MBUNIFU wa mavazi wa muda mrefu Fatma Amour anatarajia kufanya onyesho la mavazi aliloliita Fastive Collection katika kusherehekea siku kuu ya Wanawake duniani.
Onesho hilo lililopangwa kufanyika tarehe 8 Machi, 2008 kwenye ukumbi wa Movienpick limeandaliwa mahsusi kusherehekea siku kuu wa wanawake duniani ambayo ilishajiishwa na wanawake wafanyakazi na ilianza kuandaliwa kama siku rasmi ya kimataifa na Klara Zetkin wa Ujerumani mwaka 1911 imekua ikiadhimishwa kila tarehe 8 Machi.
Asili ya siku hiyo hasa ni kupigania haki za wanawake na imeendelea kuadhimishwa kuwa ni siku ya wanawake duniani kwa kuwakumbuka wanawake waliotoa mchango mkubwa wa kimaendeleo.
"Wanawake wenzangu waliopambana na mfumo dume bila woga, wanawake waliosimamia misingi ya amani, umoja na upendo, Yapo mengi yanayowakabili wanawake duniani, hayo ndiyo yanayoibuliwa katika siku hii inayoadhimishwa kimataifa ingawa kila nchi inaweza kuwa na kauli mbiu yake kutegemeana na changamoto zilizomo ndani ya nchi husika, mimi nimeona ni adhimishe kwa kuonyesha ubunifu wangu kama changamoto ya kuonyesha wanawake wenzangu kuwa inawezekana," alisema. Alisema/
Onyesho hilo ambalo ni la kwanza kuadhimishwa mwaka huu Ujumbe wake ni “Salute to Womanhood” Akiangalia role ya mwanamke katika jamii yetu kama mama, kama mke na kama mfanyakazi.
Alisema onyesho hilo litapambwa na burudani safi kutoka kwa wanamuziki kama Unique sisterz na wengine na kuongeza kuwa Tiketi zitakuwa zinapatikana kwa shilingi 20000/- tu, na kila atakaye nunua tiketi atajipatia kopi moja ya jarida la Excel BURE.
"Tiketi zinapatikana Movienpick, Shoppers Plaza, Sea Cliff Village, Best Bite, J mall- Famozo, Mlimani City na Famour Design Kinondoni karibu na sheli ya Bonjuor (opp THT)" alisema.
Onyesho hilo limedhaminiwa na Redds Premium Cold ambao ndio wadhamini wakuu, Jarida la Excel, Dollywood Tanzania Ltd, Sofia Records, Vayle Spring, JD Entertainment, Wilna International, C2C, Clouds FM na Erick Amtallah Saloon.
THANK YOU FOR SURPOTING FASHION INDUSTRY IN TANZANIA.
(MADE IN TZ)
MUCH APPRECIATED.
THANK YOU.
Hivi neno sahihi hapa ni nini babu Michuzi; ONYESHO au ONESHO? Maneno haya yananipa kigugumizi napoyasoma katika habari moja
ReplyDeletekweli mtu wangu hta mie huwa nasjaaabu hapo maana hayo maneneo sijui iankuwaje hapo.
ReplyDeletena pia nakupongeza designer mwenzangu fatma kwa kupiga hatuaa fulani ingawa niko mbali kidogo nawe lakini usijali tuko bege kwa bega na isha allah mungu atajali tu!
haji designer
Neno sahihi hapo wadau ni ONESHO NA SIO ONYESHO kwani root ni ONA wakati neno ONYESHO root yake ni ONYA.Hii ni kwa mujibu wa Gwiji la kiswahili Mzee Ruksa. Atakubaliana akiona hili maana nimeambiwa mara nyingi tuko naye humu.
ReplyDeletedear famour designer hongera sana kwa kufika hatuwa hii kwani mwanzo ni mgumm na nakupa hongera sana kwa kujituna na kufanikisha zowezi hilo kila la kheri mama
ReplyDeletetunaitaji mwanawake wenye kujituma kama wewe tunakuombea, na nitakuja kukusaport usikate tamaa fatma
ReplyDeletejamanai tuwe tunawapa moyo mabinti wanaojituma, kwani ndio kuendeleza taifa ivyo kwa mambo ya talent pia.
ReplyDelete