hii ni picha ya baadhi baadhi ya mashujaa walioshiriki kwenye mapinduzi ya zanzibar ya kuntoa mkuku sultani na kutwaa nchi. toka shoto saidi iddi bavuai, hamisi hemedi nyuni, abdullah natepe, pili khamis, abeid amani karume, seif bakari, hemedi ameir na hafidh suleiman

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Okello mbona hayupo kwenye picha?

    ReplyDelete
  2. Acha uwongo michuzi, mapinduzi ya zanzibar hayakumtowa madarakani sultani, ni uzushi na ujinga uliopandikizwa vichwani mwa watanzania. Mapinduzi ya mwaka 1964 january, yaliyoongizwa na John Okelo chini ya mabri ya Abeid Karume yalikuwa ni mapinduzi ya kumtowa madarakani MPEMBA (Mohamed Shamte), hakukuwa na muarabu madarakani wakati huo, rejea historia ya zanzibar vizuri(tafuta kitabu kinaitwa 'ukweli ndo huu'). Mwandishi mwenye mwamko kama wewe hata kama ni miongoni mwao (CCM) lakini hutakiwi kuipindisha historia kwani muda wakusema njano ni nyekundu na nyeupe ni nyeusi umekwisha. Sasa "Liite pauro kuwa ni pauro usiseme ni kijiko kikubwa" USIBANIE HII COMMENT

    ReplyDelete
  3. sahihisho:
    isomeke yaliyoongozwa na si venginevyo, na isomeke ambri (sio mabri)
    ahsanteni

    ReplyDelete
  4. Haijalishi hata kama alimtoa mpemba wote sawa ilhali aliingia madarakani Black mpingo tunawasifu wote waliowandoa hao."Africa is for Africa, Black African".Hao sijui wapemba au waarab this is not there country.Big up KARUME,OKELLO and all wanamapinduzi.
    Dont get me wrong,africa ni nchi ya watu weusi.

    ReplyDelete
  5. sasa kilichomkimbiza Sultani Jamshid nini? haya basi tuseme Mapinduzi yaliyomtoa Mpemba Mohamed Shamte, na Sultani Muarabu Jamshid.

    Okello naye alipinduliwa kwa kukamatwa uwanja wa ndege daresalamu. baadaye alihamishiwa uganda ambako Iddi Amini Dada alikuja "kumshughulikia."

    ReplyDelete
  6. cha chandu london..

    Since when is Africa a country??

    ReplyDelete
  7. Michuzi! Kati ya hao wana mapinduzi nani yupo hai na nani katangulia mbele ya haki? Habari nilizonazo wkt wa mapinduzi Karume alikuwa Dar, aliletwa na mashua kuja kupewa madaraka na amewatosa mashikaji wote hao, leo hii hao jamaa familia zao zina hali ngumu sana.....tunajivunia nini juu ya hawa wanamapinduzi?????

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...