Mambo vipi Kaka Michuzi na wadau wote popote mlipo.
Leo nimeona ngoja niwape link hii muone wabongo tulivyoharibu Ukerewe hapa. Sasa mkiona yale ma-Vogue na magari mengine ya kifahari kule Bongo msidhani yameingia kihalali maana wazee wa Interpol wataingia si muda mrefu kuyarudisha yaliko ibiwa kaa mkao wa kula kama ulininunua gari la kifahari kupitia njia ya panya sasa ukalifungie garage mapema lisije ikawa hadithi tu tena.

Na nyie wabeba box tukiona picha za magari ya kifahari bongo msipande na mzuka wa kutaka kurudi nyumbani mkadhania kuna hela kiiivyo kumbe lazima uwe mwizi na kama wizi uwezi basi tuliza ball hapo ulipo ulipwe unachostahili.
Msiwe na tamaa sasa wale wanajijua wana magari ya wizi wajue hela walionunulia wameitia chooni wenyewe na afadhali mngewapa maskini mpate swawabu zenu kwa mungu. hata ukilificha chumbani magari yote ya kifahari Ukerewe wameyawekea tracker wazee wakija na mtambo wao tu wakipita nao mtaani wanatapa signal kutoka kwenye tracker labda ujue wameikifit sehemu gani ukitoe lasivyo moto unao.
Bonyeza link hapo chini uone mambo

http://icbirmingham.icnetwork.co.uk/sundaymercury/news/tm_headline=police-smash-alleged-luxury-car-theft-ring%26method=full%26objectid=20635641%26siteid=50002-name_page.html#story_continue


Powa kaka Michu kama kawa yetu email kapuni.
Asaalam
Mdau UK

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 16 mpaka sasa

  1. Kama una gari kama hilo la wizi lipigishe shot wakati linawaka. Alafu zima chomoa battery. Kama tracker iliyokuwa installed ni Leo au Clifford hata Peugeot systems hazitafanya kazi. Kuna baadhi ya vitu utabidi ununue baada ya hapo though.

    ReplyDelete
  2. Sasa unataka kusema wote waliofanikiwa maisha bongo wezi sio kweli unaweza kutumia Akili yako vizuri na ukawa Tajiri kwahiyo unawadanganya watu wabebe box mpaka kufa nakataa hiyo na wasiwasi ulipotokea

    ReplyDelete
  3. @ Any 10:52am

    Thats your own interpretation, and I have never said that, if you go back and read the comment posted on the above post-ZAHAMA COVENTRY and NOT this post as you suggested.

    By Mchangiaji.

    ReplyDelete
  4. ebwana inawezekana sana wabongo wameiba sanamagari kule south aAfrica na walibabwa sasa wameamia ukerewe, hapa bongo watu kibao wana vogue tena ni hajabu tena wengine ni wakurugezi wa mashirika ya umma katika hili haki itendeke.

    ReplyDelete
  5. UTAKALIA TU KUANDIKA NA KUBEBA BOX, SISI TUNATELEZA TU NA WATU WANAJUA NYUMBANI WAMEISHA SHEHEREKEA X-MAX KUMI HAUPO, BADO HUNA HATA PLOT.

    ReplyDelete
  6. Deal za wizi zipo na sio wote wenye magari mazuri ni wezi ila wapo wasio jiweza na ndio wanaiga kunya kwa tembo sasa wanaenda na magari ya wizi hizo sio tz tu ukifika dubai zipo hizo deal,japan,usa,uk ,nigeria,kenya kwa kifupi kila mahali kuna mijitu inataka misifa wakati uwezo mdogo so wanaishia kununua za wizi,sio mara ya kwanza yaliingia sana magari ya kuibiwa toka south africa na watu wakayaficha wee na mengi kukamatwa so ni tamaa tu wewe uwezo wako butiama restaurant kwa nini unataka kula kili kempisk ndio hao wanao nunua vya wizi.Ni mafisadi wengine uwezo wa mkopo wako ni toka benki ya posta na unakwenda bot kisa kuna wizi wote huu ni ufisadi

    ReplyDelete
  7. Jamani msimsikilize huyu mtu kuhusu kurudi Tanzania rudi ila tafuteni kwa nguvu zenu wenyewe nikiangalia kwa kina inaelekea ametokea maisha magumu sana anaogopa kurudi bongo kina weza mchachia basi jiandae au unataka upelekwe kwenye hizo nyumba za vikongwe ukizeeka ANON 10:52am umechangia vizuri

    ReplyDelete
  8. Hii inanikumbusha zamani sana mzee wangu alini tusimulia, Jamaa aliibia gari Dar-es-salaam. Kwenda Kenya kaikuta gari yake ime park sehemu hapo hapo kaenda police. Gari akaipata hasa watu wa Arusha wezi sana wa magari. Tanzania ma Gari yanaenda msumbiji,kenya,malawi. na ya msumbiji yanaletwa Tanzania kutoka South Africa. wizi huo jamani ushaishiwa sawa na wizi wa Cheki za pesa. tufanye vitu vya halali wanadamu hata miaka 70 siku hizi hatufiki tumuombe mungu tu.

    ReplyDelete
  9. Huyu bwana akisha maliza kifingo chake ni bora wam deport kabisa. Tatizo wenzetu waingereza watamfunga miaka 2 au 3 na kisha kumuachia huru.

    ReplyDelete
  10. JAMANI ZA MWIZI AROBAINI...ILA SIE WENGINE TUTAMISS CHAMPAGNE ZAKE, HUWA ANAPENDA KU SHARE MAFWEZA YAKE NA WASHKAJI, KWANI YULE MDAU WA DERBY NAE ILE MERCEDES NAYO YA WIZIIII????NA HUYU WA NORTHAMPTON NAE??? MANA HAWABEBAGI BOX.. ANYWAYS, WATAJIJU..

    ReplyDelete
  11. Kwani Wananigeria type, wapo hata TZ, na wengi huko sehemu za Mbeya, wachawi na wanapenda sana fedha.. ILA nyerere aliwatia adabu kuwabana, sasa wako nje ya makabati.

    Jamani hakuna wanamuziki wenye kuendesha magari ya wizi huko....toeni majoka pangoni.

    INTERPOL wanakutafuteni.

    WEZI, MAJAMBAZI, WAHALIFU WAKUBWA,

    ReplyDelete
  12. Sio wote wenye magari mazuri ni wezi. Mimi ninalo lakwangu ambalo nimenunua kihalali na kodi zote nimelipia na litakuwa barabarani throughout the so called msako. Nobody can dare say anything sababu ni legitimate na kazi yangu ni halali. Na nipo Bongo baada ya kurudi toka UK miaka 10 iliyopita! And I'm not even 35! Sasa nyie wabeba mabox huko mtasema lakini usiku mtalala.

    ReplyDelete
  13. Mimi naona huo ni ujanja, nyinyi hamjui hawa jamaa (wazungu) wanavyotutesa, kwa hiyo mimi naona wakizubaa tu basi inabidi wapigwe chini, jamaa kwa bahati mbaya amekamatwa !!

    ReplyDelete
  14. Huu ndio mimi naita ujanja wa shamba. Wanaona wenzao tunaofanya kazi mafala!!Siwaonei huruma kabisa hawa wanatuchafulia jina taifa letu. Soon tutakuwa kama Wanigeria, ukifika tu watu wanachunga waleti zao. I hope atachukua mvua ya kutosha na apate na mume huko gerezani which no doubt atapata.

    ReplyDelete
  15. Anony march 31st 8:31 am who cares mbona unahaha sanaaaaa......kama lako la halali kaa kimya tulione barabarani.....tutajuaje kama hiyo miaka kumi iliyopita ulikua unauza poda ukarudi home...kwani wangapi tunawajua wana magari ya halali bongo lakini hela waliipata kwa kuuza poda...?????

    Just mind your life...stop blah blah blah ....si umesoa news na wameonyesha kuwa magari yameibiwa nayamepelekwa TZ na Kenya sasa wakija kupekua kama lako la halali wewe pilipili inakuwasia nini? Yaani eti wasije kusearch kwa vile wee kazi unayo....doooo

    ReplyDelete
  16. anon Monday, March 31, 2008 5:39:00 PM EAT, tuliza makalio chini kuna polepole kama yanakuwasha sio uje ukunie hadharani
    wanachafulia jina la taifa letu? we unasafisha vipi jina la taifa? kwa kufanya kazi nursing home kutawaza vizee kila siku? ili tukijitambulisha tunatoka tz straight forward wajue wote tunaosha vinyesi vya vizee vya kizungu?
    tuliza mpira chini acha makeke uwanja mkubwa huu mpira wenyewe hata hautangazwi
    we safisha endelea kutunza vibabu endesha kimkebe chako hamna mtu anakusumbua

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...