kama ulidhani ni dar pekee ambako wadau wanazuiwa kufaidi jasho lao kwa kupumzika kwenye bustani zilizojengwa kwa kodi zao, umenoa. mwanza nako ngoma droo. unaambiwa bustani hiyo karibu na mawe yaliyopandana ufukweni mwa ziwa victoria ni marufuku kugusa kama wewe si mhusika wa sehemu hiyo kama huyu jamaa ambaye ni mfanya usafi wa eneo hilo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Nashukuru misupu umenikumbusha nyumbani kwetu rock city

    ReplyDelete
  2. Ni kweli walipa kodi haturuhusiwi kubarizi maeneo ya 'bichi' lakini zamani ilikuwa ruksa kwa kila mtu kupumzika pale, pakaharibika sana na kugeuka sehemu za kujisaidia ovyo, vichaka vikashamiri, ukabaji n.k. Acha tu watukataze, ili paendelee kuwa safi. Kitunze kidumu!

    ReplyDelete
  3. Mimi nakubaliana na anon hapo juu kwamba sehemu hii ilikuwa wazi kwa watu wote lakini ndiyo hivyo tena, sijuwi ni kwa sababu ya watu kutokuingia madarasani au uzembe au ushamba au ujinga sielewi, sehemu hii iligeuka toileti na dampo...huwezi amini kwamba sasa panapendeza hata kwenye picha. Wacha wazuie, wataruhusu watoto walioko shule wakimaliza kusoma

    ReplyDelete
  4. Sawa tulifanya makosa, dawa si kuzuia bali kuweka sehemu ya kujihifadhi (choo) hata kama ni cha kulipia. Nimeona sehemu nyingi TZ ambapo kuna mikusanyiko ya watu, vyoo vya kulipia vimeshakubalika. Mambo ya bongo bwana funga funga tu. Hakuna mbadala?

    ReplyDelete
  5. Wacha wafunge kwani ustaarabu wa watumiaji wa mandhali some time unakuwaga ni ZERO, kwani garden hizi huwa ndio zinageuzwaga kuwa gesti house, vyoo na madampo ya takataka.
    Bora wafunge watu waone kwa mbali kama tunavyoona katika picha hii

    ReplyDelete
  6. Nakubaliana na watangulizi watano kwa maoni yao, kuna usemi unasema ustaarabu ni kitu cha bure, ila kwetu inabidi tuulipie garama ili tujifunze huo ustaarabu.Kuna m.f mingi kwenye mauwanda kama hayo usishangae kukumbana na masazo ya kondom zilizotumika zimetupwa hadharani wakati nyie mmeenda kupumzika kumbe usiku watu wakishughulika huko.na pia hao wanaopumzika huacha masazo yao ya makopo na machupa akitegemea sijui nani aje awaondolee, wacha watuzuie ili tujue kutunza sehemu ziwe zinapendeza ukiangalia tu au wakija wageni wowote wawe wanapeleka sifa kua ukipita sehemu flani pazuriiii inatosha.

    ReplyDelete
  7. kuzuia na kutoruhusu watu kupumzika ni makosa makubwa sana na wanaofanya hivyo hawana Akili hata chembe,kwa sababu wanawanyima raia haki yao ya msingi ya kutembea ndani ya nchi yao pasipo kikwazo,kwani Polisi wapo wapi na watu wafanye ujinga wa kujisaidia ovyo.Ni wajibu ya manispaa kuhakikisha jiji linakuwa safi na ulinzi na usalama wa raia pia.Nadhani kunasheria ambazo mtu akishikwa anafanya tendo ambalo ni kinyume na Taratibu za mila na desturi zetu adhabu ichukuliwe dhidi yake mfano Fine au kusafisha eneo hilo,Lakini kufunga sio solution hata kidogo labda tu eneo hilo liwe hatari kwa binadamu kufika na kupumzika.Sijawahi kusikia nchi yoyote duniani inazuia raia wake wasifike eneo zuri.bado tunabaguana hata sehemu gani za kwenda na sehemu gani za kutokwenda.Tuacheni ujinga kwani makosa ya wachache ndio adhabu wapate mkoa mzima au wananchi wa nchi nzima.Nia sahihi ni kuweka sheria kwamba yoyote ambaye atakutwa anakojoa hapa adhabu yake ni fine ya Tsh 10,000 then tuone kama watu watakojoa sehemu hiyo au adhabu itakuwa kusafisha eneo hilo kwa kipindi cha mwezi mmoja.lakini kufunga ni kunyima haki walipa kodi na watoto wadogo ambao wanamengi ya kujifunza katika maisha yao.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...