MH. SPIKA AFUNGUA KIKAO NA KUSEMA JK AMEKUBALI OMBI LA KUJIUZULU KWA WAZIRI MKUU MH EDWARD LOWASSA NA KWA KUSEMA HIVYO BARAZA LA MAWAZIRI LIMEVUNJWA ATOMATIKALI NA NDIO KUSEMA HALIKO TENA.
NA KWA KUWA SERIKALI HAIKO MH. SPIKA AMESITISHA SHUGHULI ZA BUNGE HADI SAA KUMI NA MOJA AMBAPO KIKAO HICHO KITAENDELEA. SHUGHULI HII IMECHUKUA DAKIKA 6 TU

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. Ahsante kwa taarifa! Nilikuwa najaribu ku-tyuni RTD kwenye kiredio changu cha Ofisini ili nipate News za new PM!

    ReplyDelete
  2. Lazima tujue tunaenda wapi maana hawa viongozi hawaridhiki na mali walizonazo wanataka zaidi... Tunataka kujua mengine mengi ambayo yanafichwaga kwaajili ya takrima... Angestahili kuvunja na Bunge zima UCHAGUZI URUDIWE TENA...

    Hamna mwenye afadhali... WANATIA AIBU SANA...

    ReplyDelete
  3. UKISOMA MANENO YA WAZIRI MKUU UTAJUA JINSI MANENO YA MTU WA KUTAPATAPA YANAVYOKUWA. BADALA YA KUTOA HOJA YENYE NGUVU ANALALAIKA KAMA MTOTO AU [MAMA]. ETI, NAJUA TU NI HUU UWAZIRI MKUU NDIO WANAONA NIONDOKE.

    ANATUHEFUA KWELI. KAMA NCHI ZA WATU WAKIPIMA HOJA ZAKE ZA KUJITETEA, UKIACHA ILE YA KUTOHOJIWA, ANAONEKANA KAMA MTU ASIYE NA POINT KABISA. KAMA NI MAHALA PA SHERIA ANGESHINDWA KABISA.

    KWANZA WANGEMHOJI ANGEWASUMBUA KWA KIBURI CHA UWAZIRI. MBONA YEYE HAKUMSHAURI JK ASIMFUKUZE KAZI BALALI? JE, ALIHOJIWA WAPI?

    MKUKI KWA NGURUWE? KWA BINADAMU MCHUNGU?

    MICHUZI, MFIKISHIE HIZI BWANA.


    Mdau mwenye machungu ughaibuni.

    ReplyDelete
  4. Mzee 6 ulikataa nini ulipombishia zitto kabwe jana? we spika usiwe dikteta acha wabunge wetu wapinganeeeee humo ili sisi tupone usikae hapo kwenye kiti kuwalinda wachafu na walowezi watufisidi, we mwanasheria sio dikteta. Nammiss Amina wa chifupa jamani Pangekua hapatoshi bungeni ingekua unyago wa kima kibwebwe mkia aaaah mungu mraham peponi, walijua wakamziba mdomo milele ila mungu atatufungulia njia kwa mama Anna Kilango/malichela naona nae ameshachoka kukaa na majipu yanamuunguza ndani ya kifua. na kila anaeficha ukweli Limkerekete limuunguze na limhilikishe mpaka aseme. Viva wabunge mnaopanua vinywa vyenu bila hofu hata wakiwatoa bungeni mjue umetimiza wajibu wako ipasavyo.
    WABUNGE SEMA sema msiogope sema
    wabunge sema HATUWATAKI MAFISADI WATUFISIDI SEMA

    ReplyDelete
  5. Angalau kwa mara ya kwanza wabunge wa chama tawala pamoja na serikali wameonyesha uzalendo na kuacha ushabiki wa chama. Siku zote faida ya ulafi ni kuharibikiwa na hiyo ndio imetokea kwa PM na wenzake, wakati maskini wa TZ wakilalamikia umeme wao wanachekelea! hata mwenyezi Mungu hawamwogopi. Bila shaka mheshimiwa Rais amepata fundisho na hatathubutu kuweka mawaziri wa namna ile maana CCM ilikuwa inaelekea pabaya.

    ReplyDelete
  6. Sasa nani na nani atarejea, sidhani kama raisi Kikwete atawarejesha wote kuacha hao walijiondoa.
    Nafikiri ingekuwa muda muafaka wa kuchambua na kuondoa wale wote ambao wana kashfa na pia kama ingewezekana, sijui kama muda utatosha, angejaribu kufuatilia historia nzima za hawo atakaowachagua. Unajua siri ya mtu, na tafsiri yake imeanzia katika mlolongo mzima wa maisha yake.
    Ni vyema watu wakajua kuwa kiongozi mzuri anajulikana kuanzia udogo wake na mlolongo mzima wa nini alichokuwa akikifanya katika maisha yake, hadi hapo alipofikia. Mwizi/fisadi atajulikana tu, kwani hiyo ni tabia iliyojijenga tangu huko alikotoka. Tuchague viongozi wenye uchungu na nchi, wenye upendo na wasiojali ubinafsi. Je kweli watu wa namna hii hawapo?

    ReplyDelete
  7. Hi mambo ya kulalamika hakuitwa wala hata haina maana.

    Tume ilishasema kua mwenye ushahidi apeleke, yeye anang'ang'ania aitwe, anamdengulia nani??

    Iliytakiwa aende mwenyewe bila kuitwa, hizo tabia za kuringa ringa wanaume kamili hua hatunaga.

    eti "SIKUITWA", khaaaaa!!!!!!!, huyu jamaa kweli maji shingoni

    ReplyDelete
  8. hiyo inaitwa MENEMENE TEKELI NA PERESI ee bwana we juzi mzee wa kunajimu aliitoa hiyo kwenye luninga kumbe alikua anamtabiria mtu maono aloyaona danieli walah kitanga kilitokea ukutani dodomyaaaa

    Mungu ibariki Tanzania na wote wanolipa fidia pasi na kujua ilhali tu washibishe matumbo yao tangu lini mzalendo akawa BEPARI tulijitoa kwenye ubwanyenye sasa huu ni nini mtu kiingiza kiulaini kwa kuwakamua wenzie ee bwana mungu hamtupi mja wake na kila wa aina hiyo mw/Mungu amuumbue kama alivyoumbuka mzee mzima, uliskia wapi haq ya mtu inaliwa, makupe wakubwa mnawapa majina mazuri ya nini eti fisadi? ni KUPE

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...