hapa ni sekondari ya old moshi katika njia ya kuelekea kibosho

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 26 mpaka sasa

  1. Hellow Bro Michuzi nashukuru sana kwa kunikumbusha shule yangu hii niliyosoma A'Level PCB almost twelve years ago,the gate and fance still the same as I left them,Hope wenzangu niliokuwa nao miaka hiyo wakina Somo Tesha wamefurahi pia kuona hii picha ya shule maridadi,Thanks Michuzi kwa kazi nzuri ya kutuhabarisha na kutukumbusha Tulikotoka.

    Mdau,Minnesota,USA. (Sio mbeba Mabox lakini msije kuchonga washika Dau..!!)

    ReplyDelete
  2. Hili ndio chama langu PCB form V & VI, masela wa Old School aka Old Moshi Sec mko wapi? Inabidi tushushe bonge la Reunion moja bomba sana na totoz zote bomba kutoka Weruwetu, Kibosho, Machame Girls, Mawenzi. Mademu mliokuwa mnasoma Moshi Tech hatuwataki mlikuwa mmekomaa sana kwa kubeba vyuma hahaha tehtehtehteh

    ReplyDelete
  3. Hapo ndipo nilipokomaa na PCM miaka 20 iliyopita, geti halijabadilika!

    ReplyDelete
  4. Jamani mnakumbuka donati za bubu??Mama recho je??Big Up Saaana Michuzi kwa kutukumbusha Old School yetu. For Sure tumejifunza mengi enzi za Msele,Rambau,Kimaro Mbao,Mama Nkya,Samki,TOD,Kirumbuyo na wengine.
    Bati lilikuwa likigongwa tu,inabidi uanze mbio,otherwise una-miss na inabidi uwahi kwa mama Recho kupiga wali wa 200.Naikumbuka sana TV ya Ushirika. Kwani tulikuwa tunajiburudisha nayo siku moja moja tukiwa tumechoka kupiga buku.
    Jamani mnayakumbuka mapambano(Vyoo vya Shimo)??Ukiingia mapambano lazima uvue shati. No way!!Baada ya shughuli lazima mtu ajue tu kwamba umetoka mapambano. Anyway,shule nayo ilikuwa mtindo mmoja na namshukuru Mungu kwamba ilikuwa inasogea na ilitutoa mpaka hapa tulipo. Thanks Michuzi and Big up Saaaaaana once again......

    ReplyDelete
  5. Wazee wa GOLD MOSHI mpoooo!
    Umenikumbusha mbali kinoma michu!
    KG.

    ReplyDelete
  6. Shukran bw Michuzi, umenikumbusha mbali sana. Nilipiga buku hapo enzi za headmaster akiitwa Mzee Asseri (msela hakuwa na noma na mtu) na makamu wake Munuo (alikuwa na mustachi fulani ambao point zake zote za maana zilikuwa zimejificha humo, akitaka kutoa point lazima anyonge mustachi kwanza!) Kisha kulikuwa na Discipline Master akiitwa Temba, siye tulimwita "Mwovu Temba" maana alikuwa katili hasa! Christopher ole Sendeka alikuwa rais wa wanafunzi akinitangulia darasa moja (akiwa Form 6 wakati huo), na alipomaliza muda wake alimwachia uongozi classmate wetu mmoja mpole sana, Horogo John (sijui yuko wapi siku hizi). Chama kilishika hatamu, mwenzetu aliyekuwa kiongozi wa umoja wa vijana wa CCM akiitwa Charles Mukocho alikuwa na nguvu kwelikweli, karibu sawa (au zaidi) ya Headmaster! Jamaa zangu tuliokuwa pamoja bweni la Kibo block 8 kina Marco Misana, Lawi Masembejo, John Kilasi, John Kulwa, Rashidi Hemedi (Baruti), Halfan Chambo, Mesaka Kyando, Patroba Kyando ambao wote sijui wako wapi siku hizi!

    Lile duka letu pale Kitandu (kwa Muro) bado lipo? Na baa ya mbege "Kibom Mwafrika Bar"! Hayo ndiyo yaliyokuwa maeneo yetu ya kujidai!

    Michuzi umenikumbusha mbali asante sana!

    ReplyDelete
  7. ohh yaani nimefurahi sana hapo ndio kwanza wasichana wa pili sie kuaingia Old moshi. it looks exactly the same. nimemiss sana. wadau mliomaliza mwaka 1999 tutafutane basi. Email yangu ni gweeny_mbaga2006@yahoo.com. love u all

    ReplyDelete
  8. Michu asante umenikumbusha shule yangu A-level PCM 2000.Big up sana,anywa hilo geti linanikumbusha tlikuwa tuna simama hapo kuangalia vijana wa mwema wanavyofundishwa ukakamavu opposite na geti hilo, kuna chuo chao.thanks man

    mdau-canada

    ReplyDelete
  9. Hahahahaha, this reminded when we use to go for debe(Kijidisco). Weruweru and Old Moshi. Some of us were lucky and got ourselves some smart guys......lol. That was 8 years ago.

    ReplyDelete
  10. Kweli michuzi unajua kuchokoza watu mi nimetulia miaka mingi sana katika hii blog yako lakini hapo umenigusa ile mbaya , nimesoma hapo form one mpaka form six 81-87 science one PCM, hapo getini naingia night kali nishalewa mbege sanaa!
    hehehehehe
    nawatafuta watu hawa tony jannah, samson mpangala,lucas mbago,Ngowi Donald,andrew shimba tasafavali mniandikie patltp@yahoo.co.uk

    ReplyDelete
  11. Michuzi hii ni Bomba sana, dah umenikumbusha Mbali nilikuwa pale 1989 to 1991, Mambo ya Bomba Place, Mama Recho, Mbege kijijini dahh

    ReplyDelete
  12. duh , michuzi unajua kugusa watu na hii blog yako,hiyo shuke yangu bana, maintellectual wa kumwaga wanatoka humo, hehehe
    .....sema watoto wa ashira walikuwa wanatuzingua sana na unifomu zao za vizibau kama kunguru...siku hizi wote choka mbaya....chama la watu wa hanang 28 mpo pillip kiure,kaakufui donald,uhuru wanka,hassan ernest tall,athumani naneka,tito nombo heehehheheheheh! duh maisha hamna tena! michuzi ungeingia ndani upige stadium zetu kuna viwanja viwili vya mpira humo morumbi na pacaembu hata ukiingiza bwawa la maini humo hamtoki bao tu!

    ReplyDelete
  13. Michuzi umenikumbusha mbali sana, machizi wangu wa Shengena(1986 - 1988) hawa wapi? Salim Mbwana, Mikidadi Hamza, Nobert Mbowe, Tony Jana, Beatus Mwaigomole, Samson Mpangala, Andrew Shimba, Goodluck Mwagile, Patrick Kamera, Julius Sabuni, David Sengati, Victor Gabone, Fidelis Newa...na wengine Moddy Hamisi, Peter Masele(Jah Luna), John Kilas, Job Msuya, Abeid Kasanga, Peter Simeo, duh listi ndefu, tutafutane basi!

    ReplyDelete
  14. Hapa Michu umegusa mahali yake babake.
    Mida ya jioni kama buku halipandi au jmosi naingia kitandu kula mbege au gongo. Kama sina kitu navuka korongo naingia Ushirika kuwatch TV na kama kuna harusi lazima nizamie. Ushirika ikiwa na gemu kwenye ligi naenda panda juu ya mti au naruka ukuta kama wadau wa shengena washamuwahi mshkaji kilema na kibaskeli chake!
    Usiombe utoroke bila uniforms afu mtaani ukutane na Mdudu Mwenguvu, Muovu Temba, KJJ, Mama Nkya au Mangesho- umekwisha. Walimu poa walikua Mama Semiono(RIP) na TOD.
    Wilson Gideon (Mbokomu),Emanuel Mbilinyi, Gerald Mtui,Abbas Mchemba, Lawrence Sebastian, Ben Maeda, Omari Mandari (Dewji), Gurisha Eliwangu, James Mrema, Ernest Mbugu, Nick Mtui na wengine mliomaliza
    early 90s tuwasiliane kupitia wakudata@hotmail.com kama mmenisoma hapa.
    Thanks Michuzi.

    ReplyDelete
  15. katika picha uliopiga hujawahi kupiga picha kama hiyo toka uzaliwe michu....
    umenigusa ile mbaya mazee...

    mi pia nawatafuta watu hao hapo juu, anayemuulizia uhuru wanka alifariki kule mbeya akifanya kazi manispaa ya mbeya huyo alikuwa ngombe wangu and he was a great guy in person and a great footballer! naishi UK but will be glad to communicate with people from that fantastic school.....81-87
    peter masele,david sengati,julius sabuni,toni janah,samson mpangala,andrew shimba,deogratius kabuteni,bennet charles,beatus mwaigomole,dudu,ally amir etc,just a line to say hi.. hehe...
    hivi umoja wa wanafunzi waliosoma hapo bado upo? hapo pametoka vichwa vya kufa mtu michu paone hivo hivo pachafu pachafu
    donmicky@yahoo.co.uk

    ReplyDelete
  16. Duh! brother Michu hiyo ndiyo ilikuwa chama yangu(87-89).Shengena ndiyo bweni yangu karibu na Ushirika. Sikufahamu kuwa Mama Semiono aliishafariki.Ni miaka 20 so tuwasiliane ktk
    eli_20012000@yahoo.com( jamaa kibao kama akina Peter mang'enya, Yohana John, Karim Mattaka, Mzungu Hemed, Yonah Nko, Saidi Bafe, Hussein Rashid, Gilbert Chawe, Hamis Ramadhan na wengine tuwasiliane)

    ReplyDelete
  17. JAMANI NAOMBA MWENYE UHAKIKA KUHUSU MAMA SEMIONO ATUHABARISHE. ALIKUWA BOSI WANGU KAMA ACADEMIC MISTRESS NA MIMI KAMA ACADEMIC PREFECT.
    MICHUZI HIYO INAITWA GOLD SCHOOL PALE MWANZO TULIONGEZA G NAONA WAMEIFUTA. WADAU WA 1995 - 1997 TUTAFUTANE JAMANI MWE.

    Eng. JUMA H MSONGE aka BWANGA

    ReplyDelete
  18. Aisee juma uko wapi wewe? nakukumbuka kwa hilo jina Aisee its long time. tuwasiliane kwa kupitia gweeny_mbaga2006@yahoo.com

    ReplyDelete
  19. Mwenye info za Ngoromiko aniwekee humu, alikua mnoko sana na revenge yangu ni kumpa dinner siku nikitua bongo!

    ReplyDelete
  20. Sio mchezoo Michuzi long time sanaaa unanikumbusha ,enzii za mzee Ramwasi na Lisapita (mtaalam wa kamera)wapi Mbwax,Rwakataree,Ras Coby,Festojr,Luhwa(Dalali),Tibaijuka,Arajigana masela wooteee wa Meru16.

    ReplyDelete
  21. Michuzi wanitoa machozi kwa uchizi wa picha hiyo!

    Enzi za Baba Mtui (RIP). Bweni Shengena (aka hospitali). Mwalimu wa bweni Kimaro 'mbao'!

    Mwenguvu secondmaster!


    We acha tu.

    ReplyDelete
  22. AnonymousMay 17, 2009

    Brother Michuzi nashukuru sana kwa kuweka picha ya geti la Gold Moshi. Nilikuwa hapo 91/94..Thos are the most memorable moments of my life. Reading down the comments I discovered that I share the same passion with a lot of great guys. I took some pictures five months ago that I would like to share with other Die Hard Old Moshi funs. I started a facebook group Old Moshi Secondary School is an open group so anyone with facebook account can join. Aliyeulizia mwl Mchilli AKA Ngoromiko siku hizi yupo Jangwani Sec Dar es Salaam. Nilipita Old Moshi nikakutana na Mwl Chisuse AKA "Royal Sumayi" wakati ule Royal Sumayi ilikuwa inashindana na Fresh Shamba lakini watoto wa wakulima tukitoka shule usafiri wetu ulikuwa Gogo...Treni na mabasi tuliyaona tu kwa mbali. Kulikuwa na wadau wengi na kama mmoja wetu alivyosema Old Moshi ilitoa vichwa vya nguvu ambavyo vimetapakaa dunia nzima. NAJIVUNIA KUWA MMOJA WAPO. Unaweza kuwasiliana nami kwa barua pepe mtafiti@gmail.com.
    Kila la kheri wadau

    ReplyDelete
  23. Imenikumbusha mbali sana. Nilisoma shule hii kuanzia 1986 hadi 1988. Baadhi ya jamaa tuliokuwa nao ni kama Gidson Marco, Ramadhani Mwakitubu, Charles Mesha, Oscar Bukuku, na wengineo wengi. Nakumbuka siku ya graduation kuna jamaa walifakamia gongo hadi wakazimika. Nakumbuka sana sehemu jirani kama Ushirika, CCP na KCMC ambako tulikuwa tunakwenda kujiliwaza. Imepita miaka mingi sana lakini hi ni kumbukumbu nzuri.

    ReplyDelete
  24. AnonymousJune 11, 2010

    any of you guys on facebook join us in the group OLD MOSHI SECONDARY SCHOOL. we are trying to see what we can do for the school join us there. I was there 90-92 PCM.

    ReplyDelete
  25. AnonymousJune 15, 2011

    OLD IS GOLD. never let life let udown

    ReplyDelete
  26. Mimi nimewakumbuka mademu wa old moshi Shamimu na Zamzam hivi wapo wapi kila mtu alikuwa anawataka.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...