shughuli nyingi hasa za usafiri katika barabara ya kwenda moshi zimesimama leo kwani hakuna gari liloruhusiwa kupita toka asubuhi hadi jioni kutokana na ujio wa bush

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 24 mpaka sasa

  1. Seriously...entire day!! kweli tutaendelea kama you can't even commute around? Uchumi utakua vipi?

    ReplyDelete
  2. Tuta inarisha uchumi sio kwa kazi bali misahada,Acha watu wakeshe mtaani kumsubiri Bush

    ReplyDelete
  3. kweli umaskini mbaya sana,kuja kwa bush ndiyo kila shughuli za mji,nchi zisimame.Bush anapokwendaga sehemu nyingine duniani mbona hatusikii ujinga huu?

    ReplyDelete
  4. Kweli huu ni usumbufu kwa wananchi wengi, hasa kutokana na kutokuwa na njia sambamba (dublicating roads) kati ya miji na vitongoji.Say kwenda Airport kuna barabara moja tu. Nyingina inabidi kuzunguka mno au hakuna kabisa. Hali hii ilikuwepo tangu wakati wa Nyerere, na sasa itaongezeka kwani JK ni boss wa AU, na wageni wengi watakuja. Hata kama SS zao sio powerfull kama za Kichaka, SS yetu watafunga njia 3 au 4 hours kabla hata ndege haijatua! Na wanafunzi kibao watakaa barabarani na vibendera....
    By the way, Bush ana sikukuu leo (pamoja na wadau wote wa US). Leo ni President Day. Hongerani kwa holiday pay wote mlioko kazini. Na Kichaka mpongezeni pia.
    Blackmpingo

    ReplyDelete
  5. Mbigiri acha uongo! Nakumbuka nilisoma Forodhani na kila kiongozi wa nje akija, Dar inasimama. Wakati wa UN Presidents` Summits hata NY inasimama.
    Sisemi kuwa hiyo ni vizuri, lakini nchi nyingi hiyo ipo. Hivyo Kichaka tusimuonee bure.

    ReplyDelete
  6. MICHUZI ICHEKI PICHA NA. 6 WAWEKEE WASHIKAJI.
    < http://news.bbc.co.uk/go/em/fr/-/2/hi/in_pictures/7250651.stm >

    ReplyDelete
  7. Nyie mnaojidai uchumi utahadhirika...uchumi gan? hivi mnajua bongo au mnaisikia tuuuu ....people are very slow and easy. Kazi ya siku moja inafanyika wiki nzima kwa hiyo siku moja kupotea sio big deal. Jamani kama uchumu kupotea ulishapotea siku nyingi sio kwa ajili ya bush tu...hata wabunge wakipita mtaa mzima unafungwa sembuse president of the world!!!!!!

    ReplyDelete
  8. Hii ni changamoto kwa nchi yetu inatakiwa iboreshe miundombinu kama barabara ili hata kama kuna ugeni wa kitaifa shughuli nyingine za kila siku ziendelee kama kawaida.Sio kufuja tu pesa za misaada!Tena Bw.Kichaka ametoa mshiko mrefu ngoja tusubiri tuone kama hizo barabara za TDM-S'WANGA,TUNGURU-SONGEA,HOROHORO-TA kama zitajengwa!?au ndio fungu litaenda kwny kampeni kama zile za BOT!

    ReplyDelete
  9. acheni mambo yenu wabongo, huyu mtu kutembelea tanzania ni jambo kubwa sana la kujivunia, mambo mengine wekeni pembeni.

    ReplyDelete
  10. Nyie subirini makaratasi yenu huko, penine sasa hata hao watu wa uhamiaji watawajua mmetokea wapi kuliko siku za mwanzo walikuwa wanafikiria hii nchi hivi iko wapi ndani au nje ya msitu wa Kongo? Lakini sasa aah watawajua kuwa mmetoka East Africa. By the way ujio wa Mzee Mzima hautadhiri utoleawaji au unyimwaji wa makaratsi yenu ya kijani huko mliko. Msifikiri ndio mtapeta kiulaini.

    ReplyDelete
  11. Wewe anon 7:33pm nani alikudanganya kuwa NY inasimama pakiwa na UN summit?watu wengine simjui mnaishi dunia gani mimi niko hapa marekani na bush(si nyc)bush hata atembelee mitaa kumi toka nilipo huwezi kuona watu wanajishughulisha kuacha kazi zao.kila kitu kinaendelea kama vile hakuna cha rais kuwepo ndani ya mji,kitongoji ama kijiji.Haya mambo yanatendeka huko kwetu(afrika,tz) tu,sehemu nyingine huwezi kuona haya mambo.Hii ziara ni ya kiserikali wala haikuwa lazima kila kitu kusimama.Ina maana hata shule zimefungwa sababu ya huu ujio wa bush,ama madaktari,manesi watashindwa kwenda kutoa huduma hospitalini(kama wanazitowa ktk siku za kawaida) sababu bush yupo tz?

    ReplyDelete
  12. bana kuba amri moja funga njia zote naleta jeuri eeh teh teh teh

    ReplyDelete
  13. kaka michuzi, Nakushuuru sana kwa jinsi kazi yako ilivyomahiri, keep it up kaka. Mimi naomba wasomaji mniwie radhi maana kuna mambo nikiyasikia huwa najihisi kama nimedata vile. Huu ujio wa Bush umenifanya niwaze mengi, hatimaye nikamkumbuka sana yule jamaa aliyeandika kitabu cha hekaya za abunuwasi. Mimi nilidhani enzi za "UJUHA"ziliisha na zile hekaya lakini nimengámua kuwa bado tuna majuha wengi sikuhizi tena waliofuzu kuliko wale wa Abunuwasi. Hebu fikiria, mji wa Arusha unahudumia wananchi zaidi ya milioni mbili wa Arusha na Milioni Mbili na nusu wa Kilimanjaro wa uchache, kwa siku zaidi ya wananchi 60,000 hufanya shughuli zao kwa kutumia barabara ya Arusha-Moshi. [hawa ni pamoja na wasafiri wanaokwenda au kutoka mikoa mingine kama Singida, Shinyanga, Mwanza, Kagera, n.k] hebu fikiri ni kero ya jinsi gani hawa watu wanapata, kwa kuwa eti 'rais wa dunia' amekuja. Ok anyway, mtu aweza kudai kuwa si amekuja mara moja tu? [Mgeni aje mwenyeji Akome]kumbuka kuwa kama alivyo Bush na haki ya kwenda kokote atakako hata bwana Michu unayo hiyo haki madhali binadamu wote ni sawa. Kwa kuwa USA imepiga hatua sana kwenye teknologia, kuna sababu gani ya kuwawekea kizingiti hawa maskini 60,000 ambao hawajui kesho itakuwaje? kwanini USA isitumie teknolojia yake kuepusha kero hizo kwa wadanganyika? Ni nnini hatma ya hawa watu karibu milioni nne watakaoathirika na kuzuiliwa kwa mtiririko wa biashara? hizo dola alizomwaga Bush zitawafikia kweli kabla hawajagadunia? wauza maandazi pale kiboriloni leo wanalala njaa, wauza maparachichi pale kwa sadala leo wanalala njaa au wale mtaji [maparachichi] wauza nyanya pale maji yachai inabidi wazile wanywe maji, walale. wauza samaki pale usa river nao kasheshe, wakina mamayoyoo pale sanawari nao inabidi zile ndizi mbivu ziwe kitoweo laa sivyo karagabaho. Waliokuwa wakisafiri kuwahi shughuli zao, interview za kazi nk kupitia hiyo njia nao inabidi wawe wapole, Wale waliokuwa wakienda hospitali KCMC, Mount Meru, Machame nk kuchukua marehemu wao, inabidi watie kondoo maana kaburi halilali wazi kwa mila za kaskazini, waliokuwa wakisafirisha mbege ya kibosho kwenda Singida inabidi wawagawie waandamanaji wanaomsubiri Bush. wapiga debe wa vi-ford leo inabidi wakabe ili kufidia siku n.k Yote haya ukimweleza Bush na wenzie ngozi nyeupe wanasema "kwa kweli sijaona majuha kama hawa" Juzi Bush alifurahishwa na watu waliokuwa wamejipanga njiani kumlaki maana huko kwao kama siyo kununiwa basi ni kuzomewa kwa kwenda mbele.Anyway, Mgeni aje wenyeji wakome na wengine wapone.

    Sisi tumenyanyaswa kiasi cha kutosha, tumepuuzwa kiasi cha kutosha na tumedharauliwa/kuonewa kiasi cha kutosha UJUHA wetu ndio umetusababishia!
    Mbona hawa waheshimiwa Bush, na wababe wengine wakienda nchi za wengine hakuna hizi kero za kiaina? Ujuha wetu umesababisha hizi kero kwa mipango mibaya na ya kijuha tuliyojiwekea. kwa nini tuwe na njia moja tu ya uhakika ya kaskazini kuunganisha hii mikoa? vita ikitokea [hatuombei] lakini itakuwaje? Naomba niangalie mbali zaidi jinsi Mji wetu wa DSM ulivyo tengwa kwa utallam wa kijuha ule ule! Unajua uki-block barabara ya morogoro eneo lolote kati ya chalinze na mbezi utasababisha ziki dsm? Hebu fikiri kwa nini kwa kipindi takriban miaka 40 hatukuwa na daraja la mkapa? na baada ya hapo kwa nini bado usafiri wa kusini haujatengemaaa? Pesa za bush nasikia zitasaidia hata barabara, ila mipango tunayo? au ujuha uleule?
    Sasa wadau wanaohusika na miundombinu hebu tujadiliane tufanyeje ili angalau Magufuli arudishwe barabarani? Tuacheni ujuha jamani, hivi huyo Chenge amefanya nini tangu apewe hiyo dhamana? Kuna tazizo la ujuha katika mipangilio ya mambo yetuau nakosea jamani? Ujio wa bush sasa utuondoe kwenye ujuha, tuache kuwa majuha. Katika mchakato wa mafisadi wa richmonduli eti nilisoma kuwa katibu mkuu wa wizara ya fedha alikiri kudanganywa na Richmond huo sio ujuha?, eti karamagi nae hakufahamu utapeli wa richmonduli? huo nao sio ujuha? Eti lowasa hakuitwa kwenye kamati ya mwakyembe wakati kamati ilikaribisha kila mtu anayejua kuhusu richmond ajitokeze, hayo malalamiko hayadokezi ujuha? pamoja na ufisadi pia kuna ujuha ambao nadhani ndo unatuponza wengi, eti kamati ya Mwakyembe imemsamehe lowasa huo sio ujuha? na hatima yake mtego wa panya unawanasa waliokuwemo na wasiokuwemo! kwa sababu ya ujuha

    ReplyDelete
  14. Kufunga barabara ya Arusha-Moshi ni upuuzi mtupu tena ni uchuro kabisa. Utaniwia radhi bw Michuzi, hivi akija Bushi kwetu ndio kusema hata wagonjwa wanaozidiwa pale Mount Meru Hospital hawawezi kuwahishwa KCMC kwenye rufaa, ati kisa kaja Bushi? Bushi wa nini sasa huyo, kutuua? Huo ni ulimbukeni kabisa, samahani bwana Michuzi kwa lugha hii, lakini huyo aliyeamua au kukubali ushauri wa kipumbavu wa kufunga barabara muhimu kama hiyo kwa siku nzima ni mpumbavu sana ama ni taahira kabisa!!!

    ReplyDelete
  15. We anony wa 8:10pm. Una akili timamu kweli? au unatania! Huyu mtu aliyeamrisha watu wauwawe huko mashariki ya kati kwa ajili ya kuiba mafuta. Wewe ndio unajivunia ujio wake. Anyway sikufahamu wewe mwenyewe kimaamuzi, huenda ukawa kama au zaidi ya kichaka kimaamuzi.

    ReplyDelete
  16. Nimeona kwenye News nasikia amepapenda sana Arusha na weather haikua that tough...na watu walikua wengi wamempokea kwa vizuri sana...hakutegemea kuona watu wote hawa barabarani....

    Na pia wamesema alikula lunch na niece wake anayefanya humanitarian work hapo Bongo...

    Jamani we have to be happy japo ni siku chache lakini tumesave sana hela za kuitangaza nchi yetu...Lile tangazo lilicost shillin ngapi? Leo ni free publicity....I am sure tuta double watalii...apart from burungutu alilotupa

    ReplyDelete
  17. Guys, the gentleman has paid his dues, US $698m is no joke guys, ni kashfa 22 za richmond hizo, au EPA kama 10 hivi. Let him close the roads for a while, he has certainly paid for the privilledge.

    ReplyDelete
  18. Mie nafagilia sana ujio wa bush... mkandie hadi mlie.... Nimefurahi kishenzi

    ReplyDelete
  19. Wewe unayesema USD 698m ni hela nyingi fanya hesabu kidogo. Zikigawanywa kwa watanzania takriban mil 40 kila mmoja atapata kama dola 18. Bado waziona nyingi?

    ReplyDelete
  20. Mtapiga kelele weeeeeeeeeeeeeeeeeee, lakini kuna mambo dunia hii ndivyo yalivyo mtake msitake, hakuna usawa Duniani, mmkubali msikubali, nyumba yetu inaungua mchawi sio Bush, vyandarua milioni tano mchezo?? si kwa sababu mnakula rushwa. sio siri kesho atawaletea misaada mpaka ya kutujengea vyoo!!, achilia mbali misaada ya kondomu, ujinga huu wa kujilaunmu sisi wenyewe jamaa hawana shida.ITV wakisema tupeleke michango ya watoto yatima tunagoma, huku bia kwa saana.hivi bila Bush watoto hao yatima nani angewatunza:serikali!!?? ya nani hii hii, au umefurahishwa na kichuguu kilichotikiswa cha richmond wakati kuna milima ya Rushwa kibao.Hao waache wakae tu mtaani ndio furaha yao!! hakuna atakaye kufa.Mpaka akili itakapokuja...........

    ReplyDelete
  21. hapa ni udini tu unaendelea,kweli shukrani ya punda ni ........!?hawa jamaa wangeweza kutoa hizo hela kwa nchi yoyote wanaotaka,lakini jamaa wameamua kuipa bongo lakini watu bado wana run they r mouth,hawa jamaa wako juu mtakate msitake kuna kitu kipi cha ajabu kufunga mtaa bongo kulinganisha na hela waliyowapa,nyie jifanyeni jeuri kam hamjaishia kama zimbabwe.

    ReplyDelete
  22. Michu,
    Blogu hii inatusaidia kupashana habari kuelewa sababu ya A-town kuwa na idadi kubwa ya marasta na watu wanaojivunia 'Black Power'
    .
    WaTZ wanapaswa kufahamu kuwa eneo la kati ya Arumeru na Usa-river Mkoani Arusha, kuna wakimbizi wa kisiasa toka Marekani waliopewa makazi vijijini kando kando ya hiyo barabara ya Arusha Moshi.
    Hivyo hata Rais Clinton alipokuja na sasa George Bush jamaa wa FBI na usalama wa USA wameomba hawa jamaa wakimbizi wa kisiasa toka Marekani wabanwe.
    Wakimbizi hawa baadhi yao sasa ni wazee wa vijiji wilayani Arumeru na wanaheshimika na wanavijiji kwa kuchochea maendeleo kutokana na misaada toka kwa jamaa zao waliowaacha Marekani. Kwa habari zaidi nenda ktk webu: USA members of Black Panther who are now political refugees in Tanzania.
    Mdau
    SeniorJunior
    London

    ReplyDelete
  23. michuzi nisaidie hicho kidude kipo kati ya barabara kinafanana kama kuku mkubwa wa matambara ni kitu gani?

    ReplyDelete
  24. Anon ni mama anasukuma toroli.Nafikiri alikuwa anafanya usafi wa mwisho mwisho.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...