hii kitu bado ipo kwa sana tu hapa bongo, na hamna noma wala nini. mie nnazo pea tatu...

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 17 mpaka sasa

  1. Michuzi ufisadi huanza hivyo hivyo pea tatu za nini? maana hizo katambuga hazitofautishwi kwa style kama nguo au viatu vya aina nyingine na kwa jinsi katambuga zinavyodumu ni sahihi kutumia ule msemo "alinunua babu na mjukuu anatumia"

    ReplyDelete
  2. Ebwana hiyo ndo bana matumizi haswa hii, manake MGUU NAKUFA KIATU NABAKI.......
    Zidumu katambuga...!!!!

    ReplyDelete
  3. HAYA MARAIYOO YAMETUTOA SANA MIAKA HIYO HASA ULEWAKATI AMBAO HUWEZI KUPATA RABA ZA ASANTE NYERERE KWAKUWA SIO ALAIKI.KIPINDIHICHO RABA IKIISHA JUU SOLI INACHUKULIWA INASHONESHWA MIKANDA YA TAIRI HILO INA KUWA MALAPA UNAANZA KUFLIP FLOP NAYO MTAANI. SOLI YA KIATU IKIISHA ILIKUWA INATUSONGESHA.LAKINI BADO NI MKOMBOZI YA WATU WENGI . HONGERA MKOMBOZI WETU. BADO WATANZANIA WENGI HATUWEZI KUMUDA GHARAMA YA MAKATAMBUGA HAYA TUTASAIDIANAJE TUMUDU MAMBO HAYA. WACHUMI JAMANI MSAADA.

    ReplyDelete
  4. Mungu nisamehee sio na kejeri sikujua kama hivi viatu bado vipo kwenye huu ulimwengu kweli.sasa kweli Tanzania bado ipo kwenye hali ya vita ya pili ya dunia du.ANON March 3, 2008 7:05:00 umenichekesha sana

    ReplyDelete
  5. Nyerere angekua hai,wote tungevaa mipira tairi hizo...na baada ya kuvaa siku nzima,jioni harufu hatari kwani hata ukisfisha miguu na chapa mbuni harufu mpaka wiki ijayo!!!

    ReplyDelete
  6. Hayo ni poa kwa kubana matumizi,Nitumie na mimi pea mbili

    ReplyDelete
  7. Haya ni mazuri sana tu. Kibaya ni sisi wenyewe hatujui kuwa creative. Tungeyauza mpaka soko la duni haya ila tu hatujajua cha kufanya yasiunguze miguu wakati wa jua. Jua la bongo utakuta mtu anashika viatu mkononi yuko radhi atembee pekupeku kwa vile hayo makatambuga sio raha tena yanakua tabu miguuni.

    Bongo hivi vitu kama bado vipo basi bongo tambarare saana tu

    ReplyDelete
  8. BONGO TAMBATAREEEEEE

    ReplyDelete
  9. anon wa mar 3, 8:03 na mar 4, 1:31
    yaelekea hii kitu munaifahamu vilivyo sana, ila kitu kimoja nawausia kuwa dau limewavusha sasa limekua gogo?. Poa tuu pamoja na yote bado bongo tambarare kwa sanaaaa.

    ReplyDelete
  10. viatu vinanikumbusha baba wa taifa, na sera zake za umasikini! baba wa taifa akirudi sasa hivi atashangaa kuona mafisadi wanavyotanua bila wasi wasi wala nini tena kwa kutumia madaraka waliyonayo! itabidi ahutubie kama siku mbili hivi
    kisha aombe kurudi alikotoka! kwa jinsi watu wasivyosikia na huo ufisadi

    ReplyDelete
  11. Michuzi tumekustukia! kumbe na wewe una tabia ya kujilimbikia mali kama mafisadi! Sasa pea tatu zote za nini? Tuna mpango wa kukuundia tume! Te te tehhh!

    ReplyDelete
  12. Hizo katambuga ndo vilikuwa viatu! Mtu anaenda kazini/ofisini na katambuga chini! Kabla mitumba/kafa Ulaya hazijaruhusiwa. Enzi za Mwalimu bwana! halafu mguu unakuwa mweusi!

    ReplyDelete
  13. mi namwonea huruma mchizi anayetengeneza anaonekana hajapata shawa siku kadhaa sio kwa kutaka bali hali ngumu ya maisha, bongo noma

    ReplyDelete
  14. Duh nayakumbuka maraiyoo sana.....
    Hayo ukivaa lazima utoke magamba (sagambazzzz). Sasa enzi hizo ukiwa na vile viatu vya plastiki au baadae raba za DH na njumu za maradona ambazo zishaanza kuisha baada ya kwendea church kwa miezi sita, inabidi uzipige kwa muda mguu ulainike tena na sagamba ziishe then ndo urudi kwenye araiyoo.
    Michuzi ungetuambia yanapatikana wapi maana nimeyamiss sana....

    ReplyDelete
  15. Kaka Michu!
    Kweli hii ndiyo wale wakerewe wanaita recyclingi. Ila sasa hii ni kali na inalewesha kaka, maana gari limeshindwa kutumia ambalo linavesha chuma halafu mwili wa binadanu unavaa. Kweli inabidi tuangaliye kama haiwezi kuleta madhara kwa matumizi ya binadamu. Ila bora hilo kuliko kuchomwa na msumari au mwiba ukafa na Tetanasi kaka. Ningeshauri jamaa awe na website ili tuwe tunatoa oda kupitiya mtandao kaka.
    Naomba kuwasilisha
    Mdau Mshongosho

    ReplyDelete
  16. Michu,haya madude bomba sana.Ukivaa kama vibaka wanakutafuta hawawezi jua umeelekea wapi,unaweza hata kumpoteza bosi kama umetoroka kazini,harafu hayaishi.Wahindi wanasema "iko isha miguu kiatu bado"
    Mdau,
    Mbeya.

    ReplyDelete
  17. Hizi mimi ninazo hapa marekani sama ikifika tambarare kwa sana na miguu yangu myeupe pye nawatia kizungu zungu tu wadau.Msikonde kwenu ni kwenu tu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...