Hatutangazi Utalii UK kwa matatizo ya Kenya
Na Mwandishi Maalum, London
SERIKALI ya Tanzania imesema haikufanya kampeni ya matangaza ya utalii nchini Uingeleza kwa sababu ya matatizo ya Kenya, bali ni mpango ambao ulikuwepo muda mrefu kabla ya matatizo hayo ya kisiasa yalityotokea nchini huko hali iliyofanya kupungua kwa idadi ya Watalii kwa nchi za Afrika Mashariki wanaotoka Ulaya.
Akizungumza katika uzinduzi kampeni kubwa ya matangazo ya Utalii hapa Uingereza juzi katika ubalozi wa Tanzania, Katibu Mkuu Wizara ya Malisili na Utalii,Bi Blandina Nyoni alisema Serikali ilishaweka bajeti yake ya matangazo tangu mwaka uliopita wa fedha na sasa kinachofanyika ni utekelezaji.
Bi Nyoni alisema awali Serikali ya Tanzania ilifanya kampeni kama hii kule Marekani mapema mwaka jana na kuzindua matangazo kwenye televisheni ya CNN, hivyo awamu iliyobaki ilikuwa ni Ulaya na kuichagua Uingeleza kwani ndiyo inayoongoza kuleta watalii wengi hadi sasa.
Katika uzinduzi huo uliohudhuliwa na vyombo mbalimbali vya habari duniani, wafanyabishara, wawekezaji na wadau mbalimbali wa sekta ya utalii,ulifuatia kukatwa kwa utepe wa basi moja lililokuwa nje ya ubalizi wa Tanzania kuashilia kuzinduliwa rasmi kwa kampeni hiyo.
Alisema hivi sasa Tanzania imeamua kujitangaza na kuvitangaza vivutio vyake katika kuhakikisha tunapata watalii wengi zaidi ili tuweze kuongeza pato la Taifa na haifanyi hivyo kwa matatizo ya Kenya, hali ambayo imeathili kwa kiasi fulani kupungua kwa watalii, lakini sasa hali imerudi kawaida.
“Kweli tunaishukuru sana kampuni ya Jambo Publication kwa kutufanyia kazi hii, kweli imefanyika kama sisi tulivyotaka na tuna imani hata huko siku za baadae tutaendelea kufanya nao kazi, kwani wana uchungu na nchi yao na pia wanaijua vilivyo,” alisema Bi Blandina.
Alisema Serikali inakusudia kuongeza matangazo zaidi ya utalii kwa Uingereza kwa sababu imekuwa ikichangia sehemu kubwa ya pato la Taifa kutokana na watalii wengi wanaongia nchini, hali inayofanya idadi yao kuongezeka mwaka hadi mwaka.
Bi Nyoni alikitoa tathmini ya watalii wa Uingeleza wanaotembelea Tanzania alisema mwaka 1997 walifika watalii 25,000 hadi 2006 walifika 69,160 na mwaka 2007 idadi hiyo iliongezeka.
Tanzania imeweka matangazo 100 kwenye mabasi ya London na matangazo manne katika uwanja wa ndege wa Heathrow.Matangazo hayo yameratibiwa na kampuni ya Kitanzania ya Jambo Publication chini ya Mkurugenzi wake, Bw. Juma Pinto.
“Tutashilikiana na balozi zetu kuhakikisha tunafanya juhudi kubwa za kuhakikisha tunafanikiwa katika kuutangaza utalii na kuna mikakati mingi tumeifanya na sasa ni utekelezaji wake unaendelea,” alisema Blandina Nyoni.
Alisema wameamua kuanzia matangazo yao kwa nchi za Ulaya hapa Uingeleza kwa sababu ndiyo sehemu muhimu hapa Ulaya, kwani ndiyo nchi ambayo inapokea wageni wengi kuliko nchi nyingine yoyote hapa Ulaya, hivyo kujitangaza hapa ni sawa na kujitangaza duniani.
Awali Balozi wa Tanzania Uingeleza, Mwanaidi Senare Maajar alisema tayari ubalizo wake umekuwa ukifanya kazi kwa karibu na wizara ya utalii tangu mwaka jana na hivi sasa wao mbioni kutafuta wafanyakazi watakaofanya kazi katika sekta ya utalii hapa ubalozini.
Balozi Maajar alisema Uingeleza ni ufunguo muhimu katika sekta ya utalii wa Tanzania, hivyo wameweka mikakati mikubwa ya kufanyia kazi soko la utalii ili kuongeza idadi ya watalii na pia lengo la pili ni kuitangaza Tanzania.
“Tanzania tuna vivutio vingi sana ambavyo vinahitajika kutangazwa,na haya yaliyotangazwa katika matangazo ya sasa ni vichache tu katia ya vivutio vingi,serikali yetu inafuata misingi ya demokrasia na hata hali ya kisiasa ni nzuri na wananchi wake wana upendo mkubwa sana,” alisema Balozi Maajar.
Tangazo zuri na fahari kuitangaza Tanganyika. Lakini naona ni bora wasitumie neno Tanzania kama wanataka kuitangaza Tanganyika peke yake. Naona katika hizi picha sikuona kivutio chochote cha Zanzibar.
ReplyDeleteNasikia huko Marekani kunatangazwa Tanzania katika CCN na Zanzibar inatajwa. Sasa huko London naona Tanzania inatangazwa bila ya Zanzibar. Vyereje?
Mdau
Zenji.
Yakhe Michuzi,mbona unayabana maoni yetu...ukweli kweli unachoma!!!
ReplyDeleteHongera sana Mama Blandina Nyoni kwa kazi nzuri. Mama Maajar you look very good. Keep it up! We are proud of you both.
ReplyDeleteNYI VIPI? MNATANGAZA UTALII KWA KULA JUISI NA SAMBUSA, KWANINI HAMKUBEBA ULANZI NA MATOBOLWA, PIA PROUNZI WA NCHI KAVU ( SENENE ), WANGEKUWA KIVUTIO AU MLIONA AIBU KUWA NI VYA KISHAMBA? NUJUA MAVAZI SI KOSA LENU KWANI HATUNA MAVAZI YA ASILI ZAIDI LA KIMASAI.
ReplyDeleteWe Anonymous ulishaambiwa na mwalimu nanii kwamba kufikiria Tanganyika na Zanzibar ni 'primitive nonsense'cha kufanya ungewashauri wizara ya utalii moja moja udhaifu unaouona kwenye Tangazo,you have a point lakini ulivyoi-present sivyo.Hatutaki kusikia mambom ya Zanzb na Tangnyk.
ReplyDeleteWadau nadhani tusikae kuponda tuuu,nadhani serikali(Wizara) wamefanya jambo zuri kwa hili,offcourse walichelewa.Matangazo hayana uhusiano na kenya kwa sababu hivi vitu tunavyo kwenye ardhi yetu(wengine wanatangaza vitu ambavyo havipo kwenye ardhi zao!).
Ushauri kwa serikali:Matangazo ya biashara yaendane na uboreshaji wa infrastructures.Shirika letu la ndege liwe na midege ya kisasa kuwafuata wazungu huko kwao siyo kuletewa.Barabara kulelekea kwenye vivutio nyingi si mbaya sana lakini.Mfano Kutoka Mwanza kwenda Rubondo Island kupitia Geita,barabara ni'mbavu za mbwa'Asanteni
Congratulation on the efforts to advertise Tanzania.
ReplyDeleteLakini sasa the advert its self.
Why is Tanzania in small prints.
I went to the website (www.mnrt.go.tz) how is one to associate the website with Tanzania tourism ,and the website below standard, did you bother to visit the Tanzania Tourist Board website.
http://www.tanzaniatouristboard.com/
you could have learned a thing or 2
Have you been there? Where.
If you have been given the cash, please use it and put something that is going to be effective, use professionals.
There is a BIG room for improvement
Michuzi, nakumbuka niliwahi kuzungumzia udhaifu wa haya matangazo ya kuijenga Tanzania hapa Uingereza.
ReplyDeleteLakini kwa busara zako uliamua kufuta niliyoandika, sababu huenda nilisema ukweli, au nilichemka au uliona napiga majungu.Pamoja na yote, nilisema kwamba tusubiri tuone hayo matangazo yenyewe, na baada ya kuyaona, utakubaliana nami kwamba hayako professional.
Tatizo kubwa kuliko yote, matangazo hayana FOCUS.Kuweka picha za simba na twiga bila maelezo ni upuuzi - nchi ngapi zina simba tujiulize.Jamaa wameweka website ya wizara ya maliasili na utalii badala ya Tanzania Tourist Board.Watu hawapendi kuelezwa ukweli wa mambo, lakini hii pesa ni ya walipa kodi.
Hebu angalia hapa uone jinsi tulivyoandika, na Michuzi ukaondoa posts zenye kutoa ushauri wa kukosoa hitilafu.
Anon anayesema Zenji haikutangazwa na aangalie kwenye hilo basi kulia hapo kwenye mlima kilimanjaro kuna nembo ya jahazi rangi ya manjano, ni nembo ya Zanzibar.
ReplyDeleteKama unafuatilia vizuri hii blog ungeshaona yale matangazo ya mwanzo.
Chini ya matangazo kuna Land of Kilimanjaro and Zanzibar.
Nyie wa Zenji kwa kulalamika hamuishi, ngoja tumipe kanchi kenu tuondokane na kero zenu.
Mnaboa
Michuzi jamaa anahitaji miwani, muwekee ile picha ya mwanzo kabla hio kampeni haijazinduliwa
Kwanza hongera for the advertising ila key points MR. PINTO umekosea kwenye campaign ya matangazo
ReplyDelete1.Website iliyotangazwa kwenye basi ni ya wizara ya serikali. www.mnrt.go.tz.
Hamna MTALII atakae kuwa na interest na website ya wizara ya MADINI.
Chukua hela kidogo kama pound 50,000 tumia professionals wakutayarishie website recognised the world over ya kuvutia mtalii.
WTF, yaani yaani hapo UMECHEMSHA BIG TIME.
2. Linganisha promotion za mabasi ya nchi kama cyprus , south Africa, Greece... kuna jinsi ya kutangaza kwenye billboard unatumia slogan inayotambulika k.m "visit cyprus".
Ya tanzania sijaielewaelewa... "have you been there" again big time cock up.
3. The overall quality la tangazo ni mbaya , tangazo lipo TOO BUSY,
Mpita njia mpaka akae asome ndio ajue kinachoendela. Hamna mpita njia london mwenye nusu sekunde ya kusoma tangazo kama halivutii na kupa ujumbe instantly. Angalia campaign ya virgin atlantic service to Nairobi ilivyokuwa simple.
Simple solution ni kuwalipa agency ya matangazo wakutengenezee kitu cha nguvu again sio hela KIBAO ni kama pound 100,000.
Otherwise kwa laki 700,000 you can do beter.
Wadau mnaoishi UK ambao mko karibu au mmeshaona hayao matangazo,mnaweza kuwaulizia hao wainge"le"za,Kama message wanaipata kupitia hayo matangazo,kama message wanaipata basi,hakuna la kubishana hapa.Michuzi ngoja niangalie hii website aliyosema mdau nipate cheka kidogo
ReplyDeleteYes,nimerudi.Anachosema Anony 2:56:00P.M ni kweli.Tanzania tourist board wana website of high quality lakini www.mnrt.go.tz mmmmh.Sasi nani aliwambia watumie website ya kiwango cha chini,balozi naye akuangalia???
ReplyDeleteWAZANZIBARI KWA KULALAMIKA,NIMEWAVULIA KOFIA.
ReplyDeleteMimi nimefurahia hayo matangazo, hiyo ni hatua ya kwanza. Hatua ya pili iwe ni kuboresha miundombinu yetu (huduma za viwanja vya ndege(international na local), huduma za hoteli, mahotelia wetu bado uwezo wao wa kuhudumia wateja (customer service) upo katika kiwango cha chini sana, kuboresha barabara na vyombo vya usafiri. Pia utangazaji uwe wa kudumu - throught, non stop - kama biashara nyingine zinavyotangazwa duniani. Nina uhakika nchi inaweza kupata pato kubwa sana litokanalo na utalii endapo sekta hii itaangaliwa vizuri, na kama kutakuwa na financial investments ambazo zitaelekezwa huko kwa nguvu
ReplyDeleteNimesoma haraka haraka, lakini nakubaliana na baadhi ya watu waliosema kwamba matangazo lazima yawe na focus - au full informative. Kuwe na address za namna ya kupata information zaidi, kuwe na "approximate cost" za tour, kuwe na "trustworth, reliable, dedicated website yenye link na reputable banks(citibank Tanzania au Barclays Tanzania) itakayotoa information zote na kupokea malipo online kwa wale wanaotaka kulipia online
ReplyDeleteTutaomba kama Mheshimiwa Balozi UK adedicate muda kupitia hizi comments zote, kwa kuwa nyingi zipo constructive, na zifanyie kazi kwa kuwa-consult watalaamu katika nyanja husika (IT, Designers na Financial Institutions) tuweze kusonga mbele kwenye issue ya utalii ambayo ni muhimu sana, na ambayo inaweza kutunyanyua sana kiuchumi
ReplyDeleteNdugu zetu wa Zenj, mambo yakiwa tambarare huwa hawisifii Tanganyika hata siku moja. Hamna jema...Soon mtapata uhuru mnaoulilia na lawama zitutoke wabara.
ReplyDeleteMpunguze kusononeka ndugu zangu, aliyetunyima sie ndie aliyewapa nyie
michuzi and mithupuzzz naomba kuuliza je kuna wahusika wowote wanaopitia hizi comments? kama hapana, Je kuna jitihada zozote za kuwafikishia hizi comments? mimi pia niliwahi kukutumia article kuhusu web ya atc na ya kenya airways uangalie tofauti na ukiuliza bei ya kutengeneza hizo web inaweza kuwa sawa
ReplyDeleteKwa aliyesema service standard iko chini hajatembea. angetembea kwanza then aseme
ReplyDeleteNiliyesema service standard ipo chini nimetembea sana, Tanzania, Africa Mashariki/Kusini, Asia, Europe, Marekani na hata sasa hivi nipo nabeba maboksi majuu. Kwa hiyo ninapozungumzia kiwango cha huduma nina uhakika na ninachokisema. Unaweza kumlipa mhudumu Tanzania, na ukakaa kusubiri chenji muda mrefu mpaka ukachukia, na wakati mwingine kama ni kiasi kidogo unaamua kukiachia na kuondoka. Wahudumu hawawezi kutoa huduma kwa haraka, huwa wanatoa huduma kwa kujivuta (speed of giving service is low). Communication skills za ma-operator wetu zipo katika kiwango cha chini, wakati mwingine wanashindwa ku-handle business/official conversations/kuweka appointments na huishia kukata simu. Uwezo wa kuelewa different accents ni mdogo. Hizi ni kasoro ambazo inabidi tuzikubali kwamba zipo tunazo. Ni tatizo letu, tusilikimbie. Tusikimbie ukweli, tutafute namna ya kulirekebisha hilo. Na hii inawezekana through training. Tu-train wahudumu wetu katika viwango vya juu ili tuweze kukuza soko la utalii
ReplyDeleteService standards kweli zipo chini, japo sio kwa kiasi cha kuleta malumbano MAKUBWA. What's important ni trainings; business and communication skills + ICT.
ReplyDeleteJamani, tujitahidi kuwekeza kwenye sekta ya utalii (na kwingine) ili kuleta ushindani utakaorekebisha matatizo yaliyopo. Kulumbana sawa, lakini vitendo muhimu. Walk the talk guys. Unaweza. Believe Begin Become!
SEV
mi nafikiri tunapozungumzia utalii bongo lazima tumzungumzie arusha, kwa anaesema wafanykazi hawana skills aende arusha aangalie hotel za kitalii na aseme ka service standard iko chini. hata mi nabeba box states na nimeshatembea ulaya, australia, asia nimeona vitu vingi ndio maana nasema service haiko chini kama unavyosema
ReplyDeleteNAKUBALIANA NA WAZO LA WADAU WENZANGU JUU YA KUUTANGAZA UTALII BADO UTALII NCHINI UNAHITAJI MATANGAZO NA PIA NGUVU NYINGI ZAIDI ZIONGEZWE KUWEZA KUPUNGUZA LANDING FEES ZA VIWANJA VYETU VYA KIMATAIFA LEO HII MTALII ANAPOTAKA KUJA TANZANIA YAANI NI RAHISI ZAIDI KUSHUKIA NAIROBI ANAOKOA DOLA 300 ANAPANDASHA SHUTTLE YA DOLA 15 ANAKUJA ARUSHA WIZARA HUSIKA INGALIANGALIA HILO, TUJE KWENYE SWALA LA GHARAMA ZA KUENDESHA KAMPUNI YA UTALII GHARAMA HIZO ZINGEPUNGUZWA ILI KILA MTANZANIA MZAWA AWEZE KWENDA KWENYE MAONYESHO YA UTALII SASA INAONEKANA MAONYESHO MNGI SANA YANAYOFANYIKA NJE YA NCHI NI MAKAMPUNI MACHACHE SANA YA WAZAWA YANASHIRIKI ZAIDI UNAKUTA NI MAKAMPUNI YA KIGENI AMBAZO KWA KWELI KAMPUNI HIZO NYINGI ZA KIGENI WANA AKAUNTI ZAO NCHINI MWAO NA PESA INAYOINGIA NCHINI NI KIDOGO SANA YA KUENDESHA TU KAZI ZAO.WAJITAHIDI SERIKALI KUWEKA TOFAUTI KUBWA BAINA YA MAKAMPUNI YA WAZAWA NA WAZUNGU ILI MTANZANIA AIFAIDI NCHI YAKE.
ReplyDeleteTUNAMUOMBA BALOZI AONGEZE BIDII PIA KWA NCHI ZA SOUTH AMERICA KWANI KWA HIVI SASA NI NCHI KAMA CHILE,PERU NA ARGENTINA SI WENGI WANAIUJUA TANZIA.
MDAU.
Wandugu. Nauliza Swali Juma Pinto na JK wakoje? Majibu!!!! Mie nakubaliana sana na hili swala la kuitangaza Nchi yetu lakini.... tumefanya research kabla ya kujitangaza? Watalii hawaji kwa wingi Tanzania kwa sababu zipi? Hili nimuhimu kwanza kabla ya kutupa mapesa yote kama yaliyotupwa. How can you pay £2500 for 2 weeks for holiday in Tanzania ikiwa unaweza kutumia £1000 kwenda Jamaica kwa wiki hizo hizo (Mfano)
ReplyDeleteYaani hapa wanapongeza wizara kwa hatua hii ndogo muhimu ni wachache sana. Watanzania tuweni na moyo wa kukosoa kwa kujenga, watu humu humu wanalaumu tuuuuu.
ReplyDeleteNdugu yangu mwingine hapo juu anafananisha holiday ya Jamaica na Tanzania..!! Wandugu tuwe makini kidogo, wahusika wanasoma haya maoni na wangependa kuyafanyia kazi.
Suala la kuitangaza nchi au bidhaa yoyote ni majaribio, hakuna fomula kama zilivyo fomula za hesabu. Tuwapeni maoni ya kujenga na sio kulaumu tuu.
Hayo ni maoni yangu.
Mi naona ni kama richmond tu kwasababu sijasikia tender kitangazwa wala wahusika sidhani kama wana uzoefu wa haya mambo.Watanzania tuwe macho ni vizuri kutangaza nchi yetu lakini ni kivipi?
ReplyDeletekazi ipo kweli kweli hapa nafikiri umefika mda sasa haya mambo ya ubabaishaji tuyaache jamani kwanza matngazo hayana quality au kitaalamu tunasema grabbing the attention kwa mdau au huyo mlengwa na huu mchezo wa kupeana peana kwa kitu kitogo sijui utaisha lini.
ReplyDeleteHuyu juma pinto tangu lini anajua matangazo so sioni ajabu ubabaishaji ukaandelea hizo picho kila mahali zipo tuwe na style ambayo inalipa sio copy and paste.Ni aibu kumuona mama balozi naye anshabikia ujinga ujinga huo wapo wataalamu jamani wa matangazo wapewe sio wababaishaji kama pinto wazo la kutangaza nchi sawa laikini liwe la kitaalamu na lenye plan nzuri.
Kaka hapo juu, nadhani kama alovyosema Lowassa wakati anajiuzuru tatizo siyo tangazo, tatizo ni JUMA PINTO kupewa hiyo kazi, lakini myonge mynonge haki yake mpeni jamaa amejitahidi sasa kama wewe mtaalam basi peleka idear zako serikalini.Akitangaza mzungu, mhindi tangazo litakuwa halina tofauti.Tangazo nasikia wameli signe TTB jamaa amepewa kazi ya kubandika tu.Huo ni vitu wa kitoto buni jambo lako na wew, watanzania tusiwe hodari wa ku- critisize, pia re- greate idear ambazo ni nzuri kwa faida ya Taifa.
ReplyDeleteOngereni pinto na team yako.Tunawasubiri Gemrany