MARA TU BAADA YA DK. MSABAHA KUKETI SPIKA AMEMPA UKUMBI DK SLAA AMBAYE NDIYO ANACHANGIA SASA, AKIANZA KUSOMA VIFUNGU VYA SHERIA VYA KATIBA.
ANAMSIFU MH. LOWASSA KWA KUAMUA KUOMBA KUKAA KANDO JAPO HAKUNA USHAHIDI KWAMBA ANAHUSIKA, ILA IMEBIDI AWAJIBIKE KWA VILE NI MSIMAMIZI MKUU WA SHUGHULI ZA SERIKALI
AMESEMA USHAHIDI NI MWINGI KWAMBA RICHMOND NI KAMPUNI TAPELI NA ANADAI ANA UHAKIKA BARAZA ZIMA LA MAWAZIRI LINAJUA HILO NA KWAMBA KAMPUNI HIYO ILIPEWA TENDA WAKATI HAIJASAJILIWA.
AMETAKA WAZIRI MKUU NA BARAZA LAKE LOTE WAWAJIBIKE KWA KUSHINDWA KUSIMAMIA SHUGHULI ZAKE KUHUSIANA NA ZABUNI.
AMETAKA PIA TANESCO IPONGEZWE KWA KUIARIFU SERIKALI KWAMBA ZABUNI IMEKWENDA KINYUME LAKINI BARUA ZAKE ZOTE HAZIKUJIBIWA. UWAJIBIKAJI NI MAWAZIRI NA MAKATIBU WAKUU WA WIZARA HUSIKA ZOTE.
AMEOMBA KILA ANAYEHUSIKA AWE MNYOFU NA KWAMBA UCHUNGUZI WA KINA UFANYIKE ILI KUJUA NINI KILITOKEA KWANI DILI LOTE LINANUKIA RUSHWA.
Du!
ReplyDeleteMichuzi hii kali kwa kweli!
Mbona mambo moto!
Kifungu cha Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 57 (2)(e) WAZIRI MKUU anapojiuzulu ni kuwa SERIKALI NZIMA inajiuzulu kwa hiyo Baraza la Mawaziri linatakiwa kuvunjwa na Kuundwa tena. Kwani Serikali haina kiongozi Bungeni.Sasa naona mjadala bado unaendelea kivipi?
ReplyDeleteMichuzi, hata mimi nashangaa kuona Bunge linaendelea wakati Mkuu na kiongozi wa Bunge amejiuzuru.Sasa nani anasimamia hilo Bunge? Ningewaomba Mawaziri wengine wanaosimamia shughuli za Serikali wamwige kiongozi wao ili kumrahisishia Rais kufanya maamuzi.
ReplyDeletemzee wangu slaa tunawapongeza ujasiri wenu, mimi nilikuwa najua tuu haya mambo ya serikali hii ya ccm wanayoyafanya yatakuja kuwa na mwisho wake, sasa cha kushangaza hawa wabunge wa ccm na viongozi wa serikali wa ccm walikuwa wanajua kinachoendelea halafu wakawa wanakaa kimya, mpaka kina zitto walivo anza kushikia bango na mambo kuwa hadharani ndo wanajifanya nao wako mstari wa mbele kuwakosoa kin lowasa, mi nasema hata hao wabunge wa ccm wananuka rushwa.. wanafki tu..
ReplyDelete