Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 27 mpaka sasa

  1. Hi Mzee Michuzi, hongera sana kwa blog yako hii si mchezo naifagilia sana, picha ya Shule ya msingi Kiezya huko Kigoma imenikumbusha mbali sana, asante

    Mdau JK

    ReplyDelete
  2. Kama ningekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania basi ningeamua na kuagiza shule na hospitali zote zilizokuwa zikiendeshwa na Misheni zirudishwe kwa wenyewe. Maana ni dhahiri kwamba serikali imeshindwa kuziendeleza katika hadhi inayotakiwa.

    Imani.

    ReplyDelete
  3. mheshimiwa Muhonga Ruhwanya amesoma hapo.

    ReplyDelete
  4. vaileth mzindakaya amesoma kiezya hii shule ilikuwa ya watoto wa wakubwa (asilimia 70 ya wanafunzi) enzi hizo siku hizi naona ni twende kazini imepoteza ubora.

    ReplyDelete
  5. doh! hiyo shule inanikumbusha enzi za utoto nilipokua kigoma,tulikua tunakwenda kula maembe maana kulikua na miembe mingi,siju mpaka leo kama bado ipo.

    ReplyDelete
  6. sasa michuzi unatudanganya, wewe upo ujerumani, hii shule umeipigaje picha!! tena fanya umaliza ka likizo, sababu tunakumiss sana vituz vyako, blog inakuwa frozen for long!! halafu sio kutembelea ujerumani tu kila likizo, hata hapa austria kuna watanzania, czech na slovakia vile vile.

    ReplyDelete
  7. Asante Michuzi. hii picha imenikumbusha miaka yangu ya ajira pale kigoma 1978/84. hapo mbele ni kanisa la Roman. Chini yake kuna shule ya Msingi Kigoma na ukishuka chini zaidi ni Railway Station na ofisi ya mkuu wa Wilaya (Bomani) nilipokuwa nikidunda mzigo!

    ReplyDelete
  8. Kwa kweli bwana Misupu, wewe huna mpinzani. Big up Michuz. Siamini macho yangu maana kaw kuiona hiyo shule nimekumbuka mbali sana, kuna jamaa zangu tulisoma nao mwaka 1979/80 wakati mhe Makamba akiwa mkuu wa wilaya, Keenja alikuwa RDD, Mwambulukutu nadhani alikuwa ndiye Mkuu wa mkoa, mimi nilikuwa mtoto wa mkulima tu enzi hizo, Namkumbuka sana Mzee Nombo jirani yetu kwa samaki aliokuwa akituletea, nakumbuka mambo kibao, kwa kweli Michuzi kazi yako ni bomba sana. Nikikumbuka embe nilizokuwa nikichucha, maeneo ya kuzuguka shule na lile kanisa kubwa, sijui kama ile miembe bado ipo jamani. Michuzi udumu.

    ReplyDelete
  9. kwa kweli hii shule imenikumbusha mbali hata mimi, nilisoma hapo na nikamaliza mwaka 199, mwl mkuu alikuwa Mr Kalumbilo, na walimu wengine kama, kuzenza, Kantuka nk nadhani mliosoma muda huo mnakumbuka vizuri, na hilo linaloonekana kwa mbali ni kanisa kotoliki.
    Big up blog ya michuzi

    ReplyDelete
  10. Hapa ndipo alisoma ALIKIBA?

    ReplyDelete
  11. Hii shule umenikumbusha mbali, nimefurahi mno, maana enzi hizo kina Vai Mzindakaya, Vicky Mzindakaya, Nelly Nsolezi, Consolata Deus, Ben Kaminyoge, bila kuwasahau Headmaster Kalumbilo, Kina Doto na Kulwa Kalumbilo, na wengine wengi ambao sijawataja majina. Shule hii imesoma watoto wa wakubwa wengi mno na watu mbalimbali ambao sasa wameshikilia nyadhifa mbalimbali Serikalini na kwenye Mashirika binafsi.

    Nawapa BIG UP!!!!!!! wote waliombaliza STD 7 mwaka 1988. Nawakumbuka sana. Mimi ni D.K. Mpatwa.

    ReplyDelete
  12. NJE YA MADA, michuzi weka habari hii ya Ndugu yetu Hasheem
    http://www.courant.com/sports/college/husky/men/hc-beawards0312.artmar12,0,7501278.story

    ReplyDelete
  13. Mdau anony... namba 2 nakuunga mkono kwamba ungekuwa president ungeagiza shule ma hospitali zilizokuwa za misheni zirudishwe lakini kumbuka serikali ya sasa ni kichwa ngumu huwa inakula bati hata kama inaona kitu kinaharibika, na ni serikali isiyojali.
    Elimu imeshuka wao kimya.walizichukuz shule na hospitali , wanashindwa kuziendela , sasa ni heri wawarudushie tu.
    Asante.

    ReplyDelete
  14. Nakuunga mkono wewe uliyesema kuwa michuzi awe anatembea nchi nyingi na siyo ujerumani tuu, mimi namshauri aende pia baghdad iraq atuletee mambo ya kule. Kenge

    ReplyDelete
  15. Naomba nipingane na wadau wanaosema shule zirudishwe kwa misheni. Misheni kwanza ni kina nani? hivi nyinyi hamjui kwamba ndiyo akina mtikila mnaotanguliza udini? Kwa nini msihamasishe watu wachangie maendeleo ya elimu ili iboreke na watu wengi wapate elimu bora badala yake mnataka shule ziwe za wachache? Misheni hela wanapata wapi kama siyo sadaka kubwa kubwa zinazotolewa na mafifisadi au michango kutoka kwa mashoga. Hivi hamjui kwamba wanaopeleka watoto wao kwenda kusoma shule za misheni ni watu wenye vipato vikubwa na siyo watanzania walalahoi? kwa nini misheni isijenge shule mipya nyingi kama kweli wanataka kuwakomboa watu badala ya kulalimika ili wapewe shule walizonyang'anywa ambazo wala siyo nyingi? ACHENI UNAFKI, unaweza pia kutoa mchango wako katika shule ili iboreke kitaaluma badala ya kuwategemea misheni. Tusitegemee pesa za mashoga ili tupate maendeleo yetu

    ReplyDelete
  16. Michuzi,

    Naomba tu umuulize Mjengwa kuwa gazeti lao la kila Jumatano Mtandaoni la RAIA MWEMA liko wapi au limehungiwa nalo kama ilivyokuwa Jambo Forum?

    ReplyDelete
  17. Standard Seven class of 96. Michuzi wewe kiboko, mie nimesoma hapo mzee. Tulikuwa tunakimbiza Kigoma nzima kwa kufaulu and what not.

    Edward Senkondo, Ephraim Butati, Maftaha Seif, Jumanne Jamberi, just to name few folks tuliosoma nao.

    ReplyDelete
  18. Wewe D K Mpatwa (ulimaanisha Kyunyu Mpatwa?). Hata mimi nilikuwa kwenye hilo darasa. Kuna majina mengine umeyasahau kama: Joan Masanja, Juliana Masanja, Racheal Udoba, Evans Mwakulinga, Jenard Lazaro, Anna Manjale, n.k.

    D K Mpatwa, hebu nitumie namba yako ya simu na ikibidi tuwasiliane kupitia E-mail yangu: phillip_jr1973@yahoo.co.uk

    ReplyDelete
  19. Ahsante Michuzi kwa hii picha ya Kiezya.

    Mara ya mwisho niliiona hii shule ni mwaka 1977 wakati nilikuwa ninasoma shule iliyopo jirani ya Kigoma a.k.a Kigoma H H The Aga Khan.

    Ninakumbuka wakati ule kuliuwa na timu nzuri sana ya mpira wa miguu ikiongozwa na mchezaji wa zamani Thabit Mgunda na vijana wengine ambao majina yao nimeyasahau.

    Nakumbuka alikuwepo Mwalimu Mkuu akiitwa Segule, waalimu wengine mama Shindika, Lupembe nk.

    Wakati shule ya Aga Khan alikuwepo Mwalimu Mkuu Mama Shayo walimu wengine Moshi, mama Lyatuu, Ms Londa, 'Mjeshi' Basike, mama Hussein nk.

    Nakumbuka pale Aga Khan tulikuwa na wachezaji maarufu baadae kama Yusuf Abeid a.k.a. 'Y'. Huyu alikuja kutokea kuwa golikipa maarufu sana akichezea Pamba ya Mwanza na Taifa Stars. Nakumbuka Golikipa Mengi Amani naye alikuwa mzuri sana.

    Kumbukumbu nzuri sana.

    ReplyDelete
  20. Umenikumbusha mbali kweli. Nimemaliza Kigoma primary 97 lakini nilikuwa na washikaji kibao hapo kiezya....Steven Shekiondo, Maganga Malewa, Jane and Edina Bella mko wapi?

    ReplyDelete
  21. JAMANI MICHUZI BASI TUWEKEE NA SHULE YA MSINGI KIGOMA,MAANA PIA HAPO KULIKUWA KUNA TOTOZ SANA.

    ReplyDelete
  22. chonde chonde kamichu,tuwekee shule ya msing kigoma labda tutamwona cinderella ,du maskini Ali kiba,kwikwikwki

    ReplyDelete
  23. Sasa mbona umetuwekea picha kiduchu? Tunataka kuona picha kubwa bwana!

    ReplyDelete
  24. Haha kweli hii picha inanikumbusha mbali; mi nimesoma hapo class la 95; enzi hizo mwalimu mkuu alitoka Kalumbilo akaja mwingine nimemsahau jina alikuwa anafundisha English meno yake ya chini hayajawahi kuonekana; pia kulikuwa na mwalimu anavaa suti ya Bluu kila siku hajawahi kubadilisha alikua anafundisha sayansi kama amedata vile;
    tumesoma na kina Kokushubila Mkamdala; Mansoor; Maria Mgella; Teresia Magesa; Teopista Ruguye; Zainab Ruhwanya{Kadogoo} sijui amekua saivi??; Sylvia Kinyondo; Clara Ndunguru; Aisha Kabeza; Regina Kumba; Marehemu Munema; watoto wa wakuu wa mikoa wote ilikuwa lazima wasome hapo; Jamani tukumbukane kama kuna mtu kamaliza 95 anitumie mail at kiezya@hotmail.co.uk yaani hii nimeifungua special kwa ajili ya kuwasiliana na wenzangu wa 95 na watakao jisikia.
    Nawatakia kila la kheir!

    ReplyDelete
  25. Michuzi umenikumbusha mbali sana tena ni hivi karibuni nilikuwa nawaza sana hii shule.Nimesoma Kiezya na akina Vaileth Mzindakaya Victoria Mzindakaya,Zaituni Walele ,Kokutona Msika my best friend sijui kwa sasa yuko wapi.Nakumbuka na Zito Kabwe alikuwa shule fulani pale Kigoma.Faustine Mwanambili alikuwa timekeeper wetu,Deo Mwanambilimbi alikuwa mpiga ngoma wetu wa band ya shule akikosekana tu siku hiyo lazima utajua mapigo ya ngoma si mazuri.Kina Juliana Masanja .Recho Udoba,Magreth Mzindakaya,Grace Ezekiel,Diana Mpatwa,Lucy Mbano, yaani ni list ndefu sana chini wa Mwalim mkuu "Kalumbilo" na mkumbuka na mwalím Skazwe kwa viboko vya mathematics na mwalim Mazoko English yaani ni balaa tupu,Shule yetu pinzani ilikuwa The Aga Khan tukikutana kwenye mchaka mchaka ni balaa tupu KIEZYA yaani we acha tu,Mimi kwa sasa niko nchini AUSTRIA nafanya MSc hivyo naomba wadau mliosoma Kiezya 1986-92 tuwasiliane nina list ndefu ya majina ila kwa hao wachache niliowaaandika nadhani watanikumbuka ,Tulikuwa tuna kaa msajili wa majumba karibu na duka la urembo au wengine walipenda kumuuita dingi yangu mzee wa JUWATA maana ndo alikuwa akifanya kazi hapo.Tafadhari tuwasiline kwa atakayependa kwa email ifuatayo
    celina@uccmail.co.tz

    ReplyDelete
  26. hi michuzi yaani umenikumbusha mbali sana nilisoma hapo nilimaliza std 7 1988 pamoja na hao wote waliotajwa juu. the list is too long to name. nilienda kigoma sec 1989 lakini nilihama to korogwe girls nilipomalizia 0level zangu. nilikuwa namtafuta rafiki yangu mkubwa rehema m. ambaye tulimaliza naye std 7 tukawa naye kigoma sec uko wapi??? mawasiliano yalipotea watu kadhaa nilibahatika kuwaona waliniahidi kunipa no yako rachel.

    ReplyDelete
  27. Jaman mi nmechelewa sana kuiona hii lakin lazima niseme. Wap mwlm rwegoshora, mpamo meno yake ya juu hatukuwah kuyaona mpaka tunamaliza. Nmefurah sana. Enz hzo maandaz sh 5 na barafu za ukwaju.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...