sio vibaya mdau ukajaribu ujasiriamali kama huu huko ughaibuni. kwa habari zaidi bofya hapa







Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. michu wewe kiboko, haya wadau tuunge mkono vazi la khanga, kudumisha umoja tanzania.

    ReplyDelete
  2. michu kuna baadhi nawafahamu hawaogopi kabisa kujivunia khanga kwa mtu yoyote, wanavaa hata kwa shughuli za kiafrika.

    ReplyDelete
  3. Ninyi mnatafuta lawsuits..unafikiri Mmarekani atanunua hiyo kwaajili ya kubebea mtoto kama unatumia mafundo..wanajali safety standards..what will be the safety standard for Khanga? Siyo kwamba napinga ila nadhani we need to improve our products to meet the standards of these countries...!! It can be used to do something else but not "as it is" to carry a baby..!! Sorry..!!!

    ReplyDelete
  4. Umachinga mpaka Ulaya? Au nako kuna kuomba wapunguze bei mpaka 5Euro 5 kutoka Euro 29? Bei hizo kwa kitenge ni madafu 50,670 na kwa khanga ni madafu 43,914!!. Huu ni ufisadi pia hata kama anayefanyiwa hayo ni Mzungu!

    ReplyDelete
  5. Jamani kuna starehe nzuri anayoipata mtoto akibebwa mgongoni hasa kwa kanga na lile joto anolipata akiwa mgongoni na kanga hata kama alikua analia utamsikia kanyamaza kimyaaaaa mwisho anasinzia,mimi nilikua nanunua mbebeo ya kitenge au kanga nzito kila nikijifungua maalum, kwa kumbebea mwanangu ikifika miezi mitatu tu namtia mbelekoni kumpa raha na mapenzi mwanangu,

    ReplyDelete
  6. HONGERA MDAU KWA UJASIRIMALI. HII NDO TUNATAKA. SAFETY STANDARDS NI MUHIMU NA NI CHALLENGE. WEWE UNAYELALAMIKA MADAU ELFU HAMSINI: UNAWEZA KUZIONA NYINGI BONGO, LAKINI KWA ULAYA EURO 29 NI PEANUTS...NI BEI YA KAWAIDA KABISA! NA HUWEZI KUJUA JASIRIAMALI AMEPRICE VIPI...KUMBUKA KUNA LOGISTICS, TAXES INCLUDING VAT, INSURANCE FOR EMPLOYEES AND PENSIONS....

    KMUSHI

    ReplyDelete
  7. Waafrika wengi wakiwa Ulaya au Amerika hawathubutu kuwabeba watoto wao kwa Kitenge wala Kanga. Hapa suala sio safety standards wala nini ni suala la kuona aibu utaonekana kama vile bado uko porini kwa mtazamo wao. Lakini kitenge na kanga zetu za Urafiki ambazo ni nzito (sio za India nyepesi,hizo matumizi yake chumbani kwa kazi maalum) kiko safe kumbebea mtoto. Tulibebwa na wazazi wetu na wazazi wetu walibebwa na wazazi wao miaka dahari sijasikia manung'uniko ya safety. Vitu vyetu vizuri wazungu wanaviiga lakini sie wenyewe tunaona aibu.

    Siku moja niliona mtoto wa kizungu kafungwa leash/mshipi kama mbwa analia kweli kweli hataki kutembea kana kama miaka miwili hivi au zaidi. Roho iliniuma nikasema jamani mtoto anakokotwa kama mbwa! Nikatamani nimbembe mgongoni masikini lakini nikapita mbali kweli kweli maana unaweza kupata kesi isiyo kichwa wala miguu kwa kumgusa tu mtoto wa watu wakati kwetu unaweza msaidia mzazi mwenzio hata kumbeba au kumpakata mtoto wake ndani ya basi.

    Pamoja na kuwa na uwezo wa kununua hayo mabebeo ya kizungu, sijawahi kuyanunua hata siku moja na wanangu wote wamekuwa kwa kubebwa na kanaga au kitenge mngongoni.

    Nenda kwa wazungu wa Scandnavia waliowahi kufika Africa utakuta, table cloth aidha batiki au kitenge, vigoda, ngoma, mpaka mapicha ukutani. Ingia nyumba ya mswahili popote imejaa uzungu mtupu IKEA furniture HIFI N.k. Na wamefikia hatua ya hata kuwakataza watoto wao wasiongee kiswahili!

    ReplyDelete
  8. Anon 8:01 am, kubeba box kwako marekani kusikufanye kajiona na wewe mmarekani. Kwani wewe ulibebwa kwenye mbeleko gani? baba yako kijijini au babu yako alibebwa kwa mbeleko gani? jee wewe ulianguhswa? babu yako na baba yako waliangushwa? Acha kujifanya unajuwa sana safety ukijifanya na wewe mmarekani! Hata uruke vipi nzi huwi njiwa! Unadharau kilicho kukuza. Wewe ndo wale wanao laani kuzaliwa waafrika, wewe ndo wale wanaowakataa hata mama zao kwakuwa wana hali dĂșni. Usinge kwenda marekani hiyo mbeleko ya kizungu ungeijulia wapi? Angalia unachokisema usijione wewe peke yako ndo umefika marekani, watu wamezaliwa huko na bado wanatumia mbeleko za kanga na vitenge! safety unaijuwa leo, ungemwambia mama yako akushushe mgongoni alipokubeba kwa kitenge na kanga ili usianguke...mso haya we.

    ReplyDelete
  9. Acheni bwana kuna wafrika kibao hasa toka Magharibi mwa afrika wanawabeba watoto wao kwa mbeleko(kitenge,khanga) mgongoni hapa marekani.Nawaona kila siku hasa wakati wa joto na hakuna mtu yeyote anayewapeleka mahakamani.Nyinyi mnaosema haya hayafanyi ni wale mnaofanya kazi za live-in(a.k.a housegirl,houseboy)ndiyo maana hamna muda wa kutembea sehemu mbalimbali hasa maeneo ya weusi na kujionea haya kwa macho yenu.Kwa upande wetu waafrika tunaotoka mashariki huwa tunaona aibu kufanya yale mambo tuliyokuwa tunafanya afrika.

    ReplyDelete
  10. Nafikiri ni kweli kwamba waafrika huwa tuna ona aibu kuonyesha utamaduni wetu,mimi nimebeba wanangu wote kwa kanga nikiwa nyumbani lakini sijathubutu hata siku moja kutoka barabarani huku nimewabeba wanangu kwenye kanga,lakini nimewabeba wanangu kwenye baby carrier ya kizungu nikienda kufanya shopping zangu,kuona hii post imenifanya nitafakari sana,nakuji kosoa why as africans we are not proud of our culture and heritage but leading in showing off other people's culture.
    Mwisho wa mwaka jana nimeona mzungu inawezekana ni scandnavian lady,kabeba mtoto kwa kitenge lakini hicho kitenge kimeshonwa kama baby carrier,kwahiyo nafikiri washonaji wa nguo wangefikiri na hili jambo la kubuni designs za baby carrier zilizo tengenezwa kwa kanga au vitenge,labda zikifanywa fashionable kina mama na baba hawato ona haya ya kubeba watoto na vitenge au kanga huku ughaibuni,na anon aliesema swala la safety standards nafikiri ana point nzuri,kama tukitaka kanga na vitenge tuvifanye biashara ya kimataifa yaani sio sisi tu waafrikla bali hata wazungu wakiona wanunue wakijua wananunua kitu high quality,lets be real they do mind about safety.

    ReplyDelete
  11. Asiwadanganye mtu, kanga ndo mambo yote. Anayefikiria safety nampa pole.

    Wengine sie tusingekuwa hapa tulipo kama sio kanga. Cha muhimu ni kuiheshimu na kuenzi kanga na wala si kukashifu. Kanga ina raha yake yakhe si kubwatuka tu kama mahayawani mambo ya safety oohh mara umachinga. Kwani hao wazungu waliombelekesha watoto wao kwa kanga safety hawaijui?

    Ushamba mwingine umejikita kwenye mawazo. Mimi ukitaka unipe raha, niletee kanga, tutaheshimiana milele...hakuna cha usomi wala umasikini kwenye kanga.

    Kanga kanga na wewe uliyesema mambo safety kama ni mwanamke ...nakupa pole kwani hayajakufika ukaona umuhimu wa kanga

    Bahati yako hapa ni kijiwe cha Michuzi, mipasho hairuhusiwi, ningekushushia mvua ya taarab ikunange vizuri, maana inaelekea malezi huna wewe

    ReplyDelete
  12. haya wadau muwe mnatangaza mavazi ya asili, mkiw anyumbani na hata nchi za nje, ndio utamaduni.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...