feabruari 3, 1980: bingwa wa ndondi duniani muhammad ali akiwasili bongo kwa ziara. mwenye mkangafu ni tom mweuka wa kituo cha habari cha marekani enzi hizo.
"ohooo... mjomba utaumia hapa, shauri yako" anaonekana kusema mshabiki huku akikunja shati tayari kutwangana na muhammad ali wakati wa hafla hoteli ya kilimanjaro

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. We Michuzi acha kutuyeyuha hapa! Huyo mwenye mkangafu (Tom Mweuka) alikuwa anafanyia Television gani wakati huo?!! Kulikuwa hakuna television zaidi ya ile ya Zenj! Zetu za tisini mwanzoni

    ReplyDelete
  2. We Michuzi acha kutuyeyuha hapa! Huyo mwenye mkangafu (Tom Mweuka) alikuwa anafanyia Television gani wakati huo?!! Kulikuwa hakuna television zaidi ya ile ya Zenj! Zetu za tisini mwanzoni

    ReplyDelete
  3. Mjomba Michuzi katika siku Uliyonikuna basi leo kwa kutoa picha hizi, Huyo mzee anayekunja Shati ni mjomba wangu alijulikana Kwa Jina La Mzee Sheni ambaye alikuwa mpishi Hotel Kilimanjaro enzi hizo. Mzee huyo sasa ni Marehemu kwa watu wa Kagera Rangers Mwembe chai watamfahamu na alikuwa na Bar Yake mtaa wa Mengo na Kagera ikiitwa Sheni Bar enzi hizo. Ahsante bwana michuzi ni mimi Mbegu tena

    ReplyDelete
  4. Watu wengine wanapenda kubisha kila kitu, hata kama haitakiwi kufanya hivyo. Soma habari vizuri kabla hujatuma comment yako.Michuzi hajaandika kwamba huyo bwana alikuwa kwenye kituo cha Television, kaandika kwamba alikuwa akifanya kazi kituo cha habari, P'se!!

    ReplyDelete
  5. Mtoa maoni Anonymous wa 8.55pm
    Unaejiita Mbegu wewe ni Mbegu uliyesoma Lugalo Primary School?

    ReplyDelete
  6. Historia ya picha hii!


    Mohamed Ali alkuja Tanzania kama mjumbe wa Marekani. Mwaka huo Marekani alikuwa inafanya kampeni ili nchi zisusie michezo ya Olympic yaliyofanyika Moscow, USSR. Sasa ilikuwa ilikuwa ni uvamizi wa USSR nchini Afghanistan.

    Huyu anayekunja ngumi alikuwa kocha ngumi Tanzania. Ninamkumbuka kwa jina mmoja tu, BADRU.

    ReplyDelete
  7. kumbukumbu nzuri

    ReplyDelete
  8. Badru Hussein aliyekuwa kocha wa Bandari alimkunjia ngumi Mohamed Ali uwanja wa ndege siyo Kilimanjaro Hotel. Huyo pichani si Badru Hussein inawezekana akawa Mzee Sheni kama alivyosema anon..

    Mohamed Ali alipata mapokezi ambayo yalimfundisha kuwa Tanzania ilikuwa mstari wa mbele kwenye ukombozi wa kusini mwa Afrika. Waandishi wa habari walimuita kikaragosi cha wazungu.

    Wanaokumbuka tunaomba habari zaidi.

    F M Tungaraza.

    ReplyDelete
  9. Anon uliyesema huyu Mzee alikuwa anaitwa Mzee Sheni umenikumbusha. Kama sikosei huyu Mzee Sheni wafanyakazi wenziye pale Kilimanjaro Hotel walikuwa wanamuita jina la utani Mzee Binaisa.

    Asante,

    F M Tungaraza.

    ReplyDelete
  10. Issa Michuzi huyo ni Mzee Sheni, Sio Badru Issa michuzi pic zengine wewe ulikuwa ukisoma bado, unapoweka fanyia uchunguzi kwanza. Issa Michuzi tunaomba tafuta za Malcolm X alipokuja Tanzania ila namjuwa mtu anayo ya Malcom X na Abrahman Babu aliyekuwa NCCR walipiga pamoja.

    ReplyDelete
  11. Ni mimi Mbegu tena narudi Kwanza napenda kumjibu jamaa aliyeniuliza kama nilimaliza Lugalo la Mimi nilimaliza Karume Primary School na ndio maana namjua vizuri sana huyo mzee Sheni kama nilivyosema ni mjomba wangu na lingine ni kwamba hiyo picha sio kama hapa kwa michuzi ndio mara ya kwanza kuiona niliona na Nakumbuka Mohamed Ali alivyokuja hapo Bongo, Picha hiyo ilitolewa kwa mara ya kwanza ktk Gazeti la Michezo lililokuwa likitolewa kila Mwezi kama sikosei na hata Marehemu Mzee sheni mwenyewe alikuwa na Original copy ambayo alikuwa ametunga Sitting Room kwake. huyo jamaa aliyesema huyo Badru si kweli, Mdogo wake mzee badru tunayehapa Coventry, UK Khamisi Badru naye amekataa, Ni kwamba huyo ni mzee Sheni na kama mdau alivyosema wafanyakazi wa Kilimanjaro wakimtania Binaisa. Ana Watoto Watatu Moshi Sheni, Selemani Sheni na Tabu sheni ulizia Kagera Rangers Mwembechai.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...