Home
Unlabelled
kp leo
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
Kipanya hajatulia kbs.Lkn ni kweli wema mwingine unaweza muua mgonjwa hv hv.Siku zote hizo aone kitanda na Omlet/spanish ujio wa Bush.Na matabasamu ya kufa mtu kutoka kwa manesi.
ReplyDeleteHureeeeeeeeeeeee Kipanya..
kp umenivunja mbavu hapo ila napenda kukukumbusha hiyo ni heshma kwa mgeni anapokutembelea lazima mazingira na makosa madogomadogo yawekwe sawa ili mgeni asipeleke sifa mbaya anaporudi, kuwa huko nilikokuwa ni wachafu sana, maskini wa kutupwa hata vitanda hawana wanalala chini, ila mjomba mpoto alishamwaga cheche mzee wa kujikuna utosi anayajua yote na pongezi atatoa kwa matayarisho hayo, ndipo hata mataa yaliwaka siku hiyo balbu zote ziliwaka brabarani tangu al-asir jioni.
ReplyDeleteDuh hii kali...
ReplyDeletekweli mgeni aje mwenyeji...apone
KP umeonyesha unasanii unaofanywa na watoa huduma wengi wanapotembelewa na viongozi wa kitaifa na kimataifa.
ReplyDeleteNimefurahishwa sana na jinsi mgonjwa alivyozungukwa, maswali anayoulizwa na jinsi anavyowashangaa kwa kuwa ni wahudumu hao hao waliomlaza chini na ndiyo wanaotoa majibu ya nyodo kwa wagonjwa. Inatakiwa tujipange ili tutue huduma nzuri kwa wagonjwa na siyo kuleta usanii wa kuvutia misaada kutoka kwa Bush. Wagonjwa ni watu waliokuwa disturbed kisaikolojia, hivyo kuwapa huduma nzuri ni sehemu muhimu sana katika matibatu yao. Mimi naona baada ya Bush kuondoka inatakiwa tufanye tathmini katika maeneo tuliofanikiwa kuyafanya vizuri kwa muda mfupi(usafi, lugha nzuri kwa wagonjwa, taa za barabarni nyingi kufanya kazi etc) na mbinu tulizotumia ili tuboreshe jiji letu la Dar pamoja na huduma hospitali kwani kwa jinsi tulivyomuonyesha Bush tunaweza kabisa kufanya mambo mazuri. Naomba tunayaonyesha wakati huu Bush akiwepo bongo usiwe usanii bali iwe tabia yetu katika maisha ya kila siku ili tupige hatua kimaendeleo.
BIG UP KP
KP HONGERA,MGONJWA ALIYEKUA AKILAZWA CHINI LEO KAWEKWA KITANDANI HICHO KITANDA KILA SIKU KILIKUA WAPI?MPAKA MGONJWA KAJIHISI SIKU YAKE YA KUFA INAWEZEKANA IMEFIKA.MANESI MADAKTARI NAFIKIRI WANGEBADILISHA HUDUMA ZAO NA LUGHA VILEVILE ILI KUMSAIDIA MGONJWA APONE HARAKA ZAIDI RESEARCH INAONYESHA MGONJWA ANAEPEWA UPENDO NA HUDUMA BORA ANA POA HARAKA ZAIDI KULIKO ANAEPEWA DAWA AKAACHWA BILA HUDUMA NYINGINE YOYOTE.A TOUCH,A SMILE, OR EVEN STOP AND CHAT TO THE SICK IT MAKES ALL THE DIFFERENCE.
ReplyDeleteKP kweli wewe ni kiboko...nimewaonyesha wenzangu picha hii hapa AMANA hospital imebidi tuanguke kwa vicheko kwa sababu ni kweli kabisa hiki ndicho kilichotokea hapa wiki iliyopita....yaani ni exactly (hiki kiingereza ni kuonyesha msisitizo) ya mambo yalivyotokea...tunashukuru sana kwa kuanika ukweli kupitia kwenye kiponzo..Mungu akubariki uanze kuchana nywele!!
ReplyDeleteMdau aliyesema ni heshima kuweka mazingira safi mgeni akija ni vizuri ila usituchekeshe, Sawa nak uwa mchafu kwako siku wageni wakija ndio unasafisha, ila watanzania hospitali zetu tujitahidi kusaidia wasiokuwa na uwezo kwa utu uzuri.
ReplyDeleteWadau hapo ndio inaonesha ma Nasi wetu wanazarau na chuki wameona mgeni ndio wanajifanya watu wazuri,
ni bora wangewacha vilevile tuzidi kusaidiwa tunaficha makucha yetu machafu bora tuoneshe tusaidiwe vizuri.
Mdau Mmoja alisema kuja kwa bush tutawapita kenya tuwacheni ujinga, wa africa tushikamane tusikosoane tusaidiane tusitengane kuja kwa bush ni kuzuri ila sio ndio kuwanyenyekea.
Tizama wanavyozauliwa waandishi wetu wa habari hapa hapa nchini kwetu na wamarekani, UHURU wa africa hatuna UHURU hautolewi na Binadamu wenzako UHURU unatolewa na Mwenyezi Mungu. UHURU upo kwenye Moyo wako na Roho yako.
MMh kaka Kp hapo you nailed it ..Big up keep up the good work .!!!!
ReplyDeleteBasi hat aBush akiondoka uzi uwe huo huo. Mgonjwa aweza kupona kwa huduma tu si lazima dawa.Inaitwa Tender Loving Care.
ReplyDeleteJamani Kp....unastahili sifa kemkem!!Hufanyi makosa!Unashabaha...!Natumaini wahusika wanakupata vyema.
ReplyDeleteShikilia uzi huohuo.
Hiyo kali...kumbe sio umasikini wetu wakutokua na vitanda bali hata wahudumu wenyewe ni balaa...
ReplyDeleteInabidi wabadilike roho nzuri haihitaji hela...kama hulipwi mshahara mzuri usimtolee hasira mgonjwa ....nenda kwa mwajiri wako.....
nimecheka weee hadi basi kweli KP umewapa ukweli kabisa kama bush amekuja wanajua kucheka na vitanda vimepatikana why not kila siku ???? Omlet na spanish hehehehehehehehe
ReplyDeleteKaka kipanya umenichekesha. Pamoja na hayo hii inaonye mafisadi wako kila mahali hizo pesa za kitand au kitanda kimepatikana toka wapi, lazima kuna watu wanjua, Inabidi ufanyike utafiti je hicho kitanda kitaendele kuweko au kitaondoka Bush, TZ in mambo.
ReplyDeleteRaisi Bush kaleta hela kwa ajili ya manesi,madaktari na wagonjwa kwa nini huduma zisiwe nzuri?
ReplyDeleteUnategemea huduma zibaki mbovu wakati mwanaume wa Shoka keshakuja na kamwaga pesa? Na uhakika wa Pesa upo.
Kila mtu anaweza sasa kutoa huduma nzuri.Uhakika wa bajeti upo.
Changamoto kwa kila mtanzania aliyeko nje ni kuwa si vizuri kusema tu na ku-amplify matatizo ya Tanzania ni vizuri tuwe wachangiaji katika huduma za Afya.Mfano tujiulize wodi ngapi zimejengwa kama msaada toka kwa watanzania wa Nje ya nchi,au msaada wa madawa kiasi gani umetolewa nao mahospitalini?
Watanzania nje ya nchi bure kabisa hasa kwenye uchangiaji wa huduma za jamii nchini Tanzania lakini ni wa kwanza kupiga tarumbeta kuwa huduma za Afya Tanzania mbaya na wepesi kutoa statistics kwa kiingereza kilichonyooka.Mnataka nani azitengeneze hizo huduma za jamii ziwe Nzuri?Shame on evey Tanzanian Abroad ambaye hachangii huduma za jamii Tanzania zikiwemo za afya.
Huu siyo wakati wa kusema kuhusu huduma mbaya za Afya Tanzania ni wakati wa kummunga mkono Raisi Bush kuchangia huduma za Afya.Yeye kaanza kuonyesha njia watanzania wa ndani na nje ya nchi wafuate.Si vizuri kumwachia Raisi Bush pekee akichangia inabidi tumuunge mkono jamani na sisi kwa kutoa michango yetu kwa ujenzi wa ma-wodi,n.k
Koloboi@yahoo.com
habari za wakati wadau,naomba niwape mwongozo tu wale waliokuwa wanauliza vitanda vilikuwa wapi na bushi akiondoka vitaenda wapi au wagonjwa wataendelea kulala chini,ukweli ni kwamba baadhi ya wagonjwa walihamishiwa hospitali jirani na wakaachwa wale wachache kulingana na idadi ya vitanda....so msiulize tena vitanda vilikuwa wapi..naomba kuwasilisha wadau
ReplyDelete