Nampongeza Rais wetu Kikwete kwa ujasiri alioufanya kwa taifa zima kwa kufanya mabadiliko muhimu na mazuri ya viongozi aliowateuwa. Hongera Mzee Pinda tunakuamini. Pongezi kwa mawazri Chikawe, Mkuchika na wote walioteuliwa taifa liko mikononi mwenu tupeni raha.

Raisi wetu Kikwetu hongera kwa kumpokea vizuri Raisi wetu Geoge Bush sisi wa Tz tulio Mrekani tunaona mafanikio ya juhudi zako kitaifa na kimataifa.
MUNGU IBARIKI TANZANIA

MAMA BISHANGA
OHIO
USA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 29 mpaka sasa

  1. Hi mama Bishanga, kumbe ulipotelea Ohio!!!!

    ReplyDelete
  2. Mama Bishanga umependeza! Ama kweli ulaya ulaya tu, asikudanganye mtu!

    ReplyDelete
  3. Tuwapongeze zadi wabunge wa upinzani, zalio zikalia kidedea issue zilizo wafanya mawazili kutangaza kung'utuka

    ReplyDelete
  4. hivi ni kwa nini mh. mizengo pinda anafanana na robert mugabe??, je wanafanana akili pia??

    ReplyDelete
  5. Ohio bwana wana mambo sana....hayo mambo ya columbus...mh mh mh

    Huyu mama naye amepose huku na handbag ndani ya nyumba....anauza hizo handbag au antafuta naye mchumba???

    Tuelezaane bwana mana USA tena age ain't nothing but number

    ReplyDelete
  6. Huyu mama Bishanga kashapata na uraia kabisa, naona Bush rais wake, hehehe!

    ReplyDelete
  7. Huyu mama Bishanga kashapata na uraia kabisa, naona Bush rais wake, hehehe!
    Ivi yule mkamwana wako wa kuzungu karudi au ulimtimua Jumla, maana vituko vya ITV visihamie home, please.

    ReplyDelete
  8. mama mwenzetu mkimbizi wa kutoka wapi ? au ulikwenda nje kwa hela za umma ? kama mkimbizi huna haki kuipongeza serikali ya ccm, na kama ulikwenda nje kwa hela za ufisadi, kumbuka wabongo vijijini wengi hawana maji safi au matibabu, watoto wengi wanaozalishwa na wakunga wa kienyeji wanafariki kwa sababu ya usafiri mbovu (barabara)kutokwenda penye huduma,wazungu wanatoka kwao kuja kusaidia wananchi vijijini, watu kama nyie ambao si chote wala chote mnadhania bongo ni uwani kwenu.

    ReplyDelete
  9. Mama Bishanga naomba tuwasiliane kwa anuani hii:

    joe.tino@yahoo.com

    ReplyDelete
  10. Mama Bishanga naungana nawe katika kumpongeza Mh Rais kwa hatua za makusudi kabisa alizozichukua katika kuleta utengamano wa kisiasa nchini kufuatia mtikisiko wa kisiasa ulioikumba nchi yetu.Mengi yamesemwa sina haja ya kurudia.Kikubwa hapa ni kutaka kukuunga mkono katika kumpongeza Mh JK na watanzania wote kwa mapokezi makubwa sana yenye moyo wa ukarimu na upendo wa hali ya juu kwa Mh.George Bush na ujumbe wake. Mapokezi hayo yamekuwa gumzo kubwa katika vyombo vya habari vya hapa USA. Heshima waliompa Mh.Bush imeenda sambasamba na heshima ambayo Rais Bush ameipa nchi ya yetu kwa kufanya matukio mawili makubwa na ya faraja kwa nchi.
    1.Ameweza kusaini msaada wa karibu bilioni 700 za kitanzania kiwango ambacho kimeelezwa kuwa ni kikubwa kupata kutolewa na nchi hii ya Marekani kwa mara moja katika misaada yake kwa nchi yoyote duniani.Ni heshima kubwa sana hii.
    2.Pili kitendo cha kuamua kukaa Tanzania kwa siku nne nacho kimekuwa cha kihistoria kupata kutokea katika historia ya taifa hili lenye nguvu kubwa za kiuchumi na kijeshi duniani kwa rais wake kukaa muda wote huo katika nchi moja hususani barani Afrika.Matokeo yake ni kwamba Tanzania imekuwa mdomoni mwa wamarekani wengi kufuatia picha za ziara ya Mh.Bush zinazorushwa kwenye luninga mbalibali hapa Marekani zinazomuonyesha akiwa katika maeneo mbalimbali ya nchi yetu.Katika hali ya kushangaza kabisa hata magazeti ya kawaida kibisa (local newspapers) yamekuwa yakiandika ziara ya bwana mkubwa huyo.Hapa chuoni kwangu kuna gazeti la chuo linalochapishwa kila siku.Katika toleo lake la leo limekuwa na habari za ziara hiyo, huku likiisifu sana nchi yetu,Tanzania. Leo ilibidi niwe na kibarua cha ziada cha kuitangaza nchi yangu kwa maprofesa na wanafunzi wenzangu ambao baada ya kuona kwenye luninga,na kisha kusoma kwenye gazeti la chuo wakawa na shauku kubwa ya kutaka kupata maelezo ya kina kuhusu Tanzania hasa kwa kujua kuwa natoka huko. Katika hali ya kuonyesha kuvutiwa na Tanzania,tayari kuna profesa mmoja ambaye ni mkuu wa kitivo cha elimu,ameonyesha nia ya kuanzisha ushirikiano wa kimafunzo kwa wanafunzi wanaochukua shahada za elimu(exchaging program) kutoka Tanzania na kutoka hapa chuoni.Kwa hiyo ninachotaka kusema ni kwamba ziara ya Mh.Bush, mbali ya kuweka matukio ya kihistoria na yenye tija katika maendeleo ya taifa letu,imeweka pia msingi mzuri sana wa ushirikiano katika nyanja mbalimbali katika ya Tanzania na Marekani kwa siku za usoni.Natoa wito kwa watanzania wote tulioko hapa katika maeneo yetu, tutumie kikamilifu kuitangaza nchi yetu kufuatia ziara hii ya kihistoria kwa watanzania na wamarekani.Na yote haya kama ulivyosema mama Bishanga ,ni matunda ya kuwa na kiongozi mwenye maono makubwa na mikakati ya wazi kabisa ya kuleta mabadiliko makubwa sana katika maisha ya watanzania.Ni wajibu wetu watanzania kuunga mkono jitihada za dhahiri za Rais wetu mpendwa Jakaya Kikwete.Tumpe muda,tutashuhudia mabadiliko makubwa.Mungu ibariki Tanzania,Rais wetu na watu wake!
    Tumsifu Mwasamale
    Bowling Green State University,Ohio,USA.

    ReplyDelete
  11. Wee mama bishanga,tangu lini Rais Joji Bushi akawa rais wenu nyie waswahili mnaoishi marekani?au nimesoma vibaya.Una marais wawili?Mrisho na Joji au una uraia wa marekani.Naomba jibu haraka email yangu ckaluu@yahoo.co.u

    ReplyDelete
  12. Aisee Mama Bishanga kumbe ushatukimbia Bongo ndio maana nina muda mrefu sijakuon ktk runinga sio siri nilikuwa napenda sana ulivyokuwa unaecti ktk runinga mungu akujalie maisha mema upo ulipo.

    ReplyDelete
  13. Mama wa Kibantu naona umetulia tuli. Hizi ni salamu kweli ama ...

    ReplyDelete
  14. anon Feb 19,8:51 paragraph yako ya pili imenisisimua kusikia hizi habari, ni kitu ambacho kitatoa mwanga na kufuta wingi wa uzushi na upotoshi kuwa tanzania iko wapi kwa wale wanaosikia habari za mitaani huko kwa wenzetu.nilikua nchi moja tulikua tunaongea kiswahili super market, mara kuna mzee mmoja akatuuliza mnaongea lugha gani, akasema mnatoka wapi? nikamueleza, hakupata picha, ndipo akaniuliza unatoka hakuna matata? yaani kenya nikajua kweli bado kabisa nchi yetu hatujajitangaza na kujulikana kama wenzetu wa kenya. Hayakuishia hapo akanieleza yeye anatoka syria na palepale alitoa simu yake ya mkono na kunionyesha Picha ya raisi wake Bashar al-assad, mh! pale pale nilijifunza vitu vingi sana kwa kipindi kile alipokua ananieleza juu ya nchi yake na jinsi anavyompenda raisi wake hadi picha imo kwenye gallery yake ya simu. Haya waosha vinywa, sisi tuendelee kupigana madongo humu kwenye blog ya michuziiii eti raisi wake, raisi wako, raisi wao mh! kaaaaazi kwelikweli

    ReplyDelete
  15. We Mama HATIA yaani kwa kuwa we ni Mmachinga basi ndio unawapongeza Mawaziri ambao ni wamachinga wenzio tu-Chikawe na Mkuchika? Wacha ukabila huo!
    Hivi Afrika ya Kusini ulishaondoka sasa uko Marekani!?!
    Hongera.

    ReplyDelete
  16. Mama Bishanga hiyo handbag ya nini sasa?au ni bashara unatangaza? Hongera kwa kuwa mmarekani maana unatushukuru wabongo kwa kumpokea raisi wako Bush.....kumbuka tanzania bado haijaruhusu uraia wa nchi mbili......ohoooooo

    ReplyDelete
  17. Mama Bishanga, tunashukuru kwa kukata ukimya maana wengi wetu tulijua kile kipaji cha uigizaji kwenye luninga kilikuwa ni nguvu ya soda ndio maana nilikuwa sikuoni tena kwenye luninga yangu ya digital. huko mtaa wa Ohio, bado unaendeleza libeneke au nawe unapiga box?

    ReplyDelete
  18. Mama bishanga naona box limekukubali

    ReplyDelete
  19. Kwani huwezi kutoa pongezi bila kuweka picha yako??Sisi vijana wa mjini tunadhani unatubeep!!!!!

    ReplyDelete
  20. teh!teh!sasa mama mbeba maboksi wewe ni mmarekani au mbongo???au umeamua kutubipp sisi hatujali umri.umependeza lakini sasa nimuvuzishie email.sunchekap@hot.cm.tz

    ReplyDelete
  21. Du kwa hali hiyo, Mama bishanga piga box, manake umependeza!! au wewe unaosha vibibi?
    Kweli raisi wako bush anakujali

    ReplyDelete
  22. somo usijali maneno ya viumbe,we ndo umependeza mwali.Afu anayesema usiwaongeza mawaziri wako nani! usimjali somo ,kama ni mbunge wako kapata uwaziri jee unune,hata maaaana!

    ReplyDelete
  23. Chonde chonde mama hao mawaziri waume za watu. Hizo pongezi zimekaa kikabila kabila kama anony wa 12:16 alivyosema. Kuwa mzalendo zaidi au tutakuhisi vinginevyo

    ReplyDelete
  24. TUNAENDA NAUKWELI WATANZANIA UMASKINI AUTO ISHA MAMA BISHANGA NA WADAU WENGINE TOKA UK AND USA WAKITUMA SALAMU WATU WANATOA MAONI YA AJABU ACHENI WIVI ANGALIENI MAISHA YENU WANAKUMBUKA KWAO THAT IS WHY WANATUMA SALAMU MIE MWENYE I WISH KUTUMA SALAMU KWA WATANZANIA WENZANGU ILA NAOGOPA MAJUNGU.TUSHIKAMANE TANZANIA NDIYO NCHI ILIYO BAKI NA AMANI EASTAFRICA TUMUSHUKURU MUNGU KWA HILO TUOMBEANE STOP STOP MAJUNGU MAONI YA MAJUNGU NI YA WATU AMBAO AWAJASOMA.LOWASA,KARAMAJI NA WENGINEO WAFUNDISWE ADABU TANZANIA TUNAANGAIKA WAO WANA KULA PESA ZETU TUSIKUBALI TUNAOMBA WARUDISHE MALI ZETU.
    FROM MANCHESTER UK

    ReplyDelete
  25. mama bishanga fanya umchukuwe mwanao bishanga na yeye abadili life yake .

    ReplyDelete
  26. Hawa ndio ma-celebrity, ma-super star wa bongo. Walitu-intateini lakini, wakati wa ujamaa na TV channel tatu tu nchi nzima-Tanzania. Hongera mama Bishanga, mwnao Bishanga, Kenny, Bikidude, Mzee Small na wengineo. Nyie ndio waanzilishi wa modern theater art in our country. Hakika mta-go down in history as the founding fathers/mothers wa modern theater art and modern local TV-Series in our country. Later on tutakapo re-write history nna uhakika majina yenu yatakuwemo.

    Inaelekea wewe mjanja zaidi ya wenzako walioamua kubaki Tanzania na U-Celebrity without money. Kaa uku tengeneza real money.

    Sasa baada ya siasa na sifa zote nilizokumwagia, naomba nijitambulishe kama mzee mwenzako Kamugisha wa Alabama. Yule baba bishanga si umemwacha bongo. Tuwasiliane basi kwa jjkamugisha@yahoo.com, maana no-disrespecting- umeng'aa!

    ReplyDelete
  27. teh teh teh teh naona watu(midume yenye uchu)mnavyojituma kutoa e-mail zenu kwa huyo mama bishanga,hamjatulia hata hamjali kuwa ni mama mtu mzima au kwa vile anang'aa?
    wabeba box bwana!
    huyu mama nae anajibebea zake box ili afanye maisha kwahiyo msimlaghai na kumchanganya.

    ReplyDelete
  28. michuzi kwanini umebana coment yangu.....

    huyu mama kapendeza na anaonyesha uzalendo. ila hii picha hakupigia nyumbani kwake. ndo maana na hand bag na official shoes. mama hongera ila chako ni chako. si ulimuona chibiriti hapa alivyoonekana jenuini. watu walimponda lakini ndo hali halisi

    ReplyDelete
  29. anon feb 20 6 ;15 hivi hujui kama mzee kamugisha ameshafariki?yet u pretend to be him kisa kumtonesha mwenzio kidonda?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...