leo nimepata bahati ya kukutana na mabosi wa idhaa ya kiswahili ya deutche welle. shoto ni mh. mohamed abdulrahman (naibu mkuu wa idara ya kiswahili) na othman miraji. nashukuru DW kwa heshima waliyonipa kutembelea kituo hiki cha kimataifa cha redio ambapo juzi idhaa ya kiswahili imeadhimisha miaka 45 ya huduma iliyotukuka. Hongera sana DW na asante kwa ukarimu wenu
niko na kaka abdul mtullya (kulia) alex mwakideo na anti samia othman
niko benet na malkia wa utangazaji ummy oumilkheir hamidu
niko na mwenyeji wangu abubakar liongo na mdau wa karlstruhe mamdogo janet

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 18 mpaka sasa

  1. Hongera DW kwa huduma nzuri...ushahuri wangu kwenu niombi la kufunguwa studio eneo la maziwa makuu...jamani ndani ya miaka 45 hamna studio yeyote eneo hili?? Hapo ndio BBC wanapowapigia bao...sio wabahili..budget yao ni ndefu na wanastudio kila kona ya pembe ya maziwa makuu.

    ReplyDelete
  2. Hongera mama oumilkheir kwa sauti yako ya kuvutia wakati unapotangaza. Mimi binafsi nilikuwa nawaza kwamba wewe ni mzungu na sikujua kama wewe ni mweusi kama mimi. Binafsi huwa nafurahishwa na jinsi unavyotamka maneno wakati wa kusoma habari. Ulijifunzia wapi huo utaalam wako? Endelea hivyo hivyo mama, wanao tunakufagilia sana

    ReplyDelete
  3. yaani nimefurahi sana kuona picha ya umilkheir....maana napenda sana utangazaji wake...na kutokana na kuwa na sauti nzito marafiki zangu wengi walikuwa wanafikiri kwamba ni mwanaume ila kwa kujua kwangu kiarabu nikawa najua maana ya hilo jina la ummylkheir nikawa ninawaambia maana yake ni mama wa kheri...nimefurahi sana kuona picha yake and tell her am her number one fan.Allah akupe akupe maisha marefu Ummylkheir labda nikija Germany kutembea nikutane nawe ili nipate kupiga picha na wewe.Je kutembelea hicho kituo ni free au mpaka uandike maombi?
    Mdau Sweden.

    ReplyDelete
  4. Asante Michizi kwa kutupa Picha za hao wakogwe wa utangazaji wa Sauti Ya Ujerumani maana mi tngu nikiwa mdogo namskia Athman Miraji na Oumilkhel,na picha yao ya Mwisho niliona mwaka 1991 sasa naina wamenenepa na kuzeeka,Vipi yule wa Kipindi cha Michezo hukuonana nae?tupe picha yake kama unayo.Na Fulana....

    ReplyDelete
  5. Bwana michuzi nakuomba ilo tangazo langu la shughuli ya ngoma uliposti kama tangazo na wala siyo kama comment. Sina utaalamu wa kuposti moja kwa moja ndo maana nikapitisha kama maoni. Asante.

    Bwana Kilemela hapa, London, UK.

    ReplyDelete
  6. michuzi utakaa kijijini kwetu mpaka lini?
    na huyo dada Janeth wa Karlsruhe anapatikanaje?
    tunakukaribisha sana kwetu Baden Baden

    ReplyDelete
  7. Michuzi naona hiyo fulana ina irizi sio utani!!haiwezekani kabisa ukawa unaivaa tuu!!ni wablog wangapi tanzania hawakupata nafasi ya kwenye ujerumani wewe umechaguliwa??achana na ushirikina michuzi

    ReplyDelete
  8. Nguo ya bahati.......

    ReplyDelete
  9. NDIO BABAKE LEO TUMEKAONA KAFULANA KAMERUDI MAUNGONI, SIJUI NI KAPYA HAKA AU????????????/, MICHUZI NINI SIRI YA HAKO KAFULANA KAKO??!!!!!!!!!.
    MDAU HUKUHUHKU ULIKO.

    ReplyDelete
  10. Nashukuru sana Bro. Michu kutuletea picha hasa ya huyu mama Ummul- Kheri (mama wa kheri). Nikimsikia redioni tu huyu mama, ila sauti yake iliyojaa vionjo na madaha ya kiume ndiyo iliyonifanya nimfurahie zaidi pale anapokuwa anawakilisha habari na kuwa makini na kuweka msisitizo pale panapotakiwa. Ukweli ananifurahisha sana anapotagaza.

    ReplyDelete
  11. Michu,
    Ni mimi tu ninayeona hili, mbona watangazaji wote ni WAISLAMU TU, AU NDIYO TICKET YENYEWE HIYO!!!!

    ReplyDelete
  12. DW nawafagilia sana kwa matumizi mazuri ya lugha yetu adhimu ya kiswahili...watangazaji wamekomaa, hawachapii chapii kama wa redio nyingine...taarifa zao za habari na ripoti nyingine wanaziandaa kwa kina na wanazisoma kwa tuo...mamaa Ummylkher, unanikosha sana tangu nikiwa mdogo hadi sasa nazeeka bado unatisha kwenye utangazaji!
    mdau wa baden baden tuwasiliane.....

    mdau, Germany

    ReplyDelete
  13. We Michu inaonekana unawashwa sana na mikono. Ipo siku itakuja kukuletea zali, shauri yako!

    ReplyDelete
  14. Asante sana kutuma picha hizi. Kumbe DW bado inaendelea?

    Mama Lao
    UK

    ReplyDelete
  15. huyo mama mdogo nani?nii mbona yuko
    hoi!ameshapima huyo?

    ReplyDelete
  16. Uislam na uzanzibar ndio tiketi ya kujiunga na DW!kama kiswahili chako
    ni cha cheche unakaribishwa
    lakini kama una kiswahili cha kusema wanakwendaga!badala ya nenda!hapa una chako.

    ReplyDelete
  17. Jamani kweli?kama alivyo uliza mdau hapo juu?na mimi swali langu hilo hilo!vipi Mama mdogo? umepima
    Ze ngoma? jarubu kupima maana huko majuu uduma nje nje,ukipima unyonge
    ulikuwa nao utakutoka.
    na kama ulikuwa na wateja wengi siku za nyuma bora kapime

    ReplyDelete
  18. AnonymousJune 01, 2008

    Michuzi huyo unayemwita Alex Mwakideo siye! Huyo ni ndugu Josephat Charo!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...