MTANZANIA AU WATANZANIA WANAOISHI NCHINI KAMERUNI, MJINI YAOUNDE AUDOUALA, WANATAFUTWA NA MTANZANIA ANAYEISHI MAREKANI AMBAYE AMEOMBAJINA LAKE LIHIFADHIWE LAKINI ANAFAHAMIKA NA BLOGU HII. TAFADHALI TUMAHARAKA E-MAIL YAKO NA SIMU ZAKO KWENYE E-MAIL YA BLOGU.
ASANTE!

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. WEE MCHAWI NINI YAANI UNATAFUTA MTU YOYOTE SASA MIMI NAISHI CAMEROON SHIDA YAKO NINI SAMAHANI LAKINI SIFANYI KAZI ZA HARAMU KWA HIYO NITOE KWENYE LIST YAKO

    MOH AL NASSOR

    ReplyDelete
  2. Huyo anayemfauta lazima atakuwa FISADI! Kwanini jina
    lake anaogopa lisitajwe!? Ni uhuni huo na hupati mtu FISADi wewe!

    ReplyDelete
  3. Hey! wape watu hata sababu kidogo ya kutuma email zao huko unakotaka. Yaani kwa vile wewe ni mtanzania au kwa vile wewe uko USA ndio maana watu wakurupuke tu na kutuma email zao?

    Humu kwenye blog ya michuzi hamna anayefahamika zaidi ya Chiribiti

    ReplyDelete
  4. Mimi niko huku cameroon ila kama ndio unaitaka dawa ya kukuza mawowowo usitegemee kama tutakusaidia ila ungeongea shida yako tungeweza kukushauri

    ReplyDelete
  5. Aaaahhhh !!!!
    mijitu mingine bwana !!!
    yaani wewe unatafuta mtu halafu usemi jina
    kwani sie Psychics?
    address yako hujatoa
    mwe !!!!
    sasa unataka usaidiweje? eti mtu anatafuta mtu, watanzania tupo zaidi ya milioni 35
    loh !! usipoteze muda wetu hapa.
    move get out of the way !#$@# we have important things to do

    mdau Canada

    ReplyDelete
  6. JAMANI NI RAHISI MNO, HUYU JAMAA ANAOMBA CONTACTS NA MTANZANIA ALIYEKO CAMEROON, KAMA UKO TAYARI WASILIANA NAYE, KAMA HUTAKI ACHA! HAKUNA SABABU YA KUMLAANI KWA KUWA HAMJUI ANA JAMBO GANI, KAMA ANA JAMBO BAYA ASINGECHAGUA KUACHA USHAHIDI KWA MICHUZI. WATANZANIA TUKO NEGATIVE MNO, KWA NINI KAMA WEWE UKO CAMEROON UFIKIRIE JAMBO BAYA TU? KAMA MIMI NINGEKUWA HUYO JAMAA HATA MTU AKITUMA CONTACTS SASA NITASHUKU KWAMBA SI MKWELI, KWA KUWA WALIODAI KUWA WAKO HUKO TAYARI WANAONEKANA KUWA NA TATIZO.

    ReplyDelete
  7. JAMBO USILOLIJUA BWANA NI KAMA USIKU WA GIZA

    ReplyDelete
  8. ELIMU KIDOGO KWA WASIOJUA MEDIA

    Kama umewahi kusoma matangazo ya nafasi za kazi kwenye magazeti bila shaka unakumbuka yale matangazo ambayo huwa hayataji Jina la Kampuni inayoajiri.

    Huwa yanasema tuma maombi kwa Vocha namba XXXXX.

    Kinachoendelea ni kwamba kwa sababu moja ama nyingine Mwajiri ameamua kuficha identity yake na hivyo maombi yatapokelewa na Media ambayo itaforward kwa Mwajiri.

    Sababu kuu huwa ni kwamba mwajiri anataka waombaji watume maombi kutokana na kazi iliyotangazwa sio kutokana na nani aliyetangaza.

    Hivyo huyu ndugu yetu wa Marekani ametumia staili hii kwa kujificha nyuma ya pazia la Issa Michuzi.

    Mlioko Cameroon natumai hamutamuangusha.

    Kama wahenga wasemavyo "usikatae wito bali kauli"

    ReplyDelete
  9. kwani huyo chibiriti ni nani aliyetajwa hapo juu

    ReplyDelete
  10. Jamani mimi niliyetoa tangazo hili siyo mjinga, kama hakuna Mtanzania mwenye nia, basi nahamishia tangazo hili kwa Wakenya halafu muone watakavyochangamka, labda wawe hawapo huko Kameruni. Issue siyo mimi ni nani, ni kwamba kama una nia changamka, huna nia acha. Hakuna haja ya kutukana wala kushambulia, acha tu kama hutaki na ulicho nacho.

    ReplyDelete
  11. Ndugu yangu mimi niko Gabon, nimeoa huku, si mbali sana na Cameroon, kama nafaa kwa hicho unachotafutia mtu, niambie. Inaelekea watu hawajui biashara za kimataifa zinavyokwenda, hii inaonekana kabisa ni kitu safi lakini watu hawaelewi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...