pichani ni waliokuwepo kwenya shughuli ya kuwasaka wataoshiriki kwenye kumtafuta pop idol wa ist afrika mashariki imeanza leo dar ambapo vijana kama 500 wamedahiliwa kwenye awamu ya kwanza ya zoezi hilo katika ukumbi wa ubungo plaza. awamu ya pili itakuwa siku ya jumapili mahali hapo

lucy kihwele akiwa amewapiga konozz nakaaya sumari (pili shoto) na banana zorro (pili kulia) wanaomsaidia katika zoezi la kusaka pop idol wa bongo. kulia ni mwandishi wa habarileo na shoto ni msaidizo wa lucy. picha ya kati inaonesha washiriki wakitoka kuchukua matokeo ya udahili wao ambao ulihusu kupigwa picha za video huku wakiimba wimbo wautakao. washindi wataungana na wenzao wa kenya na uganda huko nairobi ambako mshindi wa afrika mashariki atapatikana baada ya kukaa na kuonesha vitu vyao huku wakipigiwa kula. jumla ya vijana 100 watakuwepo kwenye hatua hiyo ya fainali

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 22 mpaka sasa

  1. huyo sio Anastazia jamani?? yaani ndio amenenepa hivyo?? si mchezo!!! kweli duniani hakuna mtu mwembamba!!!!

    ReplyDelete
  2. Mbona tunatoa photocopy ya kazi ya wengine bila hata kuwa na chembe ya uoga? Kwa hizi picha tu..hii pop Idol ni xerox ya American Idol. Angalia neno Idols kwenye hizi picha (fonts zake na rangi yake) kisha nenda ka google American Idol uone jinsi zinavyowiana. Kisha angalia maudhui ya hii show compare na ile nyingine. Sio vibaya tukiwa na shows za kutafuta talents, nafikiri ni vyema watu wakawa creative kidogo kuliko hivi, maana naona tumecopy to the extereme

    ReplyDelete
  3. Naona Lucy ana personal assistant. Duh hongera dada. Kwa mantiki hii na mimi kuanzia leo naanza kutoka na house girl wetu.

    ReplyDelete
  4. MBONA BONGO HUWA HATUNA ANY ORIGINAL IDEA KILA KITU TUNAIGA TU? NI KWAMBA HATUNA UPEO WA KUFIKIRIA VITU VIPYA AMA TU WAVIVU WA KUFIKIRI? SASA HII SI AMERICAN IDOL THEME KABISA? NA WALE WENGINE WAKAIGA AMERICA'S NEXT TOP MODEL, PEOPLE BE CREATIVE KHA!! YAANI SAA NYINGINE INABOA.

    ReplyDelete
  5. Kwania mutumia nembo/Log ya American Idol, rangi pia, jamaa hawajui Copyright laws,

    ReplyDelete
  6. Safi sana waandaaji wa IDOL..mnatupa moto sisi tulioko nje ya nyumbani..big up waandaaji

    ReplyDelete
  7. HONGERA SANA WAANDAAJI..MNAJITAHIDI HONGERA ZENU..HIYO NEMBO/(NENO) ..IDOL.. INAIKUZA/ INAWAKILISHA NEMBO/SHINDANO YA NCHI ZA KIGENI..MNAWEZA TUMIA NEMBO AMBAYO ITATUTANGAZA NA SISI NYUMBANI NA DUNIANI...TUJARIBU KUWA WABUNIFU..KWANINI NENO...IDOL..LISITAFSIRIWE..KISWAHILI..NA MENGINE MENGI YAKAFUATIA...TUNAWAJIBU WA KUKUZA/KUTANGAZA LUGHA YETU, UTAMADUNI,MALI ASILI NA MAZINGIRA.....kumradhi kama nimewagusa pasipo stahili.

    ReplyDelete
  8. MICHUZI MI HUYU HUYU NAKAAYA TU YAANI NAMZIMIA KINOMANOMA, NAOMBA NAMBA YAKE IF U DONT MIND BRO........SI UNAKUMBUKA YALE MAMBO YETU YA YMCA MIAKA YA 90sMI NILIKUWA PALE NA SENSEI MAWALA.
    MDAU UGHAIBUNI

    ReplyDelete
  9. @ 8:56 do your homework kabla hujachambua watu copy right ni USA ndio watoe . Unajua American idol ni version ya UK pop idiol? Kabla haijawa maarufu ilikua show ipo UK kwanza. Ipo australia na nchi nyingi tu za Europe sasa. Kwa hiyo mwenye kugawiwa copyright sio mmarekani

    Ila bongo wasije wakalipua lipua tu kama majudge ndio hao wakina nakaaya basi itakua bomu tu. Kujua kuimba sio kujua mtu mwenye kipaji...randy, simon cowell na simon fuller ni maproducer wa muda mrefu sana. wamevumbua vipaji vya wengi sana kabla hawajaingia kwenye hii show

    ReplyDelete
  10. oyaa!mshikaji unayetaka contact ya nakaaya umechelewa nakaaya ana mchumba,try some where else.

    ReplyDelete
  11. This is a law suit waiting to happen! Hiyo ni copy right infringement on a name and design that has been trade marked. Waki ona wenyewe mbona mtakoma! ITV au sijui ni mama Rita Paulson (spelling) wasubiri law suit! Be origino jamani! ayayaaaa !

    ReplyDelete
  12. We anon 3:12AM - It doesn't matter if copyright/trademark imetolewa US au UK au popote pale, ila whoever owns the copyright anaweza aka sue because it belongs to them. Simon Cowell kama mwanzilishi doesn't matter kama ni ya UK, US au Australia ni ya kwake! so lazima muwe careful na property za watu. Na kama ina tumika kwengine au kama unataka kuitumia lazima upewe ruksa na mwenyewe. Kwahiyo hatujasema kuwa haiweza kutumika ila lazima wakupe ruksa. Ni kama vile magazeti yalotumia picha za Bro Michuzi bila kumwomba ruksa - ni plagiarism. Na hii vile vile is the same situation. Lazima mupewe ruksa na uwape credit the owners.So you do your homework!

    ReplyDelete
  13. huyu nakaaya simpendi, ni nipeni kontakti za huyo demu wa kushoto kabisa

    ReplyDelete
  14. Hi Wadau,

    The Idol show is run by a company called Endamol, they are based out of UK with branches in SA and other major continents. These are the same guys who did Big Brother. As someone who is working in media in TZ, I would recommend you research issues and ask for clarifications. The show has been done before last year in Kenya and involved Tanzania and Uganda. Naakaya was a TZ rep who never made it to the finals. This year, same format. People vote via SMS to kick people out of the house. No infringement. Just pure globalization of media properties that proved to work.

    Regards,

    Mdau

    ReplyDelete
  15. @11:12 am ....Sasa mnajuaje kama wameshapata copyright? Nyie mko huko? Do your homework before you critisize people. Tangazo lao la hiyo audition ya East Africa yametolewa hata huku USA. Niliona sasa kama ni kufringe si wangeshashtukiwa?????

    ReplyDelete
  16. Mdau hapo juu at 7:27. Naona ume miss their point. Hawazungumzi the show. Wanachozungumzia ni logo design.

    ReplyDelete
  17. Mtasema sana lakini idols wanataka kufranchise kampuni yao kwa kila mtu ..ni hela yako tu ..hata kama unataka kuanzisha Dr es salaam idols wewe wacontact walipe ushuru wao ...then unaendeleza libene lako

    ReplyDelete
  18. HUYU LUCY NA HAWA IDOLS WAWAONESHE MFANO VIJANA WENZAO KWA KWENDA KUPIMA AFYA ZAO PIA. NI MATUMAINI YANGU PICHA IJAYO ITAKUWA IKIONESHA WAKIPIMA AFYA ZAO KWANI TUMEKWISHA WAONA WAKIWA MIKUMI NA SEHEMU NYINGINEZO.

    ReplyDelete
  19. kwakweli wadau ambao mko nje baadhi yenu ni wachemfu,mnakimbilia kuponda hata msivyovijua. Idols (West africa Idols,East Africa Idols) na pop idols hazijaanza kufanyika jana afrika kama alivyosema mdau wa media hapo juu.Mara ya kwanza Tanzania mshindi alikuwa Banana Zoro na ni miaka kadhaa iliyopita.mashindano yote haya yanafanyika yakiwa yamepewa baraka zote na hao wenye copyright ambao kimsingi ndiyo waandaaji wenyewe> kuwa kwenu marekani au kwingineko kusiwafanye muwe mnajua sana Intellectual Property Laws nyie wenyewe,nyumba nzuri nyie wenyewe,muziki mnaujua nyinyi,nguo nzuri mnazijua nyinyi.jamani acheni ubwege,jaribuni kuja na vitu constructive muda wote siyo kuponda hata msivyovijua.ingependeza kama mtu angetoa angalizo ili aweze kupata ufafanuzi kabla ya kurukia mada msizozijua! naamini michango yenu ya maana inahitajika kutokana na exposure mliyonayo lakini itolewe katika namna ambayo ni ya kujenga na siyo kuponda.

    Asanteni,Mzalendo(nyumbani ni nyumbani)

    ReplyDelete
  20. Mdau 2,

    Let me say it in English, the logo and show format is the same because the show is being done by the same production company that owns the rights.
    Since you are slow, is Kwanza Bottlers infringing on copywrites by producing the same coke as the US and using the logo? (Dumb Question, Yes!)
    Similar to what your comment is. The show rights globally are owned by Endamol. Same as Big Brother UK - Original and all spin-offs including Big Brother Africa.
    The logo is a key part of the show identity. By the way you all can google Idol Nigeria, it was shown on MNET last year.

    Regards,

    Mdau 1

    ReplyDelete
  21. Hata nyie wa Uk mnajidanganya, mwazilishi anaitwa Jon Endemol na sio Endamol kama mnavyoandika, Huyu Jamaa ni mdachi na ndio mwanzilishi wa kwanza wa big brother na Idol kule Uholanzi ndio Endemol akauza hati miliki kwenye dunia nzima hii, Endemol ni tajiri mkubwa kwenye show business kule Uholanzi.

    La pili nikwamba mbona dunia siku hizi imegeuka? wanaume wanasuka nywele na wanawake wananyoa vipara.

    Nakaaya na Banana imekuaje?

    ReplyDelete
  22. mimi naomaba contact za lucy unajua ni mkubwa lakini bado yumo.Ni mrembo na anahadhi ya kimataifa

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...