Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Mawasiliano ya Umma na Uandishi wa Habari cha Chuo Kikuu cha Cha Dar es Salaam, Ayub Rioba (kulia) akibadilishana mawazo na Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu n a Utawala Bora Jaji Mstaafu Amiri Ramadhani Manento (kushoto) baada ya ufunguzi wa warsha ya waandishi wa habari iliyofanyika Dar kuhusu umuhimu wa vyombo vya habari katika kutetea haki za watoto

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. Tanzania hatuna Chuo Kikuu Kishiriki cha Mawasiliano ya Umma na Aandishi wa habari, bali tuna Taasisi ya Mawasiliano ya Umma na uandishi wa habari ya chuo kikuu cha Dar es salaam (Institute and Journalism and Mass Communication of the University of Dar es salaam). Taasisi huongozwa na Mkurugenzi (Director), Chuo kikuu Kishiriki huongozwa na Mkuu wa chuo (Principal). Inabidi uelewe tofauti ya Taasisi na Chuo Kikuu kishiriki

    ReplyDelete
  2. kaka ayub...unawakilisha vyema wadogo zako enzi zile za Meru Hall Ilboru......wapi kaka seleman lilumba,malila shindika?yaani hii ni safi sana.....mzee wetu bino akiona hizi anafurahia matunda yake ya uongozi thabiti pale ilboru...wadogo zako tupo tunawakilisha vyema kila sehemu tulipo.....

    ReplyDelete
  3. duhh, mwalimu rioba, namkumbuka enzi hizo anafundisha pale tsj_ilala, amechanaa!!!!

    ReplyDelete
  4. Hivi ni kweli Ayoub Rioba ameshakuwa Mhadhiri Mwandamizi (Senior Lecturer)? Au ndio mambo ya kasi mpya, ari mpya, nguvu mpya hadi kwenye taaluma?

    ReplyDelete
  5. Ndio Rioba, mwanaharakati na mwandishi mashuhuri. piga msasa vijana wa taasisi hiyo wawe kama wewe sio kuzalisha makanjanja.
    ila umri unakwenda Bia na ubwabwa wako tutaula lini???
    weka mwanamke ndani.

    ReplyDelete
  6. Mdau wa 12:28 nimeipenda Comment yako, lini tutakula Ubwabwa.

    ReplyDelete
  7. duuuu!Rioba amechana abnomal,lakini dada manka amekuona kaka Rioba sasa nadhani atakufuata pale Chuoni.naona baadhi ya vigezo unavyo kama gari una benz na range rover.shavuuuuuuuuuuuuuuu

    ReplyDelete
  8. Hivi ni Rioba au Ryoba??? samahani kuulizasi ujinga..Ayub nimesoma naye Ilboru nakumbuka jina lake lilikuwa linaandikwa Ayub Ryoba!!!

    ReplyDelete
  9. jamani hatuna institute, siku hizi inaitwa shule kuu ya uandishi wa habari na mawasiliano ya uma au kwa kiingereza School of journalism and mass communication (SJMC)

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...