MPIRA UMEISHA NA YANGA WANAONDOKA NESHNO KIFUA MBELE KWA KUILA AS ADEMA BAO 2-0 HIVYO KUSONGA MBELE KWENYE KOMBE LA WASHINDI LA AFRIKA NA SASA ATAKUTANA NA TIMU KUTOKA LIBYA.
HUKO ETHIOPIA TUNAAMBIWA SIMBA IMETOKA DROO 1-1 NA AWASA YA HUKO KATIKA MGUU WAO WA KWANZA WA MCHUANO WA KLABU BINGWA AFRIKA, AMBAPO MSHINDI WA MGUU WA PILI UTAOCHEZWA WIKI MBILI ZIJAZO HAPA NESHNON ATAKUTANA NA ENYIMBA YA NIGERIA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 29 mpaka sasa

  1. Uwiiiii Raha tupu babake. Haya mwaga mapicha watu tujinome !! Go ""Dar Young Africans we got the name we got the Game""

    ReplyDelete
  2. Mkuu naona mambo yamekuwa mengi. Simba walishawatandika Awassa 3-0 hapo Neshno. Kutegemeana na matokeo ya mechi nyinginezo huenda wakawa wanatakiwa kukabiliana na Enyimba katika hatua inayofuata.

    ReplyDelete
  3. mi nilifikiri arsenal kumbe yang! bongo kuna mpira au mdebwedo? hivi lini taifa star itacheza kombe la dunia au hiyo yanga au simba itacheza na manchester?n azitafunga mabao mangapi?

    ReplyDelete
  4. Hivi wewe Michu ulizani waoshavinywa bado tumelala sio?Huo mguu wa pili hapo nashino Simba acheze na nani tena?Acha fix nadhani hata matokeo uliyoweka yanaweza kuwa si sahihi.

    ReplyDelete
  5. Michuzi hebu eleza vizuri hiyo habari ya Simba, unasema mshindi baada ya mechi ya pili atacheza na Enyimba, kwani Simba hiyo haikuwa mechi yao ya pili, si walishacheza na kushinda bao tatu bila majibu hapo Dar katika mechi ya kwanza na hiyo ni ya marudiano? au umeandika hivyo kwa sababu za ushabiki wako kwa Yanga? maana kama wametoka sare basi mnyama anasonga mbele kwa jumla ya mabao manne dhidi ya moja lao, na hao yanga wako unaowafagilia hapo wameshonga kwa ushindi wa mabao mawili dhidi ya moja la hao jamaa, sasa nani mkali hapo, hebu rekebisha hiyo habari hapao! samahani kama utakasirika lakini nimeandika kwa ghadhabu kidogo baada ya kuona kaushabiki kamezidi hapa!!

    ReplyDelete
  6. Wewe upo dunia gani???Au ushabiki umekudhuru.Simba walishinda 3 bila nyumbani.Mechi hiyo ya marudiano ni mashindano yako.Wacha Uyanga wako sema kweli.

    ReplyDelete
  7. Wacha ushabiki wako.Penda Yanga lakini sema kweli.Simba alimchabanga Awassa 3 mtungi wiki mbili zilizopita.Au ulikuwa kwenye coma na sasa ndio umezinduka????

    ReplyDelete
  8. huenda unapendelea au hujui kinachoendelea.Simba ndiyo wamefuzu kwa uhakika kuliko Yanga - walishinda mechi ya kwanza 3-0 Dar Es Salaam two weeks ago, kwa hiyo kama wametoka 1-1 ugenini ina maana aggregate score ni 4-1 kwa Simba.tafadhali rekebisha story yako Mich.thanx 4 your efforts, though.

    ReplyDelete
  9. Asante vijana wa Jangwani! Wembe huo huo hata kwa walibya!!

    ReplyDelete
  10. Hebu acheni ushabiki wa kijinga,sasa hao Yanga si walitoka drooo kule Madagasika,na Simba kutoka drooo kule Etopia kuna aibu gani,si wote wawili wamesonga mbele!!!ahhh ujinga kweli hauna mwisho...tufurahie timu zote zosonge mbele,by the way,poleni Miembeni!!!

    ReplyDelete
  11. Hebu acheni ushabiki wa kijinga,sasa hao Yanga si walitoka drooo kule Madagasika,na Simba kutoka drooo kule Etopia kuna aibu gani,si wote wawili wamesonga mbele!!!ahhh ujinga kweli hauna mwisho...tufurahie timu zote zosonge mbele,by the way,poleni Miembeni!!!

    ReplyDelete
  12. hongereni yanga na simba kwa ushindi wa kuvuka raundi hii watanzania wako juma yenu

    ReplyDelete
  13. We Michuzi unazungumzia nini??

    Kwa taarifa yako hii ndio mechi ya Pili,

    Ya kwanza tulimtungua AWASA 3-0,

    sasa unachokiongelea ni nini,

    Labda kama kuna kombe lingine au kirafiki ndo Awasa watakuja hiyo wiki ijayo yako unayoisemea

    ReplyDelete
  14. wee unaposema simba mmmm... droo mbona inatosha sana?! mguu gani tena wa pili wakati first leg watu walichanja 3, we vipi?

    ReplyDelete
  15. Michuzi habari hiyo umechemsha. Simba wameshapita raundi ya awali baada ya kushinda mechi yao ya kwanza goli 3-0, sare ya leo ya 1-1 inamaanisha Simba wamevuka kwa jumla ya goli 4-1. Simba Oyeeee!!!.
    Mdau

    ReplyDelete
  16. michuzi mbona unatuchanganya?? maana naangalia kwenye tovuti ya bbc wanasema simba alishinda mechi ya kwanza na awassa 3,0.na leo ndo mchezo wa marudiano ila mpaka sasa hawajaweka matokeo,samahani naomba unifafanulie hili!! maana nategemea sana blog yako kupata habari za bongo!! ahsante

    ReplyDelete
  17. OYAA MICHUZI MWAMBIE MSIKAJIWAKO JK ASHUSHE BEI YA UMEME,INATUBANA SANA

    ReplyDelete
  18. Uliyeandika habari za sport inaonekana huipendi Simba binafsi inakuwaje kusifia Yanga wakati ilipoteza mchezo wa kwanza na Simba walishashinda mchezo kwa kwanza National Stadium 3-0 dhidi ya Awassa kwa uwiano huo Simba wameondoka na point nne kwa kushinda mchezo mmoja na kutoka sare wa pili wakati Yanga wameshinda mmoja na kupoteza mwingine.Hariri vizuri habari zako za kukandia Simba (USA)TAIFA KUBWA na kusifia Yanga UMOJA WA MATAIFA unaoshindwa hata kutatua migogoro ya Dafur.

    ReplyDelete
  19. UMECHEMKA MICHUZI.SIMBA WALISHAWAFUNGA AWASSA CITY TATU
    BILA TENA MIMI NILIKUWA BADO DAR
    WAKATI HUO.SASA IWEJE WARUDIANE
    TENA TWO WEEKS AHEAD.HEBU REKEBISHA
    OTHERIWSE UMEZEEKA.

    ReplyDelete
  20. MICHU WACHA UNAZI SIMBA MMMH NDIO NINI? VILE VILE NAKUFAHAMISHA JAPO MIMI SIPO HAPO BONGO SIMBA ISHAIFUNGA AWASSA BAO 3 KWA 0 KTK UWANJA WA NASHINO SASA HIYO MECHI YA WIKI MBILI ZIJAZO UTACHEZA WEWE NA HAO YANGA (MGONGO WAZI) SISI SIMBA TUNAMSUBILI MSHINDI KATI YA INYIMBA NA TIMU MOJA YA WALA NYANI (CONGO)

    ReplyDelete
  21. Mkuu, naona unatangulia mno kuzeeka
    kuliko mimi. Wiki mbili zilizopita Simba alicheza na huyo jamaa akamtundika TATU kwa KURUDUMU, na kwa maana hiyo amemtoa jamaa kwa magoli 4-1! Usijali, najua utakuwa umepitiwa tu kidogo. Au we YANGA???

    ReplyDelete
  22. We Michuzi umelala saa hizi?
    Unapitwa huku Jengo la Ushirika hapa mtaa wa Lumumba linaungua.
    Tuwekee mitundiko humu

    ReplyDelete
  23. CHIBIRITI yeye mpira umempitia kando.

    ReplyDelete
  24. Yanga safi sana, maana ni raha kwa kwenda mbele. Na huyu nayelalamika kuwa Michuzi anapendelea Yanga ana maana gani?

    Usiposhangilia Yanga, Msondo na CCM hapa Tanzania utashangilia nini?

    Robert Mujuni

    ReplyDelete
  25. Hapo wadau unashidwa kuelewa michuzi ana maana kuwa Yanga wamesonga mbele na watakutana na timu ya libya. Mmmh ya michuzi sio katika matokeo ya droo kkwenye hii mechi ya pili bali anafahamu fika kuwa simba wamesonga mbele kwa 4-1 baada ya kushinda awali kwa 3-0 zelo ila issue ni kuwa watakutana na NEYIMBA hapo ndio Michu anashtuka na kuguna mmhhh....Muwe mnafikiari basi mara moja moja wadau si kazi kubeba MABOX tu....

    SHABIKI WA SOKA BONGO

    ReplyDelete
  26. Wewe anon wa hapo juu acha kutetea ujinga.Michuzi alikosea kusema Simba na Awassa zitacheza baada ya wiki mbili.Kwa kuandika kwake hivyo ina maana kwamba hamna mshindi na suala la kukutana na Enyimba halipo hapo.Michuzi anaanza kuondoka Pan na kurudi Yanga.Ni bora akasema wazi na sio kuleta ushabiki wa kitoto.Nakumbuka Simba alipomtungua Yanga huko Morogoro basi Blog ya michuzi ilikumbwa na matatizo ya kiufundi kuandika matokeo.Simba walipowachapa Awassa 3 Michuzi alikaa kimya au amekumbwa na selective memory loss.

    ReplyDelete
  27. Na wee mdau ambaye kila picha ni lazima umtaje Chibiriti tuondolee NONGWA zako kwenye eneo letu hili...Mtoto wa kiume unakuwa na gubu kama nini, bwana! Kama umempenda chiiriti mfuate huko aliko sio kila Michuzi akiweka picha watu wanachangia wee una kazi ya kumtaja Chibiriti! wee, vipi????????????Tunaanza kuwa na wsiwasi na wewe sasa!!!

    ReplyDelete
  28. Ngoja nimsaidie Bro. Michu kidogo hapa maana naona wadau mmemuandama kama nyuki na asali. Pia si walaumu kwa kushindwa kutegua mtego wake. Michuzi hakuwa na nia mbaya kusema Simba mmmm. Alikuwa ana maana Yanga Oyee na Simba ameunguruma huko Ethiopia. Lakini kwa kuwa inaonyesha wengi wetu tumeshakaa nje na hata kusahau mlio wa simab ndio maana tukashindwa kutegua mtego huu. It's me Start boy!!

    ReplyDelete
  29. KWA TATHMINI YA KITAALAMU NA YENYE KUFUATA MAADILI YA UANDISHI WA HABARI, SARE YA SIMBA YA BAO 1-1 DHIDI YA AWASA HUKO ETHIOPIA NDIYO INGETAKIWA KUPEWA UZITO MKUBWA KWA SABABU IMEFANUIKIWA KUSONGA MBELE KWA JUMLA YA MABAO 4-1!
    USHINDI WA YANGA WA MABAO 2-0 NA HIVYO KUIFANYA ISONGE MBELE KWA JUMA YA MABAO 2-1, ILIPASWA KUCHUKUA NAFASI YA PILI(UZITO WA PILI).
    NASEMA HIVYO KWA SABABU TIMU IKICHEZA UGENINI NA KUPATA MATOKEO MAZURI YA KUSONGA MBELE, INAKUWA NA UZITO MKUBWA KWANI WENGI WATATAKA KUJUA MCHEZO HUO ULIKUWAJE.
    MECHI YA YANGA AMBAYO LICHA YA KUTANGAZWA REDIONI, KUONYESHWA KWENYE TV NA WALIO NYUMBANI KUSHUHUDIA MECHI HIYO, INAKUWA IMEPOTEZA MVUTO WA AINA FULANI.
    LAKINI KAMA MJUAVYO, WAANDISHI WENGI BONGO NI VIHIYO NA SUALA UPENZI LIMEKAA MBELE, HAINISHANGAZI KUONA MICHUZI AMECHEMKA NA KUDAI SIMBA INASUBIRI MECHI YA MARUDIANO DHIDI YA AWASA NDIYO IWEZE KUSONGA MBELE!
    LINGINE AMBALO HUYU JAMAA YETU, NI MGUMU SANA KUOMBA RADHI YA KUSASAHIHISHA MAKOSA YAKE KWA VILE ANAJUA ANAMILIKI HII BLOG. LAKINI KIMAADIDI YA KAZI, HUYU JAMAA YUPO NYUMA KAMA KOTI.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...