picha hii ya kijana ombaomba akiwa na senti alizojipatia siku hiyo jijini harare imeletwa na mdau ambaye aliiona katika tovuti ya bbc na kuona heri tushee naye adha iliyoko huko kwa jongwe

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. Ha ha ha ha lol!

    kweli ukisema kwako kwa unguwa ujuwe kwa mwenzio kwateketea.

    Naskia huko ukitaka kununuwa mkate inabidi ujaze pesa kwenye kiloba tena ushindilie aka lumbesa.

    Naipenda nchi yangu Tanzania.

    ReplyDelete
  2. RAIS Robert Mugabe wa Zimbabwe, Jumamosi iliyopita, Februari 23, alifanya sherehe kamambe ya kutimiza umri wa miaka 84. Sherehe hiyo inakisiwa kugharimu pauni 610,000 (Sh. bilioni 1.4).

    Zaidi ya ng’ombe 100 walichinjwa katika sherehe hiyo iliyoambatana na vinjwaji na kuhudhuriwa na mamia ya wanachama na wafuasi wa ZANU-PF; hasa kwa sababu iliambatana na uzinduzi wa kampeni ya Mugabe ya kuwania tena urais katika uchaguzi mkuu wa mwezi ujao....kudadadek fisadi Mugabe

    ReplyDelete
  3. kule sasa inflation rate ni asilimia laki moja!!!!!!!!11
    hapa kwetu ni 4 to 7 na bado tunaona joto ya jiwe sasa kule kwa babu mugabe je
    mzee kashafika 86 years kama skosei lakini bado yumo tu , kweli africa bara giza

    ReplyDelete
  4. Bei ya mkate Zimbambwe ni million tano! Wenzetu wako kwenye hali mbaya sana.

    ReplyDelete
  5. Hivi kwanini hakuna migomo huko?

    ReplyDelete
  6. Hebu acheni kumkashifu mzee Mugabe...si hali yetu sawa tu,kwani kuna utofauti gani?Mbona mna kumbukumbu fupi...zile foleni za sukari na mkate za enzi za mzee Mwalimu mmezisahau!!!

    ReplyDelete
  7. Yaani Mugabe anataka kugombania urais tena? Si apumzike amalize siku zake ametulia! Jamani! Zimbabwe wana hali mbaya kuliko hali tuliyokuwa nayo enzi za Mwalimu!

    ReplyDelete
  8. Cash rules everything around me (c.r.e.m.e) get money dollar dollar bill yo!! 0hhh my bad, Zimbabwe Dollars...lol. Even though their economy sucks but you cant knock the kid's hussle.. get your money duffle bag boy..

    ReplyDelete
  9. Kwa hiyo izo hela alizonazo bwa mdogo hapo ni sawa na buku unusu ya tanzania. ni mtazamo tuu:-)

    ReplyDelete
  10. Africa is resourcefully rich but economically poor because Africa lack leadership.

    Sisi wachache tuko tayari kuacha kazi zetu za maana zinazolipa $100,000 na kuendelea na kurudi kujenga nchi ila tatizo ni wananchi wenyewe.

    Wananchi hawaelekei kukerwa na ukandamizaji wa Serikali zao na ndio maana kila siku wanazichagua!!

    Nasubiri Waafrika wabadilike ili na mimi ndio niweze kujitolea kuja kuchangi maendeleo

    ReplyDelete
  11. ukweli ni kwamba huyu mtoto amezawadia hii mihela na kampuni ya tigo

    ReplyDelete
  12. Wewe hapo juu (Sun,6.52) unaesema kwamba ungaacha kazi yako ya malipo mazuri ili uende kuendelea nchi yako kama wananchi wangeonyesha moyo wa kukereketwa!

    Yaani unangojea wakutafunie wewe ukatafune? Kwanini usiende ukajumuika nao ili mpiganie maendeleo yenu pamoja. Kwa maana hiyo huna tofauti nao.

    ReplyDelete
  13. Watanzania wenzangu hili suala la Zimbabwe siyo la kulifanyia utani ndugu zetu kule wanawakati mgumu.Maisha hayakamatiki.Supamaketi ziko tupu hazina bidhaa.Bei ya mkate ukibahatisha kuupata moto wa kuote mbali.Zimbabwe haikuwa hivi.Mugabe bado kang'ang'ania madaraka na anagombea tena awe Rais kw miaka mingine 5 ijayo hivi sasa akiwa amefikisha umri wa miaka 84 na ametawala kwa miaka 27 sasa akiwa Rais wa Zimbabwe.Kumbukeni Watanzania ndiyo tuliokuwa mstari wa mbele kabisa katika kwasaidia ndugu zetu wa Zimbabwe wakiongozwa na Mugabe ili waweze kujikomboa kutoka katika utawala wa kikoloni na kibaguzi.Sasa ndugu zetu wa Zimbabwe bado watahitaji kusaidiwa tena waondokane na Uongozi Mkongwe uliodumaa kifikra na kiutendaji uliong'ang'ania madarakani hata pale alama za nyakati zilipo ashiria kwamba sasa ni wakati kwao kuondoka madarakani na kuwapa nafasi vijana wa Zimbabwe waendeleze mapambano kwa maslahi ya Taifa.Jamani Rais Mugabe amechoka anahitaji kupumzika.Naamini Zimbabwe wanazungumza sana Kiswahili.Mitandao hii ya Internet wanaipata na ujumbe huu wengi watausoma.Watanzania wenzangu kwa moyo uleule uliolikomboa Bara la Afrika Kusini basi tuwape Moral Support ndugu zetu wa Zimbabwe wazinduke na kupata ujasiri wa kumwambia Rais Mugabe kwamba sasa inatosha.Wakati umefika kwa kijana zaidi kushika uongozi kupitia uchaguzi wa kidemokrasia ulio wazi,huru na wa haki.Simba Makoni ni miongoni mwa wagombea wa Urais.Kma hawata mtaka mgombea kutoka Upinzani basi Wana Zimbabwe wana chaguo la zida kwa Simba Makoni.Wasije wakafanya kosa lingine tena kwa kumrejesha Mugabe katika Urais katika kipindi hiki kigumu.Lazima yawepo mabadiliko.Lakini mabadiliko hayo yataletwa na Wana Zimbabwe wenyewe.Waafrika wengine wataweza kutoa Moral Support tu itakapo wezekana.Pengine siye yeye mwenyewe Mugabe anayependa kuendelea kuwa Rais tena hivi sasa akiwa na umri mkubwa mno na amechoka anahitaji kupumzika.Pengine ni wale waliomzunguka Mugabe ndiye wanaye mlazimisha Mugabe aendelee kugombea Urais wakihofia kupoteza nafasi zao za Uongozi.Wengine wakihofia kufikishwa mbele ya sheria kwa maovu waliyoyatenda wakiwa viongozi.Tunawatakia WanaZimbabwe wote kila la kheri katika uchaguzi mkuu ujao.Chagueni kwa makini,Chagueni Kiongozi atakaye watoa katika taabu na shida kubwa inayo wakabili hivi sasa.Tunathamini mchango wa Rais Mugabe akiwa Kiongozi Mkuu wa Zimbabwe lakini sasa tunasema inatosha bora apumzike na kupisha kijana mwenye akili na nguvu zaidi aweze kuendeleza zaidi pale atakapo achia yeye.Zimbabwe bado itakuwa salama bila ya yeye asiwe na wasiwasi wowote!Aondoke watu wangali wanampenda na kumhitaji.Asingoje atimuliwe madarakani kama Paka Mwizi!Ni ushauri tu.

    ReplyDelete
  14. Nyie semeni tambarare tu ndio tunapoelekea huko. ona makonda wanvyobebab hela mkononi fanya research leo kama wameanza kuweka mkononi note ya elf kumi tumeisha.
    The truth ni kwamba kila mtu ni millionea zimb ila ni majina tu hela aina thamani nilikuwa naongalia news hapa bbc jamaa katoa tip millioni mbili IoI na jamaa hapa wasivyompenda!
    Londoner

    ReplyDelete
  15. Asante Mungu kwa sababu nilizaliwa Tanzania. Nakupenda tanzania, nilivyoona matangazo yako CNN nikazidi kukumiss.
    Naomba Mungu atubariki ili tusije kufika hali waliyonayo Wazimbabwe, lkn pia naiombea zimbabwe.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...