WADAU KUNRADHI. HIVI MTU UNAPOKWENDA KUABUDU HUWA UNAKWENDA:
1. KUSALI?
2. KUSWALI?
SAMAHANI. KUULIZA SI UJINGA NA HILI SWALA LANITATIZA KITAMBO SASA
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
A na B yote sawa
ReplyDeleteALRIGHT, SIMPO KUSALI WANATUMIA WAKRISTU NA KUSWALI WAISLAM UPO HAPO! thanx........
ReplyDeleteAlhamudu lillahi Rabil l'aamina, WASWAlaatu wasalaam waala ashrafu lmur'salina waala alihi waas abihi aj'maaina. ama abaadu.
ReplyDeleteas' saalaam aleykum warhamatu llwahi wabakatuhu.
nimefurahi sana kuona umeingiza hoja hii ambayo natumai waumini wa dini zote nao watafurahi kuchangia mada hii muhimu.
licha ya kwamba kugusia neno hili, pia ina tia moyo kuona watu wengi hivi sasa(pengine michuzi ukiwa mmoja wao), wameamua kumrejea mola na kutaka wakubaliwe maombi yao kupitia sala.
bila kupoteza muda, kwanza kabisa ningependa kuchambua neno sala au swala kama linavyotamkwa na wengi.
katika mtazamamo wangu, neno SWALA limetokana na lugha ya kiarabu ambayo huwa linatamkwa mara kwa mara waumini wa Kiislamu pale wanapotia nia kuQimu Sala.
Kila sala(alfajir, adhuhur, Alaasiri, Magharibi na Ishai), au hata kama sala ya kumwombea maiti, huwa wanaanza na neno hili, "USWALI" halafu wanaendelea na aina ya sala wanayotaka kutimiza.
Kwa vile lugha ya KISWAHILI imekomba maneno mengine kutoka kwenye lugha ya KIARABU( kwa sababu ya waarabu wengi kuishi mwambaoni enzi ya UTUMWA), neno hilo kutamkwa SWALA badala SALA hainishangazi hata kidogo.
Neno hilo ambalo limetokana na ALFABETI iitwayo SWADI kwenye suurat ya kwanza (ALIF), Waswahili wengine wamekuwa wakilitumia badala neno halisi la lugha ya KISWAHILI ambalo ni SALA.
Hata kwenye hiyo surat ALIF, pia kuna herufu iitwayo SINI ambayo ni sawa na herufi "S".
Kwenye Lughat L'Arabia, huwezi kutamka neno SWALA kwa kuanzia na herufi SINI kwani kufanya hivyo itakuwa BATWILI.(BATILI).
HUWEZI KUSEMA "USALI" badala "USWALI".
Kwenye lugha yenyewe ya KISWAHILI, neno SWALA linatumika sehemu nyingi lakini hapa tunazungumzia hili la SWALA;
1)Mtu anapouliza jambo fulani au anataka kufahamu kitu fulani, basi neno hilo huitwa SWALI. Au ukitaka kufahamu jambo fulani, basi neno hilo huitwa SWALA; mfano; (Ningependa sana kufahamu SWALA hili limefikia wapi).
2) Neno SWALA hutumika kumtaja mmoja kati ya wanyama maarufu na mwenye mbio huko misituni. Jina lake kamili MBAWALA au PAA au KULUNGU. Yote hayo ni majina yake.
KWA HIYO BWANA MICHUZI NA WENGINE WATUMIAO NENO SWALA, SIONI KAMA WANAKOSEA SANA KWANI NENO HILO LIMETOKANA NA herufi ya KIARABU "SWADI".
Mtu akisema ana SWALI anakuwa amejichanganya kutamka neno hilo kwa KIARABU( USWALI).
Au akisema ana SALI, atakuwa ametamka neno hilo kwa lugha kamili ya kiswahili sanifu ambayo maana yake ni KUFANYA TENDO LA KUABUDU.
Ukitaka kujua uhalisi wa SALI kama ni KISWAHILI SANIFU, sikiliza waumini wengi wa dini nyingine huwa wanasema "TUNAKWENDA KANISANI KUSALI".
Sijawahi kusikia wakisema TUNAKWENDA KANISA KUSWALI kwani kwao wao neno SWALA linakua limeibua neno la KIARABU la SWADI ambalo nimelielezea hapo awali.
Waasalaam Alleykum Warahmatullwahi Wabarakatuhu taala wabarakatuhu.
Wakristo mara nyingi tunasemaga "kusali" ila ndugu zetu waislamu mara nyingi wanatumia neno "kuswali." Sijawahi kusikia mkristo akisema, "nimetoka kuswali rozari." Correct me if I'm wrong.
ReplyDeleteKwanza hili ni SUALA na si SWALA (myama)
ReplyDeleteHalafu huku ni KUSALI (kuabudu)
KUSWALI maana yake ni kuuliza swali
Kusali - kwa sie wakrito, na kuswali - kwa walio waislamu
ReplyDeletekusali ni wakristo na kuswali ni waisilamu
ReplyDeleteKuabusu ni (kitendo) cha kufanya ibada. Na ibada ni mchakato ulio na mwanzo na mwisho. Katika huo mchakato ndani yake kuna kusali (kwa wakristo) na kuswali (kwa waislamu). Kusali ni kufanya ibada kwa upande wa wakristo, lakini jambo hilhilo hitwa kuswali kwa upande wa waislamu. Kwa uelewa wangu ndo hivyo na wengine pia watatoa mawazo yao. Nadhani pia unahitaji kujua maana ya neno kuabudu pamoja na minyumbuliko yake (Ibada, ibadani n.k.)
ReplyDeleteRAHISI MBONA. KU SALI NI KIMISHENI NA KU SWALI NI KIISILAMU. REJEA SALA YA JUMAPILI NA SWALA YA JUMAA
ReplyDeleteKwa jinsi ulivyoandika hilo neno "KITAMBO" tu nimejua kuwa wewe pengine ni mkenya au haujaishi kwenye mazingira ya watu wanaotumia kiswahili kama lugha ya Taifa. Waislamu hutumia neno KUSWALI sababu wanafanya Ibada kwa vitendo (practical), na Wakristo hutumia neno KUSALI sababu Ibada yao huwa ni ya neno kwa neno (theory),labda ni pale tu wanapo piga goti na kuomba labda ndio kivitendo zaidi,lakini mda mwingi huwa wanakaa, lakini waislamu Ibada yao huwa ni vitendo zaidi, kwa kifupi ni kama mazoezi. Kama nimekosea naomba mnikosoe, jamani.
ReplyDeleteKwa mtazamo wa Kp ni kupiga ngema msikitini au kuruka ruka kanisani,
ReplyDeletekwa mtazamo wangu mtu anapokwenda kuabudu huwa hajenda kusali wala kuswali bali ameenda kuongea na mungu wake anaemuamini.
Na watu wengi siku hizi wamo kwenye kuabudia pesa, mana ndizo wanazoziamini kuliko kitu chochote ulimwenguni.
wamesahau alieumba hizo pesa pamoja na wao.]
ni hayo tu:-)
Kila siku lazima uvumbue viswali vya kuona watu wanavyochangia/ pingana ilimradi siku imeenda.
ReplyDeleteAnyway, maana ni moja tu. Ila naona kama wakristo tunatumia sana Kusali,ilhali ndugu zetu Waislamu nao wanatumia sana Kuswali...
hapo lazima ujue vizuri kiswahili na kuunda sentensi.kuna KUTENDA na KUTENDWA.bondia matumla AMETENDWA na CHEKA,maana yake AMEPIGWA,hivyo mtu anayeTENDWA inamaana ni MNYONGE mbele ya MTENDAJI.hivyo basi tunapokwenda kuabudu,tunaenda KUSWALI na sio KUSALI kwa sababu sisi ni WATENDWA mbele ya MWENYEZI MUNGU(SA)kwani yeye anaweza akaTUTENDA(kukuadhibu)
ReplyDeleteKuabudu MUNGU wa waislamu kuswali.
ReplyDeletekuabudu MUNGU wa kiklisto kusali
Kaka Michu, "kusali" na "kuswali" ni nahau yenye maana moja, ikimaanisha kitendo (lugha huhusika,iwe ni kwa sauti ama kimya kimya/kimoyo-moyo). Kuabudu ni ngeli ya sifa ikeelezea furaha anayoilekeza/fanya/nyenyekea yule tunayemwelezea kwamba ameenda kusali/kuswali. Tunayatumia haya kwa sababu tuna Dini kuu mbili nchini mwetu na japo najua yafahamika, ila si vibaya nikifafanua kwamba kwa matumizi ya kiswahili sanifu; Wa-Kristo wanaliita tendo hilo "kusali" wakati wa-Islamu wanakiita kitendo hicho "kuswali". Wawili hawa wote wanaongea na yule yule ambaye pia huitwa Mwenyezi Mungu, Al-Qudus, Mola na majina mengine ya lugha asili anayozungumza huyo mwenye kuweza kutenga muda wake kusali/kuswali ili aweze kuongea na anayeamini kuwa ni muumba wake, (wakati akifanya tendo hilo). Ili kuongezea tabasamu, nitawakumbusha kwamba kinyume cha ku-abudu ni "ku-tubu". Wakati wa kutubu (wengine wanaita "ku-ungama"), muumuni huyu anajaribu kujirudi na kumsihi huyo anayeongea naye amsamehe/amsameh kwa yale ambayo amepotoka na kufanya mambo ambayo kwa imani yake anaamini hakutakiwa kuyafanya. Hali nzuri ya furaha ya muumini ktk kuelikeza unyenyekevu wenye furaha na sifa na hali yenye kufanana na hilo tutasema muumuni huyu ana "abudu", pale muumini anapokuwa anajutia dhambi zake, anapojirudi na kutubu tutasema anatubu (kama kinyume cha hali ile nzuri ya kujivunia kama nilivyojitahidi kuielezea)
ReplyDeleteNajua mdahalo utapamba moto, ila kwa sasa Kaka Michuzi, naomba niwakilishe. Kaka Yenu
Kumuomba mungu
ReplyDeleteYote mawili au mojawapo hufanyika. Kuswali ni kutimiza wajibu hata kama huna shida yoyote unayoenda kuomba, yaani unatimiza amri ya kidini kuwa muda fulani ukifika wende msikitini ukatende kama ilivyoelekezwa katika muda huo. Huko ndiko kuswali, unatimiza uliyoagizwa na Mungu. Lakini kusali ni kumuomba Mungu akujaalie mambo fulani uliyopungukiwa. Kwa hiyo watu wanasali kwa ajili ya shida zao, lakini wanaswali kutimiza maagizo ya Mungu. Kusali kunafanyika wakati wowote na mahali popote unapokuwa na shida ama hitaji la kumlilia Mungu, lakini kuswali kunafanyika katika muda maalumu na mahali maalumu palipotengwa kwa ajili hiyo.
ReplyDeleteyote sawa, lakini vilevile inategemea na lafudhi, kuswali ni moo arabik sasa inaangukia ki islam,i mean kiarabu... ukiangalia tena mara nyingi ndugu zetu husema 'kusali'slightly bit diferenti,lakini kamwe hawasemi kuswali,mimi naona tofauti ni AIR EMIRATES!hahaaaaa
ReplyDeleteKUABUDU NI KIFUPI CHA KULA KIBUDU.
ReplyDeleteneno swalaa neno limetoka katika lugha ya kiarabu .kwa hiyo wewe mtamkaji ukileta maana ya kusali na kuswali yote inamaana ,hakunakosa katika maneno hayo katika lugha ya kiswahili maana neno hili hasili yake ni kiarabu,kwa sisi wabantu kutamkaa katika lugha ya kiarabu maneno mengine yanatushinda.kwa mfano muhindi hawezi kusungumza kiswahili vizuri yatamtatanisha ,kwa mfano ngo'mbe atasema gombe wao hawana ngo.
ReplyDelete"ANGALIZO" Mara nyingi mijadala inayohusu IMANI hua haiishii vizuri inaishia kwa watu kutupiana maneno yasiyo na msingi. Ningeshauri tu kua huyo muuliza swali aende akasome vitabu vyote viwili vya wanaoswali na wanaosali ataelewa kuabudu iko wapi na nini maana yake. Baada ya hapo ataweza kukata shauri kwenda KUSWALI AU KUSALI!
ReplyDeleteBwana Yesu asifiwe. Nimefurahi kuona mswaada kama huu kwenye Blogu hii. Ningependa kutoa majibu ya hoja hii kwa wale wanaojua maadili ya SALA za KIKRISTO.
ReplyDeleteKwanza ningependa kusema kwamba SALA ni mawasiliano ya moja kwa moja na MUNGU.
Tukija kwenye Kuabudu, au Kumwabudu MUNGU hii ni Ibada au naweza kusema ni Mchanganyiko wa SALA na SIFA. Kuabudu ni Ibada ambayo inafanyika kati ya MUNGU na MWANADAMU naweza kusema ni mahusiano ya Mwili na Kiroho na MUNGU.
KUSWALI sasa huku ni kwa wale Ndugu zetu Waaislam.
Ahsanteni sana na MUNGU awabariki.
PASTOR.
Asalaam alyka/aleyki ustadhi/ustadhat.Mashukur kwa kufafanua kwa kirefu juu ya suali uliloulizwa na br, Michu.
ReplyDeleteanon mar.7, 12:41 sentensi yako ya kwanza umenena vema, ila sentensi ya tatu ,umejichanganya kidogo. Kumbuka kwenye Kutamka na kuandika kuna tofauti kidogo matamshi huleta raha au karaha kwa pale mtamkaji ( ATATOHOA)atatamka neno visivyo ambalo huenda likaharibu maana au likabadili maana nzima.
kwenye kuandika utaandika neno sahihi lilivyo, ila kutamka unaweza kubana baadbi ya herufi kwa kuweka madaha ili kulete raha unapowasiliana mf, suali kuandika na swali kutamka kwa haraka na madaha, pia kuna maneno yenye maana mbili au zaidi kutegemea ni wakati gani unapolitumia ili kushabihiana na jambo unalozungumza mf baba kwa maana ya mzazi wa kiume au kibaba kwa maana ya kopo ka kupimia vitu visivyohesabika, au swala mnyama au swalaa kwa maana ya tendo la kuabudu. Pia kuna lafudhi kwa maana ya matamshi hapo ndipo wengi hupata mtihani katika kuutumia ulimi, eidha kutokana na sehemu uliyotokea au mfuma mzima wa maisha uliyopokua nayo mukiwasiliana, au mazingira uliyonayo, hivyo kuna herufi wengine hutamka (harufu)kama hazitumiki kisawasawa ndipo pale karaha inapotokea na kuharibu maana kamili ya neno.
Kuhusu suali lako Bro, michu mimi nijuavyo KUSWALI iwe dini yoyote kati ya hizo mbili zilizokusudiwa hapo juu, kama wenzangu walivyotagulia kueleza kua lugha swahilia nitaiita kama waarabu wanavyoita inimetawaliwa mno na maneno ya kiarabu pamoja na lugha baadhi. kwa vile ndimi zinashindwa kutamka sahihi ndio pale utakuta mtu katohoa neno la kuleta maana tofauti kabisa na lililokusudiwa.au mti hudiriki mpaka kuweka kilugha chake kidogo wakati anajitahidi kufikisha ujumbe ndipo palw maneno yanaanza kupoteza lafudhi au maana nzima. samahani kama nitakua nimetoka zaidi ya msaniati wako au sijajibu sawa ila mwalimu wangu wa kiswhili akitucharaza sana mboko pale tulipokua tukishindwa kutamka neno sahihi kwa kuto kulitambua au kulisahau na kutumia nahihii badala ya nanihuyu na ninihino badala ya ninihii, hivyo imeniathiri kidogo kwani nikisikia mtu anazungumza neno kisha akalitohoa nakarahika kidogo na kuona ooh amechapia hapo.
Usiwe na wasiwasi Bro. Michu kweli kuuliza si ujinga, na KILA SUALI LINA JAWABU, wadau tuendelee kuelimishana.
MICHUZI MIMI NADHANI KISWAHILI KINAJICHANGANYA SANA NA NAHAU, NGELI HASA WAKATI WA KUTENGENEZA SENTENSI.
ReplyDeleteKWA MFANO NENO "SENTENSI" SI LA KISWAHILI BALI LIMECHOMOA KATIKA LUGHA YA KIINGEREZA NA KULITUMIA KAMA LA KWAKE.
PAMOJA NA HOJA HIYO, MIMI HUWA NASHINDWA KUNYUMBULISHA NA KUCHAMBUA MAANA KAMILI WAKTI MTU ANAPOSEMA SENTENSI ZIFUATAZO;
1) NITAKULA WALI "NA KIJIKO".
2) NIMEKWENDA KWAKE "NIMEMKUTA" HAYUPO
3) JUMA HAYUPO "AMEONDOKA" MJINI
HAYO NI BAADHI TU LAKINI KUNA SENTENSI NYINGI AMBAZO HUWA ZINATAMKWA SANA NA BAADHI YETU AIDHA KWA UVIVU WA KUTUMIA VIUNGANISHI ILI KUIPA MAANA SENTENSI.
KAMA MFANO HUO WA KWANZA KWA KUSEMA-"nitakula wali na kijiko"
UKITAKA MAANA HALISI YA HIYO SENTENSI NI KWAMBA; nitakula wali na mboga iitwayo KIJIKO! au
Nitakula wali pamoja na KIJIKO chenyewe! au
Nitakula wali pamoja na rafiki yangu aitwaye KIJIKO!
LAKINI TUKITAKA KUTUMIA LUGHA HALISI NA SANIFU, SENTENSI HIYO INGETAMKWA HIVI;
"NITAKULA WALI KWA KUTUMIA KIJIKO".
HAPO NDIPO TUONAPO UVIVU WA KUTUMIA KUINGANISHI KIITWACHO (KUTUMIA) AMBACHO KISIPOTUMIKA, NDIPO SENTENSI YA (nitakula wali kwa kijiko) INAELEA BILA KULETA MAANA KAMILI.
SHUKRANI NYINGI;
MDAU WA KITENGO CHA KISWAHILI, CHUO KIKUU DAR ES SALAAM.
Issa Michuzi kilichonifurahisha sana hapa maalim issa michuzi, kuhusu kuswali na kusali. ni kwamba waislamu wa humu na wakiristo wa humu kwenye blog yako hawatupiani madongo wanapendana wanaitana ndugu. huu ndio utanzania wetu mzuri ukienda jambo blog kule ukisema asalaam alaykum tu wakati ni salamu tu basi unatukanwa mpaka basi tushikamane jamani nawapa pongezi issa michuzi blog na watu wake ndomana haifi. Ijumaa Njema.
ReplyDeleteNdugu yetu Anon 7 mar 10:10, watoa hoja wote waliotangulia hakuna aliyeongea vibaya au kumkwaza mwenzake kila mtu anajitahidi kujaribu kueleza ufahamu wake juu ya maneno hayo, mawili sijamuona alovuka mpaka hapo ila wewe ndo unaanza kukaanga sumu, na unakuja kwa kivuli cha angalizo kwani wadau hawalijui hilo ndio maana hata Bro. Michu mwenyewe anabania wale wavuruga amani humu kwenye mjadala sidhani kama watapata fulsa . Bahati nzuri wengi walioongea wanaonekana wana hofu ya Mungu na wanaheshimu uhuru wa ibada ya mwengine kama katiba na taratibu za nchi yetu al-muradi huvunji sheria.
ReplyDeleteNa sio swala ni suala. Swala ni aina ya mnyama.
ReplyDeletewanaposema swali kabla hujasaliwa wanamaanisha nini jamani
ReplyDeleteMichuzi, kwanza nikusahihishe kidogo.
ReplyDeleteSi "KUNRADHI" ni "KUMRADHI"
Kuhusu KUSALI na KUSWALI, hakuna KUSALI, ni KUSWALI tu. Hili neno limetoka kwenye lugha ya kiarabu na ndiyomaana waislamu wanalipatia na kulitamka vizuri KUSWALI kwasababu uislamu uko kwenye kiarabu. Mtu anaposema KUSALI anakosea, kwa sababu neno hilo KUSALI halipo. Pengine wakristo waliamuwa tu kulipindisha na kulitamka KUSALI kwa sababu walitaka kukwepa uarabu ambao unaambatana na uislamu. Kama hivyo ndivyo basi sawa tu, na itabidi ijulikane kuwa neno hilo ni la kikristo linalomaanisha KUSWALI. Lakini si la kiswahili fasaha.
Hao wanaosema KUSWALI ni kuuliza swali wanachemsha, kwa sababu kuuliza swali ni KUSUALI au KUSAILI na si KUSWALI.
wee anon wa friday, march7,2008 10:02:00 pm
ReplyDeletenaona hapo umechemsha ndugu yangu, na kwa jisi ulivyo na matatizo hata hata tafsiri yako haileweki, hebu angalia wenzako walivyotafsiri vizuri hapo,anyway nazidi kukuombea maana unahitaji maombi wewe si bure una lako jambo.