
Matangazo ya Tanzania kuanza kuonekana kwenye mabasi ya London, Heathrow Airport
Habari na www.tanzaniaone.co.uk
KUANZIA wiki ijayo Serikali ya Tanzania itazindua mpango wa kuitangaza Tanzania kwa kuweka matangazo yake kwenye mabasi ya abiria na uwanja maarufu wa ndege wa Heathrow.
Mpango huo utakuwa wa miezi sita.Kwa mujibu wa barua za mwaliko kwenda kwenye vyombo mbalimbali vya habari hapa Uingereza, zilizosambazwa na kampuni ya Jambo Publication inayoratibu matangazo hayo ilisema uzinduzi huo utafanyika katika ubalozi wa Tanzania uliopo Bond Street, katikati ya jiji la London.
Taarifa hiyo ilisema mgeni rasmi katika uzinduzi huo atakuwa Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Mwanaidi Maajar, lakini pia Wizara ya Utalii itawakilishwa na Katibu Mkuu, Blandina Nyoni na maofisa kutoka Bodi ya Utalii Tanzania (TTB).
Taarifa ilisema uzinduzi huo utakuwa matangazo manne yatakayokuwa katika sehemu ya kuchukulia mizigo na inatarajiwa kwamba watu milioni 4.6 watayaona wakati kampeni hiyo itakapokamilika.
Sehemu hiyo ipo karibu na idara ya uhamiaji ambayo abiria wanaweza kuyaona matangazo hayo hata wakiwa sehemu ya uhamiaji, jambo ambalo linaweza kuleta mvuto mkubwa kwa watumiaji wa uwanja huo. Mbali na Heathrow, pia katikati ya London kutakuwa na mabasi 100 yatakayokuwa na matangazo hayo na inakadiriwa zaidi ya watu milioni 30 watakuwa wakiyaona kila wiki.
Matangazo hayo yatakuwa yakionyesha mlima Kilimanjaro, Simba, Swala, Chui na Tembo anuani ya mtandao wa TTB na Wizara ya Utalii, huku yakiwa na maneno The Land of Kilimanjaro and Zanzibar, Discover the wonders of the world na Have you been there?
Mwaka ujao wa fedha kuna uwezekano mkubwa kuweka matangazo kwenye treni za chini ya ardhi na kwenye viwanja vingine vikubwa vya ndege vya Gatwick, Manchester na Birmingham.
Kampuni ya Jambo ndiyo inayochapisha jarida la Jambo Tanzania linalosambazwa katika balozi mbalimbali za Tanzania.
SIO KUTAKA MSIFATU HAMJASEMA NI FEDHA KIAI GANI ZA WALE MASIKINI WALALAHOI ZITATUMIKA? KWANI INJI HIIHAINA BUREEE, WANDUGU
ReplyDeleteBro michuzi hii imetulia big up sana wabongo haya ndio mambo tunataka kusikia.
ReplyDeleteWatanzania kwa kulalamika kweli angalia huyo hapo juu yaani watu kuridhika ni ngumu sana si bure mnabaki masikini.anyway wamefanya la maana halafu wangejaribu kufanya kama wenzetu wa kenya kutengeneza documentary ziwekwe sana kwenye Discovery channel najua ziko lakini chache sana natujaribu kutengeneza wenyewe zaidi.tutumie vitu kama Tanzanite yetu kazini kwetu kuna mama ameolewa last month pete yake ya engagement ilikuwa Tanzanite nzuri nimeona watu watu wanavaa lakini tutafika tu inshallah
ReplyDeleteANON WA 11:07PM DAWA YA UGONJWA WAKO HAIPO,HAYA NI MAMBO AMBAYO KILA MTANZANIA ANATAKIWA AFURAHIE SIO KULALAMIKA.HONGERENI MLIOKUJA NA HII IDEA,PICHA INAVUTIA SANA.MUHIMU NI KU CONTROL MAFISADI WALIO NYUMBANI,KUNA TABIA YA MA TAXI DRIVERS KUIBIA WAGENI KWA KUTOKUJUA BEI HII TABIA INGETAFUTIWA DAWA,NI AIBU NA BADALA YA KUONYESHA UKARIMU NA AMANI YETU TUNAONYESHA UJAMBAZI WETU KWA VILE TUNA NJAA AU SERIKALI INGE ANZISHA SYSTEM YA KU CONTROL TRANSPORT KWA AJILI YA WAGENI WANAO KUJA KUTEMBELEA NCHI YETU.
ReplyDeleteThis comment has been removed by a blog administrator.
ReplyDeleteAna umwa ugonjwa wa kulalama huyo anony wa kwanza, sijui analalamikia nini wakati biashara ni matangazo. Walivyokuwa hawajatangaza kila siku ilikuwa ooh ona Kenya wanatangaza mlima Kilimanjaro uko kwao nyie mmekaa kimya! Wanatangaza tena mnalalamika ooh mnatangaza mnataka misifa sijui hakuna bure. Hata wangetangaza Dar pia wasingetangaza bure. Sijui huko Dar wangmtanganzia nani wakati asilimia zaidi ya kumi ya watalii wanatoka UK. Na utalii ni sekta ambayo ikiimarishwa inaingiza pesa nyingi kwa Taifa. Nchi mbali mbali uchumi wao kwa sehemu kubwa unategemea utalii na watalii ni hao hao inabidi tugawane, badala ya kwenda Maldives, Tunisia, Thailand basi waje kwetu Tanzania watu mnaanza kupiga kelele, sijui watu wengine wana matatizo gani? Shule jamani nendeni shule! Msikalie kublogu tu humu mtachekesha!
ReplyDeleteSidhani kama hapa Uholanzi kuna ubalozi wa Bongo.Licha ya kwamba uholanzi inatoa watalii wengi bongo ila wadachi wengi zaidi wanajua Kilimanjaro iko Kenya.Wanajua uwepo wa Serengeti na Mlima Kilimanjaro ila wanajua kitu kiko kenya.
ReplyDeleteBravo Maajar UK, balozi zingine nazo ziige.
We anony wa kwanza hapo juu unaonekana huna upeo kiasi,kwaufupi unaonekana kichwani huna unalolijua hapa chini ya jua.Watu wanafanya advertisement unasema misifa.Pole sana,matangazo ni muhimu katika kupata wateja wengi zaidi.Imetulia
ReplyDeletesafi sana Juma Pinto na wenzako,huo ndo ubunifu.if you can not beat them copy them.Kenya walizidi kujishobodoa kwamba Mlima Kilimanjaro uko kwao ngoja tuone sasa,kwa matangazo haya wataipata fresh.
ReplyDeleteThis comment has been removed by a blog administrator.
ReplyDeleteMtafiti hapo juu anatoa strong points hasa anapozungumzia kuhusu matangazo yetu kukosa mvuto na kutokuwa specific vya kutosha.Kama anavyonena "mtafiti" jaribuni pia kuweka matangazo tofauti yanayosifia kila eneo kwa wakati wake. TTB jifunzeni kutoka wenzetu wa South Africa. Angalia matangazo yao CNN uone jinsi yalivyo specific na yalivyo na mvuto. Matangazo yetu ni mazuri ila yanahitaji kuboreshwa zaidi. Mfano kwenye matangazo yetu slogan ni " The Land of Kilimanjaro and Zanzibar lakini kwenye picha inawekwa Kilimanjaro na wanyama tu bila angalau kuonyesha beaches au historical sites za Zanzibar ambazo ndiyo zinavuta watalii wengi wanaokuja Tanzania
ReplyDeleteWajameni na tungoje next week ya wiki ijayo si mbali.Hongera kwa wazo jema. tawile!
ReplyDeleteThis comment has been removed by a blog administrator.
ReplyDeletemi natoa pongezi zangu kubwa kwa serikali kwa kuamua kitu cha namna hii kwani ni maendeleo makuubwa hayo,nashangaa mtoa maoni mmoja anawapa pongezi wakina pinto,pinto nani katika tanzania?zaidi ya kashfa ya ushoga?acha habari zako za kuwapa watu wa ajabu ujiko usiokuwa na kichwa wala miguu!
ReplyDeleteHivi kweli itatokea kuweka matangazo yetu kenye mabasi na Heathrow Airport?
ReplyDeleteKama kweli itakuwa ni Big Step kwa Serikali ya Jakaya Kikwete na kuweka historia kwani haijawahi kutokea kufanyika kitu kama hicho.
Sisi Watanzania sasa tunaweza kutembea vifua mbele kwa kuutangaza utalii wetu.
Pili ongerea balozi Maajar nadhani hizo ni busara zake kuhakikisha mabalozi nao wanafanya jitihada za kuitangaza Tanzania.
Mabalozi wengine igeni mfano wa huyu mama kweli JK amechagua Iron Lady Uingereza.
Pili ongereni kina Jambo kwa wazo zuri kwa Serikali.Jamani kuna vitu vingi sana Watanzania tunatakiwa kuisaidia Serikali hasa kwenye masuala ya biashara.
Kweli inapendeza, inavutia na inatamanisha kuona matangazo yetu kwenye sehemu ambazo hatukutegemea kuyakuta.
Good Work
tangazo la vivutio vya tanzania linaloonyeshwa na cnn kwa udhamini wa vodacom ni zuri na linavutia , tunahitaji matangazo kama yale mengii , weka majungu pembeni
ReplyDeletelabda maajar amejitolea, wengine ni vigumu sana, kwani osifi za serikali wamegeuza kama zao, tena huku huku ulaya.
ReplyDeleteJust to respond to 2:43:00 PM EAT's comments, I think you have missed the point.
ReplyDeleteThey put the teaser ad not be praised 100 per cent, but rather to gauge the reaction and improve upon suggestions, criticism and things like that.
Of course they can't satisfy all Tanzanians, but macho mawili si sawa na manne.Tatizo ni kwamba, watu mmezoea kupenda kusifiwa tu na upande wa pili hamtaki kuusikia [embedded katika culture ya chama tawala na mfumo wa serikali yetu]; mathalan nimekosoa lakini pia nimetoa solutions and suggestions nini cha kufanya waweze ku-improve, sikufanya blanket criticism kama ambavyo wewe umezoea kufanya.
I hope tuko pamoja, ndiyo maana wenzetu wana professional critics - wanasifu na kuponda bila kuonea aibu product au service.
NI HABARI NZURI KWELI KWELI ILA UBALOZI WETU LONDON UNATUANGUSHA NA WEBSITE YAO YA KIBABAISHAJI..
ReplyDeleteJAMANI KAMA HAWAWEZI SI WATEMBELEE ZA WENZAO WAIGILIZIE.....!!!PICHA ZA KU SCAN MPAKA LINI......???????
JAMANI MUWAJIBIKE MUNATUMIA FEDHA NYINGI ZA WALIPA KODI HALAFU WEBSITE INA MIEZI IKO UNDER CONSTRUCTION.
NINGEKUWA NI MIMI NINGETUMIA MSHAHARA WANGU KUKODI WATAALAMU WA KUPIGA PICHA NA WEBSITE DESIGNER KUONDOA AIBU HIII.......!TUNAWAELEKEZA WAGENI WETU WANAKWAMA.
INANIUMA KWELI KWELI KWELI.....!