Wadau wa globu hii ya jamii. Napenda kuwakumbusha kidogo soka ya Tanzania Miaka ya Themanini.
Kumbukumbuku yangu haiwezi kuwa sahihi kwa timu zote na ninaomba tuchangie vikosi nitakavyovisahau.wakati huo nilibahatika kuona na kufuatilia Timu tofauti ambazo udhamini wake ulikuwa wa nguvu na wenye malengo.
Wachezaji walikuwa na Afya,walikuwa wanapatiwa mahitaji ya muhimu kama mishahara,Nyumba,usafiri wa jumla na ajira za kudumu.
Baada ya Mashirika mbalimbali kuyumba na kujitoa katika maswala ya michezo timu kama Pilsner,Ndovu,Pamba ,Ushirika,Biashara zote,CDA,na nyinginezo hazikuweza kujitegemea kiuendeshaji na hivyo kusambaratika.
Miaka ya Tisini na kuendelea Timu zilijitahidi kwa kusuasua hapa na pale kwa kuwategemea watu binafsi na mwanga haukuwa mkubwa sana kwa timu za mikoani kwani wachezaji wengi walikimblia Simba na Yanga.
Vikosi ni kama ifuatavyo:
Pamba-Rwechungura,Deo,Bori,R Abdallah,Masatu,Mao,Msonga,Masha,Kitwana,J Amiri-Pele,Fumo-Mwalimu Muksin Maftah
Coastal-Mwamba, Kolongo, Muhani, Hassani Juma,Elisha,Maumba,Aggrey,Kassa,Mgunda,Mwakuluzo-Ruga,Abubakari Hassani-Mwalimu Kinanda
Pilsner: Pazi,Jamhuri,Andrew Godwin,Washokera,Kondo Khamis,Muba Lindimu,Kaingilila,Msami,Athanasi,Mrisho -Zicco,Frank Mhando-Mwalimu MzirayAfrican Sports:Salimu waziri,Mandoza,Ali Mtumwa ,Banda,Mdeve,Raphael John, Mchemba,Twaha,Mkanwa,Mchunga Buruhani-Kakoko-mwalimu Mziray.
Ndovu-Arush Kisaka,Pande,Kishoka,Mkulila,Mkodo-Kijiko.Mwanga ,Mahamoud Omary,Bob Chopa,Khamis Gaga, Mateneke-Mwalimu Gwaja selemani
Ushirika-Moshi: Ndulute,Kaunda,kussi,Rodgers,Saidi,Michael,Mwakalukwa,Poisant,
Kalambo,Mahamoud Abbasi,Maliva-Korroso Daniel
Simba:Mkandawile,Raphael,Twaha,Nkoma,Twalibu,Lenny,Sagala,
Mwikalo,Eduward,
Zamoyoni,MalotaYangaSahau,Minziro,Kenny,Chama,Mwaibambe,
Issa,Abubakari,
China,Mziba,Makumbi,Keegan.
ReliMorogoroMsumari,Mtono,Mkwera,Lupindo,Magoso,Mtwa,Butinini,
Boniface,Mbuyi,Mihambo,Roland Michael-Mwalimu Semkoko
Naomba tusaidiane kuzikumbuka timu na majina ya wachezaji wa kipindi hicho.Nilishuhudia marehemu Mchemba akiwafunga Simba bao tatu bila pale Mkwakwani.Marehemu Gaga alimgonga Muba Lindimu na Kiwiko pale Arusha Stadium,Khasimu Mwajeki alikuwa awafunga mara nyingi Yanga akitokea Bench. Vichwa vya habari ilikuwa Coastal Wafanya miujiza kule Kenya.
African Sports yawa bingwa na kwenda Mbambane .Fumo Felician mwiba kwa Yanga.
Naomba anayekumbuka vikosi kama Majimaji,Tukuyu.R.T.C zote,C.D.A.Wakati huo wachezaji wengi walionekana kutoka mashule ya Sekondari ,nawakumbuka wakina Hassani Matani,Francis Mwikalo,Hassani Juma,Athumani China, Nteze, Lunyamila, Khashimu Walele, Aggrey Chambo.
Nini kifanyike ili tuweze kuona burudani kama ilivyokuwa miaka hiyo ya Themanini?
Mdau
Mdau umenikumbusha mbali sana.Majuzi tu tulikuwa tunabishana kwenye 'chinywaji'kwamba wale wachezaji of that type(kama uliowataja wakienda wapi???)Bora maximo angekuja enzi zile.Michuzi kipindi hicho kijijini kwetu tulikuwa kwenye kiredio cha jirani yetu mmoja(kijiji kizima!!)kesho yake wa Dar wanaamkia kuangalia picha za michuzi kwenye magazeti(Uhuru,mzalendo,daily naniii)
ReplyDeleteAnyway.
Nyota nyekundu.
Steven Nemesi Moris Nyuki,Mbaraka Mohamed,Mohamedi Nyauba,Pazi Ally,Faustin Kibingwa,Stephen chibichi,Hamis Dilunga,Ayoub Mzee,John Manyama,Roster ndunguru.(Kunradhi sina uhakika kama kuna marehemu kwenye hao.)
Kikubwa kifanyike ni kubinafsisha timu hizo.manake wanachama wamekuwa ndio wanau mpira kwa kuleta migogoro.makampuni yashawishiwe kununua timu hili ziendeshwe kibiashara kama sio hivyo hatutafika popote.na majina hayo ungeyaongezea majina yao ya utani walio pachikwa ndio inaleta raha zaidi.
ReplyDeleteMakampuni/Mashirika ndiyo yanaweza kuunyanyua mpira wetu lakini tukumbuke vile vile dunia inabadilika ndugu zangu,watu wenye uwezo wanaweza kumiliki timu na ikafanya vizuri,mchezo wa wanachama umepitwa na wakati.Mpira uliharibika mwanzoni mwa 1990s baada ya mafisadi kula hela zote za Pilsiner,Ndovu,Ushirika,Pamba,Mecco,RTC(Biashara),Pamba,n.k.This was after Kambarage stepped down in 1985.miaka 5 baadaye makampuni/mashirika yote yakaanza kuliwa na mchwa.Timu zote zibinafsishwe,wanachama wakae kando.
ReplyDeleteEnzi za themamnini ndio kiwango cha soka hapo nchini ilishuka kama meli iliyozama...acha uthemanini,kumbuka usabini na viwango kama vile vya Omar Mahadhi,Athuman Mambosasa,Kitwana/Sunday/Kassim Manara,Abdallah king pele Kibaden,Abdulrahman Juma,Thuen Ali,Maulid / Abbas Dilunga,Haidar / Khalid Abeid...niendelee???
ReplyDeletemwishonimwshoni iliibuka milambo (mirambo) tabora, pita poka, jobe ayubu, baribari, et al. simba akienda tabora anapelekwa mchakamchaka mpaka anaamua kucheza ubabe na anafungwa vilevile. jamaa wakija dar wembe uleule simba analia ... anayekumbuka stori za karandinga la simba kule tabora atueleze
ReplyDeletelakini kabla ya hapo alikuwepo ibrahim mbuzi beki mstaaarabu (tukuyu?) majix2?) john makelele, sikinde mbunga,
kama chaaz hilary anasomaga blogu hii atukumbushe enzi zake rtd
NYOTA NYEKUNDU;steven nemes,musa kihwelu(marehem)raphael mapunda,abas kukka,frank kasanga'bwallya'muhidin pazi,zonte mahundu(meneja)stephen chibichi,mahmmed mgalike,john mngazija..meneja;king kibaden mputta
ReplyDeleteWengine:
ReplyDeletePAMBA: Beya Simba, Ally Bushiri,Yussuf Abeid,Hamza Mponda, Nteze John...nk
COASTAL U:Mohamed Mwameja, Abuu Yassin Napili, Iddrisah Ngulungu, Razak Yussuf, Abdallah Tamimu, Joseph Lazaro....nk
YANGA: Doto Ruta Mokili, Yussuf Bana,Athumani Juma Chama 'Jogoo', Makumbi Juma 'Homa ya Jiji' Abeid Mzima,Juma Kampala, Hussein Idd, Isihaka Hassan 'Chukwu', Allan Shomari, Sanifu Lazaro......nk
TUKUYU S: Suleiman Mathew, Steven Mussa, Godwin Aswile, Jimmy Morerd....nk
MAJIMAJI: Peter Mhina, Samli ayoub,Octavian Mrope, Mhando Mdeve...nk
PAN AFRICA:Leodgard Tenga, Jellah Mtagwa,Mohamed Mkweche, Jafar Abdulrahman,Ally Katolila, Peter Tino,Juma Burhani, Carlos Mwinyimkuu....nk
C.D.A:Jummanne Chale,Justine Simfukwe,Omar Mgeni,Charles Mngodo,Madaraka Suleiman,Yussuf Ambwene...nk.
.....na wengine jazieni...!!
MSISAHAU SIGARA CHINI YA MANSOUR MAGRAM JAMANI ILIKUWA KIBOKO.
ReplyDeleteRELI NA TUMBAKU ZOTE KUTOKA MOROGORO.
CDA WALIKUWA WAKIKURUPUSHANA NA KURUGENZI PALE DODOMA.
NAKUMBUKA NILIKUWA NAFANYA MAZOEZI NA KURUGENZI ENZI HIZO CHINI YA MUKHTAR SIMBA, IDD, INNO NA WENGINE KIBAO.
Coastal hii ni vigumu kwenu vijana wa leo kuikumbuka,nakutajia kwa namba.Saidi Jeki,Dondo Ali,Hemedi Morocco,Hassani Shengo,Yahaya Dondwe,Salimu Amiri ,mohamed Kampira,Titus Bandawe,Mohamed Salimu ,clement kwagila,Saidi George.
ReplyDeletePan Africa
Juma Pondamali,John Faya,Mohamed Mkweche,Leodga Tenga,Jellah Mtagwa,Adolf Rishard,Godian Mapango,Hussein Ngulungulu,Peter Tino,Juma Buruhani,Juma Matokeo
Mtoto hatumwi hasokoni hapo.Wasoma Blog jamani naomba vikosi vya Themanini,Tukuyu,Cda,Biashara nakuendelea.
Miaka ya sabini ilikuwa na wataalamu nakubali na walikuwa na maumbo makubwa na tofauti na miaka ya Themanini.Vivyo hivyo kadri miaka inavyozidi kwenda ndivyo tunavyozidi kuwa na wachezaji wenye maumbo madogo na pengine viwango kushuka pia.
ReplyDeleteMiaka ya Themanini tuliweza kupata wachezaji zaidi ya Miaka ya Sabini,na watu wengi wa miaka kuanzia Arobaini na tano mpaka thelathini na nane waliweza kupata kuwaona watu wa waliocheza miaka ya Themanini.Hawa wa miaka ya Sabini wengi wetutuliwaona wakati wanastahafu.kWA MFANO Simba ya kina Mahadhi.
Mahadhi,Daudi salumu,Athumani Juma,Bakari Tall,Njohole,Kikwa,Kulagwa,Sabu,Kibadeni,Thuweni
Walikuwepo wakina Madale,Bana,Masha,Isihaka Hassani chuku,Gibson Sembuli,Sunday Manara,Kitwana Manara.Naamini wapo watu watatupa kumbukumbu nzuri za miaka ya sabini.Tuzidi kupeana List za zamani tafadhali-samjo
Majimaji,
ReplyDeleteKichochi,Samli Ayubu-beki mstaarabu,Abdallah Mbuzi,Mhando Mdeve,Peter Mhina,Octavian Mrope,Kevin Haule Dadi Faresi,Innocent Haule,...?...Celestine Sikinde Mbunga
Naomba jazia nilipoacaha wazi au kukosea-Samjo
Jamani Octavian Mrope kachoka sana na alikuwa anapiga six kuliko maelezo.
ReplyDeleteilikuwa wakati unaweza kusikiliza mpira redioni na ukafurahi sana....enzi za marehemu david chilambo.....safi sana kwa kumbukumbu bora...
ReplyDeleteMNAHARIBU TIMU ZA WENYEWE, NYIE BAKIE NA SIMBA NA YANGA ZENU, TIMU ZILIKUWA HIVI:
ReplyDeleteCDA ya 1984 ilikuwa: Dan Poka, Yusuf Ambene, Suleiman Abeid, Charles Suleiman/Mnubi jumanne,Lilla Shomari/Hakim Byemba Africa, Charles mgodo, Hamisi Kamungu, John Challe/Adolph Kondo, Abasi Mtuli, Omari Mgeni, Justine Semfukwe.
Pan African ya 1984: Juma Pondamali, Jafari Abdurahman, Mohamed Mkweche, Rashid Idd/John Faya, Jella Mtagwa, Mohamed Rishard, Gordian Mapango, Husein Ngurungu, Peter Tino, Abdallah Burhani, Ibrahim Kiswabi.
TUKUYU Star 1985: Mbwana Makata, Ali Kimwaga, Taisi Mwalyoga, Godwin Aswile, Suleiman Mathew, Aston Pardon, Yusuph Kamba, Peter Mwakibibi, Richard Lumumba, Justine Mtekele, Karabi Mrisho.
Coastal union 1988: Hamisi Makene, Saidi korongo, Joseph Lazaro, Idrissa Ngurungu, Yassin Napili, Ali Maumba, Mohamed Kampira, KAss Mussa, Juma Mgunda, Husein Mwakuluzo, Razaki Yusuph.
Africa Sports 1988: Duncan Mwamba, Kajembe,Christopher Elisha, Hamza Maneno, Mhando Mdeve, Rafael john, Abass Mchemba, Twaha Omari, Victor Mkanwa, Mchunga Bakari, Juma Burhani/Abdul Donoa.
PILSNER 1988- Iddi Pazi, Selemani Mkati, Andrew Godwin, Hamisi Kondo, James Washokera, Rajab Rashid, Kaingilila Maufi, Charles Msami, Atanasi Michael, Saidi Mrisho, Frank Mhando.
NDOVU 1988- James Kisaka, Ali Pande, Simon Kishoka, Juma Mkulila, Lilla Shomari, Charles Mgodo, Mwanga Luheya, Mahmoud Omari/Mhidini Cheupe, Feruzi Juma, Hamisi Gaga, Mohamed Mateneke/Ayoub Shabani.
Soccer in wenyewe jamani acheni kuharibu lineup za watu, haya uliza tena unataka lineup ya timu gani?,lakini sio simba na Yanga hizo kila mtu anajua.
ANGEKUWAPO MAXIMO SI AJABU KUSINGEKUWEPO NA MCHEZAJI WA SIMBA WALA YANGA KWENYE NATIONAL TEAM.
-MTU WA MPIRA
***siwaamini Steven Nemes hajawahi kuchezea nyota nyekundu,alichezea majimaji akaenda Yanga,akaenda simba.Get it right.
ReplyDeleteHebu acheni ushabiki wa wivu...TZ's most succesfull club:Simba SC is a Tanzanian football club based in Dar es Salaam. Their home games are played at National Stadium. Simba SC is one of two biggest football clubs in Tanzania, their archrivals being the Young Africans. The club had several names during its history, when it was founded in 1936 it was called Queens, then changed to Eagles, Dar Sunderland and later, in 1971 changed to its actual name, Simba (that means Lions in Swahili).
ReplyDeleteSimba is the biggest also the most titled club in Tanzania.
[edit] Achievements
The highest level of success that Simba SC achieved was getting to the final of the CAF Cup in 1993 where they lost to Stella Abidjan of Ivory Coast. It was the highest achievement on continental competitions reached by any Tanzanian team. One of the most memorable years for the club was 2003 when it knocked off the then reigning champions Egyptian giants Zamalek on its way to qualify for the group stages of the CAF Champions League. In the first round of that year's competition, Simba SC eliminated Santos of South Africa.
Tanzanian Premier League: 16
1965, 1966 (as Sunderland)
1972, 1973, 1976, 1977, 1978, 1979, 1980, 1993, 1994, 1995, 2001, 2002, 2004, 2007
Tanzanian Cup: 3
1984, 1995, 2000
Tanzanian Tusker Cup: 4
2001, 2002, 2003, 2005
CAF Cup:
Finalist : 1993
CECAFA Clubs Cup: 6
1974, 1991, 1992, 1995, 1996, 2002
Acha wewe Duncan Mwamba hajawahi kuchezea Sports,Wala Christopher Elisha,Wala Kajembe.Salimu waziri,Mandoza/semkiwa,Martin Mahimbo-Winter Green,Hassani Banda,Mhando mdeve/Hamza Maneno,Raphael John/Steven Kinduru,Dadi faresi/Abbbasi Mchemba/Twaha,Mkanwa,Mchunga,Buruhani/Donoa
ReplyDeleteUmeshawahi kumsikia Golikipa anaitwa Mwarami?
Steven Nemes alitkea timu moja na John Mngazija kwenda Nyota Nyekundu.Walitokea Bagamoyo
ReplyDeleteKabla ya kuwika na Coastal Union, Duncan Mwamba alikuwa African Sports.
ReplyDeleteChristopher Elisha alikuwa African Sports, usimchanganye na Elisha John aliyekuwa Coastal na akaja Yanga.
Na wee unayejifanya mtu wa mpira mwaka 1988 Salim Kajembe aliisha acha kucheza mpira!!
NEMES KACHEZEA NYOTA NYEKUNDU,WAMWSHUKA DARAJA YANGA WAKAMCHUKUA
ReplyDeleteNakumbuka ligi daraja la kwanza Tanzania bara 1989 Arusha Ndovu versus nyota nyekundu, Ndovu 1 Nyota Nyekundu 0. Tukiwa Sheikh Amri Abeid Stadium tunaangalia mechi hii lakini masikio yetu yalielekea Mwanza na Tanga. Mjini Mwanza Pamba anacheza na RTC Kigoma, mtangazaji marehemu Dominick Chilambo. Hapa Pamba anatafuta ushindi akiwa nyumbani kwake dhidi ya RTC Kigoma inayoshuka daraja huku akiomba Coastal Union huko Tanga amsimamishe Yanga ili ubingwa uende kwa Pamba. Yanga ilikuwa inatafuta ushindi wa aina yeyote ile ili awe bingwa. Dar es Salaam Simba alikuwa na African Sports ya Tanga huku ikiomba Pilsner ya Dar iifunge Kurugenzi ya Dodoma kwenye uwanja wa Jamhuri pia CCM Kirumba kule Mwanza Pamba iifunge RTC Kigoma ili Simba anusurike kushuka daraja. Hadi mwisho, Simba 1 African Sports 1. Pamba 1 RTC Kigoma 0. Pilsner 1 Kurugenzi 0. Simba alinusurika. Mjini Tanga Mkwakwani Stadium Joseph Lazaro aliunawa mpira eneo la hatari, Fred Felix Minziro akafunga kwa penalti. Yanga akautwaa ubingwa
ReplyDeletenani ana kumbuka kikosi cha samba League Kuu Tanzania mwaka 1991.
ReplyDeletenaomba kupata majina tu ya wachezaji wote waliokuwamo kwenye team hiyo