Jeshi la Polisi Nchini limetoa onyo kali kwa wananchi wanaojichukulia sheria mikononi na kuwaadhibu watu wanaotuhumiwa kupora mali au fedha mitaani kwa kuwaua, kuwatesa vibaya na kuwajeruhi au kuwachoma moto hadi kufa.

Tabia hii mbaya inaendelea kujipenyeza na kujijenga ndani ya jamii ya Tanzania kwa dhana potofu ya kupamabana na uhalifu.

Onyo hili limetolewa leo na msemaji wa Jeshi hilo Kamishna Msaidizi wa Polisi Esaka Mugasa alipokuwa akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake baada ya kukithiri kwa vitendo hivyo katika maeneo mbalimbali Nchini.

“Tabia hii ikiachwa na kuendela ndani ya jamii yetu itazaa tabia ya ukatili (culture of violence and sadism) na kuwafanya watu kutokuheshimu utawala wa sheria na kutumia njia za mkato ambazo si kwamba ni hatari kwa amani na utengamano wa nchi lakini pia si njia sahihi ya kupamabana ana uhalifu”, alisema Bw. Mugasa.

Msemaji huyo wa Jeshi aliendelea kusema kuwa wananchi wanawajibu wa kuimarisha usalama wao, amani na utulivu huku wakiheshimu katiba, sheria na kanuni za nchi hii ni kusema kuwa hakuna uhuru usio na mipaka na hakuna haki isiyo na wajibu.

Bw. Mugasa alisisitiza kwamba pale mhalifu atakapotenda kosa ni wajibu wa mwananchi kumkamata na kumfikisha katika kituo cha Polisi na kumfungulia mashtaka lakini kujichukulia hatua mikononi kwa kuamua kumuua au kumjeruhi ni kukiuka haki za binadamu hivyo basi yeyote atakayebainika kufanya hivyo atachukuliwa hatua kali za kisheria”.

Aidha Kamanda Mugasa alimalizia kwa kuwaomba wananchi wazidi kushirikiana na Jeshi hilo katika swala zima la kupambana na uhalifu ikiwa ni pamoja na kuunda vikundi vya ulinzi jirani katika maeneo yao ya makazi ambayo ni kata na Shehia.

Kwa vile wananchi ndiyo wanaobaini kero za uhalifu katika maeneo yao wakianzisha ulinzi jirani ambao hauna gharama kubwa itawasaidia kushirikiana bega kwa bega na Jeshi la Polisi na kupunguza misuguano baina yao na vyombo vya dola na kujenga imani na vyombo hivyo .

Maeneo ya Kata ya Upanga Mashariki mtaa wa Kibasila jijini Dar es Salaam kuna kikundi cha Ulinzi jirani kijulikanacho kwa jina la Ulinzi wa Jamii Kibasila (UJAKI) ambacho kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi kimeweza kupunguza uhalifu katika maeneo hayo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Serikali kupitia vyombo vyake vya dola ijipange vzr kwa kuongeza mbinu na nguvu za kukabiliana na uhalifu, huu ndio ufumbuzi wa swala hili na sio kuwapiga mkwala wananchi....Ukikumbwa na vijana ambao wapo tayari kukupiga bisibisi, kukuchoma kisu au kukupiga nondo just because haujawapa hela kdg ya mboga(Tsh 1000) au hauna simu wanayoitaka, ndio utajua umuhimu wa sheria mkononi na ukibisha wakamate na uwapeleke polisi uone km kesho yake haujakutana nao mtaani, na imagine kitakachotokea kwako ni nini?
    So, Serikali ijipange vzr na sio kupiga watu mkwala.

    ReplyDelete
  2. Sasa kama serikali haifanyi kitu watu wafanyeje jeamani. Kibaka anakamatwa leo kesho yupo mtaani tena anapokonya watu


    Uwizi unarudisha nyuma maendeleo ya watu sana...Unajikwinja kunua kasimu kako kesho kanaibiwa

    Ukitaka kujua serikali haina maarifa ni pale unapoona kibaka akiiba anakimbia polisi anajua huko ndio atapona wakati nchi zenye sheria kali mtu akifanya kosa hataki kuwaona hao police kabisa.
    Akiiiba anakimbilia mitaani sasa ujue vibaka washazoea....msipofanya kitu kuonyesha kuwa wakiiba wanafungwa na kulipa vitu vya watu basi watabondwa wengi tu

    ReplyDelete
  3. Jambazi anaingia nyumba yako eti umshilie mpaka polisi waje, huu ndio upumbavu, unamwasha na risasi au mapanga kwanza kwani usipofanya atakumaliza wewe baadaye ndio unawaarifu hawa jamaa kuja kuchukua mzoga wao.

    ReplyDelete
  4. NANI AANZE KULAUMIWA KWA KUJICHUKULIA SHERIA MIKONONI, MWIZI AU MUIBIWA? MWIZI ANAYOHAKI YA KUPELEKA MADAI KWENYE VYOMBO VYA SHERIA KAMA HARIDHIKI YELE ANAYETAKA KUMPORA KUWA NA KILE KITU ANACHOONA YEYE PIA ANA HAKI NACHO. HIVYO AENDE MAHAKAMANI KAMA MAHAKAMA IKIONA ANA HAKI BASI ITAMPA ILE MALI AU ITAGAWA SAWA KATI YAO. ULE MUIBIWA NANAYOHAKI YA KUJILINDA NA KUZUIA UHALIFU WA BAADAYE USITOKEE HIVY KWA KUSHIRIKIANA NA WATU WENGINE KAMA WAHALIFU WANAVYOSHIRIKIANA WANAYOHAKI HAKI YA KUMDHIBITI MHALIFU. JAMBO MOJA LINALOHITAJI UFAFANUZI NI KWANINI MHALIFU ANAPOMSHAMBULI MTU MWEMA INAONEKANA KAMA NI MCHEZO WA KUIGIZA NA KUPEWA SIFA ZA USHUJAA NDANI YAKE, JE NI KWA SABABU UHALIFU NI CHANZO CHA AJIRA KUBWA (POLISI, MAHAKIMU, WANASHERIA, ASKARI MAGEREZA NA HATA WAPISHI WA WAFUNGWA ) HIVYO KUWAADHIBU NJE YA VYOMBO VYA SHERIA KUNAWAKOSESHA KAZI HAO WAAJIRIWA? KWANINI MTU AIJERUHIWA NA MHALIFU HUWA HAKUNA KELELE ZA KULAANI KAMA ZILE ZINAZOTOLEWA ANAPOJERUHIWA MHALIFU?

    ReplyDelete
  5. inakera sana unajua? eti mtu anakamatwa kwa kosa labda la ubakaji tena watoto wadogo baada ya siku au siku haiishi jioni unamuona mtania anakatiza na kashfa juu kuwa eti police ni washkaji zake,hata kama ni wewe ni mzazi wa yule mtoto alibakwa utashiriki kwenye lile zoezi lilotokea ka kuchoma kituo cha police. Au unampeleka mhalifu hakuna hatua za kinidhamu zinazochukuliwa, na ikiwezekana wao police wabaya wenye uroho wa pesa nawajihusisha na vitendo vya ujambazi, au unatoa taarifa umevamiwa wanajivuuuta mpaka wakija tukio limeisha mda mrefu, hapo si hasha utajiuliza kulikoni kitokeo cha hapo raia hasira zinapanda wanajionea wamalize mzizi wa fitna, ufupi imani imepungua kwa polisi wetu.full stop

    ReplyDelete
  6. Ikiwa serikali haifanyi kazi inayotakiwa sisi wananchi tutajilinda wenyewe.mtu anajipendekeza na mali yangu shoka la shingo linamhusu.
    Kama tabia ya kuchukua sheria mkononi imekithiri ina maana ujambazi,mauaji yamezidi pia.Na serikali haifanyi chochote kusaidia wananchi.
    KAMA WADAU HAPO JUU WALIVYO SEMA UNAMKAMATA JAMBAZI UKITEGEMEA ATAFUNGULIWA MASHTAKA KESHO UNAKUTANA NAE MITAANI ANA PORA KWENGINE NA WEWE UNAKUA MOJA KATIKA TARGET ZAO.

    ReplyDelete
  7. HAPA NINA MASHAKA. AIDHA HUYO POLISI ALIYETOA HIYO KAULI ANA TABIA YA KUJIGEUZA NA KUWA JAMBAZI WAKATI WA USIKU, AU ANA MTU, KIKUNDI NA HATA PENGINE NDUGU ANAYEJISHIRIKISHA NA MAMBO YA UJAMBAZI.
    DUNIANI KOTE SIKU HIZI SUALA LA WANANCHI WANAOVAMIWA NA MAJAMBAZI KUCHUKUA HATUA AU SHERIA MKONONI DHIDI YA MAJAMBAZI, LINAKUBALIKA.
    KWA NINI USIFANYE KAZI UIBE MALI ZA WATU KWA KUTUMIA SILAHA, PANGA NA HATA SILAHA KALI?
    KITU GANI KINACHOWAFANYA WASILALE USIKU NA KWENDA KUVUNJA MLANGO WA MTU(UHARIBIFU WA MALI) NA KUTAKA KUIBA AU PENGINE KUIBA HUKU WAKIWA NA ngao ya polisi KWAMBA HAWAWEZI KUCHOMWA MOTO.
    ACHENI HIZO. HII DAWA YA KUCHOMWA, KUPIGWA IPO TANGU KABLA YA UHURU NA INATAKIWA IENDELEZWE KWA NGUVU ZOTE.
    KUMBE NDIYO MAANA BILALI KAINGIA MITINI? MTINDO WA KULINDANA BADO HAUJAPITA TUUU...DAMN!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...