Wito kwa wasanii kushiriki mwakani

12 - 17 February 2009
Wasanii mnakaribishwa kutuma nakala za rekodi zako za hivi karibuni, zitufikie kabla ya tarehe 31 Agosti 2008, kwa ajili ya tamasha la mwakani.
Zaidi ya vikundi mia mbili tayari vimekwisha shiriki katika matamasha yaliyopita ya Sauti za Busara baadhi yao ni Jose Chameleone, Juma Nature & Wanaume Family TMK, Saida Karoli, Didier Awadi & Phat 4, Eric Wainaina, Bassekou Kouyate & Ngoni ba, Seckou Keita Quartet, N’faly Kouyaté, Culture Musical Club, Chibite na wengineo wengi.
Jopo la uchaguzi litakutana mwanzoni mwa mwezi wa September kuchagua wasanii watakao shiriki tamasha la Sauti za Busara 2009.

Maombi yako yatashughulikiwa katika uchaguzi endapo tutapokea maombi kutoka kwako kabla ya mwisho wa mwezi wa august:
Form ya maombi iliyojazwa
Nakala moja au mbili za kazi zako (CD, DVD au MP3)
Unaweza kututumia maombi kwa njia ya barua pepe au kwa njia ya posta.

Tafadhali hakikisha kuwa umetuma maelezo mafupi ya kundi (yasiyozidi maneno 1000)
Unaweza kutuma nakala za kazi zako kwa njia ya barua pepe. LAKINI tafadhali usizidishe ukubwa ! Ukubwa wa kazi uliyoambatanisha uwe 5MB kwa barua pepe.
Pia unaweza kutuma nakala ya kazi zako katika ofisi zetu (tumia anuani hapo chini.)
Kwa wasanii watakao chaguliwa kushiriki katika tamasha au warsha, waandaaji wa tamasha watagharamia malipo kwa ajili ya onyesho wakiwa Zanzibar, ikiwa ni pamoja na usafiri, malazi, chakula na matumizi madogo madogo.


Kwa wasanii kutoka nje kawaida wanatakiwa kutafuta wadhamini kwa ajili ya gharama za usafiri.

Busara Promotions
PO Box 3635
Zanzibar
Tanzania
between Africa House and Serena, opposite Amore Mio.

Shanghani, Stone Town,

Zanzibar,

Tanzania

fomu zinapatikana kwa kubofya hapa

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Na sisi linitutakua wa kwanza.Ata ikiwa nchi ya kwanza kwa UJINGA

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...