MAREHEMU JOSEPH NATIANOTA (SHENGI)

Familia ya marehemu Joseph Natianota (Shengi) tunapenda kutoa shukrani zetu za dhati kwa ndugu, marafiki, majirani na watu wote kwa ujumla walioshiriki pamoja na sisi kwa njia moja au nyingine katika msiba wa kufiwa na mtoto wetu, kaka yetu na mjukuu wetu mpendwa aliyeaga dunia tarehe 14 Februari, 2008 katika hospitali ya Oxford Radecliffe iliyoko Uingereza na kuzikwa katika makaburi ya Kinondoni, Dar es Salaam, Tanzania tarehe 23 Februari, 2008.

Tunapenda kutoa shukrani za kipekee kwa makundi yafuatayo:-

§ Madaktari na wauguzi wote wa hospitali ya Wexham Park na Oxford Radecliffe zote za Uingereza kwa jitihada zao za kujaribu kuokoa maisha ya marehemu.

§ Jumuiya ya Watanzania wote walioko Uingereza na sehemu zingine za dunia waliojitolea kwa hali na mali hadi kuweza kuusafirisha mwili wa marehemu kutoka Uingereza hadi Tanzania kwa mazishi.

§ Ubalozi wa Tanzania na tawi la Chama cha Mapinduzi huko Uingereza walioshiriki kikamilifu katika msiba huu huko Uingereza.

§ Uongozi na waumini wa Kanisa la Christian Revival Centre lililopo Birmingham, Uingereza kwa ushirikiano wao.

§ Uongozi na wanafunzi wa Chuo cha London School of Commerce kwa ushirikiano wao mzuri.

§ Uongozi wa Waumini wa Kanisa la St Mary’s la Slough, Uingereza kwa kuendesha ibada ya kumuaga marehemu huko Uingereza.

§ Uongozi na waumini wa Kanisa la KKKT Usharika wa Msasani, Dar es Salaam kwa huduma za kiroho wakati wote wa msiba na katika mazishi ya marehemu.

§ Mtandao wa Issa Michuzi -Michuzi Blog- ambao ulitumika katika kusambaza taarifa za msiba sehemu mbali mbali.

§ Kampuni ya CORONA (T) LIMITED iliyoshughulikia kuusafirisha mwili wa marehemu kutoka London hadi Dar es Salaam na hadi kuuzika Kinondoni.

Tungependa sana kuwashukuru kila mmoja wenu kwa majina yenu lakini kwa ajili ya wingi wenu tunawaomba mpokee shukrani hizi kwa ujumla wenu.

Mwenyezi Mungu awaongezee baraka zake ninyi wote.

HERI WENYE REHEMA : MAANA HAO WATAPATA REHEMA (MAT. 5:7)

Familia itatoa sadaka ya kushukuru Utukufu wa Mungu katika Kanisa la KKKT, Usharika wa Msasani, Dar es Salaam katika ibada ya Jumapili ya saa 3:30 asubuhi tarehe 9 Machi, 2008.

WOTE MNAKARIBISHWA.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. so young,so promising,never knew you in person,but rest in peace buddy,will meet you in heaven,so long

    ReplyDelete
  2. ULALE SALAMA

    ReplyDelete
  3. Mungu Yesu alimuumba, na Mungu Yesu amemchukua. Jina la Mungu Yesu libarikiwe. Amen.
    mbarikiwa@gmail.com

    ReplyDelete
  4. Rest In Peace Shengi... R.I.P

    ReplyDelete
  5. rest in peace bro...asnath

    ReplyDelete
  6. Ulale salama Shengi. Umetungulia sisi tunafuata. Kazi ya mungu haina kipingamizi. Amen.

    ReplyDelete
  7. Kazi ya Mungu haina makosa.

    Mungu aiweke roho ya Marehemu mahali pema peponi. Amina
    -Robert B. Mujuni
    TBT

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...