kiongozi mpya wa bendi ya tot ali choki akiwa na mwanamuziki mahiri wa kongo werrason wakati choki alipokuwa kinshasa kusaka wanamuziki kwa ajili ya bendi yake hivi karibuni. choki amesharejea na wanamuziki takriban wanne na sasa wako kambini wakijifua kabla ya kutoka upya

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Komba wewe bwana kazi yako kuchukua wanamuziki na kuwapotezea vipaji wasisikike kabisa , wako wapi akina Kocha wa Ulimwengu ,Mwinjuma Mumin,Badi Bakule , Toka wahamie TOT ..hatuwasikii kabisa ,hakuna mtu aliyetamba wakati muziki wa Dansi unarudi kwenye chati kama Mumin, lakini komba umemmaliza ,sasa na wewe ALICHOKI KUHAMAMA angalia usije ukapotea bado tunakuhitaji...vile vile mimi kila likizo nikienda DAR . sijaona hata siku moja Onyesho la TOT dansi kama vile TWANGA ., FM , au hiyo bendi ni kwa ajili ya kampeni za chama tuu...

    ReplyDelete
  2. Duu Choki nimekukulani u mfupi mzee yaani nusu ya Werrason

    Mimi naungana na Mtoa maoni wa kwanza yaani TOT ndio ehemu ya kupotezea vipaji vya wasanii sasa hizi tamaa za Ally Choki kuhama hama kwa kuona pesa za mkupuo zinaweza kukuharibia maisha yako kwa sababu sidhani kama leo ukitoka tena huko Asha Baraka atakupokea tena labda urudi ukalime au ujiunga na taarabu ni maoni tu ila mwana maendeleo yanapatikana kwa kutulia sehemu moja si kuhama hama Take care

    katochi)

    ReplyDelete
  3. Huyu bwana anapozi huyu check hapo utadhani Werason ndio kaomba kupiga naye picha!!!
    Haya bwana kila la heri!

    ReplyDelete
  4. hivi wanenguaji wamekosa bongo mpk wanaenda kutafuta congo? mnawapa ulaji wakongo baada ya kusaidiana nyie na wabongo wenzenu,wat a shame

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...