poleni na hongereni kwa kuwafichua wala rushwa wetu. Namsifu sana kijana wetu na mzee wetu JK, nitatoa maoni yangu baadaye, lakini leo, poke picha ya WaTz waishio Sydney wanavyowafundisha watoto wao kucheza michezo ya Kiafrika. Hapa Mzee Mark, au Mzungu mweusi akiwafundisha watoto mchezo wa 'Simba ni Mkali aliua mama' - sijui waswahili mnauitaje, nafahamu wimbo wake tu, lakini wengi watakuwa wanaujua. Ni muhimu kutunza mila na desturi zetu.
Mdau Sydney
Kama pesa zenyewe nje ya nchi ndio zuinatafutwa hivyo nimebadilisha mawazo ya kutoroka nchi naenda kijijini kulima.
ReplyDeleteLoh! salaaaaale huyo simba mtu hiyo kaptura ikipapuka hapo mambo yote hadharani. kwekwekwekwekwekwekwe.......
ReplyDeleteInafurahisha kidogo mana jasiri haachi asili, msisahau ukuti, Hiyoo ngoda ngodani, rafiki yangu nani nani nani, kiyoo kiyoo,kupishana kupishana ndiyo kilimwimwengu ikiwezekana lunch ugali wa muhogo na nguru mkavu au nyanya chungu au dagaa upapa ili siku wakija kuwatembelea ma-aunt zao isiwe mzigo, maana huku vyakula vya kopokopo hatupendelei sana
Duhhhh...mbona wanafanana na MaAborigino!!!
ReplyDeletekwani aborigino cyo watu mtu mzima ovyo una mvutoooooooooooooooooooo
ReplyDeleteBabu Seya alianzaga hivi hivi..LOL
ReplyDeleteMIBONGO UTAIJUA TU, INASHANGAA SHANGAA, MAWAZO YA AJAAABU KWASABABU HAINA MUDA WA KUWA NA WATOTO WAO!
ReplyDeletewashamba utawajua tuna comments zao. kwani nani kakukatalia kwenda kijijini kulima. Wewe unasubiri uone picha za watu ndio udecide what to do with your life?
ReplyDeleteAcheni maneno ya kijinga jinga.
Hongera kaka yangu kwa kujitahidi kutunza mila. Hawajui what you are talking about waonee huruma tu. Hawajui umuhimu wa kuspend time na familia ndio maana wanakandia. Na nini kupass kwa watoto wetu wasiokulia bongo.
Ni wachache sana wanaopenda kufundisha watoto wao mila za bongo ukilinganisha na wahindi, wachina, waspanish wameishi nje ya nchi miaka mingi sana tu lakini wanakeep mila zao sana tu
heads up my bro
WEE ANONY WA KWANZA HAPO, KWANI NANI AMEKWAMBIA KAMA HUYO ANATAFUTA HELA HAPO??? SI UMEAMBIWA ANAWAFUNDISHA WATOTO MICHEZO YA KIAFRIKA!! HEBU SOMA KITU UKIELEWE KWANZA KABLA YA KUCOMMENT, NA KAMA AKILI YAKO NI PUNGUFU HEBU HARAKISHA KWELI KURUDI KIJIJINI UKALIME MAANA MJINI HAUWEZI UKAPATA KAZI NA UKOKO HUO ULIONAO.
ReplyDeleteWazungu wanaweza kusema kuna Child Abuse hapo!
ReplyDeleteWazungu wanaweza kusema kuna Child Abuse hapo!
ReplyDeletewe tuplionyu acha zako.child abuse iko wapi hapo? au na wewe umekurupuka kutoa comments bila kusoma maelezo ya hiyo picha. wazungu wazungu? mbona wao ndo wanaongoza kwa kucheza na watoto. au kwa vile picha hiyo ya m-bongo ndo maana unaleta zako za kujidai wazungu. acha uzungunaizesheni. toa maoni yenye akili..
ReplyDeleteMiye nawashangaa waBongo na akili zetu finyu, sasa nawajibu kwa busara ndogo wale wote wanaojifanya wanajua sana. Wewe unayesema wanafanana na aboriginal, kwani wewe unajiona unathamani kuliko nani, au ndiyo nyie mnaoona wazungu ni bora kuliko wengine? Uzuri wako umekaa wapi, nyie ndiyo mnaendekeza ubaguzi wa kipumbavu badala ya kuangalia maendeleo.
ReplyDeleteWewe unayesema hapo mtu anatafuta hela, baba yako alivyokuwa anacheza na wewe alikuwa anatafuta hela kwa nani? Kwa hiyo ukikaa na watoto wako huchezi nao mpaka upate hela? Ndiyo watoto wanawaona kama Simba, ukiingia ndani wote wanakwenda kulala.
Wewe unayesema child abuse, asili yako iko wapi? JE ULIPOKUWA UNACHEZA NA WAZAZI WAKO ILIKUWA NI CHILD ABUSE? Kwa hiyo hutacheza na watoto wako kwa sababu utaogopa child abuse! By the way, unafahamu maana ya child abuse, au unaisikia tu kwa hiyo umeibeba hivyo hivyo tu mpaka unashindwa kuishi isipokuwa kila kitu mzungu kasema ni abuse.
Kibaya zaidi kwa nchi yetu ni kwamba tuna watu waliokua lakini vichwa vimepumbaa sana, na bado vina fikra za kutawaliwa, hakuna kitu chetu isipokuwa mzungu kasema tuishi hivi!
Obama anataka kubadilisha mindset ya Wamarekani, we need someone to change the mindset ya WaBongo, vinginevyo tutabaki nyuma tu.
Kumradhi wasomaji, nilikuwa nakemea pepo wabaya