issa,
naomba usome hili tangazo la utallii kwenye gazeti la mirror jana . wenzetu wanakimbia wakati siye ndo kwanza twatambaa. hahahaa kumbe zanzibar iko kenya????? ilikuwa kwa kurasa mbili nzima za gazeti
DOS SANTOS

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 38 mpaka sasa

  1. watu wengine bwana! utadhani hawakuenda shule. tangazo la zenj iko kenya liko wapi! Jamani tuache uzushi.

    ReplyDelete
  2. kunradhi ndugu Dos Santos na kaka Michu, mbona sijaona sehemu yoyote ilipoandikwa kuwa Zanzibar iko kenya katika habari hii!?

    ReplyDelete
  3. Hakuna aliyesema Zanzibar iko kenya kwenye habari nzima - na sidhani kama kuna sheria iliyovunjwa cos if anything they're actually boosting our tourism industry by using Zanzibar to maximise their tourist's experience! So its all good - halafu sio kama waliingia bure - But good on you for being concerned - Mdau D!!!

    ReplyDelete
  4. Wee uliyeleta hii story hapa utakuwa mbumbumbu na kimombo hakipandi kabisa, hakuna mahali waliposema kwamba Zanzibar iko Kenya, sijui umetoa wapi huo uzushi.

    ReplyDelete
  5. Sasa ni wapi wamesema kwamba Zanzibar ni sehemu ya Kenya? Dunia hii kila mtu anajua kwamba Zanzibar ni sehemu ya Tanzania, itakuwa sembuse Waingereza waliowahi kuitawala East Africa. Kumbe vihiyo wengi sana hapa.

    ReplyDelete
  6. Mbona katika maelezo yote kwenye link uliyosema hakuna hata sentensi moja inayosema Zanzibar iko Kenya? Au mdau mleta habari kiingereza hakipandi nini? Pole sana Maimuna!

    ReplyDelete
  7. Issa Michuzi Waambie MP wa TAnzania wawe macho, Sie tunaisaidia Kenya matatizo yao kama u Africa mzuri, wao wanapitisha watu Mombasa mpaka Pemba na Pemba Mpaka Unguja Bila Haki Na Sheria inavyotakiwa wanachukuwa kidogodogo Bandari za Pemba ndio ilalamikiwe sana Bunge wanaionaje hii, kinachouma sana sie utalii tunasifia visiwa na mbuga wakati Lake victoria ukubwa iko kwetu Tanzania, Ila Kenya kisehemu kidogo wanaipamba kweli tunatambaa wao wanatembea.

    ReplyDelete
  8. Mbona sijaona mahala pameandikwa Zanzibar Iko Kenya? au kidhungu changu kimepauka?

    ReplyDelete
  9. Erooooooo! I'm back, after a week full of boxes to take care of.

    Labda kiswanglish yangu haiko sawa, mi sioni kama imeelesa sansibari iko kenya mi naona imeelesa stori nsuri na imeelesa namna ile wao mefanya kubuku safari yao.

    Kuna kitu kimoja wengi wetu hatujafahamu. zaidi ya nusu ya watalii wanaokuja Tanzania wanatoka kwa travel agents wa Kenya na south Africa, mtalii anapofanya booking anaomba kutembelea sehemu ambazo anazipenda yeye, sasa travel agent hawezi kukataa kuuza safari coz yeye yuko kenya au aanze kueleza kuwa zanzibar ni tanzania sio kenya. Guide atakae wapokea hao watalii ndio atawapa historia ya zanzibar. Mi naona hiyo article haina makosa labda kama sijaielewa.

    ReplyDelete
  10. Zanzibar na mlima kilimanjaro viko kenya, hamkuwa na habari ?

    ReplyDelete
  11. Please read the article and understand it before you post things in public.....There is no where in the article that mentions Zanzibar to be in Kenya, besides the heading that bears a story of those people traveling in different destinations, including Zanzibar....BUT nowhere in the story that it indicate or imply that Zanzibar is in Kenya..

    ReplyDelete
  12. ebu misupu tuabarishe kuhusu twiga stars ili watu tupumue bana, we vipi?

    ReplyDelete
  13. Haraka ya nini bwana,then acha umbea mambo mengine hayakuhusu!sisi turio karibu na zenji kazi tunaiona hao wakenya watawawezea wapi hao wa zenji wanajishaua tu!anyway may be suala la utalii lina kuumiza kichwa,mambo mzuri hayataki haraka babaaa!tukimaliza ya Richmond,Epa,Buzwagi then tutaanza kushughulikia masuala ya kimaendeleo nadhani agenda ya utalii na Advertisement,Promotion,na Locco Community develepment management Planning itafuata.pole kwa kuku diss

    ReplyDelete
  14. WADWANZI HAWA WALIOANDIKA HII ARTICAL,ANYWAY UKISHANGAA YA MUSA NA FIRAUNI JE!!!!!!!!!!, WENZETU WATANI WA JADI HUSEMA KILIMANJARO IKO KWAO PIA NIMEKUWA NIKIONGEA NA WASCOTISH WENGI TU HAPA NILIPO WENGI WAO WATAKWAMBIA WANA BOOK SAFARI KWENDA KENYA KUUPANDA MLIMA MREFU KULIKO YOTE AFRICA...........MHN HAHAHAHAA

    ReplyDelete
  15. I went through the article in the linked posted,there is no any direct claim that Zanzibar is in Kenya from the narrator,rather explaining that their trip started from Kenya(Masai Mara et)to Zanzibar.So lets not bring controvesy and contradictions,and cncentrate in improving tourism,advertisement and means of attraction.Kenya is far ahead is true,and thats why they even get the compliments of Mt Kilimanjaro,while its in Tz.

    ReplyDelete
  16. Hiyo ni sawa na sisi Watanzania kujifanya wamarekani kwa sababu tu ya hali halisi ya kule kwahiyo wakenya wameona nawao wajizidishie umaarufu kwa kujipa eti zanzibar ipo kenya Good luck 2them

    ReplyDelete
  17. NIMESOMA, SIO TANGAZO NI ARTICLE. PILI, HAJASEMA ZANZIBAR IKO KENYA, AMESEMA WALIKUWA KENYA NA ZANZIBAR PIA!

    ReplyDelete
  18. Ama kweli lugha ya watu ni lugha ya watu na tuwaachie wenyewe. Wewe umesoma ukaona wamesema Zenj iko Kenya hapo? Dah.

    ReplyDelete
  19. AMAKWELI LUGHA YA WATU NI SAWA NA TRAY LA MAYAI. KULIBEBA BILA KUYAVUNJA NALO LINAHITAJI UZOEFU..HAPO NI WAPI PAMESEMA ZENJI IKO KWA KENYA. HIYO MITU NAPOST HI HABARI APANA KUJUA MSURI KISUNGU. SISI NATAKA IGA KENYA NAFANYA NAMNA GANI KUPLOMOT TUALISIM..APANA KUJA NA MNENO MNENO MINGI BILA KUA YA MSINGI.

    JADUONG

    ReplyDelete
  20. Mbona kazi nimesoma yote story nione wapi kumeonyesha Zanzibar ipo Kenya wala sikuona....
    Unaadvertise au uko serious with your story?

    ReplyDelete
  21. Jamani nyie mnaolalama eti hakuna mahali paliposemwa Zanzibar iko Kenya msiwe mazuzu, alichomaanisha huyu Mtanzania mwenzetu ni implication inayozaliwa na hii habari nzima. Heading yake inasema walikwenda Kenya, halafu wakala maraha Masai Mara, Mfangano na Zanzibar. Hebu jiulize ni kitu kitakachomsaidia Mwingireza au Mmarekani asiyejua kuwa Zanzibar iko Tanzania kufahamu kuwa hiyo si sehemu ya Kenya, huku heading ikisema walikwenda Kenya? Nimeshangaa kuona yaani kundi lote hili na Watanzania limeshindwa kuelewa hii habari? Yaani ina maana Watanzania tuna understanding ndogo hivi? Ngoja nitoe mfano, nikiandika habari kwamba nilikwenda Mbeya nikatembelea Tunduma na Nakonde, kwa asiyejua kuwa Nakonde ni upande wa Zambia atapata ujumbe gani hapa? Au nikikwambia kuwa nilikwenda Marekani nikatembelea New Calton, Salisbury na Saint Catherine, nani anaweza kuniambia ipi kati ya hizi ipo Canada kama hajawahi kutembelea Niagara Falls? Tuacheni upuuzi Watanzania, tutaishia kupigwa bao kila siku. Angalie Wazungu siyo tu wanafikiri kwamba Mlima Kilimanjaro uko Kenya, wanadhani pia Ziwa Victoria liko Kenya tu, Serengeti iko Kenya na Tanzanite inachimbwa Kenya. Tuamkeni jamani. Yaani bado siamini kwamba watu wote hawa hawaoni athari ya hii habari, this is another shame after EPA and Richmond.

    ReplyDelete
  22. we anony wa March 10, 12:53 acha kutetea upuuzi. Hakuna kitu chochote kilichokuwa implied, unless uwe mbumbumbu wa kutupwa. Wewe na huyo aliyeleta habari wote lugha ya malkia inawapiga chenga ndio maana mnaanza kudandia stori.

    ReplyDelete
  23. Yaani huyu bwege aliookota hii news ni mbumbumbu mzungu wa nne. Ukiskia wapiga box ndio mmoja wapo huyu, maana kazi kukimbizana na mabox tu hata lugha hajui zaidi ya protocol zinatotumika warehouse kwenye ma cage. Mabox yatakuuwa wee bwege, kwenye hiyo news wapi waliposema zenj ipo Kenya? Soma kitu uelewe we ngombe mzee usirukie mambo tu bila hata kujua kinachozungumzia.I hope next time utakuwa makini na unachotaka kukianika.

    Papadakis

    ReplyDelete
  24. Anon wa 12:53am umezungumza hata mimi niliona jinsi kichwa cha habari kinavyotangaza kuwa jamaa alikwenda Kenya na Zanzibar ni kweli mtu asiejua anaunganisha kuwa Zanzibar iko Kenya...na sie Watanzania hatujitangazi ipasavyo...juzi juzi tu niliona matangazo ya utalii Tanzania wakati wote huo tulikuwa wapi?? Good start anyway...

    ReplyDelete
  25. Brow Michu, Please please waeleze watu wa hii Blog wajifunze kutoa comment zao wenyewe na sio kuigana, Soma story nzima then toa comment yako

    Hapa hii story inajieleza wazi kuwa Kenya wanavutia soko lao la utalii na wanawaeleza wazi wazi kuwa wanapitia kenya ila hapo kua Sehemu wanaingia Mara na Zanzibar je huko ni Kenya? Na Mlitaka mchorewe ramani kuwa Hii ni kenya na hiki ni kijiji cha Zanzibar ili mmwelewe huyu mdau? Jamani Jamani tuache uelewa mdogo huyu mdau anaeleweka kabisa kama mtu umeisoma hii Story vyema ila kama hukusoma unawaiga ambao tayari wameshatoa comment's zao na wewe unatoa hapo Neno basi hutakaa umwelewe huyu Mdau.

    Hata yeye hakuwa na maana ya kuwa Kenya Zanzibar iko hapana yeye amezungumzia jinsi Kenya wanavyoweza kutunyonya kwa kuitumia pia sehemu ya Nchi yetu kujitangazia biashara yao.

    Watanzania/wanablog hii ya Bro Michu please tutachekwa kama mtu hutafikiria kuwa unafanya nini na unataka kusema nini unaanzika tu kwani umesoma ya kwanza na ya pili ukakuta imeandikwa . Numshukuru sana Anony March 10,2008 12:53>00AM EAT kwa kutoa ufafanuzi mzuri kwani huyu inaonyesha ameisoma vyema Story na ndio akatoa Comment yake. Asante sana either Auncle or Aunt.

    ReplyDelete
  26. wabongo wenzangu msiumie vichwa bure hata kama wazungu wakienda zanzibar kupitia kenya ni lazima watajua kuwa zanzibar sio kenya ni nchi nyingine kwani kuna sheria za uhamiaji ambazo watazipitia kabla hata ya kuona hiyo sehemu aliyozaliwa mercury'cha kufanya nyie wote wa ughahibuni;TANGAZENI NCHI YENU.

    ReplyDelete
  27. Nilidhani niko peke yangu. Asante sana mdau wa March 10, 12:53 kwa kuliona hili. Jamani, hakuna mahali popote katika story hiyo, sio tangazo, panapoonyesha kuwa Zanzibar iko Kenya LAKINI tuangalie
    implication ya story yenyewe. Mmarekani na Muingereza wa kawaida mbumbumbu kule kwao atakapoisoma story hiyo hataona sentensi yoyote inayomuambia kuwa muandishi wa story yenyewe baada ya kutoka Kenya
    aliingia nchini Tanzania na kuelekea Zanzibar!!! Atakachoona ni kuwa Zanzibar ni mlolongo wa maeneo ya Kenya ambayo muandishi husika aliyapitia!! Na ndio tours agent wao wengi wanavyofanya. kwenye package zao za tours za Kenya wanaichomeka Zanzibar. Ndio maana tunapigwa bao na majirani zetu kila siku!

    ReplyDelete
  28. Anono wa hapu juu ndie anaye elewa ENGLISH.

    Yaani na mimi nilishangaa kuona kuwa watu woote hapa hawa elewi kilicho elezwa.

    Hapo haiku maanisha kwamba mwandishi ali-mention kuwa Zanzinbar iko kenya ila ukisoma story nzima hutaona neno Tanzania.

    "HUWEZI KUSEMA ZANZIBAR BILA YA KUSEMA TANZANIA"

    ...hii inaonyesha jinsi gani mwandishi asivyo taka kukubali kuwa zanzibar iko Tanzania.

    You guys must learn to think outside the box

    ReplyDelete
  29. Kwanza kabisa nawaunga mkono wote walioona implication ya hii stori.

    Pili kikubwa sasa sio kubishana bali kuanza kuchapisha news articles kwenye website za vyombo vya habari vya Ulaya, Marekani na kwingineko tunakopata watalii.

    Watalii mara nyingi hutumia internet kupanga safari zao, kwa hiyo akifanya Google search inatakiwa imletee Tanzania na Zanzibar kama kitu kimoja, sio Kenya na Zanzibar.

    Kwa anony unayesema Mtalii akija Zanzibar atajua kuwa iko Tanzania ni kweli lakini ukumbuke kuwa pesa alilipa Kenya kwa hiyo akija huku tutapata kidogo sana kwa sababu hadeal na sisi moja kwa moja.

    We have to stop that.

    Ningependa kuona waandishi wa Tanzania wanaanza kutengeneza articles za kupromoti nchi na kuzisambaza kwenye article directories mbali mbali ulimwenguni ili kuposition Tanzania vizuri katika search engines kama Google.

    ReplyDelete
  30. SASA JAMANI MSILAUMIANE BURE KWA 'ZANZINAR' KUWA AU KUTOKUWA KENYA.

    ZANZIBAR HAIKO KENYA WALA HAIKO TANZANIA. ZANZIBAR IKO AFRIKA. MNAOSEMA ZANZIBAR IKO TANZANIA MNALAZIMISHA MUUNGANO. WAO WAZANZIBAR HAWATAKI. WA BARA MNAJIPENDEKEZA SANA. NDIO MAANA WAZANZIBAR WAKAWA NA RAIS. ULISHAONA WAPI NCHI MOJA INA MARAIS WAWILI, MMOJA NDIO MKUU NA MWINGINE SIJUI MAKAMU NK? HIZO NI SIASA ZA KIZUSHI TU.

    MKITAKA MFURAHISHWE BASI SEMENI ZANZIBAR IPO MKOA MNAYOTOKA ILI MWEZE KUFURAHI ZAIDI. SEMENI KWA MFANO ZANZIBAR IKO MKOA WA PWANI MRIDHIKE.

    MNAJADILI MATUKIO BADALA YA KUJADILI MAMBO MAKUBWA? NYIE VIPI? WASIOKUWA BUSY UTAWAONA TU. MMEZALIWA PWANI NINI? NDIO ZA WATU WA PWANI, KUCHEZA TU BAO, STORY, WAKIWA NDANI YA MSURI WAKISUBIRI TU MSOSI.

    TUBADILIKE....

    ReplyDelete
  31. Elimu kweli ni ufunguo wa maendeleo kuna mmoja wetu ametowa maelezo hapo juu kwa kusema ZANZIBAR haipo TANZANIA na wala haipo KENYA na ipo AFRIKA hii ni ukosefu wakutojuwa nini mana ya TANZANIA ningependa nimuelimishe KWA TAARIFA yako TANZANIA MAANA YAKE NI MUNGANO WA NCHI MBILI ZANZIBAR NA TANGANYIKA NA NDIO IKAZALIWA HII INAYOITWA UNITED REPUBLIC OF TANZANIA, INAMAANA HAKUNA TANZANIA BILA KUTOKUWEPO TANGANYIKA AU KUTOKUWEPO ZANZIBAR .NI VIZURI ZAIDI UNGESEMA ZANZIBAR HAIPO TANGANYIKA INGELETA , KULIKO ULIVYOILETA HIYO MADA (USISAHAU BILA YA HIZO NCHI MBILIHAKUNA KITU TANZANIA) PIA NAKUOMBA WAJUILISHE WWAKE WALIOKUWA BADO HAWAJUWI NINI MAANA HASA YA TANZANIA .HUKU NDIKO KUELIMISHANA NA TUSI WENYE KUPOTOSHA UKWELI

    ReplyDelete
  32. Elimu kweli ni ufunguo wa maendeleo kuna mmoja wetu ametowa maelezo hapo juu kwa kusema ZANZIBAR haipo TANZANIA na wala haipo KENYA na ipo AFRIKA hii ni ukosefu wakutojuwa nini mana ya TANZANIA ningependa nimuelimishe KWA TAARIFA yako TANZANIA MAANA YAKE NI MUNGANO WA NCHI MBILI ZANZIBAR NA TANGANYIKA NA NDIO IKAZALIWA HII INAYOITWA UNITED REPUBLIC OF TANZANIA, INAMAANA HAKUNA TANZANIA BILA KUTOKUWEPO TANGANYIKA AU KUTOKUWEPO ZANZIBAR .NI VIZURI ZAIDI UNGESEMA ZANZIBAR HAIPO TANGANYIKA INGELETA , KULIKO ULIVYOILETA HIYO MADA (USISAHAU BILA YA HIZO NCHI MBILIHAKUNA KITU TANZANIA) PIA NAKUOMBA WAJUILISHE WWAKE WALIOKUWA BADO HAWAJUWI NINI MAANA HASA YA TANZANIA .HUKU NDIKO KUELIMISHANA NA TUSI WENYE KUPOTOSHA UKWELI

    ReplyDelete
  33. Qn: If I visited the UK, and decided during the trip that I had the time and money to visit Paris. If I wrote an article about it and told stories about the wondeful places I saw in England, Scotland, etc. and Paris (without explicitly mentioning France in there).
    Does that imply Paris is in the UK?

    ReplyDelete
  34. TUNAOMBA MAANA KAMILI YA TANZANIA WENGI WETU HATUJUWI MAANA YAKE TUNAAMBIWA TU KUWA HII NCHI INAITWA TANZANIA NINI HASA MAANA YAKE AU KIREFU TUSAIDIE SISI WENGINE NI VICHWA MAJI NA UBONGO NI SHELISHELI

    ReplyDelete
  35. Jamani Someni Vizuri. wamesema Week ya Pili ndio kaenda Zanzibar na vipi kafika Zanzibar? Wameonesha hiyo ni Travel Agency tu wenyewe Wanamalizana ushuru na Tanzania Pengine naukitizama Kuhusu Zanzibar na Hiyo Hotel Wameweka Website yao Ambayo wakiingia wanajuwa kabisa kama Zanzibar Iko wapi. hiyo chini.

    Breezes Beach, Zanzibar (www.breezes-zanzibar.com)

    Kilimanjaro wanaosema Kenya wanatangazia Kilimanjaro yao wanapoteza mda wao hata wakitangazia basi ni nje ya Border yao Kusema Mlima Kilimanjaro ule wetu. Kuupanda hawatoweza mpaka wawe ndani ya Tanzania na kileleni juu kabisak ule kuna Bango kubwa la UHURU Tanzania. Someni jamani mjue utalii wenu. na wewe unayesema zanzibar nchi tumia basi Passport ya zanzibar kusafiria tuone kama unaweza Zanzibar ni Tanzania upende usipende wacha wacheze bao ndio washakupiga bao la uso. kula urojo tu. Soma huko wacha kumalizia la saba. hami jay.

    ReplyDelete
  36. Hangalia sasa mnajump tu kwenye comment kabla ya kusoma article critically na kuona impact yake kwenu watu wa kuropoka bwana mnapiga debe nini. IoI Yaani aibu mnafikiri Dos Santos alikurupuka tu na kuleta hapo hii article kuna kitu kinaitwa critical review kwa wale wasiokimbia umande wanajua nini naongea ndio jamaa ameangalia hapo kwa hiyo article sasa nyie la la la utafikiri wapiga debe joto likizidi nalo lina mambo yake kumbe eh!
    am outta
    Londoner

    ReplyDelete
  37. WEWE ULIYESEMA TANZANIA NI MUUNGANO WA TANGANYIKA NA ZANZIBAR, HUJUI KWANINI MIMI NIME-REFUTE STATEMENT YA KUWA ZANZIBAR HAIPO TANZANIA WALA KENYA. NIMEANDIKA HIVO KUDISCOURAGE DISCUSSION AMBAYO HAILETI MAANA "KWANGU MIMI" KUWA IPO KENYA AU IPO TANZANIA. IT MAKES NO SENSE. MAANA WHETHER IPO KENYA AU IPO TANZANIA, PHILOSOPHICALLY, IT DOESN'T MAKE CHANGE OF IT'S PHYSICAL PRESENCE WHERE IT IS. ISSUE YAGU ILIKUWA NI KUWA KWANINI MJADILI KWA MSULI KABISA KITU KIDOGO KAMA HICHO KIPO TZ NA SI KENYA. HIVI MJINGA AKISEMA DSM HAIPO MASHARIKI MWA TANZANIA, WAKATI NI OBVIOUS IPO HUKO, UNAJADILI NAYE MTU KAMA HUYO? WALA HUKUNIELEWA NILIKUWA NA MAANA GANI KATIKA KUANDIKA VILE. MIMI NAFUNDISHA DEVELOPMENT STUDIES, NA HICHO NI KIPENGELE KIDOGO SANA KATIKA MADA NINACHOFUNDISHA PIA. NAJUA FIKA ZANZIBAR IPO TZ. BUT WAS ESCAPING TO ANSWER SILLY QUESTIONS LIKE "IS THE POPE CATHOLIC?"

    NGOJA NIKUAMBIE SASA:
    TANGANYIKA + (UNGUJA NA PEMBA) = TANZANIA.

    TENA ILIFANYIKA KWA NYERERE NA ABEID KARUME WALIPOCHANGANYA UDONGO WA PANDE MBILI NA KUKUBALIANA KUUNGANA KAMA ISHARA YA MSHIKAMANO NA UMOJA WA KUDUMU.

    HATA WAALIMU WALIOKUFUNDISHA WEWE BADO HAWAJUI WANACHOKISEMA MARA NYINGI. MASWALI HATA SASA HIVI YA SEKONDARI YANASEMA HIVI: "Tanzania ilipata uhuru lini?" WAKATI TANZANIA HAIJAWAHI KUWA KOLONI, ISIPOKUWA TANGANYIKA NDIO ILIKUWA KOLONI LA MJERUMANI KWANZA, NA BAADAYE CHINI YA UINGEREZA, ALIYETAWALA KUPITIA MGONGO WA NYUMA NA ZANZIBAR PIA, ILIYOKUWA CHINI YA MWARABU. TANZANIA HAIWEZI KUWA KOLONI SABABU NI MUUNGANO 26 APRILI, 1964 ILIPOZALIWA KWA KUUNGANISHA PANDE MBILI ZILIZOKUWA HURU TAYARI.

    ANY OTHER QUESTION? NARUDIA TENA, JADILINI ISSUES, SIYO OH, ZANZIBAR IKO TANZANIA. ZANZIBAR HAIWEZI KUWA TANZANIA SABABU NI TANZANIA PIA. THE NAME TANZANIA, UNFORTUNATELY IS ABSTRACT AND CONFUSING. THERE'S NO PLACE THAT YOU CAN SHOW ME THIS IS TANZANIA, BUT THE WHOLE LAND. PIA NENO TANGANYIKA WAMELIUA WAKATI NDIO JINA LA TANZANIA BARA. TANZANIA BARA NI JINA JIPYA. JINA LAKE HALISI LIKO WAPI? KWA HIYO UNAKUTA "TANGANYIKA NDIO TANZANIA KIMSINGI, ILA WAZANZIBARI WAMEIMBISHWA WIMBO KUJIONA WAO NI WATANZANIA WAKATI WAO NI WAZANZIBAR. NA NYIE WABARA MSIO NA JINA NDIO WATANZANIA. NIAMBIENI, MTU WA BARA BESIDES TANGANYIKA UNAJIITAJE? MWENZIO NI MZANZIBARI.


    POLENI......FALSAFA......NA WATU ORDINARY HAWATAELEWA KITU....

    ReplyDelete
  38. Wakenya ndivyo walivyo! kama wamarekani wakiona kitu kizuri basi ni cha kwao. Sio lazima waseme waziwazi kuwa Zanzibar iko Kenya. Wao kuitamka Zanzibar tu katika Kenya yao ni CODE WORD tosha kabisa. Lakini tatizo ni watz wana akili ndogo sana eti oh hawajasema kuwa Zanzibar iko Kenya! Try to read between the lines sometimes!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...