Habari za leo Ndugu Michuzi,
Natoa shukurani zangu za dhati kwa juhudi unazofanya za kutupatia sis wadau wa Tanazania updated news kila siku. Kwa kweli kama nusu tu ya Watanzania wangekuwa wachapa kazi kama wewe, nchi yetu ingeenda mbali sana.
Siku zote huwa nashindwa kushangaa jinsi unavyoweza kuwa mitaani na kwenye kila mnuso halafu bado ukapata muda wa ku-update blog yako mara mbili au tatu kwa siku, it is amazing ! Congratulations and keep it up.
Mimi ni mbongo nafanya kazi huku South Sudan . Profession yangu ni Daktari, sasa kuna kazi huku nyingi tu huku ila sielewi kwa nini Watanzania hatupendi kuchangamkia hizi kazi.
Kwa mfano hao Wakenya tunao wapiga vita kwamba wanakuja Bongo kuchukua nafasi zetu za kazi huku South Sudan in both formal and none formal employment wako around 30,000. Sasa imagine kama kila mmoja akipeleka dola mia tano tu nyumbani kila mwezi, hizo ni sawa na USDs 15,000,000 kwa mwezi zinaingia Kenya .
Watanzania huku kama ni wengi sana basi nafikiri hawazidi 100. Tena infact namba kubwa ni wamasai wanaouza dawa zao za kimasai. Watu wanakuwa na wasiwasi na security; ila naomba niwaambie kwamba security sio tatizo la kutisha kwani tunalindwa na sheria za Umoja wa mataifa na hizi nchi ni signatories wa hizo sheria.
Halafu hakuna shirika linaloweza kupeleka mtu mahali kama halina uhakika wa usalama wake, and in case ukiwa field kukawa na tension tu kidogo helicopter inatumwa kuja kukuchukua kukupeleka sehemu ya usalama. Ukweli even one would feel more safe kukatiza mitaa ya huku kuliko kupita mitaa ya Manzese, Mtoni au Mbagala.
Kwa habari zaidi za haya mambo ya relief and humanitarian na kazi zake zungukieni hii mitandao;
kazi zinazotangazwa humu huhitaji kujuana na mtu, kinachohitajika ni strong well written application letter, resume (CV), academic qualifications and work experience. Last but not least apply sana mara nyingi tu usichoke mpaka umepata, kwani kumbuka kuaply ni free of charge.
Halafu usijihukumu eti hii kazi siiwezi wacha wale wanaochagua wakuhukumu; wewe apply tu. Kama kuna watu watakuwa interested na kupata habari zaidi kuhusu hizi kazi unaweza kufungua forum humu humu kwenye blog wakaniuliza maswali nami nitawajibu tu as much as I know ila naomba usitoe mail yangu kwani nahofia kujaa mails.
Sasa hili tangazo ni lakutafuta Madaktari, saidia kulipatia widest dissémination possible
; Comitato Collaborazione Medical (CCM – Italy ) is looking for the below medical proffesions to work in Lakes State , South Sudan .
1. Medical Officer an (MD) Qualifications and Experience; § Qualified Trained Medical Doctor who has successfully completed internship§ At least two years experience working independently in rural health facilities§ Should have Emergency Obstetric Care skills and capacity to perform independently life serving surgeries like caesarian sections etc. Duty Place; Rumbek State Hospital , Lakes State , South Sudan
2. Medical Officer (MD) or Assistant Medical Officer (AMO) Qualifications and Experience;§ Qualified Trained Medical Doctor who has successfully completed internship or Qualified Assistant Medical Officer with massive experience working independently in rural hospitals. At least two years experience working independently in rural health facilities Should have Emergency Obstetric Care skills and capacity to perform independently life serving surgeries like caesarian sections etc. Duty Place; Turalei General Hospital , Lakes State , South Sudan
Package; Salary; Based on qualifications and experience minimum 2000 USD
Other fringe benefits;· Food and Accommodation·
Every ten weeks you get 10 days off plus return air ticket to any Country in East Africa·
Paid one month leave plus return air ticket to any Country in East Africa once every year
Contact Person
Ada Merollemedco@ccm-italy.rg

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. Congrats doc.Not many who can do this.Ni wachache sana wenye moyo kama huuu.Hakuna cha sudan,afghanstan,Iraq,DRC(to say the least)pesa haiji kiurahisi you have to risk yourself sometimes.

    ReplyDelete
  2. South Sudan sio sawa na Afghanistan na Iraq, na hata sio sawa na DRC wao wamefikia stage nzuri kidogo. Kumbukeni hata huko nako kuna watu wanaishi. Nina rafiki zangu wanafanya kazi Somaliland, ingawa ni tofauti na Somalia lakini maisha ni kuhangaika. Jamani anachosema ni kweli, Wakenya wametapakaa dunia nzima, hapa UK kuna mkenya alikufa alikuwa anafanya kazi na alipewa mpaka na nyumba, tena basi kawavuta wenziwe kibao. Hili suala la kuvutana hata JK alishalisemea aliwauliza mbona watu wengine wanavutana nyie mnashindwa nini kuvutana? Big up mdau kwa kuvuta wengine nao kwa kuwaonyesha mchongo.

    ReplyDelete
  3. Duh...asanteee!!! kaka/dada ila du...Kamshahara kadogo sana....lol

    ReplyDelete
  4. Hapo sijaelewa, "unashindwaje kushangaa"?

    ReplyDelete
  5. Michuzi nakuomba sana tangazo hili la huyu ndugu daktari si la kizalendo hata kidogo. Sisi huku Tanzania tuna upungufu mkubwa sana wa madaktari, wa kutisha. Ukiangalia Tanzania Health Statistics Abstract iliyochapishwa mwaka jana utakata tamaa, kuna mikoa ina daktari mmoja kwa watu 130,000 (laki na thelathini elfu!). Na hao AMO's ni jitihada za serikali tangu enzi za mwalimu Nyerere kusaidia kupunguza uhaba wa madaktari, lakini bado hawatoshi. Kwa AMO's walioko Tanzania, bado kuna wilaya nyingi hospitali zake hazina daktari zaidi ya kiwango cha AMO, na ni mikoa mingi tu yenye uwiano wa AMO mmoja kwa wagonjwa zaidi ya elfu 60. Hapo kumbuka tunapigana tupate daktari (MD) mmoja kwa watu 10,000! Tutafika lini? Sasa huyu mwenzetu anataka madaktari wetu awapeleke Sudani wakati tunalalamika hatuna madaktari Kigoma, Lindi, Pemba, Singida, Rukwa, Mtwara nk! Jamani huu ni uzalendo gani wa kujenga kwa mwenzio wakati kwako kunaporomoka? Hao wakenya anaowataja kwenye hiyo tangazo yake huko kwao hawana upungufu wa madaktari kama kwetu, actually wao wanao madaktari waliofuzu wanaotafuta kazi (hawana kazi). Sisi madaktari tunawatafuta kwa mbinde, na akimaliza shule tu, kazi za ndani ya nchi ni nyingi sana (public na private), na hawajawahi kuzimaliza! Leo huyu anayejiita daktari wa huko Sudani kusini anataka kutuchukulia hata AMO wetu wanaotusaidia kutibia watu wetu huko maeneo ya vijijini, ati awapeleke Sudani! Ni dhambi kabisa! Ni sawa na kumlaza njaa mwanao wa kumzaa na kwenda kumlisha mtoto wa jirani ambaye ana watu wengine wengi tu wanaomlisha! Utachekwa!

    Hili tangazo la huyu jamaa limenichefua mie kama mzalendo wa nchi hii, limejaa ubinafsi na uchoyo zaidi kuliko maslahi ya taifa. Nakuomba bw Michuzi kwa hisani yako lifute hili tangazo, halitutakii mema hata kidogo! Huu ndio unyonyaji, wa kutaka kutunyang'anya hata kidogo tulicho nacho!

    ReplyDelete
  6. Safi sana mdau, jana Pinto katoa matangazo ya utalii, watu wamemtukana, jamaa mwingine kaomba awasiliane na Mbongo yeyote aliyeko Cameroon, wametukana, huu ujinga ndio unaotufanya tuwe maskini kila siku. Wenzetu kama Wakenya wanatuacha na iko siku watachukua kila kitu kilicho kwetu halafu tuanze vurugu. Wabongo sisi bongolala sana, sijui kwa nini hatuchangamki??? Kuna wakati India kulikuwa Wabongo 400 tu wanasoma, wote kwa msaada wa serikali, halafu Wakenya waliokuwa huko walikuwa 10,000, wengi wao kama si wote kwa pesa za baba zao, sasa hii tofauti yote ya nini?

    ReplyDelete
  7. ASANTE DAKTARI WETU KWA MOYO WA IMANI,KUTUKUMBUKA NDUGU ZAKO KWENYE ULAJI.KAZI KWAO WENYE HIZO QUALIFICATIONS.

    ReplyDelete
  8. watanzania upeo wetu wa kufikiria mbali kidogo ni finyu, tunadhani ni ujanja kuwa UK au Marekani hata kama tunabeba box. Cha kusikitisha ni kwamaba kuna watu wengine wana degree zao lakini wapo hapa wanabeba box. Asante Dokta wewe wasudani kwa kutupa dili.

    ReplyDelete
  9. Thanx 4 the links and info.. Ila swali langu.. Madokta wakishaondoka wote nchini au most of them .. RAIA WATIBIWE NA NANI?? na vipi kuhusu kuendeleza nchi kwa kujitolea?? Maendeleo hayaji kwa kuondoka nchini na kujengea ndugu zako Nyumba na kuwanunulia MAGARI..........UZALENDO SOMETIMES UNAFAA VILE VILE. So kwa mwenye uwezo wa kubaki Home na kuridhika na kilichopo afanye hivyo 4 the sake of maendeleo ya nchi na sio FAMILIA BINAFSI.Mi nipo Nje lakini ni kwakuwa tu sikuwa na nafasi huko.. Ila kwa wenye nafasi jamani .. Wasaidieni wasio na nafasi kwa kufanya kazi hapo hapo.. SEKTA YA TIBA JAMANI NI MUHIM SANA sio kama WAKANDARASI.
    Nawakilisha wanyonge jamani.. msinielewe vibaya.

    ReplyDelete
  10. Asante sana Dokta kwa kutoa habari za huu mchongo. Haya ndio matumizi mazuri ya Teknohama.

    Kwa wanaolalamika eti sio mzalendo unataka Tanzania isiwe na madaktari nina haya ya kusema:

    1. Je mna uhakika ni madaktari wangapi wanaohitajika? Isije kuwa kuna nafasi kumi tu nyie mkataka kufanya kana kwamba wanahitajika madaktari elfu moja.

    2. Madaktari nao wanahitaji pesa. Kwa hiyo nguvu za soko zitafanya kazi. Watakaoomba na kupata wataondoka kama wanaona pesa na pengine uzoefu watakaopata huko ni mzuri zaidi ya wa hapa. Na pale serikali yetu itakapozinduka na kuanza kulipa madaktari vema basi watarudi tu. Tena sio wetu tu, bali hata wa nchi zingine wakiona Bongo kuna maslahi watakuja.

    Kwa hiyo it's a simple choice kwa serikali. Kama maafisa wa TRA na wabunge wana umuhimu zaidi kwa Taifa basi iendelee kuwalipa mijipesa mingi kuliko madaktari. Otherwise madaktari wetu wataendelea kuchomoka tu kila upenyo unapopatikana.

    ReplyDelete
  11. we anony wa 6.58 acha zako.kwani huyo aliyetoa hizo links amelazimisha madoctor waondoke bongo au unarukia mambo? kila mwaka madoctor wana-graduate na sio wote wanaajiriwa automatically. so whoever could apply and get the job,let them do it. wewe si ungebaki bongo ufanye kazi za kiuzalendo. kuna barabara za kufagia,kupanda maua kwenye bustani za kupumzikia etc etc. mbona umekimbilia ughaibuni halafu unajidai kuleta story za uzalendo.hebu waache watu wenye qualifications zao wapate kazi sudan na watume dollars kwa familia zao. wewe upo nje ya nchi tayari,kwahiyo shut up and mind your own business.

    ReplyDelete
  12. Dokta asante sana kwa kutupa mwanga sisi watanzania wenzako tunaoshangaa mitaani bila ajira.Mimi sikubaliani kabisa na swala la kuacha kwenda kufanya kazi nje ya nchi eti kwasababu ya uzalendo,kazi ni popote ili mradi unaingiza kipato kinachokusaidia katika maisha yako.Hata huyo mheshimiwa JK anapenda sana watu watafutiwe nafasi nje ya nchi kwani yeye swala la uzalendo halifahamu? Milango ipo wazi kwa kila mwenye qualifications kuomba kazi,sasa kazi kwenu madaktari.Kwenda kutafuta maisha Sudan au kubaki nyumbani kusubiria ajira milioni moja za mheshimiwa JK.

    ReplyDelete
  13. Daah! Mimi ni mdau ughaibuni. Nimeutafakari huu mjadala kwa makini. Pande zote zina point lakini najiuliza, "what kind of father lets his children go hungry because he is patriotic". Kwa hiyo wadau kabla hatujamshambulia huyu daktari tujiulize kidogo. Mimi naona amefanya jambo la kiutu sana kuwaambia wadau "jamani eeh!! huku kuna opportunity!!" Hajamlazimisha mtu.. Kwa hiyo nawaomba wadau tuache jazba na kutumia vichwa kidogo sio kujibu hoja kwa pupa.

    Mdau - Boston, US

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...