forodhani hapa zenj wameshapiga bati kupisha ukarabati wa maeneo hayo maarufu kwa mapochopocho (au machopochopo?) kila siku jioni. shughuli hizo sasa zimehamia uchochoro wa ngome kongwe na jumba la ajabu. haijulikani ukarabati utachukua muda gani...

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Eee michu ile kauli yako ya kusema ukifika zenjy bila kufika foro hujala bado kumbe nkweli mana naona ile pyeeeee kutinga tu, break ya kwanza jicho lilipiga foro anyway nimekusameh maana njia ni hiyo hiyo ya kwenye mahafal uloendea huko kwa washkaji, ila kwa kukukumbusha wewe mwenyewe ulituhabarisha ukarabati utafanyika kwa miezi kumi, si tunahisabu tuuu ikigota tu, tumo ndani ya boti kwenda kujionea marekebisho kama yako sawa kiwango wanachotaka wale wenzetu, ili watakapokuja kutumia wasijeharisha kwani huko wanakoishi ni peponi hata nzi hawanjui anafananaje walayi.

    ReplyDelete
  2. Mradi utachukua miezi 10, michu soma na magazeti ya znz upate habari zaidi

    ReplyDelete
  3. Yakhe hapo ndio 'Beit al Ajab',Watawala wa kale wa Unguja yaani Masultani ndipo yalikuwa maskani yao...nasikia siku hizi ni makao makuu ya CCM...typical,kila wanachokinyang'anya lazima kiwe chao!!!

    ReplyDelete
  4. Ujenzi utachukua kiasi miezi 10. We are missing alot yakhe ! Nimezoea mara moja moja weekend kupata upepo mwannana na choma choma. Sasa inabidi tukanunue vichochoroni. Lakini bora wapatengeneze manake hapakuwa na kiwango kizuri.

    ReplyDelete
  5. Natumai mwaka huu watafanikiwa... Foro iweshafanyiwa matengenezo zaidi ya mara tatu bila mafanikio.

    ReplyDelete
  6. kwanini ichukuwe muda wote huo kwa kikubwa gani kinachotaka kutengenezwa yakhee 10 month!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...