Mjumbe wa Kamati ya Madini Zito Kabwe, ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini akiondolewa na askari wa Kituo cha Mererani baada ya wachimbaji wadogo wa madini ya Tanzanite kutaka kumvamia wakitaka kumbeba na kumshangilia muda mfupi baada ya Kamati hiyo inayoongozwa na Jaji Mark Bomani kusikiliza maoni ya wananchi leo asubuhi kama alivyoshuhudia mdau paul sarwatt

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. na hivi anapenda sifa yeye na mr misifa dully hawana tofauti. ila sishangai umri bado mdogo na kesha iba kama majority wa bongo na anajua wenzake wanaiba vipi

    ReplyDelete
  2. Yule apigae kelele sana mpatie yeye kazi ya kunyamazisha maana akinyamaza yeye wengine wote watafuata. Michu, naomba ukumbuke msemo huo JK anajua anafanya nini na kwakweli kwa saikolojia hiyo namsifu. Pia ni swala la muda tu utasikia utasikia kijana Heavy kahamia CCM. We pozi uone mambo .....

    ReplyDelete
  3. hapo mererani ndio tanzanite inapotoroshwa kinyemela kiasi cha kufanya nchi zingine ndio zinafaidika na tanzanite kuliko sisi wenyewe.lazima tanzanite ifanyiwe kazi hili hiweze kutusaidia wananchi.

    ReplyDelete
  4. kusema kweli nchi inahitaji vijana kama hawa wenye kusema ukweli hata pale ambapo bunge letu(tukufu?????) linaposema waongo na wazushi. Spika na wewe nenda huko ukasema tena kwamba zitto ni muongo uone utakavyozomewa. Hivi jamani na kampeni ile iliyofanyika nchi nzima kwa ajili ya kuwaambia wananchi uongo wa zitto nao mheshimiwa sana na mtukuka rais wetu JK anasemaje?

    ReplyDelete
  5. Dress code jamani kwa wabunge hamna! huyu ikipigwa kelele ya mwizi si anakamatwa! nilipoona hiyo picha na police nilidhani kibaka anapelekwa central! hahaha, michuzi usiibanie, zito inabidi uanze kuvaa kama mbunge!

    ReplyDelete
  6. Wewe mdau hapo juu, unafikiri dress code ni kila mahali, usiwe mjinga...kama ulishawahi kufika mererani ndo utajua kwanini zitto amevaa hivyo...usiige tu mambo ya nje

    ReplyDelete
  7. Huyo Anony kweli ni mshamba! Huyo ni mbunge wa watanzania na yuko nje ya Bunge, kwa watanzania wavuja jasho! Ulitegemea avae jumba??
    Naungana na aliyetoa usemi kwamba 'Mchawi mpe mwana alee' teh teeehh JK mjanja!? Lakini mwisho wa yote tunataka maisha bora kwa watanzania sio malumbano ya kisiasa

    ReplyDelete
  8. huyo wa dress code mjinga sana na hajamuona Zitto kwani ni kijana anayevaa vizuri kupindukia. habari ya dress code isiwaweweshe nyie mliyo ng'ambo

    ReplyDelete
  9. We annoy 8.46 na 8.51 acheni comments za kijinga! mtu yeyote anapofanya jambo jema ni budi asifiwe, na hakuna asiyependa kusifiwa kwa jambo zuri! sifa kwa jambo zuri ni sense ya respect na appreciation! zito huwezi kumlinganisha na dully!!kama wewe una akili timamu!

    Lakini ni upuuzi kufikiri kwmb ipo siku zito atahamia ccm! ni upuuzi na ujinga kufikiri kw wote wanaotetea maslahi ya umma nao wataishia kuiba!!

    Wala kikwete hafikirii ujinga huo unaowaza wewe! kamteua zito kwenye kamati ili atoe mchango ktk kunusuru sekta ya madini!! sio huo ujinga unaowaza wewe, Nawaomba watanzania tutumie vyema majukwaa haya kwa kutoa maoni chanya yenye kujenga nchi yetu! ni ujinga kutumia muda wako kutoa comments za kukatisha tamaa na kuponda watu! bora utumie muda huo kulala nyumbani!!

    ReplyDelete
  10. Napinga wanaomsema Zitto vibaya.Ye alikubali kutolewa kafara kwa ajili ya maslahi ya Tanzania,tumuunge mkono.Kushangiliwa kwake ni ishara kuwa wanamuamini na hiyo ni changamoto kwake,naamini anafanya kazi yake vizuri.Acheni mawazo ya kumsemea mtu ati anatumiwa au kuingia CCM,huo ni upuuzi.

    ReplyDelete
  11. hivi watanzania mbona tunapenda kutoa sifa za kijinga jinga kila mara moja ya kazi za wabunge na viongozi wengine ni kuweka bayana mambo ambayo yatokeayo aidha kusahihisha yale yanayokosewa na serikali na kupongeza mazuri yafanywayo na serikali sasa kitendo alichokifanya Zito Kabwe ni moja ya kazi zake alizotumwa na wananchi waliomchagua huko kwao kigoma pongezi hizo mnapaswa kuwapa wananchi wa kigoma na siyo kabwe alichokisema si kipya masikioni mwa watu wengi wenye upeo lakini kwa wasio na upeo ndio wanatoa sifa zisizofanana na yeye kwangu mimi sioni jambo lolote la maana sana alilolifanya zito,pili mererani nivyopajua mimi mwenzie ni jens na fulana na sio kama alivyovaa yeye jamaa hajui kuvaa nilishaona siku moja ktk blog hii kavaa kasuti ka ajabu sana utadhani chale champlin,tatu wananchi tuache kufagilia mambo ya kijinga watendaji kazi wapo wengi nchini na hawasifiwi ,napenda kuwaambieni hizi ni kazi zao viongozi hakuna haja ya kuwapa misifa mingi mrema nae anataka tumjengee mnara kwa vile nae ni shujaa wa kutoa mabomu hii ni akili kweli kumbukeni wapo wananchi wanaotoa taarifa nzuri za kusaidia nchi nao wajengewe minara?

    ReplyDelete
  12. kweli anapenda sifa sana si mtu wa kigoma yule

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...