacheni umbea.


Pia inatubidi kuridhika na vitu tulivyo navyo si kutamani tamani vya wengine. Hivi ukiona mtu ana mafenicha ya nguvu wewe inakusaidia nini? au inakuongezea nini katika maisha yako? Samahani mimi sipendi kusagia, lakini napenda kuwajibu wale wanao toa maoni ya kukandia sana. Mimi nimefuata kilicho nileta si makochi au computer, au wengine wanasema kuwa ukiwa mpweke wakati nimetoa salamu, wanasema nini kilicho kupeleka huko Italy si urudi? Upweke uko wa aina nyingi, hata ukiwa TZ unaweza kuwa mpweke kwahiyo acheni hizo.


Pia tusisahau nyumbani tuliko toka, maana watu wengi wanajisahau sana, hao wanao sema hivyo unaweza kukuta wamesahau nyumbani na kukataa ma kwao, kwasababu ni kijijini au hawana fenicha nzuri na vitu vizuri vya kujionyesha, wanakata makwao, kwenu ni kwenu tuuu...!!!! Afadhali yangu mimi sioni aibu hata kama nina computer ya miaka 100 iliyo pita, hamna noma mimi ninafuraha sana kutuma salamu zangu na kutumia blog hii ya watanzania yenye mambo mazuri.


Hongera sana Bro.Michuzi kwa kuanzisha, mimi nitakupa hongera daima, ni jambo zuri. Hivi mbona tunabahati ya kupata maadili mazuri ya maisha kupitia kwa Mzee wetu Baba wa Taifa Mwl.J.K.Nyerere, kwa mifano yake mbalimbali hasa ile ya kimaisha, au hatuoni hilo? Baba yetu huyu ameishi maisha ya kawaida bila kupenda makuu, ambayo huna hata uwezo nayo. Yeye alikuwa mtu mkubwa wa kimataifa mbona hakuonyesha ufahari na kujidai kama sisi tunavyo taka?


Tufuate mfano wake tufanye kazi kwa bidii, tuacheni majungu majungu na unafiki usio tusaidia chochote, ili tujikomboe na haya maisha magumu tuliyo nayo. Na tuacheni mawazo ya kuota ndoto tu zisizo na maana, kujua kuwa ukiwa Ulaya basi umeukata lazima uwe na kila kitu cha thamani, hata wazungu wanahangaika kujikomboa na haya maisha, kwa kujituma kwa juhudi zote, Mwl.J.K alikuwa akiyasema kila siku tufanyeni kazi tuache mawazo tegemezi, ya kutegemea kama haya mawazo tunayo waza ukiwa ulaya basi umeukata, tufanyeni kaziiii.


Kuna mmoja alisema kuwa sisi tukumbuke tumekulia mikeka chimbuko letu ni hili, utake usitake huu ni ukweli, tena mimi naongeza tumekulia ngozi, babu yake na babu yako alikuwa na hayo mafenicha ya kifahari? lakini tunajifanya tunasahau, nimemsifu sana na amenifurahisha sana aliye toa maoni haya, kama una uwezo si wakwako? Pia tukumbuke mambo yote ya hapa duniani ni yakupita njia tu, ufahari wako utauacha hapa hapa duniani.
Basi fanya jambo zuri kusaidia na wengine sio kujidai tu nina nyumba nzuri makochi,computer, gari n.k, wakati nyumbani kwenu kijijini baba na mama wanasota, sasa hiyo ni nini? Huo ni Ufahari?


Mimi hapa nilipo ninajua mimi mwenyewe ni nini nilicho kifuata. Samahani sana kama nimewakwaza, ni haya niliyo kuwa nayo moyoni, na kuwajibuni maoni yenu, lakini ninapo andika hapa sijakasirika ni maoni tu, maana haina haja ya kukasirika na mambo haya.


UJUMBE: Tuacheni majungu, na tukaze mwendo kupigana na maendeleo yetu ya kila siku, bila kujari wengine watanisema. Hata kama wewe ni mbeba mabox kama wanavyo sema, hamna shida kazi ni kazi tu, tukaze uzi kusaka haya maisha, usijari!


Ni mimi yule yule wa siku zote.

BARAKA FRANCO CHIBIRITI

(CHIBATARI)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 62 mpaka sasa

  1. We michuzi huyo kibiriti ndugu yako nini? Mbona anaongea vitu vya jabu ajabu na unaendelea kumweka achafue screen!?! Achana naye

    ReplyDelete
  2. Hello Chibi,
    Pole kwa mashambulizi uliyopewa, imekusaidia kujijua.Lakini na wewe umewaweza.
    Mimi nadhani ingekuwa sawa kama wangesema jihadhari, imegundulika monitor za namna hiyo zinaua macho, au kiti cha namna hiyo kitakupa ugonjwa wa uti wa mgongo au kuwa unapoteza muda mwingi kusubiri PC yako iwake kwa kuwa speed yake ni ndogo, hivyo inakutia hasara, lakini kama wewe umekwishajitahidi kiti ukaweka mto baada ya kuona kinakuumiza na monitor umeweka screen kupunguza uharibifu wa macho, sioni taabu,wewe endelea kujitafutia maendeleo na wazee na ndugu wasilale na njaa, mdau wa Tandika kwa Mbonde yangu macho.

    ReplyDelete
  3. Umenena kweli Chibiriti. Hivyo ni mtazamo wa vijana wengi siku hizi Tanzania. Jamii yetu ya Tanzania imebadilika sana na kujaa ubinafsi, tamaa, majivuno na kujikweza. Hali hii ni tofauti sana na miaka 20 iliyopita, wakati Watanzania walikuwa wanasifika kwa utu, heshima na upendo wao. Vilevile vijana wengi wa siku hizi sidhani hata kama wanamfahamu JK Nyerere vizuri, licha ya fikra zake!

    ReplyDelete
  4. Tuesday, January 22, 2008 8:07:00 PM EAT
    Maneno hayo yanaambatana na utamaduni wa jela, utamaduni wa watu ambao hawana mwelekea au fikra za maisha...loosers!

    ReplyDelete
  5. Presha presha, presha ya nini!!! pale unapotoa mada na watu wakakukandia ndo utamu wenyewe wa mada!! usione soo kaka chibiriti, unapaswa ucheke tuu halafu uuchune, achana nao eti.

    ReplyDelete
  6. mimi sina matatizo na ulichonacho ila kama nyerere kakupa busara si ungebaki kwako bongo ,kwanini unakwenda nchi za watu kutafuta kilichokupeleka huko. wewe unaonekana mdogo hujapitia tabu za nyerere, watu walikuwa wanakamatwa barabarani na mgambo wakivaa jeans kama ulizovaa. nyerere kama alikuwa ana busara angewaendelezea wananchi demokrasia ambayo wakoloni walimkabidhi, pekua vitabu kuna chama kingine congress, kuna mtu alikuwa anaitwa zuberi mtemvu, alikuwa mpinzani wa nyerere,oscar kambona aliondoka nchi kwa sababu nyerere alitaka yeye pekee awe na madaraka. leo TZ watu wameamka wanaona ndani na nnje, watu hawatakubali kurudi nyuma tena, tatizo sasa ni ccm, in a normal country,people own the party but in TZ ccm owns the people/country. kila kitu kina mwisho, legacy mbovu ya mtakatifu nyerere na ufisadi wa ccm utatokomezwa.

    ReplyDelete
  7. Huyu Kiberiti, hivi ameendaje huko Ulaya? Makaratsi nini? Mbona anaongea kama vile ameingia mitini kwa trip ya kuletwa huko kama Rajab na yule binti?! Unaweza kukuta siyo raia wa TZ!?? Rudi home chibiriti wewe!

    ReplyDelete
  8. Bro michu,
    Huyu jamaa ni boya! Unajua hawa wabeba maboksi wakipiga picha na hizo raba za dola kumi na jeans za ''rugged store'' basi wanataka tuone kila mahali na wanadhani tuna shida sana. huyu jamaa hilo pozi lake ni la kijomba! jamaa anaonekana ni mjomba mjomba tu! Nashangaa analalamika nini kiasi hicho! wacha ushamba beba boksi tuma hela kwenu!Umepoteza muda kibao kuandika huo waraka wako wakati ungeshabeba boksi za kutosha!

    ReplyDelete
  9. To be honest umemind na umekasirika na umechukua muda sana kuamua kujibu hii mashambulizi ya vilaza ambao ni majority wa hii blog. Nakuquote hapa (si ilimladi inafanya kazi? Tena inakula mzigo si mchezo! Nyinyi mnatakaga vitu nje ya uwezo wenu sasa nini hii?) mwisho wa kuquote hivii ni ilimradi au ilimladi???? seems na wewe ni among vilaza ndio maan unatetea box ha! well sometimes wanakushtua kaka kuna easy note aka laptop achana na archival devices hizo nyingi huku zinatupwa na kuchukuliwa na huyu jamaa wa any junk. The fact ni kwamba ukufanya through search kujua clients wa hii blog. ndio maana ukaibuka na kupost tu na michuzi kwa vile wote mnatoka kusini akaamua... ila Blog hii kaka aina watu wema sana ingawa wanakuremind wit...but wanatakiwa wajue hata nchi kama hizi tulizo zilizoendea hata chaki bado inatumika nini computer ya zamani all over uk utakuta simu za zamani bado zipo ni kama sover....sometimes na well zina worth kiana tax za hapa si mnaziona lakini jamani. Anyway nakutakia kila la kheri kwenye nchi ya ruhswa na nagendo kama yetu uliyopo!

    ReplyDelete
  10. CHIBIRITI THANK YOU.WAPUMBAVU HUMU WENGI SANA,WE SUBIRI UONE HAWATOKUACHA KAMA SI LEO USIKU KESHO COMMENT ZITAMIMINIKA.YOU ARE BRAVE ENOUGH TO PUT YOUR PICTURE ON THE BLOG BUT THEM COWARDS BEHIND THE ANONYMOUS DISGUISE TRY TO PUT YOU DOWN.MUHIMU UNAJUA UNACHOKIFANYA MICHUZI ANA APPRECIATE WADAU KAMA NYINYI,ALITOA TANGAZO RASMI KWA WATOA SALAMU.BIG UP!!!

    ReplyDelete
  11. bwana chibi,
    mambo ni aje?
    umejielezaaaa we, lakini mi wala hujanikonvisi,kwa sababu hayo uliyosema ni sawa na anaesema kufa ni kufa tu!anasahau kuwa kufia agakhani na temeke hospitali ni vifo viwili tofauti!au kilimanjaro bia ya masaki na ya kinyantila zina ladha tofauti!
    hayo ya kukumbushia sijui baba wa nanihii alisemaje ndio yaliyotufanya tuzijue tiivii juzijuzi tu!
    bana mimi sikubaliani kabisa na wanaosema MONEY IS NOT EVERYTHING!,hao wanajipa komfort tu katika kuzoea shida,mbesa ndo kila kitu!ndio kilichokupeleka huko sisily sijui!

    ukisema vitu vya zamani vina bei ndio unamaanisha antique??ama?

    ReplyDelete
  12. jamani kwa wale mliomsagia mtoto wa watu mwacheni. wale mnaosagia furniture na computa yake labda nyie hamna hata mkeka wa kukalia. Ndio maana wabongo hatuendelei manake kazi yetu kusagiana tu. Get a life and mind your own business. Yeye alituma salamu nia yake sio kuwaonyesha furniture.

    ReplyDelete
  13. Chiriti mwanangu,mbona unanisaliti,mimi chikukutauma upamabane na watanjania wenjiyo.Chondechonde,ni jana tu tulikuwatunachubili chimu yako hukupiga,chacha wewe unabichana na umma.Uchauri mwanangu,kafanye kaji upate hela ununue vifaa vizuri.Muda wa malumbano mwanangu utarudi uso chini,kila mtu atakucheka,maana wenjio wanarudi na magari,na vifaa vijuri.Juzi tu tulienda mpokeamtoto wa jirani anaitwa Chihadale kaja na kompyuta flat screen,na viti vizuri sana,yeye chikuwahi kumwana akibisahana na umma, wa Tanzania kwenye hii blog,hivyo chondechonde nakutegemea uchauri wangu wa bure mwanagu Chibiriti uschije kuchekwa na jirani wote.

    ReplyDelete
  14. We Kibiriti, Ulaya hapo? Si kweli! Haiwezi kuwa Ulaya hapo hata kidogo! Yaani hivyo vibiriti na vibatari vyako humoi ndani vimejazana na kusongamana namna hiyo!!?! Wabeba mabox wakikuona, watakumaliza! Maana unawadhalilisha kwa kuonyesha hali halisi ya huko!

    Maneno yako yana ukweli ili hujui namna ya kuyauza! Yapangilie tu, wabeba mabox watacharuka ile mbovu, kama kawaida yao

    ReplyDelete
  15. Hey, Bro!

    You should have risen above that, and you should not have answered them.

    Mbona Obama the presidential hopeful of a very powerful nation on earth, his grandma lives in a very very modest life, most of us in here, would not dare to live Obama grandmas life.

    Kwa hiyo achana na hizo kashfa, makusudi yao ni wivu, chuki, husda na low life, nothing much to think better than their own life.

    Most of us, we are all coming from poor, modest background, probably our nun, our grandpa or our aunties , sisters and brothers are living a very hardship life, don't have even milk to feed their kids, IMAGINE that.

    So stop these nonsense and LOOK at yourself.

    ReplyDelete
  16. Yaani nakuunga mkono kaka yangu...Hizi tamaa na ufahali ndio unawatia watu pabaya. Kwa kutaka kujionyesha ndio maana watu wengi wanaishia kuiba na kuuza vitu visivyoruhusiwa kisheria na kuishia jela. Wewe ishi according na uwezo wako. Ukisikiliza ya watu utaishia pabaya, ambaye hajapenda furniture zako na computer yake, basi akutumie za fahari anazojua yeye.
    Kuna watoto yatima, na watu wana matatizo ya kila aina kwetu huko bongo. Hizo hela unazopata kama huna kazi nazo unaweza kumsaidia angalu mtoto mmoja na upate dhawabu kwa Mungu.
    Majungu hayajengi.

    ReplyDelete
  17. Bwana Kibiriti wala hata usijali maneno ya watu. Wewe fuata kilichokupeleka huko basi, mambo ya fenicha na nini achana nayo. Ishi ndani ya uwezo wako basi hao wengi wanaosema mafanicha ya argos sijui wapi wengi wana credit cards, wananunua hayo madudu kwa mkopo halafu jinsi consumption pattern ya huku ilivyo baada ya muda hayafai inabidi akabadilishe mengine. Sasa mtu unakuwa mtumwa wa vitu tuu kila siku.

    Ni kweli wengi wetu wazazi huko nyumbani wako hoi, wengine wanalala kwenye kiza totoro hawana uwezo wa kuweka umeme au kulipia hiyo bili. Wengine hata hela ya kula tabu, badala ya kuwatoa wazazi wetu kwenye shida tumekalia nguo, vitu na matanuzi ya club kila siku ili watu wanione. Picha nyingi zinazoletwa humu zinaonyeshaga matanuzi na kujikweza.

    Ndio kukua huko kifikra na mawazo wala maskadi yaliyotolewa yasikukondeshe ila yakusaidia kuona mbali, na yakusaidie kuona kuwa tuna priorities tofauti. Iwapo wewe priorities zako ni maisha ya huko home na wazee wako, wenzio priorities zao zimelalia kwingine. Hivyo kila mtu ni wajibu kuheshimu matakwa ya mtu mwingine.

    Namalizia kwa ujumbe ule ule wa mwanzo asili yetu ni mikeka na majavi kwa watu wa pwani na ngozi kwa watu wa bara. Tangu nimefika nchi hii nyumba nilizobahatika kutembelea sijaona ambayo mtu ameonyesha asili ya kwao japo kidogo. Hivi sie tuna haja ya kutafuta identity au kuwa na identity problem kama tusojua asili yetu? Au ni sawa kweli kuona aibu kuwa mwafrika au kuuonea aibu uafrika wako. Kwenye nyumba za wazungu waliotioka Afika utakuta vibuyu na mikeka na alama nyingine za asili ya mwafrika.

    ReplyDelete
  18. Wewe Franka Chibi wacha kulia lia kama mtoto wa kike. Sasa ulitaka hao wahjinga wajinga wasiseme ujinga wao? Mangu kaumba wajinga, sasa wewe kinachokuliza ni nini?

    Wewe nia yako ilikuwa ni kutuma salaaam, umefanikisha hilo kaaa kimya na move on!

    ReplyDelete
  19. nimependa sana jinsi ulivyowajibu waosha vinywa,wengi hawajui ulaya ni kwa kutafutia pesa tu ila maisha yapo huko nyumbani, yaani hapa ni kupata elimu bora na mtaji kwani tanzania bado kuna opportunities nyingi sana ukiwa na elimu nzuri na mtaji, tatizo jamaa wengi ni washamba wakifika ulaya wanajiona kama wapo peponi na kusahau home kabisa, kuna jamaa namjua, alikuwa akija likizo bongo anafikia hotelini kwa kuwa kwao choka mbaya na hakufanya juhudi yoyote kurekebisha,kama ulivyosema pigana kwa kila namna upate kilichokuleta, achana na waosha vinywa wanaoona kuishi ulaya na marekani ni deal kumbe hakuna chochote, kwani wengi wao hata shule hawaendi na wengine kila siku wapo first year miaka nenda rudi, cha msingi timiza malengo na ndoto zako, ukweli ni kwamba tupo wengi ambao haturahishwa na message za kukuponda, naona kama mwana jamii una haki zote za kutushirikisha mammbo mbalimbali ya huko italy,nakutakia kila ufheri katika maisha yako

    ReplyDelete
  20. Sasa wewe Kiberiti, sijui Kibatari sijui kitu gani (chagua jina linalokufaa hapo), Ni nini lakini jamani kutuandikia waraka mreeeefu huu unalalamika na kulia lia hadharani jamani?
    Kama ulijua unachokifanya na umeamua kuridhika na hali hiyo na eti hupendi umbeya, ni nini sasa kuja kusutana huku jamani mwanamme wewe? Si ungekaa kimya tukuone kweli mstaarabu na sisi wambeya, kulikoni kuja kusutana huku jamani?
    Kwani ni uongo vitu vyako feki, si ni kweli au we mwenyewe huvioni? Be honest chiberiti/chibatari. Badilikaga na mikao yako ya kihasara hasara hiyo. Na mambo ya kufikishia ndugu zako ujumbe kwamba ulaya hela ngumu kea ofu michuzo blog uache, vile hununui samani za maana, tafadhali tuma pesa nyingi nyumbani sawa?
    Usituchoshe tena na gazeti lako mwe! Kujaza tu ukurasa, sasa unalalamika tukuonee huruma ama tudanganye kwamba vitu vyako bomba na sio kweli.

    Rudi nyumbani wewe............

    ReplyDelete
  21. Achana nao hao wanasema wasiyoyajua! Kwanza nakupa hongera umerudi tena kwa vishindo na kutoa ukweli. Nimependa ulivyosema kuwa wengi wao wana tamaa na vitu wasivyoviweza. Bora wewe upo honest na roho yako and you are proud of what you have. Hao typical wabongo achana nao watakufa na mapressure yao wewe kaa na moyo huo huo. I wish ningejua upo maeneo gani Italy ningejipendekeza, wewe ndiyo mwanaume wa kweli sio wale wa magari ya kuazima and all that sh*t. BRAVO bro Chibiriti

    ReplyDelete
  22. We anon Tuesday, January 22, 2008 10:25:00 PM EAT shika adabu yako.

    ReplyDelete
  23. KAKA YANGU CHIBIRITI, ACHANA NAO HAO, WATU WENGINE SI UNAJUA WIVU TU UNAWASUMBUA, WASIKUUMIZE KICHWA WATU KAMA HAO, WEWE FANYA SHUGHULI ZAKO TU. JELOUS PEOPLE NEVER WIN AT ALL. ACHANA NAO KABISA, USIJISUMBUE KUJIBIZANA NAO. WANAFURAHISHA NAFSI ZAO TU, HAWANA LOLOTE. MWINGINE HATA PAKULALA HANA ANAKUKANDIA WEWE, SASA WANINI WATU KAMA HAO. TAKE IT EASY BRO!!!!!!

    ReplyDelete
  24. wewe dogo kibiriti unakera na nafikiri una matatizo ya akili. Usituchafulie blog na mada zako za kutetea fenicha mbovu na kumtetea Nyerere aliyetulostisha. Enzi hizo tuliokuja Italy lazima tuzamie meli bila passport. passport alikuwa nayo nyerere na kawawa tu! leo hii hadi nyie mambwiga mpo italy. enzi zetu za kuzamia tulikuwa tukituma picha hatujachoka hivyo. pamba za nguvu, raba mtoni, dereki na macheni...yaani wewe unaturudisha nyuma sana. Na nyie machoko mnaokandia box acheni ujinga...mimi nimejilipua na box kama kazi.wacha nikazi buti niwahi warehouse1

    Baharia wa zamani,
    Northampton.

    ReplyDelete
  25. CHIBIRITI,
    ULIYATAFUTA MWENYEWE:
    1) NANI ALIKUAMBIA UJIPENDEKEZE NA PICHA YAKO NA SAMANI ZILIZOCHOKA KWENYE BLOG? HUONI WENZIO WANAPIGA PICHA KWENYE CLUBS, KWENYE STENDI NK. ONA HATA MICHUZI MWENYEWE HAPIGI PICHA ZAKE UCHOCHORONI. HUPIGA MAGOROFANI, HATA KAMA HANA LAKE MWENYEWE.

    2) FENICHA (SAMANI) ZAKO HIZO NDIO GHALI? WEEEEE ACHA KUWADHAILISHA WATALIANO. WATAKUMALIZA. SISI FENICHA KAMA HIZO HUKU USA TUNAZIONA MADUKA YA "GOODWILL" NA MASHIRIKA YA ST. VINCENT AMBAKO WATU BINAFSI HUPELEKA KAMA MBADALA WA KUZITUPA. UNAWEZA KUKUTA VITU VOTE ULIVYONAVYO HAPO SEBULENI VINAGHARIMU DOLA 20 HADI 30. UKIENDA SIKU NZURI KOCHI LINAUZWA HADI DOLA 3 DIZAINI YA HAYO YAKO. KOMPYUTA KAMA HIZO UNAPEWA BURE.

    3) Afu umejifanya hujachukia wakati hata usoni umekunjana hivo? Hiyo raba umeinua ukidhani ndio ionekane zaidi? Mbona Bongo zipo kali zaidi.

    POLE MWANANGU........

    NYIE MNAOMSAPOTI HUYI CHIBIRITI MNAMDANGANYA NA KUMPOTOSHA. MPENI KITU "FACT".

    ReplyDelete
  26. WAPE WAPE VIDONGE VYAO WAKIMEZA WAKITEMA HIYO SHAURI ZAO.

    KAKA BARAKA Kwanza nakupa hongera kwa kuwambia hawa vinyaragosi yalioko moyoni mwako. Wallahi inaskitisha kuona watu tunapondana kwa vitu visivyo na maana. Kwani alowambia material things ndo kuishi ni nani? Nyie mnae msema huyu kaka msikute mlivyo navyo nyie hamja lipa adi leo mna madeni adi matakoni.

    Nyie mnakuja kumsema huyu kaka kuhusu vitu vyake nyie kwenu wanavyo? Ebu acheni zenu hizo. Asilimia kubwa watu nyie huko kwenu mnashida adi kwenye nywele lkn hamuwezi kusaidia wenzenu mnataka vitu vya kifahari. Kama huna kwa nini kujitesa ? Mwenyewe ameridhika kwa jinsi alivyo ebu acheni ujinga. Kama mnapesa sana badi jengeni makwenu msikae hapa kusimanga watu.

    Angalieni maisha ya kweni kisha njooni kusema ya wenzenu kwani half of you ppl here have nothing. Prolly your in internet cafey puttin down this brother, while he is at his place enjoyin himself.

    Stop actin like shity cuz material things don metter smh.

    Peace

    ReplyDelete
  27. Bro Chibi..achana nao watu wanakuonea wivu maana unatisha.

    Ila samahani naomba kukuuliza ka swali ila usikasirike.

    Hivi hapo nyuma ya kochi ulilokaa pembeni ya picha,naona kama DAWA YA MBU yakupulizia.Au ni mambo ya eya freshi.

    Kama ni dawa ya mbu pole sana na mbu wa hapo.Lazima malaria tuitokomeze...

    ReplyDelete
  28. Chiberiti au sijui inajiita chibatari, tatizo sio majungu ila unajitangaza sana, dunia nzima sasa inajua kwamba kuna mtanzania peke yake{kama ni kweli} anayeishi cesena Italy, haya umeendaendaje mpaka ukatua huo mji peke yako? kwanini usichague Rome, Naples, Milan, Florence au miji mingine ambayo ni mikubwa ambako huko kwahakika unaweza kukuta watanzania wenzako.
    Tatizo sio kwamba wanakutakia mabaya ila mjomba unajitangaza sana. naona ingekua vizuri ukaanzisha blog yako ili watu wakakujua kiundani na mji wa Cesena kwa ujumla.
    Mdau
    Holland

    ReplyDelete
  29. Mshagua Jembe simkulima wee... computer ina faa saana hiyo as long as it get your work done!

    ReplyDelete
  30. KWA UFUPI CHIBILITI POLE SANA KWA YALIYOKUKUTA! ILA LAZIMA UJUE KUWA HIZI NDIO GHARAMA ZA KUTAFUTA UMAARUFU, KWANI NI MUDA MREFU UMEKUWA UKITUMA PICHA ZAKO KWA MICHUZI ILI AZITUNDIKE HUMU KWENY BLOG, LAKINI UNAONEKANA NI MTU WA JAZBA NA HAUNA UVUMILIVU DHIDI YA MADONGO!
    poelmart5@yahoo.com

    ReplyDelete
  31. MICHUZI WEKA HII COMMENT KUKATA ZOGO LOTE.KWAKO MJOMBA KIBILITI MIMI NAISHI ULAYA NILIONA SALAMU ZAKO LAKINI SIKUTUMA COMMENT,NAPENDA KUKUFAHAMISHA KWAMBA WENGI WANOTUMA COMMENT ZA KUPONDA NA MAMBO YA KIPUUZI SIO TUNAOISHI ULAYA,NI WALALA HOI,SANA WALIOKO BONGO,KWANI WENGI WANATEGEMEA VITU VYA WAZAZI WAO WAPIGE NAVYO PICHA WATESE,WALIO BONGO WANAMACHUNGU NA WALIO ULAYA KWANI WANAJUA KAMA AWATUWEZI KWA LOLOTE,HATA WASEME TAMBALALE NI KUTAKA TURUDI TUKASOTE NAO,USIKU KUCHA WANAPANGA FOLENI ZA VIZA KUJA HUKU,HAPA MTONO UWE MBEBA BOX AU CHIZI WA KUTUPWA BADO WEWE NI TOP KWA MENEJA WA BANK BONGO,NA PIA SIO WOTE HUKU TUNABEBA BOX NATAKA LEO NIWAFAHAMISHE NYINYI WALALA HOI WA UWANJA WA FISI NA WEWE MICHUZI PIA,WENGINE SISI NI REALY NIGGERS NEVER DIE,GET RICH OR DIE TRYING,TUNACHEZA BAD GAMES NYINYI AMUWEZI KUPIMA KABISA,WATU WA SOUTH,KWA PELE,MAPUTO WANAJUA NASEMA NINI,NA SIO WIZI WA MAGALI KAMA MNAVYOTEGEME,KULENI KIMBA NA KAKA YENU MICHUZI.UKIONA COMMENT AZINA MAANA NI WALALAOI WA UWANJA WA FISI.SASA KWAKO KIBIRITI,USILETE HABARI ZA MCHONGA MENO HAPA KWANI WATOTO WADOGO KIBAO HAWAJUHI ALISEMA NINI,PIA USITAKE KUSEMA KAZI NI KAZI,HATA KUBEBA BOX,MIMI NAISHI ULAYA MIAKA KIBAO NIMEJENGA BONGO NYUMBA 4 ZA MAANA,NA BIASHARA ZANGU ZINAENDA NA SITAKI KUSIKIA KUBEBA BOX AU KUTUMWA NA MZUNGU HATA MARA MOJA,KUNA MABO KIBAO YA KUINGIZA PESA LAKINI UWE GOLLILA'G/UNIT KWELI SIO CHA MTOTO.HAPO ULIPO WEWE NIMETOKA KUKUSANYA 200,000 JANA.KUWA MWANAJESHI NA ACHANA YA NYERERE AJAKWAMBIA KUWA ZOBA,CHANGAMKA.MAKE MORE MONEY NIGER.NAMBA YANGU INAANZA NA 00316 TAFUTA UTAJUA NCHI GANI HIYO.

    ReplyDelete
  32. Tito, Boston, MA
    Tatizo ni wewe fala, mkulima na zumbukuku ambae unafikiri picha zako kutokea kwa Michuzi kila siku ni sifa. Unatakiwa utokee kwenye blog hii na kuraise concerns au mada zinazoleweka ili watu wapate kuzichangia mawazo, na sio kutuma salamu kila siku kutoka huko upande wa mashambani wa Italy. Unajua kabla ya kwenda kiwanja chochote unatakiwa angalau upate kuishi kwenye miji mikubwa kwanza huko nyumbani bongo. Maana haya ndio matatizo ya kutoka kijijini moja kwa moja kwenda ulaya. Hatutaki kuona sura yako tena kwenye hii blog, otherwise uwe na maana la kutuelezea sio salamu tu zisizo na mwisho.

    ReplyDelete
  33. CHAPA MZIGO MJOMBA,TUMA PESA ZA KUJENGA TUZILE.HATA MSINGI HUTA KUTA.

    ReplyDelete
  34. Nilitaka kuandika, lakini naona yaliyoandikwa yanatosha. Nimeishia kucheka na Computer.

    Far East.

    ReplyDelete
  35. chibi bado uko nyuma saana kimawazo .Wadau wamekupa kitu riale hapa kuwa mjomba umechoka na umeboili.Next time uwe makini kabla ya kujianika au unalazimisha ucerebrity kwenye globe ya Issa?
    Mdau, VA .Unyamwezini

    ReplyDelete
  36. Kibiriti unayosema ni kweli lakini stop posting your pictures humu so much....I know ladda ni raha ya kuwa nje ya nchi lakini kama unataka kuonyesha kila unachokiona huko fungua blog yako. At least kuwe na balance ya news hapa. Sio kila kukicha ni Casena, Italy....Ina bore ...Once is enough I guess

    Na barua refu hivyo ...wewe ukiweka picha kwenye blog ya Michuzi unategemea nini? Watu walipiga picha na majoho wakasemwa sembuse wewe...Take it easy....

    ReplyDelete
  37. Eti ulaya pa kutafuta maisha halafu bongo ndio unakula...mhhhhh I doubt about that...wengine watarudi bongo wakiwa above 60 yrs old sasa huko kula kiulani ni wao au wajukuu..???? Bwana balance muhimu katika maisha yako....ishi reasonable life ili uweze kusave na pia kuenjoy....sio kuishi ki junk junk tu ...Afadhali ungeishi kama waspanish wanaishi zaidi ya 20 kwenye four bedrooms house lakini mavitu yao utawawakoma. Hapa Shurti kwa 63 inches plasma, masorrounding sytems...top of the line things na magari ya nguvu wanaendesha tu....Lakini na huko kwao sio mchezo nilienda Costa rica na rafiki yangu nilishangaa mavitu yake....anasave kwenye rent lakini other things big time...Ila kama wewe unaenjoy kulala mwenyewe vizuri basi rent utalipa na vitu ndio hivyo utakua navyo....Au ndio ile law of utility satisfaction

    ReplyDelete
  38. kweli maneno yako wabongo kwa kutaka makuu ndo maana wanapokonywa majumba na magari wanakimbilia mambo hawayawezi kwa kutaka vitu vizuri hata mahari wanakwenda kukopa ukweni unamkopa mjomba wa mchumba wako ili ukaowe mtoto wa dada yake makubwaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa

    ReplyDelete
  39. Nakuomba bwana chibiriti usijibu chochote, humu kuna watu wa kila aina. utazidi kujipa presha mpaka utshangaa. usijichanganye kabisa. Bwana michu usipost tena mambo ya huyu bwana tunaweza kumpoteza. ni vizuri akae kimya watu wamsahau. aje tena mwezi december au january mwakani akiwa kwenye geto jipya angalau na flat screen.

    ReplyDelete
  40. Chib. wewe ni brave mpaka nafurahia ukweli ni kwamba wasikuzimishie karama yako, wanataka uogopeogope kisha uwe nyumanyuma. Be your self fanya kile unajiskia kufanya haijalishi inasomekaje mradi huvunji sheria.wahenga walisema kelele za mlango hazimzuii mwenye nyumba kulala.

    Madongo mengiiii mambo ya kitoto hayo kutambiana, wengine hivyo ulivyonavyo hawana, we umetoa salamu za upendo na umesomeka,kila mtu anataratibu na mpangilio wake wa maisha, kumbuka nyumba ya Fred Mwaur alitusalimu na tv zake mbili nzuri na furniture zake za thamani kumbuka waliyosema hata wewe ungeweka furniture za vile bado wangebonga tuu.

    ReplyDelete
  41. ukisoma haya maoni lazima utawapenda watanzania wote walioko bongo na nje, wana wingi wa utani uliojaa mzaha na mapenzi YA UNDUGU.

    hawana nia mbaya hata kidogo, na utani huu ndio ulioweza kutufikisha hapa KWENYE KUVUMILIANA, hii ni mpaka hapo hawa wachimba chumvi wachache wanaojiita wanasiasa watakapoamua kutuvuruga kama jirani zeru.

    NAWAPENDA WATANZANIA. WE ARE UNIQUE.

    ReplyDelete
  42. SO FUNNY!
    tanzanians we r like this!we like comments, but remember people who has wisdom talk less and constructive ideas, nilifanikiwa kwenda katika sherehe za xmass na mwaka mpya huko kijijini kwetu moshi, vijana wa siku hizi wameendelea saaana huku mjini na katika sherehe hizo waliweza kurudi vijijini kuwaona na wazee,wengi wao tulikwenda na magari binafsi (tulidrive) tena mazuri sana ila kichekesho kimekuja pale ambapo vijana hawa iliwabidi warudi town kulala hotelini, ukicheck home hakuna vitanda, nyumba hata hazijawekwa sakafu, kwanza parking na njia ya kuelekea nyumbani haipo,unapaki barabarani, then unakula teke kidogo ! ha haaaaaaaaaaaaa

    kila mtu ana malengo hasa kwa mtu mwenye akili timamu, uwe unasoma , unafanya kazi, inakubidi kuishi kwa mahesabu ili uweze kusaidia familia, kwani sisi watanzania wengi wetu tumezaliwa wengi katika familia hivyo ni lazima kupigana tafu,

    guys let us THINK BIG

    ReplyDelete
  43. Wewe Mr. Chibiriti.Naona unajaribu kutafuta publicity tuu.Hayo yaliyoandikwa na maoni ya watu,ungetaka yasiwepo,ungejikalia kimya.Usituletee ULIMBUKENI wako hapa,afterall huko ulipo ni bora ungejikalia kijijini kwako.Eti nawewe unataka kujiweka kwenye kundi la waliopanda ndege,nani kwanza akakujua?Kama unajaribu kutafuta kusikika.Mtafute brotha michuzi kwa muda wako ili aweze kukupa guidelines ya kuanzisha Blospot yako.Usitukoseshe raha bure huku kwa kujiandika na kutuwekea picha zako za ajabu ajabu.

    ReplyDelete
  44. We KP chukua tano hizo...!
    Umeongea jambo safi sana na mimi nimenigusa mno. Ndo maana napenda sana kutembelea blogs, especially hii hapa. Maana utakuta mawazo yote ya Watanzania yana-converge somewhere! Akiingia mtu ambaye siyo utagundua mara moja! Safi sana wabongo tuendelee namna hii hii miaka yote. Najua hakuna anayeweza kutuchomnganisha wenyewe kwa wenyewe au na sisi na wengine. Tuko safi sanaaaaaaaaaaaaaaaaa

    ReplyDelete
  45. bwana kaka wanaosema ni kweli umeboronga hata sisi tulio nje ya Tanzania nchi za kiujamaa hatuna computer kama yako.Sasa usijitetee kwamba huwezi kununua fenicha kwani nyumba si yako,KWANI UNAISHI WAPI?unakokaa hata kama hujajenga we ni kwako kaka mweeee!!! Nna imani unakosolewa ili ufanye kazi kwa bidii ubadilishe hiyo mandhari ya chumbani kwako!!!EUROPE HATULALI CHANGAMKA KIJANA ACHA KULALA

    ReplyDelete
  46. We Kibiriti.
    Huku kwa Michuzi, wanaoposti mitundiko yao huwa hawajibugi.
    Kama unataka kujibujibu peleka mtundiko wako kule kwenye bulogi ya Maggid Mjengwa, huko ndio kuna kujibujibu. sio humu. Sawa?

    ReplyDelete
  47. CHIBILITY TAFADHALI NITUMIE EMAIL YAKO KWA tgeofrey@yahoo.com i will give you some thing for you pls do it with high agence importance. (aka) Prof Dr Ing TUMAINI GEOFREY TEMU

    ReplyDelete
  48. We Chibiliti kweli ni Kijinga-cha- Moto au Mwenge. Maana unatuonyesha hali halisi ya mapambano ya kimaisha Ughaibuni. Tulio wengi tunawadanganya walio nyumbani TZ kuwa tunaweza kufanya mambo makubwa TZ tukitanua ughaibuni.
    Lakini ili iweze kujenga nyumba nzuri au kuwa na magari mzuri kwa fedha za msoto ulaya/marekani inabidi uishi kama kaka Chibiriti.
    Wote mnaotuona tunajenga na kusomesha wadogo zetu kutokana na fedha za ughaibuni, tunalala wanne chumba kimoja, hatuna TV za flat screen na kuvaa jeans za paundi £5.
    Hongera kwa kuwa muwazi na maisha yako ulaya/marekani.
    Mdau
    Uswahilini(Hackney) East London London

    ReplyDelete
  49. Mbona kazi unayo kaka na dawa yako ya mbu hapo pembei maana Italy mbu kama bongo was there for holiday mh!

    ReplyDelete
  50. Nimesoma kwa masikitiko jinsi watu wanavyotuma comments za kashfa na matusi, sasa kama jamaa kachemsha si inabidi kumwambia tu kwa lugha ya staha? badala ya kumporomoshea mimatusi na kashfa, kusema kweli si watu wote waishio majuu hali zao ziko poa, mimi binafsi naishi UK na naongea through experience kuna watu wako hapa mambo yao yame 'KITA' kwa hivo jamaa huo ndo uwezo wake msimlazimishe kuishi ka tajiri wakati hajafikia hali hiyo pili kama unaboreka na picha za jamaa waweza skip na kuangalia picha nyingine, sina zaidi lakini at the end of the day sisi sote ni ndugu, TUWE NA UMOJA

    ReplyDelete
  51. Yaani wewe uliyeandika una nyumba 4 so what kama una nyumba 4, halafu unaponda walala hoi, hawakutaka kuwa ktk hali waliyopo, we bwege kweli, mbona wewe uliondoka home, wat bwana mkipata kidogo basi unajiona babu kubwaaaa, nenda kainvest home, inua maisha ya watu tukuone wa maana, so far nakuona fala, majigambo ya kijinga, mshamba fulani. GET REAL PEOPLE, DONT FORGET WHERE U CAME FROM. TWAT!!!!!

    ReplyDelete
  52. Achana naye huyo! Nyumba nne mtu yoyote anaweza kuwa nazo. Inategemeana unamaanisha nini kwa kuwa na nyumba nne. Nyumba inaweza kuwa sehemu ya kupumzika tu.

    Kuna nyumba bwana. Kama kweli unazo unafanya nini uko uliko?! Acha kuota mchana mchana wewe

    ReplyDelete
  53. mhhh, Baraka Franco Chibiriti, aka Chibatari! Wacha wewe! Kazi kweli kweli hii dunia

    ReplyDelete
  54. HATA MIMI NILIKUWA NA NYUMBA NZURI HUKO MISSOURI INGAWA BAFU LANGU FUNZA WALIKUWA WENGI. MZEE WEWE MGUMU SANA UNGEFUTA MAVI KAMA MIMI SIJUI UNGEAMBIWAJE. POA CHIBILITI NIKO BONGO UKIJA TUTAFUTANE BASI. UNAMCHUMBA? BASI POA!

    ReplyDelete
  55. Huyu Chibatali sijui kibiriti hana lolote, anataka kuoneysha wale washamba wenzake huko Bongo kuwa yuko Ulaya tuu, mtu gani una jitoa picha kila wakati?

    Ukimwangalia tuukwangu unajua kabisa huyo ni mtu wa aina gani, miminamuona ni mshamba probably a geek ambaye amefika Ulaya na katoka sehemu masikini au ni mshamba tuu.

    Sijaona mjanja yeyote akapiga picha na kupost humu na awe anamnekana wa kishamba kama huyu , nadhani kapeleka nasrikali ya Kijiji kuja kusoma Ulaya.

    Nakushauri next time t piga picha ngalau uonyeshe sexy body labda unaunalo ukivua shati , maana sura huna ya kuoneysha kama ulitaka kuuza sura.

    ReplyDelete
  56. ooooh boy! this so funny!
    mko wapi watu wangu!
    chibiriiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiti weweeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee!

    ReplyDelete
  57. Kuchamba kwingi,kuondoka na mavi.Leave well alone! You wont improve matters by going on tinkering

    ReplyDelete
  58. KATIKA BLOG HII WENGI UNASOMA WANAANDIKA MAMBO YA KISHAMBA TU NA UJINGA MTUPU. HIVI MTU UNA AKILI YAKO BADALA YA KUCHANGIA MJADALA UNATUELEZA UNA NYUMBA 4. WHAT DO YOU MEAN? LEAVE US ALONE. DON'T POST YOUR SHIT STUFF HERE. KILA ANAYECHANGIA ANGESEMA ANAMILIKI NINI WEWE UNGEJIONA HUNA NYUMBA. NYUMBA INAWEZA KUWA KIBANDA NAWE UNAITA NYUMBA.

    HATA "MANSION" NI NYUMBA.
    NA PIA VIBANDA NI NYUMBA.
    UNGEKUWA NA NYUMBA 4 UNGEKUWA UNASOTA NJE YA TANZANIA? LABDA UNIAMBIE UKO HUKO SABABU HUWEZI KUACHA KAZI YAKO KAMA YA UBLOZI NK.

    NANI ASIYEJUA MAISHA YA NJE AU ULAYA???
    MLIOKO TZ, NAWAAMBIA MIMI NILIYEPO HAPA KWA BUSH, MAISHA NI POPOTE. TANZANIA UNAWEZA KUFANYA VIZURI KULIKO HAWA WANAOJIFANYA WANATAFUTA NJE. UZUSHI MTUPU.

    KAMA KWELI WANA HELA, KWANINI WASIRUDI JAPO KILA KRISMAS, EID, PASAKA, MWAKA MPYA KULA SIKUKUU NA FAMILIA ZAO????? WASIWADANGANYE KITU HAWA. HAWANA KITU.

    MAISHA YA NJE YA TZ SEHEMU KUBWA NI YA KUPATA HELA NYINGI, NA KUTUMIA KAMA VILE KESHO HUTAISHI. FIKIRIA MTU ANAPEWA "TICKET" AU ADHABU YA KULIPA DOLA 2000 SABABU YA KUKATISHA KWENYE TAA ZA NJANO, KATI YA NYEKUNDU NA KIJANI.

    NINA UZOEFU WA KUTOSHA. KWA MLIOISHI USA, MNAJUA. WATAFITI WANASEMA HAMNA NCHI DUNIANI YENYE SHERIA NA TARATIBU NYINGI NA SHERIA KAMA USA. NA HII INATOKANA NA MAENDELEO YA TEKNOLOJIA NA ONGEZEKO LA WATU TOKA MATAIFA YOTE DUNIANI.

    THIS IS A MELTING POT, MAN!

    HAYA WABONGO ENDELEZENI LIBENEKE LA MAJADILIANO NA KUPONDANA.

    MDAU,

    STATES.

    ReplyDelete
  59. ai wewe chibiriti hivi nakuuliza hapo unapata usingizi kweli hivi panalalika hapo jamani wewe una lako jambo hivi naomba unijibu hivi hujawahi kujiuliza kwa nini wanawake wanakukataa haswaa ukiwaleta kwako basi hata kama huna uwezo jaribu kuwa organize ndugu yangu acha uchafu lo!!!!!!!!!! tia polish hizo mbao na weka vitu in order hata wewe utakipenda chumba chako usiwe hivyo ngugu yangu acha masifa.

    ReplyDelete
  60. da pole sana Chibiriti hope u hav learn a lesson from people's comments mimi nakushauri ujipige soap halafu mambo yakiwa mdebwedo u-post tena picha yako, nabonyeza bonyeee kuweka msisitizo........Ta ra for now

    ReplyDelete
  61. hivi chiberiti unatoka wapi?unaongea kama maboksi yamekuzidia! si urudi home tu madingi wanahitaji msaada wako,kondoo wanatoroka zizi kila siku dingi anachanganyikiwa.

    ReplyDelete
  62. jamani Chibiriti anataka kugombea mwenyekiti wa kijiji chao ndio maana amekula redio!!!!! anajifanya tu lakini kchwa kimemzidia maboksi,rudu home bwana usitutie aibu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...