Kaka michuzi,
pamoja na kuwa eneo la Tarakea, Rombo, liko mpakani mwa kenya na tanzania na shughuli za pale za kibiashara zimepunaka sana kwa hivi sasa, lakini bado kunatatizo la ukosefu wa sheli ambapo mafuta bado yanapimwa kwenye vidumu ambapo ukweli usalama wake unakuwa ni mdogo ukizingatia magari yapitayo au kwenda eneo hilo ni magari ya kusafiri mbali.
nafikiri kama kuna wadau wenye uwezo basi wawekeze pale soko liko wazi
mdau
charles salakana

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 18 mpaka sasa

  1. god point tunataka mambo kama hayo kuwezekeza wabeba mabox si mmeona hiyo dili kubwa lakini pale bado kuna wizi wa kupola na bunduki waizi sana lakini kama kuna mtu atakaye leta kuwe na ulinzi wa kamera securiteni safi,mtakula vumbi hadi makoo yaote funza wala vumbi nyie

    ReplyDelete
  2. Tatizo ni uhaba wa SHELI au vituo vya mafuta?

    ReplyDelete
  3. jamani Mramba,Massawe, Kimaryo, Mremi...angalieni hali ya ROMBO

    ReplyDelete
  4. Duh...hapo panafanana na armagedoni!!!mbona hapapendezi...utadhania'no man's land'...nilidhani TZ tambarare!!!

    ReplyDelete
  5. Mtakula vumbi hadi makoo yaote funza wala vumbi nyie!! Hivi wewe una akili timamu? ukisikia limbukeni ni wewe au unaona kuwa mamtoni ni dili kubwa sana? acha ushamba si ajabu kwenu kuna vumbi mpaka sandukuni

    ReplyDelete
  6. bwana mheshimiwa umeniacha hoi kidogo! lengo lako ni kampuni ya shell tu au lengo ni petrol station hata kama ni ya kampuni nyingine ya mafuta?naomba kueleweshwa! japo nadhani ulimaanisha kituo cha mafuta haijalishi ni cha kampuni gani!

    ReplyDelete
  7. Aisee Charles usiwadanganye watu...

    Kwanza hiyo sehemu hapo ni maili sita, kabla ya kuvuka mto kuingia Tarakea ambapo ni kama umbali wa mita mia mbili hivi.

    Lakini si unajua Tarakea kuna Sheli ya mafuta?? Tena kiko wazi muda wote??

    Tatizo sheli wanauza mafuta bei ghali, na hao jamaa wa vidumu wako very cheap. Mfano lita ya Diseli kwa Vidumu ni kama Shs 1200, while Sheli ni Shs 1400 au zaidi. Kwa hiyo mwenye kupenda gari lake aende sheli, anaependa hela yake ajaze kwenye vidumu. Mafuta yenyewe ni salama asilimia 100.
    Wadau kanunueni mafuta Rombo na sio kufungua sheli.

    ReplyDelete
  8. Tatizo hayo majizi yanayotoka hapo mpakani ndio hatari..vinginevyo warombo wasingekosa sheli..kwanza waanze kuthibiti wezi ndio mambo mengine yaingilie kati-

    ReplyDelete
  9. hivi hii kitu inaitwa SHELI au STESHENI YA MAFUTA? sheli ni jina la kampuni ambayo ilidominate petro station bongo enzi hizo ila sidhani hiyo ndo ifanye liwe jina rasmi la stesheni ya mafuta aka gas/petrol station.

    ReplyDelete
  10. Mwambie huyo Mchaga aache ushamba.
    Hizo haziitwi SHELI bora aite PETROL STESHEN au FYUEL STAION.
    Sheli ilikuwa ni mojawapo tu ya makampuni mengi yaliyokuwa na vituo vya mafuta.

    ReplyDelete
  11. Mimi niliishi hapo Tarakea, hakuna muwekezaji anayeweza ku-risk maisha yake. Majambazi wengi sana Tarakea..kawaelimishe ndugu zako kwanza waache ujambazi..Umemshinda hata mbunge maarufu Basil Mramba nani ataweza...ninyi endeleeni tu na vidumu vya mafuta maana wachagga mnapenda dezo sana..ndo maana ujambazi na wizi hamuachi..poleni...!! Wawekezaji msijidanganye mutauwawa na kupoteza pesa zote...wameshazoea hayo maisha hao Warombo...!!

    ReplyDelete
  12. mdau ulioleta hii post safi sana.nyie ndio mnaotakiwa kwenye jamii.majambazi hayawezi kukufanya mtu huogope kufanya biashara kama wewe kweli ni mfanya biashara.kama ujambazi mwingi na wewe jaribu kuweka ulinzi mkali kila kitu kinawezekana.na wadau mnaomshambulia kwa kutumia neno sheli wote ujumbe umewafikia na mmejua kaongelea nini kama hamna mawazo ya kuchangia just zip it.

    ReplyDelete
  13. Cha muhimu ni wewe kuelewa!!ummenda hapo ulaya kidogo tuu ukajua gas,vinginevyo ulikuwa hujui hata maana ya Gas...mie sio mshamba najua majina yote,nimeandika sheli ili watu wote waelewe sio wewew peke yako uliyeko ulaya..mdau Norway

    ReplyDelete
  14. yani lazima mlete ubishi hata kama mmeelewa lakini bado mnataka ligi tu kwani simeelewa sheli anamaanisha nini?

    ReplyDelete
  15. hey ...hiyo ni goodwill kama mlienda shule sana mnaelewa....mbona kila siku watu wakija dukani wanaomba colgate? inabidi waulize colgate gani?

    ndio goodwill hiyo basi kama competition ingekuwa kubwa basi wangepata biashara sana shell...watu wanaotafuta gas station wangekua kila siku wanaagiziwa kwao tu ....shell iko wapi...???? unaelezwa ...BP , exxon nazingine zote zinakua sio kitu tena

    kwa hiyo msimchambue sana mwenzenu...Yeye kawapa idea ya uwekezaji

    ReplyDelete
  16. na wewe fyuel staion ndio nini.....teh teh teh...toa borit na sio steshen au staion...ni station

    ReplyDelete
  17. We hujui kuna shell ya BP?

    ReplyDelete
  18. WIZARA YA AFYA NA MAMBO YA NDANI WANAFANYA NINI HII NI STAILI YA KUWAKANDAMIZA/KUUA WANAINCHI INAKUWAJE HAKUNA UTARATIBU... HAO VIONGOZI WANAFANYA NINI..WANAKULA NA NANI..SHERIA INARUHUSU MAFUTA KUUZWA NAMNA HII...ASALALA

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...