

Ijumaa iliyopita kwenye ukumbi wa New World Cinema kulikuwa na tafrija ya uzinduzi wa tuzo za filamu Tanzania – Vinara Film Award.
Tuzo za Vinara wa Filamu ni tukio linaloletwa na kuratibiwa na One Game Promotions kwa ajili ya kuwapa tuzo wasanii na wadau wa sanaa waliofanikiwa kuinua filamu Tanzania.Tuzo hizi zimesajiliwa kisheria na kutolewa kibali na Baraza la Sanaa la Taifa Tanzania.
Utoaji tuzo za Vinara wa Filamu Tanzania, unalenga katika kuifanya sanaa ya Tanzania kupata nguvu mpya na kuwafanya watengenezaji na wadau sanaa kufanya bidii katika ushindani wa soko la sanaa na hivyo kutengeneza kazi zilizo bora zaidi zinazoweza kuuzika kimataifa ili kuiweka nchi yetu kwenye ramani ya dunia.
Tuzo za Vinara wa Filamu Tanzania pia zinalenga kuwafanya wananchi kuendelea kuwa na mwamko wa kupenda kazi zinazotengenezwa na Watanzania wenzao ili kupata mafunzo mbalimbali yatokanayo na kazi za wasanii na pia kukuza soko kwa faida ya pande zote mbili.
Pia zimelenga makundi mbalimbali ya wadau wa sekta ya filamu katika nyanja mbalimbali wanaojitahidi kuinua sanaa ya filamu nchini.Tunatumia nafasi katika uzinduzi rasmi wa tuzo hizi kutoa nafasi kwa wadau wote wa sanaa nchini na kuwatambulisha uwepo wa tuzo hizi ambazo ni kwa Tanzania nzima.
One Game Promotions itatoa matangazo kwenye vyombo vya habari kuwaalika watengenezaji wa filamu nchi nzima ili kuwatambulisha uwepo wa tuzo hizi na jinsi ya kushiriki na kuingiza kazi zao zitazowania tuzo hizi kuonwa na majaji.
Filamu zinazowajibika kwenye tuzo hizi ni filamu za hadithi (feature films) tu na zilizokakuguliwa na Bodi ya Ukaguzi wa Filamu Tanzania. Na ni zile tu ambazo zimetengenezwa katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Watanzania wenyewe au nje ya mipaka lakini watengenezaji wakiwa ni Watanzania.
Matangazo hayo yatatolewa kwenye magazeti yanayochapishwa kwa wiki na kila siku, redio na televisheni kwa muda wa mwezi mmoja na utekelezaji wake utakuwa ndani ya siku 21 tangu matangazo yatoke.
Fomu zitatolewa bure na zitapatikana katika ofisi za waandaaji wa tuzo.Katika fomu hizo, kutaainishwa mambo muhimu ambayo mtengenezaji wa filamu atapaswa kujaza.
Kama vile; Jina kamili la kampuni iliyotengeneza filamu au video na anwani kamili, Jina la Mtayarishaji Mkuu wa filamu (Executive Producer), Jina la Mtayarishaji wa filamu. (Producer), Jina la Mtunzi wa hadithi (Story Writer), Jina la Mwandishi wa skripti (Scriptwriter), Jina la Muongozaji (Director), Jina la Mhariri (Editor), Majina kamili ya wasanii wote waliyoigizia katika filamu husika (Characters), Jina la Muongozaji wa Taa (Lightsman), Jina la Mrekebishaji Sauti (Soundman), Jina la Mpiga Picha (Cameraman), Jina la Meneja wa Mandhari (Location Manager), Jina la Mpangiliaji wa Picha (Cinematographer), Jina la Mtunzi wa Muziki (Music Composer), Jina la Studio iliyofanya/zilizofanya kazi kwa filamu husika.Fomu itakuwa na maswali mengine kama vile; filamu imetengenezwa lini , mahali ilikotengenezwa, maudhui ya filamu na lugha iliyotumika.
Baada ya fomu hizo kujazwa kwa usahihi, zitatumwa kwenye ofisi za waandaji, kwa mkono au njia ya posta kwa anuani kamili ya waandaji. Watengenezaji wa filamu husika watapaswa kuambatanisha na mkanda wa filamu (VHS/DVD/VCD).
Zoezi la utumaji fomu na kuzikusanya litaanza siku ya tangazo la kwanza na kufungwa mwezi mmoja baadae.Shughuli za utoaji tuzo, zitataambatana na burudani toka kwa wasanii mbalimbali wa nchini watakaochaguliwa kutumbuiza na kupamba shamrashamra hizo.
Kutakuwa na jopo la majaji wanane (8) watakaochaguliwa na waandaji kwa kushirikiana na Baraza la sanaa la Taifa nchini watakaokuwa na jukumu la kupitia filamu zote na kuzitolea uamuzi.Filamu zitakazoingizwa kuwania tuzo ni zile zilizotengenezwa na Watanzania kuanzia Januari 2007 hadi mwisho wa siku ya kualikwa watengenezaji kuingiza filamu zao ambayo itakuwa Machi 31.
Tuzo zitatolewa katika vipengeke vifuatavyo:-
Filamu Bora ya Mwaka, Muigizaji Bora wa Mwaka wa Kiume, Muigizaji Bora wa Mwaka wa Kike, Muigizaji Bora Chipukizi wa Mwaka wa Kiume, Muigizaji Bora Chipukizi wa Mwaka wa Kike, Mwongozaji Sinema Bora wa Mwaka, Mchekeshaji Bora wa Mwaka, Mwandishi Bora wa Filamu, Mtunzi Bora wa Filamu, Filamu Bora ya kutisha, Muigizaji Mwandamizii Bora wa kike (supporting actor), Muigizaji Bora Mwandamizi wa Kike; Adui Bora kwenye Filamu, imbo Bora wa Mwaka (Sound Track), Mhariri Bora wa Filamu.
Pia itatolewa tuzo ya heshima kwa wale waliotoa machango wao kukuza sanaa nchini.Zawadi zitahusisha vyeti na fedha taslimu na mshindi atakuwa mmoja katika kila kipengele.
Tukio la utoaji wa tuzo hizi limepangwa kufanyika mwezi Mei 2008 na litafanyika kila mwaka.
What's wrong with that dude in Arsenal's jersey?
ReplyDeleteIf he doesn't know,I am letting him know he is out of place.
Ndugu Michuzi,
ReplyDeleteNina swali kidogo. Je, nini tofauti baina ya TITI na ZIWA?
Mimi nilikuwa nataka kusema kuwa nimependa sana engo yako ya picha ya demu wa kitasha.
Ahsante sana.
hata kama ndio mwanzo wa hizo tuzo basi walitakiwa wawe na dressing code basi sio na kuja na tujezi twa emirate na makubasi chini hii ya wapi hata hao walioandaa wamekosea kualika watu kienyeji hivyo.
ReplyDeleteWasi wasi wangu ni kama muda wa kutoka sasa hadi May utatosha kupata watu wanaostahili hizo tuzo. Mara nyingi vitu kama hivi huwa inabidi vipewe muda wa kutosha ili kupunguza malalamiko ya upendeleo.
ReplyDelete...PONGEZI kwa wote waliohusika katika kuanzisha tuzo hizo. Hata hivyo si vibaya wakafikiri upya ama
ReplyDeletekupata mawazo ya wadau juu ya tuzo za:
Adui Bora wa filamu wa mwaka...!
Filamu bora ya kutisha ya mwaka...!
Jamaa wa 'Arsenal' vipi hakupata taarifa kuwa mavazi ni 'smart'au ndio kama mimi kauka nikuvae mwenzangu...maanake anaonekana yuko alone alone tu.
ReplyDeletenakwambia huyu anaitwa majuto ni mwandishi wa habari lazima atakua rafikiye misupu..kavaa mjezi ndo nini.halafu mchafu
ReplyDeletehuyo jamaa mwenye hiyo RED Jersey nadhani ana matatizo..huoni watu wanvyo muangalia kwa kushangaa na jamaa pembeni ana kausha kwa noma...but mmh yule kijana juu kabisa mwenye "Green" t-shirt ni nani??? INFO PLEASE!!!
ReplyDelete