Kuna hiki kiumbe lakini cha ajabu hapa duniani, kiitwacho Mwanaume. Ni cha ajabu kutokana na uwezo wake wa kubadilika kufuatana na mazingira kilichomokwa wakati husika. Hakika hata yule bingwa wakujibadili kinyonga haoni ndani. Angalia kwa mfano mazungumzo ya simu yafuarayo ya kiumbe hiki.
Miaka kama kumi nyuma wakati kikifahamika kwa sifa ya 'mchumba wa mtu':
"Sweetheart! Habari za asubuhi"
"Nzuri tu dear, sijui wewe !"
"Aa, mimi hali yangu sio nzuri kabisa"
"Ee nini tena Dear !"
"Nimekumiss mpenzi wangu, halafu usiku mzima wa jana nakuota tu!"
"Jamani pole sana mpenzi"
" Asante lakini haitoshi darling ! Hivi kwanza leo nitakuona saa ngapi?"
"Sijui wewe labda unifuate wakati wa lanchi !"
"Ok basi, wife to be endelea na kazi huku ukiendelea kukumbuka ule wimbo wangu ninaoupenda kukuimbia !"
"Mh? Upi tena huo dear ?"
"Aaah unaniangusha darling ! Si ule wa oh my sweet,my sugar, let melove you forever, oo yes!, umeukumbuka?!"
"Alaa! Huo! Basi nimeukumbuka! Bye dear!"
"Bye, nibusu basi.. mmmwwwwwaaaaa.."
"Baadaye dear, kuna watu hapa!"
"Ok basi!"
Haya basi miaka kumi na mbili na watoto wanne baadaye hiki kiumbe mwanaume sasa kina hadhi ya 'mume wa mtu'na sasa tunakutana nacho kikipiga simu kwa yulee mtu aliyekuwa mchumba wake miaka kumi na mbili nyuma na ambaye sasa anakwenda kwa hadhi ya "mkewe".
Mazungumzo yao kwenye simu sasa:
"Aisee........!Hujambo ?"
"Sijambo ! Za kazi ?"
" Safi , vipi hawajambo hao ?"
"Hawajambo tu !"
"Huyu aliyekuwa anaharishaharisha vipi ?"
"Anaendelea vizuri, nimempa enthoromycin naona inamsaidia"
"Sawa huyo fundi wa TV naye kishafika ?"
"Sijamuona !"
"Sawa, akija muangalie sana asiibe vitu kwenye hiyoTV !"
"Sawa, sasa Baba nanii...!"
"Unasemaje?"
"Kuhusu ile losheni"
"Umeshaanza! Nimesema nitakununulia!"
"Jamani Baba nanii.....! Mwezi wa pili huu sasa, kila siku unaniambia hivyo hivyo!"
"Alaa! Tumeshaanza kuhesabiana siku sasa sio?"
"Basi yaishe ! Mimi nilikuwa nakukumbusha tu jamani"
"Haya, mimi nitachelewa kurudi nyumbani kidogo; kuna jamaa naenda kumcheki nikitoka kazini !"
"Sawa"
"Baadaye basi"
"Sawa"
Hebu tusikilize simu hii ya mwisho ya kiumbe huyu dakika chache tu baada ya kuongea na mkewe anaongea na simu hii akiwa amevua ile hadhi ya mume na kujivika mwenyewe bila kushurutishwa na mtu, hadhi ya buzi na anayeongea naye ni kiumbe mwenye hadhi ya mchuna buzi. Patamu hapo, babu yangu!
"Haloo, darling!"
"haloo mambo"
"Poa! Unafanya nini sasa hivi darling wangu?!"
"Aaa nipo tu natengeneza nywele zangu!"
"Yees ! Zitengeneze vizuri ule mtindo ninaoupendaga,jioni nitapita hapo nikupeleke ukapate vikuku na vikopo viwili vitatu!"
"Sawa darling ! Halafu dear, vipi kuhusu vile vitenge vya Zaire wanavyopitisha wale kinamama niliokuambia!?"
"Darling na wewe ! Si nilishakwambia wakipitisha tena we chukua tu pea mbili halafu uniambie tu mimi nitakupa pesa?!"
" Asante ! Na vile viatu je ?"
"Darling sasa unataka kuniudhi ! Nimeshakuambia kuwa sio lazima uniombe ruksa kila kitu ! We chukua halafu unaniambia..."

mdau aliyetuma hii (jina kapuni kwa sababu zinazojieleza) anaomba umtumie yeyote yule umpendaye msg hii

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 22 mpaka sasa

  1. its oke dada sijui kaka, lakini angalia na upande wa pili pia ujue kwa nn men act in that way, me nafikri kwa mtazamo wangu wanawake wa nyumbani bongo siyo wote wako too dependant. yaani they expect a lot from men. ktk dunia ya leo mapenzi is about sharing kila kitu btn the couple. kama mwanaume anakununulia zawadu na wewe pia unatakiwa ufanye hivyo. utakuta demu anafanya kazi na ana mshahara mzuri still, anampiga mizinga mwanaume kama ya vocha, salon nk.mwanamke hamnunuli zawadi mwanaume mpka awe na birthday.

    ReplyDelete
  2. AND VICE-VERSA IS ALSO TR

    ReplyDelete
  3. Hii joke iniadhalilisha wanaume haifai. Sisi kama wanaume ambai globu hii mali yetu inaonyesha ni jinsi gani tunavyo tolerate tabia za akina dada.

    ReplyDelete
  4. Mhh, jamani yaani `kiumbe mume' ni wa ajabu hivyo, lakini mimi naona `kiumbe mke' naye hayuko mbali.

    Siku baada ya ndoa, kiumbe mke ni mwaminifu, ukimpa pesa ya matumizi, unarudishiwa chenji.
    `Hizi zimebakia jana mume wangu...'
    Kiumbe huyu adamu na taadhima, na wengine hata shikamoo haibunduki mdodmoni.
    `Shikamoo mume wangu...'

    Miaka nenda, au hata jirani tu kabla ya mwaka, kiumbe mke kakutana na kiumbe mwenzake aitwaye `shoga'(Viumbe hawa kwa kudanganyana bwana, hutoamini).
    `Shoga mbona we unafugwa, hutoki..
    `Shoga mimi naiheshimu ndoa yangu..
    Kiumbe shoga atamganda kiumbe mke mpaka ataingia laini.

    Siku zinazofuata hela ya matumizi haitoshi, inaishia wapi, kwenye `michezo'
    Siku kadhaa, kiumbe mke hashikiki, kila siku naomba ruhusa kuna harusi kwa dada, kwa shangazi kwa binamu...
    Na yule kiumbe anayefanya kazi anasingizia `over-time' kazi nyingi, bosi anasema tuna semina...
    Huyu yeye si kiumbe wa ajabu!

    Kiumbe huyu ambaye yeye anajiona si wa ajabu utamshangaa, wakati unamuoa alikuwa maji ya kunde, lakini sasa ni mweupe pe, mzungu kasingiziwa.

    Kiumbe huyu alikuwa anasuka mabutu na twende kilioni, lakini sasa ana nywele za chotara...
    Ama kweli kiumbe huyu si wa ajabu bali ni wa maajabu.

    Kiumbe huyu alikuwa akivaa gauni, na mtandio kichwani, sasa anavaa suruali inayobana kiasi kwamba ngozi iliyopo mwilini inapwaya....

    Majibu ya kiumbe huyu yanabadilika, ile shikamoo inakuwa `Habari yako...
    Ukimuita anaguna au au anasonya, `nawe umezidi bwana, mi-nimechoka, na wewe upikege...
    `Kila siku kila siku...
    `Na wewe unajiita mwanaume, kwenye wanaume.
    Huyu yeye si kiumbe wa ajabu!. Tusisahau kuwa kiumbe mke ni ubavu wa kiumbe mume, tabia na mienendo zinalandana.

    ReplyDelete
  5. Ila 4 what I can see viumbe wote vina udhaifu.

    kwanza huyo anayejiita mchuna buzi na mchunwaji wote wajinga, sababu mchuna buzi akijilegeza 2 na akazaa na mchunwaji naye ajue yatamkuta ya mke wa ndani, Pia asisahau kuwa akiachana na huyo mwenye mke akipata mume huyo mumewe atamtenda yale yale ya staili ya mke wa ndani, unless aendelee kuchuna 2 bila kuzaa haisaidii mume atakumbuka 2 home atarudi kwa mkewe atakudamp.

    Lazima aelewe kuwa mke ndio anapendwa kuliko yeye.

    Kama huamini mke anapendwa jaribu kumchukulia mke huyo jamaa uone hiyo mihasira yake anaua mtu. Lakini akisikia mchunaji ana jamaa atalalamika ila si sana ataachana nae na kuchukua msichana mwingine sasa si ujinga huo.

    Kweli wanaume ATM.

    yeye anatoa ofa kwa wadada akisikia mkewe kapewa ofa anamind anajua ofa zina maana gani.

    Kweli ukisema cha nini wenzio wanasema watakipata lini.

    Midume mijinga inadanganywa na small small house.

    Tulia nyumbani na mkeo kula kuku boyfriends, UKIMWi upo.

    Ku da da da de kiii!

    ReplyDelete
  6. Kaka ukipata mke mwema kaa chini mshukuru mungu.

    Wanawake wengine hatari sana

    Wanaume ndio wajinga kwa sababu wanawake ndio hatari zaid.

    Mwanamke anaonekana mpole kumbe muongo mkubwa.

    Anatembea na wanaume ndani akija hushtukii maisha yako Never!

    Utahangaika ukijua mkeo katulia anakusubiri kumbe wapiiiii!

    Wanaume poleni mnaishi na chui waliojivika ngozi za kondoo.

    MNAJIDAI VIDUUUUME!


    mWEEEEEEEEEEEEEEEEE!

    ReplyDelete
  7. Mwanaume ni mjinga sanaa, Mwanamke ni mjanja.

    Ukitaka kujua come wit me chini ukoo!

    Mungu ni bonge la mjanja.

    Mungu kiumbe mjinga hapa duniani alimweka mwanaume,

    Sasa hawezi kumkosesha yote mwanaume akaamua kumpa kujiamini kuwa yeye ndio yeye ili asione huzuni.

    Mwanamke ni mjanja sana kumbuka adam na hawa weweee!

    Mwanamke akimtaka mwanaume ataweza 2 kwa namna yeyote ile.

    kama huamini shiriki kipima joto hiki kwa kuvaa nguo fupi ya kukuonyesha kuwa wewe ni woman pita mbele ya mvulana kama ujaondoka nae huyo.

    MIjinga mijingaaaaaaaa.

    Michuzi labda unibanie itoe ili wanaume wajielewe.

    Ila wewe kaka michuzi Ni bonge la mjanja nakujua.

    waliobaki zilo. nasisitiza yaani zilo.

    Poleni mabingwa...

    ReplyDelete
  8. Mh! jamani, mbona mnajiteteea! A fact remains a fact no matter what! Kaka zetu hata mkipendwaje lazima mtaonja onja nje, Kubalini tu yaishe!

    ReplyDelete
  9. Mimi mashangaa kuona ujumbe huu.Wanawake wa leo wnadai HAKI SAWA.Ukilichukua neno HAKI SAWA kwa msisitizo kabisa,ni kwanba kila mtu ajitegemee:Mke achangie katika familia.Lakini wanawake hao hao bado wanfurahia mambo ya LADY'S FIRST,ukiwa naye anataka umtoe OUTING.Mwanamke wa leo anataka MWANAUME MWENYE KAZI,mwanamume mwenye GARI.Wanawake wengi wanapenda wanaume wenye PESA.

    ReplyDelete
  10. Changes should occur unless for a change itself! No eternal steady state of love ... Kawaida.

    ReplyDelete
  11. sina la kusema. Ingawa mimi kama mwanamume nimepata ujumbe na tabia hiyo ni kweli ninayo na nimeamua kujirekebisha. Naomba ma-brothers tujirekebishe na kina dada nao pia jirekebisheni.

    ReplyDelete
  12. Acheni kujitetea, tatizo liko wazi kwanini akachunwe na Buzi wakati anashindwa hata kumnunulia mkewe Losheni mwezi wa pili hiyo anaomba? Isitoshe inawezekana huyo mama anashindwa kufanya kazi ya kumuingizia kipato kwa ajili ya kulea watoto. Watoto wanne si mchezo, hapo mkubwa ana miaka 11 au 12 kama walioana akiwa tayari ana mimba. Hapo utakuta anajipeleka mwenyewe kufanywa ATM wakati watoto wanashindia dona na maharage bila hata mchicha kwa sababu pesa ya matumizi haitoshi. Wana kwashakor na matunda wanayalia 'makuti' Muhimbili au mpaka waandikiwe na daktari lakini yeye asubuhi anajichana breakfast ya nguvu, mchana lunch anaenda kuchunwa na jioni anapita kuchunwa pia na pesa ya kumlisha mume mwenziwe anapewa.

    Hivi mnafikiri msichana mchunaji aliyeamua kuwa na buzi au ATM hana moyo? Hajui kupenda, huyo buzi au ATM kazi yake ni hiyo kuchunwa tu lakini king'asti kiko pembeni kazi yake kulishwa na kuvishwa na kupelekwa out, kumridhisha bidada kwa pesa za ATM!

    Hakuna cha visingizio wala nini, dawa ni uzazi wa mpango ili kutomzeesha mama, na kumpa nafasi ya kufanya shughuli za kumuingizia kipato ili asiwe tegemezi. Wengine huzuia wake zao wasifanye kazi kwa ajili ya wivu na huwazuia wasijipambe au kujiremba ili wasifanane na mahawara zao.

    Take care UKIMWI upo for real na hauchagui masikini wala mwenye pesa, mwenye mke wala mseja!

    ReplyDelete
  13. IMEFIKIA WAKATI MTU ANAPOTOA UJUMBE KAMA HUU,THOUGH IT DOES LOOK LIKE A JOKE, TUMPONGEZA NA KWELI TUANGALIE MIENENDO YETU,NI KWAMBA SIO ALL GUYS WAPO HIVYO,BUT BOTTON LINE IS,THATS IS VERY TRUE ABT SISI WANAUMME,NASEMA HIVYO KWA SABABU NINA FRIENDS KIBAO WANAFANYA HIO KITU NA KWA UJUMLA TUSEME UKWELI JAMANI NDO TULIVYO NA SIO KOSA LETU NI KOSA AMBALO NI GENETICALLY INHERITED FOR ALL GUYS,MARA NYINGI WANAWAKE WANAPOOLEWA KWELI HUTULIA SANA BUT GUYS NDO KWANZA WAANZA KU-LAUNCH SMALL HOUSES TUKATAE,TUHOJI BUT THATS TRUEE,
    NAWAKILISHA

    ReplyDelete
  14. haya sasa viumbe wanaume ukweli ndiyo huo hapo, jirekebisheni sasa mtunze na kulinda familia zenu, maana hao wachuna buzi watawapunguzieni muda wenu wa kuishi bila hata ya kutegemea,mtawaponza watoto wenu wapate uyatima wangali wadogo wahangaike na dunia, na nyie mnaoitwa wachuna buzi dunia hii ya leo jamani ni nini hasa?? ukosefu wa elimu au ndiyo ugumu wa maisha?? ni tabia mbaya hiyo tafuteni wenzawenu mjenge maisha yenu kwa shida ama kwa raha, maana hao mabuzi mtayachuna mpaka lini? au mtaishi kama wachuna mabuzi mpaka lini? fikirini achaneni na hayo mambo muwe kwenye muelekeo mzuri, mungu awabariki wenye familia, mabuzi na wachuna mabuzi washindwe na walegeee kabisaaaa.

    ReplyDelete
  15. this is pure Tanzanian Men!!!!!!

    ReplyDelete
  16. one word: COMMUNICATION....

    ReplyDelete
  17. Thanks Mr. Michuzi.

    Umefika wakati wa wanaume sisi wenyewe tujitambue.

    Kuwa na mdada wa nje is not good kama una wife sio nzuri inapunguza malengo ndani ya nyumba.

    Kaa na mkeo pangianeni majukumu mtoke katika life hii ngumu.

    Kuwa na mtu wa pembeni sio dili hata kidogo.

    Ukiwa na mtoto na mke no time to waste my friend. u hv to focus what's next.

    Kaa mwekee mtoto akiba asome baadae hiyo pesa unayotoa uko ungeweka kidogo kidogo mwanao apate elimu bora.

    unakaa na mtu wa nje unaharibu pesa while mtoto au watoto wako wanahitaji future?

    Baadae unaishia kumpeleka mtoto shule ya msingi ..... while ungekuwa na uwezo hata kumpeleka ..... academy.

    Unampeleka mtoto wako shule ya msondo ngoma while uwezo wa kumpeleka academia ulikuwa nao.

    think brothers.

    Pia ukimwi upoo.

    jamani huo sio uanaume. Mwanaume ni kutulia home kuwaza life.

    ReplyDelete
  18. hahaha.. hata huyo kimada akichokwa,lugha itageuka kama kwa mkewe,simu hazipokelewi,sababu mia mia etc...
    it cuts both ways!!!!! tena kwa bongo,vicheche vimejaa kwa mafungu,ndo kabisa!!ukimwi hauishi ng'o.
    tumwombe Mungu sana,future generation inateketea right now

    ReplyDelete
  19. Well said 9:45...wanaume ambao tumeoa tusisahau kwanini tulioa!! Wengine tumejifunza kutoka wazazi wetu..Baba zetu wengine waliacha mama zetu na kuangaika na vicheche..sasa wamechoka na wanajuta (money comes and goes, vicheche will come and go, but YOUR WIFE AND KIDS WILL ALWAYS BE THERE FOR YOU, Tajiri au maskini wewe wajali na uone matunda yake)..to my fellow brothers kama unamind totoz usioe na kuibebesha familia yako mzigo..lets think with our brains not with our dicks..there is no happy ending to nyumba ndogo...asikudanganye mtu...

    ReplyDelete
  20. i like the joke na mwandishi ametoa ujumbe mzuri sana ambao ni very real ambao unahusu wanandoa.

    i believe mbali na majukumu ya hapa na pale stil penzi la wanandoa inabidi libaki palepale. tunajisahau sana tunaruhusu majukumu ya overlap mapenzi ambayo yalikuwa awali. and sababu hizi zinawafanya wanaume watoke wakatafute nyumba ndogo. but if wanandoa waki keep the passion of love alive kuteleza huko kutakuwa ni kidogo sana.

    so wote mume na mke inabidi wajireflect na sio matter ya kublame wanaume tu. iam a woman and married but yet i know how we women somethimes are. both wanawake na wanaume tunamatatizo. na mashetani kama the so called nyumba ndogo ndio wanaharibu familia za watu.

    ReplyDelete
  21. kiumbe nanii ni wa ajabu sana, japo wote tuna mapungufu lakini yameziada, wanaume wanaendekeza sana nyumba ndogo japo hata kina wanawake wapo wa dizaini hiyo hiki kiumbe ni cha ajabu utakuta kikiona ndugu zake ndi anajifanya ukukulove ili hata hao watu wake wasiongee kuwa anamambo machafu anayoyafanya

    ReplyDelete
  22. THE DEFINITION OF MEN....na haibadiliki!!!

    MEN ARE EVIL
    MEN ARE EVIL
    MEN ARE EVIL
    MEN ARE EVIL
    MEN ARE EVIL
    MEN ARE EVIL
    MEN ARE EVIL
    MEN ARE EVIL
    MEN ARE EVIL
    MEN ARE EVIL
    MEN ARE EVIL
    MEN ARE EVIL
    MEN ARE EVIL
    MEN ARE EVIL
    MEN ARE EVIL
    MEN ARE EVIL
    MEN ARE EVIL
    MEN ARE EVIL
    MEN ARE EVIL
    MEN ARE EVIL
    MEN ARE EVIL
    MEN ARE EVIL
    MEN ARE EVIL
    MEN ARE EVIL

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...